Kutofanya kumbukizi ya Magufuli ni makosa yataigharimu CCM

1. Aliitoa CCM iliyochokwa shimoni.
2. Alirudisha mavazi na sare za CCM zilizochokwa kwenye jamii ya Watanzania.
3. Alirudisha makundi yaliyoparaganyika na kujeruhiwa na uchaguzi, ikiwemo kundi la Lowassa na kundi la Frederick Sumaye.
4. Alirudisha falsafa ya kuanzishwa CCM kwa kufanya chama cha wakulima, wafanyakazi, na makundi mengine badala ya jumuiya ya wafanyabiashara.
5. Hukuitaji tena rushwa ya pesa au ya ngono au kuwa mtoto wa fulani kupata nafasi ndani ya chama na serikali.
6. Alileta utawala wa wote wa chama bila kujali wanaojiita wenye CCM. Hao waliovimbiwa na ubinafsi aliwanyoosha hasa hadi maji wakaita mma.
7. Makundi mengi yalianza kuvutiwa na kujiunga na chama hiki. Hata wasiokuwa na chama walikimbilia CCM kwa sababu ya falsafa za Magu na wenzie.
8. Alirejesha mali nyingi za chama.
9. Alikijengea chama uwezo wa kujitegemea hasa katika mikutano na shughuli za chama, badala ya kupitisha kikombe kwa wafanyabiashara.
10. CCM haikuwa tena kichaka cha wakwepa kodi, wauza unga, na wezi wa mali za umma.
11. Alisababisha CCM ikawa na akaunti iliyoshiba.
12. Aliwezesha mavazi na bidhaa zenye chapa ya CCM, ikiwemo saa, kuwa biashara kubwa kwa wajasiriamali.
13. Aliondoa hulka ya wanaccm au viongozi wake kuvimbia raia mtaani, badala yake wengi waligeuka kuwa watumishi wa watu.
14. Aliingiza wabunge wengi sana kwa shabaha ya maneno matatu; "Nipeni connection, gunzi na betri haziwashi tochi, nipeni huyu nammudu akiwazingua namuwajibisha."
15. Alirudisha imani kubwa ya chama kwa jamii.
 
Hata wabumge zaidi ya 300 aliowapa ubunge wa mezani hakuna hata mmoja aliyeenda? Mnataka mkulima aliyekichokea na maisha ndiye ashinde huadhimisha vifo?
 
Amekufa na ila mnataka kujifanya hakuwepo wala hamkumbuki. Haya good move kwakweli....
Who is chadema who is ccm
CCM imemezwa na majizi ambayo Hayati alituambia kuwa wanaiibia nchi.

Usitegemee wamkumbuke kwa sababu ukitaja jina lake tu, basi kwao chakula hakishuki.

Umesahau Mkutano Mkuu CCM walimnanga marehemu waziwazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ