Kutoana kafara kwenye familia, na Siri ya wazazi wetu

Hii iliendelea ?
 
Sehemu ya kumi na moja

Wakati nikishusha pumzi Kwa nguvu baada ya kujikuta tumefika ng'ambo salama, kutokana na kiwewe nilichopata kwenye ile boat,jamaa aliyekuwa ananicheka alinifuata na kunisalimia huku akitabasamu, alionekana ni mtu mwenye maisha fulani mazuri, Kwa namna alivyovaa,lakini hata simu zake alizoshikilia mkononi,zilimpa hadhi fulani.

Habari kaka,
Naitwa Moses , nisamehe Kwa kukucheka ,vipi ni mara yako ya Kwanza kusafiri majini nini? aliuliza.(Huku akicheka)

Hapana,nasafiri Sana tu ila vyombo vikubwa vya majini vinatulia kidogo kuliko hivi vyombo vidogo.nilimjibu huku kila mtu akishika njia yake........

Sasa endelea.................

Bro, wewe umeoa kwenye familia ya mke wangu siku nyingi,sasa niambie kuna nini sikijui maana ni kama nazungukwa
aliuliza Moses.

Mdogo wangu,Mimi sijui mengi kiundani ila,kuna namna ambayo nahisi ni Bora zaidi,achana na Zawadi,Kwanza wewe Moses huwezi kosa mwanamke,umejijenga,Una nyumba nzuri, lakini ni mtafutaji,Una sifa ambazo wanawake wa kileo wanazitaka,sasa Kwanini mtu mmoja akuhangaishe?

Haya ni mahangaiko Moses,
Hebu fikiria hasara uliyoipata,Kwa kuharibiwa vitu vyako vya thamani ambavyo ulivuja jasho kuvipata,huoni kama unapaswa ufanye maamuzi? aliweka kituo yule mgeni Kwa mtindo wa swali.

Ni kweli bro,hata hivyo mbona hili lipo akilini mwangu,wewe usijali bro Mimi nimekuelewa.alijibu kifupi Moses kisha mgeni akaondoka.

Moses aliweza kiunganisha Mawazo ya wengi,alikumbuka kuwa masaa machache Baba yake mzazi ametoka kumshauri aachane na zawadi,hali kadhalika Mshirika mwenzie kwenye biashara naye aliunga mkono Moses aachane na zawadi kwani waliona atapotea kwenye ramani ya maisha lakini si hilo tu familia ya zawadi nayo haikuwa radhi Moses awe na ndugu yao wakidai anamtesa,lakini mama wa Zawadi ndiyo kabisa.

Moses akaona ni vigumu kuachana na Zawadi lakini atajaribu kwasababu bila hivyo mambo yake yangekwenda kombo yaani vibaya.

*********************************

Siku inayofuata Moses alikuwa kwenye sehemu ya biashara yake akipanga na kupangua na washirika wake,huku wakilaumu serikali Kwa kitendo cha kuzuia baadhi ya vitendea kazi hali ambayo ingesababisha upungufu wa mzigo lakini pia ongezeko la asilimia kadhaa kwenye leseni zao liliwafanya wajikute wanakuna vichwa vyao.

Wakiwa wanaendelea kupiga mahesabu yao wajue ipi ni faida na upi ni Mtaji huku Moses akifurahi kimoyomoyo namna wenzie walivyo waaminifu kwani Kwa siku kadhaa ambazo Moses hakuwa kazini ingekuwa wengine wangecheza faulo (kuiba)lakini Kwa wale wenzie mambo yalikwenda poa.

Simu ya moses iliita, mpigaji alikuwa Zawadi.Moyo wa Moses ulilipuka nusu kukasirika nusu kufurahi.akaipokea na kuiweka sikioni...

Mume wangu , mbona umeniacha masaa yote hayo, kwanini lakini,si nilishakuomba msamaha my ,alisikika Zawadi upande wa pili.

Zawadi Kwanza hujasalimia,lakini hilo siyo suala ,habari ni kwamba Mimi na wewe tumefika mwisho wa ndoa yetu,siwezi kuwa na wewe tena,unanisumbua bwana, familia yako tu hainipendi,achana na Mimi bwana.aliongea Moses Kwa kujiamini.

Moses mume wangu mpenzi ,nimebakisha siku kadhaa niweze kujifungua,najua nimekukosea najua,lakini nisamehe nimekubebea kiumbe chako tumboni muda mrefu wa miezi yote hiyo,nasikitika kuona mtoto atazaliwa bila uwepo wa Baba yake,Moses fikiria mara mbili, nakupenda Moses, nakupenda mume wangu,na wewe unanipenda ,kifupi tunapendana Moses,achana na wengine.aliongea Zawadi kiupole mno.

Moses alishusha pumzi ndefu huku kiburi kikiongezeka,akitafuta namna ya kumjibu mkewe.

Mke wangu kipenzi hayo maneno ungeyasema tukiwa ana Kwa ana ningekuelewa lakini Kwa simu naona kama ni kejeli tu.Moses aliongea Kwa kujiamini.

Mume wangu nachukua usafiri sasa hivi nakuja hapo nyumbani tuongee, alisikika Zawadi upande wa pili

Mimi sipo lakini wewe njoo tu nitakukuta mke wangu.aliweka kituo Moses kisha akakata simu.

Siku ile ilikuwa nzuri Kwa Moses,simu kutoka Kwa Zawadi ilikuwa kama tiba Kwake ,mkwara wa kusema oooh nitakuacha ulikufa pale pale,alimmisi mkewe,alimisi tabasamu la Zawadi alikumbuka vingi anavyovijua toka Kwa mkewe,alijiwazia atakavyo libusu tumbo la Zawadi,alipanga awe mtulivu kuhusu uharibifu wa vitu hakujali ,madukani si vipo,alijua atanunua tu.

baada ya kukamilisha ratiba za kazi Kwa siku hiyo, aliingia kwenye soko dogo majira ya jioni na kufunga baadhi ya vyakula, alitoka hapo na kuingia kwenye Duka fulani la nguo na kununua nguo kadhaa za kike ,kisha akajitoma kwenye bajaji huku akili na hisia zake zikimuwaza Zawadi tu.

Maneno kutoka Kwa watu mbalimbali akiwemo Baba yake mzazi,aliyapotezea akiamini lazima ajenge familia yake bila msaada au ushauri kutoka Kwa watu wengine.njiani allibonyeza bonyeza simu na kupiga sehemu tofauti tofauti,huku akiwa amepanga kumfanyia Suprise mkewe.

Hatimaye bajaji ilikuwa uwanjani kwenye nyumba ya Moses,
Huku Moses akigundua hakuna dalili inaonesha uwepo wa mtu yeyote,

Alimlipa Dereva Bajaji huku akiziendea funguo zinapokaa na kufungua mlango.

Aaargh huu utoto huu,sasa Yuko wapi si aliniambia anakuja,sasa Kwanini anidanganye,na anapata nini akiniongopea huyu ni mjinga eeeeh,aliongea peke yake huku akipiga simu ambapo haikuonesha kupokelewa.

Hasira zilimjaa Moses,wivu ulimtesa,kuhisi anadharaulika,kuona ananyanyasika,mtu ambaye kamuoa Kwa gharama halafu anamsumbua hii ilimuumiza mno.

Simu yake iliita,jina likiwa ni My wife
Kama alivyolihifadhi kwenye simu yake,alipokea Kwa pupa huku akiiweka simu sikioni.

Hivi weee mtoto unanitakia nini mimi,
Nini unataka kwenye familia hii,
Unamtakia nini Mwanangu?

Umeshindwa kumuua ukiwa naye, Mungu akamnusuru, Lakini bado upo tu ni mpaka utakapo ridhika Kwa kuondoa roho ya Zawadi si ndiyo?

Zawadi ni mwanangu Mimi wa mwisho
Nilimzaa kipindi ambacho sikutarajia kupata mtoto Kwani umri wangu ulikuwa mkubwa,lakini Mungu ni mwema nilipata mtoto uzeeni .
Nikashukuru,na kumtukuza Mungu na kuiita ile ni Zawadi kutoka Kwa muumba,na ndiyo maana hata madaktari walimpa jina la Gift huku wakinitafsiria kuwa lina maana ya Zawadi Kwa Kiswahili.

Sasa wewe leo hii unampiga,unamfanyia fujo kadri unavyojisikia.
Hebu muache mwanangu,kwani hakuna wanawake wengine Duniani?
Mama Mkwe wa Moses aliongea Kwa ukali huku akimaliza maneno yote.

Moses alichukia,alikasirika alipiga mateke vyombo Kwa hasira,aliingia chumbani kwake akatupia ile parcel kitandani,aliziangalia nguo fulani ambazo alimnunulia mkewe , alikuja nazo kama sapraizi, naam suprise, lakini mambo yalienda ndivyo sivyo,

Moses alimpenda mno Zawadi,alimwelewa,alikaidi maonyo na ushauri wa baadhi ya watu,hakimuogopa mama Mkwe wake alipanga kwenda kufanya fujo Ukweni,hakuwa tayari kuishi bila Zawadi.

Alikumbuka utani,stori, wakiangalia runinga pamoja,kudeka Kwa Zawadi,shepu,urefu wa mkewe,sauti aliimisi,lakini hata kwenye ulimwengu mwingine Zawadi alikuwa vizuri ,Kwa hili Moses alipata taabu huku akiapa kwenda kumchukua mkewe Kwa nguvu.

Moses the last born kwenye familia mapenzi yalimtesa na kumtesa tena

Itaendelea ...........................
 
Kwa hiyo haka ndo kamwendelezo tulikokuwa tunakasubiri muda wote? 🚮🚮🚮
 
Asante JD ila usituweke sana.
 
Wakuu Edo kissy Selikavu kumbe Moses mwenyewe ni last born bhana 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…