Una maanisha tabia za kichawa?.Shida sio kafara shida ni wanaokuzunguka kwenye ukoo na watu wako wa karibu.
Kuna jamaa yetu alizaa nchi za nje na hakutaka watu wake tanzania tufahamu hata yoyote wala ndugu.ila alijaribu kuzaa hapa tz na ndugu wakafahamu yani mtoto ni wa tz ni kama tabia za Tlaatlaah
Kiongozi nimefurahi naweka makazi hapa nime miss hekaheka za Samson 😁Sehemu ya sita.
Hakuna kizuri kisicho na kasoro hata hivyo wengi wetu huwa hatukubali au kibaini kasoro za vitu vyetu tunavyohisi ni vizuri Sana, baadaye makosa,visa na tabia zitakazojionesha kwenye vitu vyetu huwa tunapagawa na kuvurugikiwa akili kwani huja ukiwa hutegemei au kujipanga.
Kisa cha Moses kimenifundisha mengi ambayo sikuyajua kabla,na hata hivyo si rahisi kutokea Kwa familia nyingi.
Sasa endelea....................
Nilipokea simu ya mke wangu Zawadi huku nikiwa nashindwa nimsemee mbovu ama nimpe nafasi na kumbeleza.
Eeeeeeh habari za asubuhi,umeamkaje mke wangu.nilisalimia.
Mimi Niko vizuri tu,ila naomba nisamehe mume wangu ,nimekaa masaa machache tu hapa nyumbani lakini najisikia vibaya,Kwanza Baba hapendi kuniona hapa,lakini Mimi mwenyewe napenda nirudi ,sasa Mimi hapa natoroka kwakuwa mama hapendi Mimi kuondoka.
Yote Kwa yote naomba nisamehe Moses,najua unanipenda,na Mimi nakupenda sana mume wangu ila sometimes sijui ni nini huwa nafanya.
Mke wangu aliweka kituo.
Karibu, karibu mke wangu.
Niliongea Kwa mkato na sauti ya chini.
Mnamuona Moses alivyo na dharau yaani tunajaribu kumwambia ukweli yeye anaamua kuongea na simu , wewe Mose sisi tumeshajua wewe unataka kujitenga na Sisi kwenye biashara,
Na wewe ungesema tu Kaka kuliko kutafuta njia za uongo uongo wanaume sikuzote tumenyooka kama unahitaji,kuwa mwenyewe,poa tu.
Washirika wangu waliendelea kuongea mambo Kwa kubahatisha huku wakikubaliana kana kwamba walinisikia nikiongea.
Oyaaa wazee mbona mnaongea vitu havipo?hebu acheni hizo mambo Mimi mwenyewe sijawahi hata kufikiria hayo Kwanza mnajua jinsi gani tunaaminiana hebu fikirieni Dunia ya Leo biashara ya kushirikiana zaidi ya watu watatu ,mbona wengi hawawezi lakini Mimi na nyie tuna mwaka wa ngapi kila kitu kinaenda sawa?
acheni hizo wazee.
niliongea Kwa kujiamini huku nikiwa na furaha isiyo na mfano baada ya kusikia mke wangu anarudi.
Sasa Moses samahani,ndugu yetu tufanye haya yameisha,tunaomba basi fanya mpango wa kupata leseni mpya si unajua mwaka ushageuka huu,tena ziwe zote leseni ya biashara pamoja na ya Maliasili.alishauri mshirika wangu.
Hiyo ya biashara nishalipia kila kitu ni kwenda Kwenye ofisi za maafisa biashara na kuzichukua tu, but kuhusu leseni za uvuvi hizo bado ,hata hivyo kutakuwa na semina Kwa wavuvi na wafanyabiashara wapya wa samaki kwani kuna Mabadiliko kidogo kwenye Sheria za uvuvi nchi nzima.nilifafanua.
Sawa wewe Moses ndiyo umeishikilia hii biashara mipango yako,ushauri wako ndivyo vitu vinaipa uhai hii biashara bila wewe pengine tungekuwa ziwani tu Hadi sasa tusingekuwa kwenye biashara.aliongea mmojawapo.
Na kwasasa sitaki kabisa kurudi ziwani Kwanza pesa ipo lakini ni ya maumivu tofauti na kununua na kuuza kama hivi.alidakia mwingine.
Jamani basi sawa,Mimi Nina matatizo kidogo ya familia hata hivyo hayajaisha nahitaji kwenda kuweka sawa.niliwaaga.
Sawa bro Mose lakini kumbuka kutujuza hata Kwa simu,ikiwa utakuwa na dharula .walishauri kisha tukaagana.
Nikiwa njiani mke wangu alipiga simu kwamba kasharudi yupo nyumbani.nilifurahi sana japo nilikuwa na maswali lukuki ya kumuuliza kwani niliona kama hayupo sawa kiakili.
**************************
Hatimaye majira ya jioni Mimi nilirejea nyumbani na kumkuta mke wangu na tumbo lake ambalo lilikuwa kubwa yupo nyumbani,nilimsalimia huku akiwa Hana bashasha kama alivyokuwa akiongea kwenye simu badala yake alikuwa kanuna kiasi cha kushindwa kuanzisha mazungumzo yeyote .
Lakini nikaona Mimi ni mwanaume sipaswi kulegea moja Kwa moja kuonesha namuogopa napaswa kumwambia ukweli.
Mke wangu,unajua umenikosea sana, kitendo cha kuondoka hapa nyumbani na kwenda kwenu na licha ya kukufuata bado ukaungana na mama ukikataa kurudi,hivi unajua umeniudhi na kuniumiza kiasi gani? Nilivinja ukimya.
Mume wangu Mimi nilijua utafurahi baada ya kuona nimerudi ili maisha yaendelee,sasa hayo maswali yako ni kutafuta ugomvi,wewe ulikuja nyumbani kunifuata mimi,hatimaye nimerudi sasa mengine ya nini.alijibu kijeuri mke wangu.
Wewee Zawadi usinichukulie Mimi Fala nitakupiga nikuumize,sitojali ujauzito wako,ohooo , nahitaji unijibu nini kilikufanya ukatoka nyumbani na kunidhalilisha,Mimi nitaonekana mwanaume wa aina gani,mtaa mzima wanajua mke kanikimbia.niliongea kwa hasira.
Moses bwana wewe na Mimi wote ni watoto wa mwisho kuzaliwa najua tabia za watoto wa mwisho,lakini tambua wewe ni mwanaume,Acha kudeka,eti watu watanionaje kwahiyo unaishi na Mimi Kwa kuwaridhisha watu? yaani Ile juzi umekuja usiku usiku ili tu uwaridhishe watu.hebu tumia hekima kidogo mume wanguuu.alijibu mke wangu huku nikijikaza Kwa hasira nisimpige kwani nilifikia kwenye kiwango cha mwisho cha hasira.
Halafuu kumbe mke wangu ulishaolewa ,tena hii kwangu ni ndoa ya tatu Kwanini ulinidanganya Zawadi?
Usikute Una watoto kabisa Mimi sijui tu.
Niliongea huku nikiomba Mungu nisiharibu chochote.
Unasemaje Moses,Nani aliolewa?
Wewe hizi habari kakupa nani?
Ahaaaa kwahiyo umeamua kutafuta kete ya ushindi Kwa kuzusha maneno siyo?
Yaani familia yoooote ifiche hili suala usijue,Kwanza linafichika kivipi?
Moses nina Imani ungejua tu serious,ni mmbea na mnafiki gani aliyekwambia haya? mume wangu naomba uniambie aliyekupa taarifa feki za kuniharibia.aling'aka mke wangu.
Zawadi ,tufanye uliolewa ukaachwa na sasa uko na Mimi naomba utulie, tulia mke wangu ili nifanye shughuli zangu Kwa Amani.niliongea huku nikiingia chumbani.
Moses,Mimi siyo mjinga nakwambia naomba uniambie ni Nani aliyekupa hizi taarifa za uongo?na alikuwa na maana gani kunidhalilisha,usiniambie haya masaa machache niliyotoka hapa tayari kuna wambea wanaitaka nafasi yangu?
Sasa nitapeleleza nitajua tu na nikimjua huyo mtu nitahakikisha hatanisahau.aliongea mke wangu akiwa kashaanza kulia kilio cha kwikwi.
Nilitoka chumbani kisha nikamkumbatia na kumbembeleza,aje chumbani,huku nikiwaza au Fetty kanidanganya?
au mke wangu kipenzi zawadi hajawahi kuolewa? Lakini mke wangu naye kwanini alie hivi au kuna ukweli ambao siujui?nilijiuliza kisha nikamwacha mke wangu kipenzi pale kitandani niliwasha taa zote huku nikitoka nje na kuona kuko kimya kuashiria watu wanapungua barabarani yaani kumekuchwa.
Niliishika simu yangu na kugundua nimepigiwa na watu wengi lakini Baba Mkwe alipiga zaidi na sikuisikia kwakuwa niliitoa sauti.
Nilizipuuza simu zote na kumpigia Baba Mkwe huku nikitoka na kwenda mbali zaidi ili niwe huru.
Baada ya kusalimiana maongezi yakaendelea,
Najua Kwa asilimia nyingi mkeo yupo kwako,yaani Nina Imani hiyo.aliongea Baba Mkwe upande wa pili.
Ni kweli Baba mke wangu yupo .kwani hakuwaaga? Nilijifanya sijui.
Mimi huyu mtoto wangu Zawadi hata sijui ana matatizo gani,hata yeye na mama yake kuna muda wanaelewana ila Jana usiku wamegombana Sana kiasi cha watu kushindwa kulala Kwa wakati usiku kucha kusikiliza makelele yao.lakini nishukuru kama huyo mjinga yupo kwako,yaani ni msumbufu mno ,kuna dada zake wengi nimewalea lakini hawakuwa wasumbufu kama yeye ila ndiyo hivyo watu hawafanani.baba Mkwe alikata simu huku nikishusha pumzi ndeefu.
Wakati narudi ndani nilishangaa uwepo wa mtu akiwa anasogea karibu na mlango huku akijificha taa ya nje isimmulike.
Wee ni Nani na unataka nini usiku huu?
Huku nikimsogelea, lahaulaa alikuwa ni Fatuma dada aliyenipa taarifa nyingi za mke wangu ambazo sikuzijua kabla,lakini pia alinikomesha akidai niache mazoea na yeye kwakuwa nilimtelekeza mgahani na kumuachia bili.
Enheee niambie Musa nilitaka nigonge mlango lakini nikakuona ukiongea na simu Kwa mbali, vipi tena kuongea na simu kwenye mapori usiku huu huoni ni hatari? Aliuliza dada Fetty Kwa sauti ya mahaba huku nikibaini lengo mapema sana.
Kabla sijamjibu chochote Fetty,mke wangu naye alitoka huku akiniuliza naongea na Nani?
Na kafuata nini usiku?macho ya Fetty na mke wangu yaligongana.huku Fetty akitazama chini,na mke wangu akitutazama Mimi na Fetty Kwa zamu huku akitingisha kichwa kama vile anakubaliana na jambo fulani huku akicheka kicheko hafifu.
Itaendelea...............................
DaahSehemu ya saba.
Duniani kila mtu aliwahi kuumizwa na mapenzi Kwa namna fulani,ila tunatofautiana sehemu mbili,kwenye maamuzi ya kuutetea moyo ili usiumie.
Wapo wanaotumia akili kwenye mapenzi na ndiyo maana ni rahisi kumuacha mtu,wapo wanaotumia hisia zaidi,hawa ndiyo wahanga na wenye kulia mara nyingi kwenye mapenzi.
Je Moses yupo kundi gani?
Atatumia akili au hisia kwenye maamuzi yake?
Atakubali waachane na mke wake kipenzi zawadi? kirahisi tu waachane?
Hebu endelea na hiki kisa.................................
Wewe Malaya uliyefukuzwa na kutelekezwa mkoani kwenu na kuja huku kwetu,umefuata nini hapa kwangu ,saa nne za usiku,unafuata nini majumbani mwa watu,(huku akicheka kicheko cha Shari na hasira) usiniambie Una mahusiano na mume wangu Moses,Kwanza siamini kama Moses mume wangu anaweza kuwa na mwanamke Malaya kama wewe
Tangu tunasoma primary Fatuma hukujulikana unakaa wapi,ulisingizia unakaa Kwa Bibi yako,Yule alikuwa Bibi yako? mbona tuna taarifa kibao kwamba wewe ulikulia kwenye vituo vya watoto yatima kabla Yule Mzee uliyemuita Bibi hajakuazima kama mfugo na kukaa na wewe.
Ndoa yako umeiharibu,sasa umekalia kutaka wanaume wa watu! yalikuwa ni maneno kutoka Kwa Zawadi mke wa Moses akiropoka huku baadhi ya walevi na wapita njia na majirani wakisogea kusikiliza kelele na maneno ambayo hayakuwa na Amani.
Mimi kuna mzigo niliagizwa na watu fulani ambao walisema nimletee mumeo,ni hii bahasha Mimi sijui ina nini.
alijitetea Fatuma.
(Huku akinyakua Ile bahasha Kwa kuipora)Kwahiyo umekosa mida yoooote ukaona uje muda huu,haya tunashukuru Kwa mzigo,umefika salama kwa muhusika,Una lingine? aliongea zawadi akionesha bado ana hasira na hajaridhika na namna alivyojitetea Fatuma.
Wakati haya yote yakiendelea, Moses alikaa kimya ni wazi alichukia mno ila alijikaza,alimchukia Fatuma Kwa kuja usiku nyumbani kwake Jambo ambalo halijawahi kumtokea,lakini alimchukia mkewe Kwa visa vyake kumshambulia Fetty akiwa Hana uhakika na maneno aliyozusha.
Wakaingia ndani wakiwa kila mtu kivyake hakuna aliyemuongelesha mwenzie.
Lakini Mose akavunja ukimya,
Mke wangu hebu nipe hiyo bahasha niangalie huenda kuna mambo ya muhimu na ya msingi,.
Zawadi akachukua ile bahasha na kumpa mumewe Kwa kumtupia ukiwa ni mwendelezo wa kiburi alichokianzisha siku si nyingi zilizopita.
(Huku akitumia lugha ya kabila la kwao kumweleza mkewe namna anavyoonesha dharau)
Mke wangu najua unajua ni jinsi gani nilikuoa Kwa mahari kubwa?
Pesa tasilimu na ng'ombe kadhaa,yote haya yalifanyika Kwa makubaliano ya pande zote mbili za familia,chini ya Mila na desturi ya kabila letu.
Heshima, nidhamu na kunitii siyo Jambo la hiyari ni la lazima.mahari yangu haikwenda bure mama,tena nikwambie tu kuwa ukiendelea hivyo utaishi na Moses mwingine kabisa tofauti na uliyemzoea, heshimu mahari yangu.mke wangu.
Moses unanichekesha Sana,Kwa mahari ndiyo nini labda eeeeeeh.
Kwahiyo ulininunua?
Yaani ni kama enzi za watumwa waliouzwa kwenda ughaibuni,kwahiyo unadhani na wewe unadhani ulininunua si ndiyo?labda nikufundishe mume wangu.
Mahari siyo manunuzi,bali ni kumuonesha thamani muhusika uliyempenda.
Mahari inakupa nguvu na uhalali wa kuniita mke kama unavyoniita,kwahiyo jitahidi kutofautisha mambo.......... kabla zawadi hajamalizia majibu yake,alikuwa keshashikwa na mikono ya mwanaume mwenye nguvu,asiweze kujinasua mkono mmoja wakushoto ulitosha kumdhibiti zawadi huku mkono wa kulia ukitumika kunasa vibao vilivyotua alipopachagua Moses.
(Niue,niue Moses niue mume wangu,si umesema wazazi wangu walikuuzia nipige ,nimalizie kabisa mwanaume huna huruma unashindwa kujua hata Niko na Hali gani? alilalamika Zawadi.
Wewe utanisimbua mjinga mmoja wewe , kabila letu hatujawahi kudharaulika na mwanamke,sasa mapenzi ya kisasa unayoniletea siwezi kukubaliana nayo.
alijibu Moses akiwa hata hajali vibao vidogovidogo vikimtoka bila shida yeyote.
******************************
Siku inayofuata Moses aliamka huku mkewe akiwa kitandani bado ,si tabia yake kulala hadi muda ule na Moses alijua kuwa Kwa magomvi na alivyompiga jana ni vigumu kuweza kumuamrisha chochote akawa amekaa tu sebuleni akiwaza na kuwazua.baada ya kukaa pale muda mrefu hatimaye mkewe aliamka akiwa hajataka kuoga,kunawa, wala kujiremba kama kawaida yake, badala yake alikuwa na begi la nguo huku akitoka nje bila kumuongelesha Moses.
Sasa mke wanguuu unaenda wapi?
aliuliza Moses huku akiinuka na kumshika mumewe na kumvutia ndani.
Moses niache,Mimi siyo gunia lako la mazoezi,niache nakwambia.
Kwakuwa Moses anampenda mkewe kuliko maelezo, hasira zilirudi upya,wakaanza kuvutana na mkewe pale sebuleni huku akimshushia kipigo heavy,kama vile mwizi.
Kupenda kubaya ,haswa ukipenda ukapitiliza, Moses hakujua nini anafanya si kujenga wala kubomoa , hakujua alichotaka nikuhakikisha Zawadi hawezi kutembea.
Baada ya kipigo kizito bila kujali tumbo la zawadi ,aliingia chumbani huku akihifadhi mkanda wake Kwa kuutupia kwenye uvungu wa kitanda baada ya kukamilisha dhamira yake.
Aliiona bahasha,akakumbuka jana hakuiangalia baada ya kutokea purukushani,kilichomtisha ni Uwepo wa muhuri wa polisi.
Akaifungua na kukuta barua ndani ikiwa ni wito kutoka Kwa jeshi la polisi,ikimtaka aende tarehe husika na akikaidi hatua Kali za kisheria zitafuata.
Nimefanya nini tena jamani,nimekosea nini? halafu wananitaka nifike saa tatu asubuhi ambayo ndiyo leo dah nitawahi kweli?aliwaza Moses akabadilisha nguo haraka haraka huku akitoka na kumuacha mkewe Zawadi akilia pale sebuleni akiwa hajiwezi Kwa kipigo.
Loading......................
Aiseee!?Sehemu ya saba.