Kutoka Arusha: Mrisho Gambo atimiza ahadi ya kuchimba kisima Soko la Kilombero

Kutoka Arusha: Mrisho Gambo atimiza ahadi ya kuchimba kisima Soko la Kilombero

Wanasema "don't argue with a fool coz pipo won't notice a difference"

Ni hivi, serikali hii ndani ya hii miaka mitano iliagiza kila Mkuu wa mkoa asimamie ujenzi wa viwanda 100. Gambo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha zaidi ya miaka 3. Mpigie simu mwambie aweke list ya hivyo viwanda, aache siasa za kipuuzi za kwenda kuwachimbia watu maji yenye kinyesi, wakati soko limezungukwa na maji safi kutoka mradi mpya wa maji. Hizo siasa za ghiliba awapelekee wenye akili finyu kama wewe.
 
Hakika CCM imedhamiria haswa.
Mbunge mteule wa Jimbo la Arusha ndugu Mrisho Mashaka Gambo ameanza kutekeleza mojawapo ya ahadi zake alizozitoa jijini humo hususani katika soko kongwe na maarufu la watu wa kipato cha kati na chini ,SOKO LA KILOMBERO.

Mheshimiwa Gambo amewezesha uchimbaji wa kisima cha maji na hivyo kuondoa tatizo la maji sokoni hapo.

MY TAKE:
Tanzania ilichelewa sana kimaendeleo hatuna budi kuchapa kazi kwa kasi kubwa.

Jiulize swali mmoja pesa katoa kwenye budget ipi wakati yeye hata hajaapishwa?

Hao waindi wanaotoa pesa za hii miradi unafikiri wanategemea kupata nini?
 
Karne ya 21 unajisifia visima, dah kazi kwelikweli

Tena kisima chenyewe katikati ya mji, huku soko lenyewe limezungukwa na maji safi ya bomba. Kila mkoa kulitakiwa kujengwe viwanda 100, na yeye alikuwa RC miezi mitatu tu iliyopita, kashindwa hiyo sehemu watu wapate ajira, sasa anafanya siasa za ghiliba zisizo na tija.
 
Vichwa panzi wanamkenulia meno
 
Kamanda toeni ushirikiano mpate maendeleo ya kweli.Arusha imeamua kuchagua Mbunge
Watu wa Arusha ndio wa kuwafanyia hayo maigizo ya kitoto? Alikuwa mkuu wa mkoa kwa zaidi ya miaka mitatu hapo hapo Arusha, kipi kilimshinda kuchimba hicho kisima? Isitoshe hapo sokoni kuna Mradi mkubwa wa maji safi ya bomba, kwani asitandaze mabomba ya hayo maji safi, bali anapeleka utapeli wa kisima kama yuko huko poroni!

Halafu huyo Gambo eti Ni kijana lakini ana utapeli kwa kizee sana. Ni hivi hajawa mbunge kwa kura bali, ametangazwa kwenye yale maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hata afanye maigizo ya kitoto vipi hana ridhaa ya watu wa Arusha mjini. Aweke list ya viwanda 100@mkoa wakati akiwa RC, visima Ni kwa watu wa huko maporini.
 
Safi sana Gambo tunahitaji MAENDELEO sio kauli za kuchochea migomo na maandamano.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge NCHI.

URT - JPM
SMZ- Mwinyi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Uchaguzi utarudiwa aache mchecheto alikuwa wapi kuchimba na alikuwa mkuu mkoa.
Ujue huu ni ujinga mtu awe mkuu wa Mkoa asifanye eti kuchaguliwa ubunge ndiyo afanye tena kwenye kampeni zake alikuwa anajidai anaongelea kero kibao mpaka nikajiuliza huyu ni mpizani au na alikuwa wapi kwani hizo kero hazijatatua akiwa mkuu wako au serikali yao ya ccm hakufanya
 
Kamanda toeni ushirikiano mpate maendeleo ya kweli.Arusha imeamua kuchagua Mbunge

Watu wa huko Arusha ndio juu yao kushirikiana na huyo mbunge waliyopewa na vyombo vya dola. Lakini huyo mbunge juzi tu alikuwa RC, kilimshinda nini kupeleka hayo maendeleo mpaka saa hii awaletee ghiliba za kitoto?
 
Acha upuuuzi
Tanzania 60 years ilikua chini ya chana gani??
Dodoma tu pale mbona hakuna maji?
Hakika CCM imedhamiria haswa.
Mbunge mteule wa Jimbo la Arusha ndugu Mrisho Mashaka Gambo ameanza kutekeleza mojawapo ya ahadi zake alizozitoa jijini humo hususani katika soko kongwe na maarufu la watu wa kipato cha kati na chini ,SOKO LA KILOMBERO.

Mheshimiwa Gambo amewezesha uchimbaji wa kisima cha maji na hivyo kuondoa tatizo la maji sokoni hapo.

MY TAKE:
Tanzania ilichelewa sana kimaendeleo hatuna budi kuchapa kazi kwa kasi kubwa.
 
vikao vya mabaraza ya madiwani vimepitisha lini huo mradi? kama ni fedha zake binafsi lazima raia mzilipe, hakuna kitu cha bure duniani.
 
Watu wa Arusha ndio wa kuwafanyia hayo maigizo ya kitoto? Alikuwa mkuu wa mkoa kwa zaidi ya miaka mitatu hapo hapo Arusha, kipi kilimshinda kuchimba hicho kisima? Isitoshe hapo sokoni kuna Mradi mkubwa wa maji safi ya bomba, kwani asitandaze mabomba ya hayo maji safi, bali anapeleka utapeli wa kisima kama yuko huko poroni!

Halafu huyo Gambo eti Ni kijana lakini ana utapeli kwa kizee sana. Ni hivi hajawa mbunge kwa kura bali, ametangazwa kwenye yale maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hata afanye maigizo ya kitoto vipi hana ridhaa ya watu wa Arusha mjini. Aweke list ya viwanda 100@mkoa wakati akiwa RC, visima Ni kwa watu wa huko maporini.
Kwa nn watu wa chuga hatujamzomea huyo fala aliye jichagua kwa msaada ya NEC?
 
Hiyo shule aliyoipa jina la Gambo aliijenga kama nani akiwa mkuu wa mkoa? Au hicho kisima chenye maji yaliyochanganyika na kinyesi ndio bei ghali kuliko shule? Ccm itatawala milele au vyombo vya dola ndio vitayawala milele? Zile kura za wizi zimeletwa vituoni na vyombo vya dola wala sio kura za wananchi. Hizo siasa za kitoto mbona zilishapitwa na wakati. Kwahiyo amepew kura na vyombo vya dola ili awachimbie wananchi maji yenye kinyesi, huku soko limezungukwa na maji safi ya bomba?
duh!!!kweli bongo utachokifanya hakiwezi kumpendeza kila mtu.
 
Back
Top Bottom