Kutoka Butiama: Exclusive news

Kutoka Butiama: Exclusive news

Mpaka Waandae Hotuba Ya Raisi Ya Mwisho Wa Mwezi Huu Kwanza

Vitu Vinaweza Kuingiliana
 
...kutohudhuria kwa fisadi Mkapa kunaweza kuelezeka kirahisi kwamba fisadi alikuwa na wasiwasi kwamba kuna kibano kizito dhidi yake hivyo akaamua kuingia mitini. Je kukosekana kwa Mwinyi na SAS kuna maelezo gani? Au ndio mmomonyoko wa CCM unaanza kidogo kidogo kufuatia chama hicho kukumbatia mafisadi?
Kikwete usanii umekuzidi, huwezi kufanya maamuzi yoyote mpaka uunde tume sasa CCM iko njia panda.

Itabidi uamue kubadilika ili kuimarisha CCM na kuleta mshikamano ndani ya chama, au kuendelea kuwakumbatia mafisadi na chama kuwa na mafarakano na hivyo kugawanyika.

JK alemewa Butiama

na Mwandishi Wetu, Musoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MZIGO mzito wa kimaamuzi unaonekana dhahiri kumlemea Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ambaye amelazimika kuviongoza vikao viwili vizito vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, vinavyofanyika Butiama bila ya kuwapo kwa nguzo zake kuu kisiasa.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili unaonyesha kwamba, kukosekana kwa wajumbe kadhaa muhimu wa kudumu wa vikao vya CC na NEC ya CCM, kunaweza kwa kiwango kikubwa kutia doa kama si kuathiri baadhi ya maamuzi mazito ambayo yamekuwa yakitarajiwa kufikiwa.

Miongoni mwa watu hao muhimu ambao kukosekana kwao kumeshaanza kuibua hali ya wasiwasi na kuonekana kupwaya kwa uzito wa vikao hivyo vya Butiama vinavyofanyika kwa mara ya kwanza eneo alikozaliwa na kuzikwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ni marais na wenyeviti wastaafu wawili wa chama hicho, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wadadisi wa mambo kadhaa wa ndani ya chama hicho waliozungumza na Tanzania Daima kutoka Butiama, wanakielezea kitendo cha kukosekana kwa Mkapa na Mwinyi kuwa jambo ambalo litasababisha kulemewa kwa Kikwete na pengine kukosekana kwa nguvu ya kufikiwa kwa maamuzi mazito yanayogusa mustakabali wa wakati huu wa chama hicho.

Aidha, wakati kukosekana kwa viongozi hao wawili ambao ni wajumbe wa maisha wa CC na NEC ya chama hicho kunachagizwa na kupewa uzito mkubwa, na kutokuwapo kwa Rais mstaafu wa Zanzibar, ‘Komandoo' Dk. Salmin Amour Juma.

Kama hiyo haitoshi, vikao hivyo vinafanyika Butiama wakati pia akikosekana mwanadiplomasia adhimu nchini, Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye naye ni mjumbe wa CC na NEC kwa pendekezo la Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho.

Mbali ya Dk. Salmin, kikao cha NEC kilichoanza jana jioni majira ya saa 11 kutokana na kuchelewa kwa kikao cha CC, pia kinafanyika pasipo kuwapo kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Kutokuwapo kwa Dk. Salmin na Dk. Salim katika vikao hivyo viwili, kunalifanya suala la kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar, na hususan kufikiwa kwa muafaka wa kisiasa visiwani humo kati ya vyama vya CCM na CUF kuwa ni wenye mashaka makubwa.

Baadhi ya wajumbe wa NEC waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa majina yao magazetini, wanakielezea kitendo cha kukosekana kwa viongozi hao wawili wanaotoka Zanzibar kuwa jambo ambalo linaweza kuyafanya maamuzi kuhusu muafaka kuwa magumu.

Jambo gumu kwa chama hicho na hususan kwa Rais Kikwete kuhusu kukosekana kwa viongozi hao wa juu muhimu wanne, ni wasiwasi ambao umeshaanza kuzingira vikao hivyo, unaoonyesha kwamba huenda wazee hao wamekosekana si kwa sababu ya kuwa safari kama inavyodaiwa na uongozi wa juu wa CCM, bali kutoridhishwa kwao na mwenendo wa mambo serikalini na ndani ya chama.

Wana CCM waliozungumza na Tanzania Daima kuhusu hili, wanaielezea hatua ya watu hao kukosekana kuwa ni dalili ya mwanzo ya CCM ya Kikwete kuanza kukosa ushawishi ndani ya mioyo ya viongozi wakuu wastaafu, ambao sasa wanakiona chama kikipoteza misingi yake ya kihistoria ya kushika hatamu.

"Kumekuwa na wasiwasi kwamba, Kikwete amekuwa akifikia maamuzi mazito pasipo kwanza kukitaarifu chama na badala yake amekuwa akifanya hivyo kwa kutumia Bunge na ushauri wa kundi dogo la watu. Hali hii inaonekana kutowafurahisha wazee," alisema mfuatiliaji mmoja wa karibu wa siasa za ndani ya CCM.

Lakini pengine pigo kubwa kwa Rais Kikwete lilizidi kuonekana dhahiri jana baada ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mzanzibari, kulazimika kuondoka katika vikao hivyo kutokana na kufariki dunia kwa mama yake mzazi.

Kuondoka kwa Dk. Shein, kiongozi wa pili kwa mamlaka katika serikali na mtu aliyetokea kuwa mshauri wa karibu kikatiba na kikazi wa Rais Kikwete, kunayafanya maamuzi kuhusu siasa za Zanzibar kuzidi kuwa magumu.

Kutokana na hali hiyo basi, Rais Kikwete atalazimika kutumia ushauri wa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wake, Amani Abeid Karume, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi mstaafu Gharib Bilal na Wazanzibari wengine wasio na ushawishi mkubwa katika kueleza kwa kina athari za kisiasa, kijamii na kiuchumi za kuhitimishwa kwa muafaka ambao unatarajia kutoa baraka za kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba, watu hao muhimu, Mwinyi, Mkapa, Dk. Salmin, Dk. Salim na Dk. Shein wanakosekana katika vikao wakati moja ya ajenda inayosubiriwa kwa hamu na Wazanzibari ni hiyo ya kufikiwa kwa suluhu ya kudumu ya kisiasa huko visiwani.

Mbali ya hilo la mwafaka, kukosekana kwa Mkapa kwa mfano kunaufanya mjadala kuhusu masuala kama lile la Kashfa ya EPA na mengine yanayomgusa yeye binafsi kushindwa kujadiliwa kwa kina.

Hali hiyo inakuja baada ya watu kuwa na imani kwamba, vikao hivyo vya Butiama vinavyofanyika hatua chache kutoka alipozikwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, vilikuwa vikitarajia kupata majibu ambayo yangekisadia chama hicho kupata majibu kamili kuhusu nini kilitokea katika EPA zama za Mkapa akiwa Rais na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.

Kama ilivyo kwa Mkapa, kukosekana kwa Mwinyi, kiongozi ambaye kimsingi ndiye anayeweza kubeba mzigo wa kuwa mrithi wa kiuongozi wa taifa baada ya kuondoka kwa Mwalimu Nyerere, kunaufanya mjadala wa masuala kama lile la Richmond lililosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri kupwaya na kukosa mashiko.

Wafuatiliaji wa mambo wanakuona kukosekana kwa Mwinyi kuwa ni pengo ambalo litamwia vigumu Kikwete kuliziba wakati huu chama hicho kikiwa katika mazingira magumu kuvunja kuimarika na kuibuka kwa makundi mengi zaidi ndani ya chama hicho, yaliyoibuka baada ya masuala ya EPA na Richmond kuibuka.

"Kwa namna yoyote ile sisi kama chama tulihitaji sana hekima za wazee wetu kama Mwinyi na Mkapa katika kuhitimisha haya masuala ya EPA na Richmond, ambayo hayajapata kujadiliwa kwa kina," alisema mwana CCM mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima Jumapili jana.

Baadhi ya minong'ono inayosikika kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo inaeleza kwamba, Mkapa hakuhudhuria vikao hivyo kwa sababu ya kuchukizwa kwake na hatua ya kuhusishwa moja kwa moja na ukiukaji wa maadili wakati akiwa madarakani.

Inaelezwa kuwa, ingawa Mkapa alimuunga mkono Kikwete katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, kutajwa kwa jina lake sana katika masuala mbalimbali, ni jambo analoliona likiwa na baraka kamili za viongozi wa juu serikalini wenye malengo yao binafsi.

Baadhi ya wadadisi wanahofu kwamba, upo uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wameanza kuiona serikali ya sasa kuwa iliyopoteza uwezo na umadhubuti wa kuhimili mikiki mikiki na hivyo wakaamua kukaa kando.

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 27 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Wakati umefika kwa CCM na Tz kwa ujumla kubadilika. Mabadiliko hayaji kiulaini na ni lazima kukubali kwamab hatuwezi tena kurudi au kutizama nyuma. Gurudumu la maendeleo na la mabadiliko limeanza na hakuna wasi wasi wo wote litawagusa na kuwakera vizito waliopita wakiwemo viongozi wastaafu wa ngazi za juu. La muhimu ni kumhakikishia Kikwete kwamba tuko pamoja nae katika juhudi zake za kuleta mabadiliko na kuutokomeza ufisadi Tz ambayo unaathiri sana maisha ya raia wa kawaida. Hao waliokataa kuhudhuria wote matumbo yao yamejaa na hawana hasara yo yote kwa maamuzi yatakayotolewa kwani wameshajilimbikizia mali za kutosha.

na kiwete, Dar, - 30.03.08 @ 09:04 | #4113

kikwete aliwahi kusema ya kua watanzania wengi hawapendi dawa chungu bali wanapenda tamu,sasa alitwambia wkt mwingine lazima mgonjwa anywe dawa chungu ili apone,sasa km kweli alikua anamaanisha basi awape wagonjwa wa ccm wakina lowasa,rostam,msabaha,karamagi dawa chungu ili wapone,asiwe anasema tu kwa wananchi,wkt ndio huu kwa kufanya ivyo.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 30.03.08 @ 09:40 | #4118

mh. kikwete chapa kazi kwa mujibu wa ilani ya chama chako hiyo ndo dira yako na mkataba kwa watanzania na wewe. hongera kwa kupambana na mafisadi.

na Shija., dar es salaam, - 30.03.08 @ 10:00 | #4122

Wakati huu ni wakati mgumu kwa Watanzania wote, siyo Kikwete peke yake kama kiongozi. Sisi kama Watanzania wenye dhamira safi hatuna budi kumuunga mkono Kikwete kwenye maamuzi haya mazito yanahusu safari ndefu ya maendeleo ya taifa hili maskini,lakini lenye mali asilia lukuki.
CCM ni lazima ikubali ukweli kwamba inabeba mzigo huu wa ufisadi katika hujuma za uchumi wa nchi hii na imechangia kwa kiasi kikubwa sana,kuanzia kulindana hadi takrima na uchafu mwingine, kama Viongozi wastaafu walivurunda wanapaswa kuwajibishwa. Tanzania siyo mali ya Kiongozi ni ya Watanzania wote, hivyo kama alifanya hujuma anawajibu wa kujibu tuhuma hizo na siyo kuingia gizani na kususia vikao. Kwanza CCM ingeondoa sheria iliyoko kwenye katiba inayowalinda wastaafu hawa wasishitakiwe kwa makosa waliyofanya wakiwa madarakani, hapa ndipo chanzo cha fitna ya ufisadi na uhujumu wa uchumi wa watanzania.

na Mahmoud, Tanzania, - 30.03.08 @ 10:04 | #4123

Kikwete! Pole sana kwa kukosa busara Rais wangu lakini pia pole sana kwa

na Ngosha Ombasa, Nyamatembe,Nassa-Magu, - 30.03.08 @ 10:14 | #4126

Jamani mbona Mkapa alisema bayana kuwa yeye hatajihusisha na maswala ya kisiasa. Kwa hilo nampenda Mkapa maama alikuwa muwazi kabisa. Iweje leo tumtegemee kutusaidia kutoa maamuzi mazuri ya mwelekeo kuwakomboa wwananchi wa kawaida ambao wapo ktk lindi la umasikini hali yeye pia amechangia kutufikisha tulipo. Ina maana hivyo vichwa vingine havina akili kufikia maamuzi mazuri kwa faida ya nchi? Rais mtukufu, sisi tupo nyuma yako, wakane hao maswahiba wako ktk vikao hivi nchi isonge mbele. Kumbuka kuwa huwezi kuwatumikia mabwana wawili.

na Aisha, Musoma, - 30.03.08 @ 10:32 | #4128

Kumbe wengine hamjaisoma vizuri hii stori. Ni kwamba hao wastaafu, hasa Mzee na Mwinyi, Salim, Komandoo, nan Msuya wamemkimbia baada ya kugundua hatashughulikia mafisadi kama walivyomshauri, wakaona ni vema wajitenge naye. Ukisoma stori hii sambamba na Makala ya MASWALI MAGUMU ya Ngurumo utagundua kuna jambo hapa. Ila inaonekana kuna ambayo wameogopa kuandika kwani kwenye blogu ya Ngurumo kuna breaking news ambayo ndiyo ilipaswa kuwa hasa habari yenyewe...sijui tofauti hizi za uandishi zimetokanana na nini. Ngja tuendelee kutafakari.

na Masamaki, Dar, Tanzania, - 30.03.08 @ 10:36 | #4129

ccm siyo chama Mkapa,Mwinyi auSumaye,kwani wakifa wao maamuzi haya fanyika?KIkwete kaza buti.achana nao wezi hao kwanza ukikaa nao wawatakuambukiza tabia zao chafu

na akim makukungumahafu, iringa tanzania, - 30.03.08 @ 10:52 | #4131

Hallo,hallo Kikwete,CCM na Watanzania wenzangu wapenda haki na wachuk

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:13 | #4135

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:19 | #4136

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:19 | #4137

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:20 | #4138

CCM-Chama Cha Mafisadi,hatimaye kisambaratikana mikononi mwa Kikwete.EPA na Richmond vitawahukumu.

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:32 | #4139

hiyo ni laana unadhani mtawadhulumu watanzania mpaka lini? kila kitu kina mwanzo na mwisho, huu ni mwisho wa mafisadi kamwe Kikwete usiogope tupo nyuma yako kaza buti baba!!!

na ndorobo, belgium, - 30.03.08 @ 11:56 | #4157

Ndiyo dawa chungu lazima inyweshwe hata kama ni kwakufunga pua na kubana midomo kama wafanyiwavyo wattoto. Viongozi wa zamani kama wameamua kutohudhulia kikao hicho ni hiari yao, na hilo lisimzuie Kikwete kuendesha kikao. Kua Rais wetu, yatima ndio maisha yao ya kila siku wajikutapo hawana wazazi, hupaswa kufikia maamuzi mazito kwa maslahi ya watooto na wadogo zao. Kaza buti askari vitani. Ila tukumbuka iatabidi kuwavua pia hao waliokaribu yako na maswahiba ambao mwenendo wao ni wa mashak. Ndiyo mmekutana Butiama, kumbuka Mwalimu ilipobidi alimtosa bestman wa Harusi yake, Bw. O Kambona, nakuweka maslahi na mtizamo na maamuzi ya chama mbele.
No one is indispensable. Tanzania Kwanza.

na Mtukwao, TZ, - 30.03.08 @ 13:23 | #4166

WEWE SHIJA HAPO JUU MPUMBAVU SANA, KIKWETE TANGU LINI ANAPAMBANA NA MAFISADI??? AMEKUPA NINI ?? USITAKE KUTUKANWA JUMAPILI HII!!

na imani - 30.03.08 @ 13:40 | #4167

KIKWETE ANACHEZEA MOTO, MAFISADI HUWA HAWALINDWI, MWAMBIENI KIKWETE HAO JAMAA WALIOKOSEKANA SI WAJINGA, HAIWEZEKANI KWA MAMLAKA YA KIKWETE ALISEMEE SWALA LA EPA BUTIMA!!!! KITU KIKO WAZI, INA MAANA ANATAKA AMWITE MKAPA AKAMSUTE MBELE YA WANACHAMA LUKUKI HUKO BUTIMA???? THIS IS IMPOSSIBLE.

JE KIKWETE NCHI HII ANAWAULIZA HAO WAZEE??

SIJUI ANAJIAMINI VIPI MTU HUYU, NADHANI ATAPATA WANAWAKE WENGI WA KUMPIGIA KURA UCHAGUZI UJAO, NA WALE WANAUME WALIOKAMA WANAWAKE(i mean ambao hawajaui maisha na kutafuta ni nini)

HIVI ANATAKA SALIM AHED SALIM AMSHAURI NINI, NYUNDO,MSUMARI KILA KITU ANACHO??

HIVI MWINYI ATAVUMILIA KUONA MKAPA ANASUTWA IS THIS MAKES SENSE???

ANACHEZA NA MOTO HUYU BROTHER, UKIWALINDA MAFISADI, HUWA WANAKURUDI, NA HII NI KUWA YEYE MWENYEWE NI FISADI SO ANAANGALIA FUTURE YAKE, KUWA NA YEYE AJE KULINDWA

NYERERE NA MWINYI NDIO WALIKUWA MARAIS NCHI HII!!!!!!!!!!!!!!!!

na imani, USA, - 30.03.08 @ 13:47 | #4168

Hao waliokosekana hawana tija ktk nchi hii zaidi ya kuwa ni wezi wanaolindwa na sheria haswa mkapa na mkewe anna.

na Dawa chungu, Dar, - 30.03.08 @ 13:49 | #4169

Kutowasili mkutanoni kwa MKAPA, SALIM, SALMIN, SUMAYE ni baraka kwa Taifa kwani matatizo yote ya ufisadi yametokea wakati wao. Ningeshangaa kama MKAPA NA SUMAYE wangekwenda Butiama. Kutajwa kwa mara kwa mara kwa MKAPA NA SUMAYE ktk ufisadi ni jambo lisiloweza kuepukika hasa ukizingatia kuwa yote hayo yametokea wakati wao wakiwa madarakani na hawakuweza kuchukua hatua yeyote.

CCM haiwezi kushika hatamu kwa kuwatetea wezi, eti kwa vile ni VINGUNGE. Ni lazima tukumbuke kuwa SUMAYE amehusishwa na ufisadi hata bado akiwa madarakani. La ajabu ni kwamba hakuruhusu uchunguzi ufanywe ktk maeneo yale ambayo ameshutumiwa. Machoni mwa watanzania Sumaye atabaki kuwa ni FISADI. Na ndio maana hakuchaguliwa CC. MKAPA hajatokea ktk vyombo vya habari na kujibu tuhuma- naye ni muovu na ndio maana hakwenda Butiama kwani hana la kujitetea na anajua wazi kuwa JK hatamtetea.

Ili CCM ibadilike ni lazima ichukue DIRA mpya- DIRA YA UTEKELEZAJI NA KUWANYOSHEA KIDOLE MAFISADI HATA KAMA WAO NI MAKADA. Umaarufu wa JK usitegemee ushikaji bali itegemee utendaji. Hilo haliwezekani ikiwa akina GETRUD MONGELA watatetewa ktk CCM japo wamekula pesa ya AU, au MKAPA asiguswe kwavile ni mjumbe wa kudumu CC.

CCM imara itajengwa kwa kuondokana na TAMADUNI ZA MAADILI YA CHAMA ZILIZOPITWA NA WAKATI. Ni vyema kutokuwa maarufu kwa CCM lakini uwe maarufu kwa wananchi. TUMUUNGE MKONO RAIS WETU ILI TUWAFUNJE MOYO MAFISADI. JK CHAPA KAZI!!!!!!!!!!

na Zawadi Ngoda, Dar es salaam/ Tanzania, - 30.03.08 @ 13:57 | #4171

Ndugu Waadnishi wa Habari naomba muwe makini katika kuandika Kiswahili fasaha na kutochafua lugha ya Kiswahili, kichwa cha habari mumeandika ( JK alemewa Butiama ) na iliyosahihi ni ( JK aelemewa Butiama ) neno: elemea na elemewa inamaana tafauti na wasojua kiswahili Fasaha wanachanganyikiwa katika ufahamu wa neno na kulibeba kimakosa katika maengezi na maandishi :

elemea - ku-elemea , elemea : ameelemea. ( ni kitendo cha mtu kumuelemea mwengine ).

lakini aelemewa : elemewa - ku -elemewa , elemewa .( ni kitendo cha mtu kuelemewa na mwengine ).

kuna maneno mengi nakuta yanaandikwa vibaya na kuharibu lugha ya kiswahili Fasaha : mfano neno : Serekali huandikwa ; Serekari . Askari huandikwa Askali n.k

Lugha ya Kiswahili Fasaha ni moja kwa hiyo kusikuweko na uandishi wa aina mbili na kuharibiwa Kiswahili.

Kusiwe na kasumba ya Uzanzibari na Ubara kuwa Wazanzibari watamke li na ndio ngeli sahihi na Bara wakawa wanatamka na kuandika ri , Kiswahili Sanifu Kilichotamkwa na Wazee tokea Enzi na kuandikwa kwa ufasaha kwa hivyo kusije Kiswahili Chengine Kichafu Kisiojulikana mizizi yake.

dumtum alaa kheir

na Mzanzibari, Zanzibar, - 30.03.08 @ 14:07 | #4173

MZee Mwinyi yuko nje akipata matibabu. Anaheshimika kwa kuwa hakufisidi nchi ila alitoa ruksa kwa kila mtu ajiendeleze. Aliefuatia akaifuta ruksa kwa kila mtu akawapa wachache kuchimba mafuta, gesi, dhahabu, almasi, makaa ya mawe na kuikamua TANESCO kwa TANPOWER, Songas,Net Solutions, Richmond na zingine lukuki. Hao waliombeza kwa kutoa ruksa sasa tumejua siri yao walijipa ruksa kuuza kila kitu bei poa kwa mradi wa PSRC.

na BITs - 30.03.08 @ 14:26 | #4176

Aina gani ya uandishi hii? Mbona mwandishi unalalama ooh mbona Mwinyi, Mkapa, Sumaye, Salmin hawapo? Je idadi ya wajumbe wa kufanya maamuzi haijakamilika? Mwandishi hatakiwi kupendelea upande wowote kama unavyofanya wewe mpaka unafikia kudhani kuwa maamuzi hayatakuwa na nguvu kwa sababu tu ya kukosekana watu wako hao.Hayo tuachie sisi wasomaji?
Kwenu wajumbe we NEC (CCM), Tanzania ya leo ni ya kuchambua mambo, sio kila anachosema mwenyekiti ni sahihi, kama amekosea mumwambie hapa mkuu spidi imezidi au mwelekeo sio sahihi na sio kuwa wanafiki kupiga makofi kila anachosema.
Nasema hivi kikao kiendelee na fanyeni kazi iliyowapeleka hapo, wenye akili zetu tutachambua kujua ukweli ni upi. Waliokosekana watajulishwa kilichoendelea. Kikwete usiyumbishwe na mtu. Maamuzi ya kupambana na ufisadi ni magumu na ya kujitoa mhanga ila matunda yake watafaidi mengi na ka muda mrefu ujao.
Kwenu watanzania hakuna njia ya mkato katika maisha, ni nidhamu ya kufanya kazi tuu. Kwenu viongozi tunataka uwajibikaji katika nafasi zenu, hatutaki masihara, maneno yenu na matendo yaendane sio yatofautiane. Kwenu watu wa system mnahitaji kubadilika. Inasikitisha nchi inaoza na nyie mliokula viapo mpo kama hampo. Sitaki kusikia visingizio vyenu. Hakikisheni nchi inakuwa na utawala wa haki na sheria sio kwa watawala tu, pia kwa watawaliwa. Haki ni pamoja na kutooneana katika mambo yanayohusu ustawi wa kila mwananchi. Lindeni misingi ya nchi, misingi ya siasa zetu na sio watu. Mtu akikiuka hafai huyo, hata kama Rais anampenda. Narudia tena mtu asijaribu kukiuka, anayekiuka hatufai. Hivyo viapo vina maana sana. Sio kuwa wanafiki kama askari wa Zombe, siku ya siku kila mtu atawajibika kivyake.
Ushauri wangu wa bure kwa Serikali, wekezeni katika elimu ndio mambo yatanza kubadilika na si vinginevyo. Jengeni vyuo na wawezesheni vijana kujiunga na vyuo hivyo sio kuweka vikwazo. Kiongozi mzuri ni yule ambae anaona mbali na matunda ya kazi yake yanaonekana baada ya muda mrefu. Sio vitu vya muda mfupi kama kujenga uwanja wa taifa wa Kisasa au kuleta kocha Mbrazili ili twende Ghana. Hayo ni mambo ya muda mfupi.Kwa hayo machache natumaini kila mmoja ataanza kubadilika katika sehemu yake ya kazi.

na cadet culture son, dsm, tz, - 30.03.08 @ 14:50 | #4181

wewe mdebwedo unayejifanya unatakasha kiswahili mwenyewe unaandika kilugha...hakuna serekali katika kiswahili kuna serikali, hakuna kiswahili chengine kuna kiswahili kingine. situletee lugha zako za mchambawima za maji ya bomba kuwa maji ya mfereji,shule kuwa skuli,mazishi kuwa maziko hizo mmezoea wenyewe huko sababu ya mlivyomdebwedo mdomoni msitake kutuambukiza mdebwedo wenu sisi huku.

na bandarini, unaposhukia ukija tanzania, - 30.03.08 @ 15:04 | #4183

Bwana dumtum alaa kheir,
Tunashukuru kwa kiswahili ulichorekebisha. ila umeongea sana. Nadhani wengi wetu tumemwelewa. hapa tunataka issues zijadiliwe zaidi mambo ya kiswahili nenda hiko wizara za elimu za CCM ambazo wameshindwa kusimamia na kutoa elimu bora. Jadili ufisadi maswala ya lugha naomba hapa tusiyape nafasi tutakuwa tunapoteza mda right?

na shapu, Uganda, - 30.03.08 @ 15:08 | #4184

SISIEMU wamekalia moto. Kwani Mkapa hasipohudhuria hivyo vikao kutakuwa na upungufu gani???????? Hawezi kuhudhuria wakati akijijua yeye ni FISADI na anajua kuwa UFISADI ni moja ya ajenda ambazo zingejadiliwa. Nafikiri sasa ni wakati Muafaka wa kumshughulikia kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni za Katiba yetu. Haoni umuhimu wa chama ambacho kilimpa nafasi ya kudokoa alichoweza. Yeye na Sumaye wanatakiwa kutueleza what happened huko EPA pamoja na kizunguzungu cha KIWIRA.

na Indume Yene, Dsm, Tz, - 30.03.08 @ 15:21 | #4185

KUTOKUHUDHURIA KWA VIONGOZI WASTAAFU WA CCM KWENYE CC , NEC,NI KIELELEZO TOSHA KWAMBA ***** YEYOTE HAWEZI KUJISALIMISHA MPAKA ABANWE KISAWASAWA.KUNA WEZI WA MALI NA WEZI WA FADHILA HAPO.
MKAPA ALISEMA WAZI KUWA ATATUMIA NGUVU ZA KIJESHI KUHAKIKISHA CHAMA CHAKE KINASHINDA ZNZ .
2.SALMINI ALITOA KAULI KAMA HAKUNA MSETO WA MAWE NA KOKOTO , BORA WATU WALE DONGO ,MPEMBA KUINGIA IKULU NI SAWA NA MBWA KUINGIA MSIKITINI.
MZEE MSOMI WA DINI YA KIISLAMU NA ALIEPATA KUHESHIMIKA KWA MKUBWA NA MDOGO ,ALITOA KAULI MBAYA SANA ETI HATA KAMA WATU WATAOGELEA KWA DAMU, LAKINI NCHI HATUTOI .
4.SALIM A.SALIM, KATIKA MAISHA YAKE YOTE HAJAPATAPO KUITETEA ZNZ PAMOJA NA NYADHIFA ZOTE ALIZO KUWA NAZO.
MH. SHEIN,ANASABABU ZA MSINGI NA TUNAMTAKIA MAMA YETU MALEZI MEMA NA KAULI THABIT INSHAALLAH.WAFIWA M/MUNGU AWEPE MOYO WA SUBRA.YEYE NI WA M/MUNGU NA SOTE TUTAREJEA KWAKE.
KWA MAELEZO HAYA SIFIKIRII KAMA WATU HAWA WANAWEZA KUHUDHURIA KWENYE KIKAO CHOCHOTE CHENYE MASLAHI KWA ZANZIBAR NA WAZANZIBAR, TANGU WALIPOKUWA VIONGOZI WA JUU WALIONYESHA UADUI WA DHAHIR SHAHIR KWETU ,HAWA SIO WATU WEMA NI MAADUI ,MAFISADI ,DHAIFU WANAFSI ZAO NA NI MAADUI WA JAMII YA WATANZANIA,TUWAPUUZE TUWABEZE NA IKIWEZEKANA WADHARAULIWE.
KAMA HII SIO MIPANGO YA CCM BASI NINAIMANI HAWA HAWAZIMI ,HAWAWASHI, LAKINI NINA WASIWASI KUWA INAWEZEKANA PIA IKAWA NI MBINU ZA CCM KUPOTEZA WAKATI NA KUPIMA PRESSURE YA UPINZANI .
HAIWEZEKANI WATU WAZIMA WENYE AKILI TIMAMU KILA SIKU KUGEUZWA MATAAHIRA.
ONYO
SIKU WAZANZIBARY NA WATANGANYIKA TUTAKAPOJUWA KAMA MNATUONA SISI ****** , MABWEGE, NA MAMBUMBUMBU , MOTO WA KIZALENDO UTAKAPO FUMUKA NA SHIDA ZA MAISHA ZITAKAPO SHINDIKANA KUVUMILIKA BASI NDIO MTAKUJA JUTA ,MTAJUTA HATA KUJA DUNIANI .
MNASHEREHEKEA MAASI MNAPALILIA MAASI MNAWAPA WATU WENU UWEZO WA KUAMUA LIKIJA LIKIAMULIWA SIO JESHI WALA POLISI WATAKAO PAMBANA NA NGUVU ZA RAIA .
TAFADHALINI MSITUONE WAJINGA KIASI HICHO ,

na ik, uk, - 30.03.08 @ 15:34 | #4187

ndug zetu raha ya ccm ina katiba na wote smbao hawakuwaili sio mitume wala miungu, hapo ukweli wajumbe wanaotimiza idadi ya kuendeshakikao imefika, mwacheni jk acheze mchezo wake. msiwapelekee wa tz hoja ambazo hazipo na kwa mtindo huu hatutafika na sioni zaidi ya kusema tusitengeneze habari bali tuandike habari za uhakika na ukweli. aidha tunaamini waliopo wataangalia maslahi ya taifa kwani kwa ccm hakuna aliye maarufu bali chama ndiyo maarufu na ushahidi upo muangalieni leo lowasa yuko wapi, jee nani maarufu ni yeye au chama, ukweli yeye ameondoka na ccm iko pale pale na hivyo ndivyo ilivyo.

na ikram, tz, - 30.03.08 @ 16:22 | #4193
 
Ndio Maana

Ccm Haijatoa Maamuzi Yoyote Mazito Kama Wengi Walivyokuwa Wanafikiria

Inshalaha

Tanzania Yenye Amani Pendo Na Umoja Tutafika
 
Mkutano Butiama: Agenda ya ufisadi yaigawa CCM
* Wenyeviti wa mikoa wataka ijadiliwe NEC, wengine wapinga
* Kikwete akiri kikao chao kitatoa maamuzi mazito

Na Theodatus Muchunguzi, Musoma
Mwananchi

WENYEVITI wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walikutana juzi usiku mjini hapa kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jana mchana katika kijiji cha Mwitongo, Butiana mkoani Mara likiwamo la kuwachukulia hatua wanachama wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa ya ufisadi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa katika kikao hicho, zinaeleza kuwa wenyeviti hao walitofautiana kuhusiana na suala la chama kuwachukulia hatua za nidhamu baadhi ya viongozi ambao wanahusishwa katika kashfa za ufisadi.

Kundi moja lilitaka viongozi hao wasichukuliwe hatua na badala yake wapewe kalipio wakati kundi lingine linataka waadhibiwe.

Baadhi ya wenyeviti walitaka kikao hicho kiweke msimamo wa kuishinikiza NEC kuwatimua wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusishwa na kashfa hizo, ikiwemo ya kushindwa kuwajibika kutokana na serikali kuipatia kwa upendeleo kampuni ya kitapeli ya Richmond kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura.

Hata hivyo, alipoulizwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Charles Makongoro Nyerere, ambaye alikuwa mwenyekiti wa muda wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mativila, kuhusiana na ajenda hiyo, alisema hapakuwepo na ajenda hiyo isipokuwa kuna baadhi ya wajumbe walitaka suala hilo la mafisadi lijadiliwe na kuweka msimamo mmoja.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa muda aliikataa ajenda hiyo na kuwaeleza wenyeviti wenzake kuwa ajenda ya kikao ilikuwa moja, ya kuwachagua viongozi wa umoja wao na kuwahi kumaliza kikao hicho ili kwenda kushiriki katika harambee ya kukichangia fedha CCM Mkoa wa Mara juzi usiku, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete mjini Musoma.

Licha ya kusema kuwa aliizima ajenda ya kushinikiza mafisadi kuchukuliwa hatua, Makongoro alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakieneza habari kuwa yeye alikuwa anaendesha vikao kwa ajili ya kushinikiza watuhumiwa wa ufisadi wang'olewe katika chama hicho, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alijiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Alisema wanaofanya hivyo wana lengo la kumchonganisha na viongozi hao na kuongeza kuwa yeye anamheshimu sana Lowassa.

Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa Mara amesema kuwa msimamo wake ni kuwa kama kuna viongozi waliohusika na ufisadi hawezi kuwatetea wasichukuliwe hatua.

Kikao hicho pia kilichagua Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Mchopa alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wenyeviti hao, akijaza nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi ambaye alistaafu mwaka jana.

Kikao hicho pia kilimchagua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas ol Mkisi kuwa katibu wao.

Katika hatua nyingine kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) ambacho kilianza juzi jioni katika kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara, kiliendelea kwa siku ya pili jana asubuhi katika ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Mara na kusababisha kuchelewa kuanza kwa kikao cha siku mbili cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Kwa mujibu wa ratiba, CC ilitarajiwa kukutana juzi wakati NEC ilitakiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia jana hadi leo kijijini Butiama.

Kikao cha CC kilianza juzi jioni na kuahirishwa kwa ajili ya wajumbe wake kuhudhuria hafla ya uchangiaji fedha kwa ajili ya chama hicho Mkoa wa Mara, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Kikao hicho kiliendelea jana asubuhi na kusababisha kikao cha NEC kilichotarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi kuahirishwa hadi saa nane mchana, na wakati kinaendelea watu wa vyombo vya usalama waliondolewa karibu na ukumbi, hali iliyotafsiriwa kuwa ni kudhibiti habari zisivuje.

Akifungua kikao cha NEC, Mwenyekiti wa CCM, Kikwete alifafanua zaidi sababu za mkutano huo kufanyika Butiama, lakini akakiri kuwa kitafanya maamuzi mazito ambayo hayatahusu mageuzi ya kisera wala kiitikadi.

Kwenye kikao hiki, yatakuwepo maamuzi muhimu yatakayofanyika. Lakini napenda kusema kuwa maamuzi hayo hayatahusu mageuzi ya kisera au kiitikadi. Nalisema hili kwa sababu wapo watu wanaotumaini au wenye hofu kuwa hapa Butiama kutatokea tamko la kurudia tena kutaifisha mali na kuziweka njia kuu za uchumi mikononi mwa dola. Wapo pia wanaodhani tutatoa tamko la kulirudisha nyuma gurudumu la mageuzi ya kisiasa yaliyoleta demokrasia ya vyama vingi na uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni yao.

Rais Kikwete alifafanua kuwa kikao hicho kitatafakari hali ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama katika chama na Taifa na kuwa katika kuzungumzia mambo hayo, yapo masuala makubwa yatakayojitokeza na kufanyiwa maamuzi.

Katika kikao hicho mambo lingine linalotarajiwa kutingisha ni suala la mwafaka wa Zanzibar kati ya CCM na Chama cha Wananchi CUF.

Waandishi wa habari walipomtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba muda mfupi kabla ya kuendelea kwa kikao cha CC jana asubuhi kuhusu mambo yaliyojadiliwa na kikao hicho juzi jioni, Makamba alisema hana cha kueleza kwa sababu CC ina kazi moja tu ya kuandaa ajenda za kujadiliwa na NEC.

Sina cha kuwaeleza kwa kuwa chama chetu kina utaratibu. Jukumu la Kamati kuu ni kuandaa ajenda za kupeleka kwenye NEC. Hata baada ya kikao hiki kumalizika,

hatutakuwa na cha kuaeleza, taarifa zote zitatolewa baada ya NEC, alisema Makamba huku akivilalamikia vyombo vya habari kuwa vimepewa ajenda za NEC lakini vinaripoti masuala ya Karamagi, Msabaha.

Badala yake Makamba alisema kikao hicho kiliwateua makatibu 10 wa wilaya, ambayo hata hivyo majina yao yatapelekwa NEC kwa ajili ya kupitishwa.

Habari za ndani zinasema wakati wa kikao hicho, agenda hizo zilijadiliwa na kuangalia jinsi ya kupenyeza agenda za ufisadi wa akaunti ya nje ya Benki Kuu (EPA) na kashfa ya Richmond.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho ndicho kingebadili mwelekeo wa agenda na kupenyeza agenda hiyo.

Habari zaidi kutoka ndani ya chama zinasema hata mpango wa kumuita gavana wa benki kuu kutoa semina kwa wajumbe jana, kuhusu hali ya kiuchumi ilikuwa inalenga pia kutoa ushauri nini kifanyike katika suala zima la EPA ambalo limekitia chama cha mapinduzi doa kubwa.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein jana alilazimika kuondoka kuelekea kwao Pemba kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.

Dk Shein alitoka nje ya kikao na kusindikizwa na wajumbe wa CC baada ya kupata taarifa hizo, muda mfupi baada ya kuanza kwa kikao hicho mjini Musoma.
 
Kikao hicho kiliendelea jana asubuhi na kusababisha kikao cha NEC kilichotarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi kuahirishwa hadi saa nane mchana, na wakati kinaendelea watu wa vyombo vya usalama waliondolewa karibu na ukumbi, hali iliyotafsiriwa kuwa ni kudhibiti habari zisivuje.

Ni siri gani iliyoongelewa ndani ya kikao hata wale wanaolinda usalama wao hawakustahili kuisikia 😕
Duh! CCM usanii mwingi, wana usalama mna waamini kulinda maisha yenu usiku na mchana lakini hamuwaamini kusikia "siri" za chama mlizokuwa mnazijadili kweli chama kimeshika utamu!
 
Unachofurahii hapa ni CCM kutotoa maamuzi mazito kwa ajili ya kulinda maslahi ya Taifa au??

Na ni Tanzania gani yenye Umoja kwa mwenendo kama huu wa kushikilia wafisadi huku mkiwaacha maskini wakiteseka?
Huo umoja upo kati ya Viongozi wa juu wa serikali na wachache wana CCm, na uku mkiwatenga maskini sio?

Huyu ndiye anajiita mwandishi na mchambuzi wa siasa na ICT .Ndiyo watanazania hawa na sasa wamesha lamba pipi wanajaribu kuja na mambo yao hapa kutufanya sote wajinga.Ignore the boy anatafuta kula huyu hana majukumu ana waya waya.Dogo anataka mkutega ili wamjue yupo apewe kula maana hajiamii ila anaamini kuishi kwa mgongo wa CCM.Anajilengesha Rostam amunone na CCM wampe nafasi ya kuandikia Uhuru .Miaka chini ya 30 unakuwa na mawazo mgando namna hii lazima mtu ujiulize .Tujikite kwenye issue yenyewe kwamba matumaini ya Watanzania Butiama yame enda na maji ya mtoni kama mnyama achinjwae mtoni hutaweza kujua maana hata damu itaenda na maji ya mtoni .
 
Iende Mbele Injili Hiyoo Iende Mbele Iende Mbele Injili Ya Ccm Iende Mbele

Ni Mwanachama Gani Waccm Aliyewahi Kusema Na Kunakiliwa Na Vyombo Vya Habari Kwamba Ccmhaina Umoja Kuna Migogoro Kama Yuko Naomba Utaje Jina Lake Na Sehemu Alipo

Yeye Amesema Hivyo Kama Nani Msemaji Wa Ccm Au Msemaji Wa Ccm Wa Sehemu Alipo?

Babah Maneno Yako Mengine Yanaharibu Sura Ya Ccm Mbeleya Jamii Kwa Kiasikikubwa Kamaunachuki Na Ccm Basi Onyesha Chuki Hizo Mwaka 2010kamautafikamwakahuo Sio Uaambukiza Watu Magonjwaya Kudanganya Angaliausiwe Dalai Lama
 
...kutohudhuria kwa fisadi Mkapa kunaweza kuelezeka kirahisi kwamba fisadi alikuwa na wasiwasi kwamba kuna kibano kizito dhidi yake hivyo akaamua kuingia mitini. Je kukosekana kwa Mwinyi na SAS kuna maelezo gani? Au ndio mmomonyoko wa CCM unaanza kidogo kidogo kufuatia chama hicho kukumbatia mafisadi?
Kikwete usanii umekuzidi, huwezi kufanya maamuzi yoyote mpaka uunde tume sasa CCM iko njia panda.

Itabidi uamue kubadilika ili kuimarisha CCM na kuleta mshikamano ndani ya chama, au kuendelea kuwakumbatia mafisadi na chama kuwa na mafarakano na hivyo kugawanyika.

JK alemewa Butiama

na Mwandishi Wetu, Musoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MZIGO mzito wa kimaamuzi unaonekana dhahiri kumlemea Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ambaye amelazimika kuviongoza vikao viwili vizito vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, vinavyofanyika Butiama bila ya kuwapo kwa nguzo zake kuu kisiasa.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili unaonyesha kwamba, kukosekana kwa wajumbe kadhaa muhimu wa kudumu wa vikao vya CC na NEC ya CCM, kunaweza kwa kiwango kikubwa kutia doa kama si kuathiri baadhi ya maamuzi mazito ambayo yamekuwa yakitarajiwa kufikiwa.

Miongoni mwa watu hao muhimu ambao kukosekana kwao kumeshaanza kuibua hali ya wasiwasi na kuonekana kupwaya kwa uzito wa vikao hivyo vya Butiama vinavyofanyika kwa mara ya kwanza eneo alikozaliwa na kuzikwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ni marais na wenyeviti wastaafu wawili wa chama hicho, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wadadisi wa mambo kadhaa wa ndani ya chama hicho waliozungumza na Tanzania Daima kutoka Butiama, wanakielezea kitendo cha kukosekana kwa Mkapa na Mwinyi kuwa jambo ambalo litasababisha kulemewa kwa Kikwete na pengine kukosekana kwa nguvu ya kufikiwa kwa maamuzi mazito yanayogusa mustakabali wa wakati huu wa chama hicho.

Aidha, wakati kukosekana kwa viongozi hao wawili ambao ni wajumbe wa maisha wa CC na NEC ya chama hicho kunachagizwa na kupewa uzito mkubwa, na kutokuwapo kwa Rais mstaafu wa Zanzibar, ‘Komandoo’ Dk. Salmin Amour Juma.

Kama hiyo haitoshi, vikao hivyo vinafanyika Butiama wakati pia akikosekana mwanadiplomasia adhimu nchini, Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye naye ni mjumbe wa CC na NEC kwa pendekezo la Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho.

Mbali ya Dk. Salmin, kikao cha NEC kilichoanza jana jioni majira ya saa 11 kutokana na kuchelewa kwa kikao cha CC, pia kinafanyika pasipo kuwapo kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Kutokuwapo kwa Dk. Salmin na Dk. Salim katika vikao hivyo viwili, kunalifanya suala la kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar, na hususan kufikiwa kwa muafaka wa kisiasa visiwani humo kati ya vyama vya CCM na CUF kuwa ni wenye mashaka makubwa.

Baadhi ya wajumbe wa NEC waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa majina yao magazetini, wanakielezea kitendo cha kukosekana kwa viongozi hao wawili wanaotoka Zanzibar kuwa jambo ambalo linaweza kuyafanya maamuzi kuhusu muafaka kuwa magumu.

Jambo gumu kwa chama hicho na hususan kwa Rais Kikwete kuhusu kukosekana kwa viongozi hao wa juu muhimu wanne, ni wasiwasi ambao umeshaanza kuzingira vikao hivyo, unaoonyesha kwamba huenda wazee hao wamekosekana si kwa sababu ya kuwa safari kama inavyodaiwa na uongozi wa juu wa CCM, bali kutoridhishwa kwao na mwenendo wa mambo serikalini na ndani ya chama.

Wana CCM waliozungumza na Tanzania Daima kuhusu hili, wanaielezea hatua ya watu hao kukosekana kuwa ni dalili ya mwanzo ya CCM ya Kikwete kuanza kukosa ushawishi ndani ya mioyo ya viongozi wakuu wastaafu, ambao sasa wanakiona chama kikipoteza misingi yake ya kihistoria ya kushika hatamu.

“Kumekuwa na wasiwasi kwamba, Kikwete amekuwa akifikia maamuzi mazito pasipo kwanza kukitaarifu chama na badala yake amekuwa akifanya hivyo kwa kutumia Bunge na ushauri wa kundi dogo la watu. Hali hii inaonekana kutowafurahisha wazee,” alisema mfuatiliaji mmoja wa karibu wa siasa za ndani ya CCM.

Lakini pengine pigo kubwa kwa Rais Kikwete lilizidi kuonekana dhahiri jana baada ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mzanzibari, kulazimika kuondoka katika vikao hivyo kutokana na kufariki dunia kwa mama yake mzazi.

Kuondoka kwa Dk. Shein, kiongozi wa pili kwa mamlaka katika serikali na mtu aliyetokea kuwa mshauri wa karibu kikatiba na kikazi wa Rais Kikwete, kunayafanya maamuzi kuhusu siasa za Zanzibar kuzidi kuwa magumu.

Kutokana na hali hiyo basi, Rais Kikwete atalazimika kutumia ushauri wa Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wake, Amani Abeid Karume, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi mstaafu Gharib Bilal na Wazanzibari wengine wasio na ushawishi mkubwa katika kueleza kwa kina athari za kisiasa, kijamii na kiuchumi za kuhitimishwa kwa muafaka ambao unatarajia kutoa baraka za kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba, watu hao muhimu, Mwinyi, Mkapa, Dk. Salmin, Dk. Salim na Dk. Shein wanakosekana katika vikao wakati moja ya ajenda inayosubiriwa kwa hamu na Wazanzibari ni hiyo ya kufikiwa kwa suluhu ya kudumu ya kisiasa huko visiwani.

Mbali ya hilo la mwafaka, kukosekana kwa Mkapa kwa mfano kunaufanya mjadala kuhusu masuala kama lile la Kashfa ya EPA na mengine yanayomgusa yeye binafsi kushindwa kujadiliwa kwa kina.

Hali hiyo inakuja baada ya watu kuwa na imani kwamba, vikao hivyo vya Butiama vinavyofanyika hatua chache kutoka alipozikwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, vilikuwa vikitarajia kupata majibu ambayo yangekisadia chama hicho kupata majibu kamili kuhusu nini kilitokea katika EPA zama za Mkapa akiwa Rais na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.

Kama ilivyo kwa Mkapa, kukosekana kwa Mwinyi, kiongozi ambaye kimsingi ndiye anayeweza kubeba mzigo wa kuwa mrithi wa kiuongozi wa taifa baada ya kuondoka kwa Mwalimu Nyerere, kunaufanya mjadala wa masuala kama lile la Richmond lililosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri kupwaya na kukosa mashiko.

Wafuatiliaji wa mambo wanakuona kukosekana kwa Mwinyi kuwa ni pengo ambalo litamwia vigumu Kikwete kuliziba wakati huu chama hicho kikiwa katika mazingira magumu kuvunja kuimarika na kuibuka kwa makundi mengi zaidi ndani ya chama hicho, yaliyoibuka baada ya masuala ya EPA na Richmond kuibuka.

“Kwa namna yoyote ile sisi kama chama tulihitaji sana hekima za wazee wetu kama Mwinyi na Mkapa katika kuhitimisha haya masuala ya EPA na Richmond, ambayo hayajapata kujadiliwa kwa kina,” alisema mwana CCM mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima Jumapili jana.

Baadhi ya minong’ono inayosikika kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo inaeleza kwamba, Mkapa hakuhudhuria vikao hivyo kwa sababu ya kuchukizwa kwake na hatua ya kuhusishwa moja kwa moja na ukiukaji wa maadili wakati akiwa madarakani.

Inaelezwa kuwa, ingawa Mkapa alimuunga mkono Kikwete katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, kutajwa kwa jina lake sana katika masuala mbalimbali, ni jambo analoliona likiwa na baraka kamili za viongozi wa juu serikalini wenye malengo yao binafsi.

Baadhi ya wadadisi wanahofu kwamba, upo uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wameanza kuiona serikali ya sasa kuwa iliyopoteza uwezo na umadhubuti wa kuhimili mikiki mikiki na hivyo wakaamua kukaa kando.

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 27 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Wakati umefika kwa CCM na Tz kwa ujumla kubadilika. Mabadiliko hayaji kiulaini na ni lazima kukubali kwamab hatuwezi tena kurudi au kutizama nyuma. Gurudumu la maendeleo na la mabadiliko limeanza na hakuna wasi wasi wo wote litawagusa na kuwakera vizito waliopita wakiwemo viongozi wastaafu wa ngazi za juu. La muhimu ni kumhakikishia Kikwete kwamba tuko pamoja nae katika juhudi zake za kuleta mabadiliko na kuutokomeza ufisadi Tz ambayo unaathiri sana maisha ya raia wa kawaida. Hao waliokataa kuhudhuria wote matumbo yao yamejaa na hawana hasara yo yote kwa maamuzi yatakayotolewa kwani wameshajilimbikizia mali za kutosha.

na kiwete, Dar, - 30.03.08 @ 09:04 | #4113

kikwete aliwahi kusema ya kua watanzania wengi hawapendi dawa chungu bali wanapenda tamu,sasa alitwambia wkt mwingine lazima mgonjwa anywe dawa chungu ili apone,sasa km kweli alikua anamaanisha basi awape wagonjwa wa ccm wakina lowasa,rostam,msabaha,karamagi dawa chungu ili wapone,asiwe anasema tu kwa wananchi,wkt ndio huu kwa kufanya ivyo.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 30.03.08 @ 09:40 | #4118

mh. kikwete chapa kazi kwa mujibu wa ilani ya chama chako hiyo ndo dira yako na mkataba kwa watanzania na wewe. hongera kwa kupambana na mafisadi.

na Shija., dar es salaam, - 30.03.08 @ 10:00 | #4122

Wakati huu ni wakati mgumu kwa Watanzania wote, siyo Kikwete peke yake kama kiongozi. Sisi kama Watanzania wenye dhamira safi hatuna budi kumuunga mkono Kikwete kwenye maamuzi haya mazito yanahusu safari ndefu ya maendeleo ya taifa hili maskini,lakini lenye mali asilia lukuki.
CCM ni lazima ikubali ukweli kwamba inabeba mzigo huu wa ufisadi katika hujuma za uchumi wa nchi hii na imechangia kwa kiasi kikubwa sana,kuanzia kulindana hadi takrima na uchafu mwingine, kama Viongozi wastaafu walivurunda wanapaswa kuwajibishwa. Tanzania siyo mali ya Kiongozi ni ya Watanzania wote, hivyo kama alifanya hujuma anawajibu wa kujibu tuhuma hizo na siyo kuingia gizani na kususia vikao. Kwanza CCM ingeondoa sheria iliyoko kwenye katiba inayowalinda wastaafu hawa wasishitakiwe kwa makosa waliyofanya wakiwa madarakani, hapa ndipo chanzo cha fitna ya ufisadi na uhujumu wa uchumi wa watanzania.

na Mahmoud, Tanzania, - 30.03.08 @ 10:04 | #4123

Kikwete! Pole sana kwa kukosa busara Rais wangu lakini pia pole sana kwa

na Ngosha Ombasa, Nyamatembe,Nassa-Magu, - 30.03.08 @ 10:14 | #4126

Jamani mbona Mkapa alisema bayana kuwa yeye hatajihusisha na maswala ya kisiasa. Kwa hilo nampenda Mkapa maama alikuwa muwazi kabisa. Iweje leo tumtegemee kutusaidia kutoa maamuzi mazuri ya mwelekeo kuwakomboa wwananchi wa kawaida ambao wapo ktk lindi la umasikini hali yeye pia amechangia kutufikisha tulipo. Ina maana hivyo vichwa vingine havina akili kufikia maamuzi mazuri kwa faida ya nchi? Rais mtukufu, sisi tupo nyuma yako, wakane hao maswahiba wako ktk vikao hivi nchi isonge mbele. Kumbuka kuwa huwezi kuwatumikia mabwana wawili.

na Aisha, Musoma, - 30.03.08 @ 10:32 | #4128

Kumbe wengine hamjaisoma vizuri hii stori. Ni kwamba hao wastaafu, hasa Mzee na Mwinyi, Salim, Komandoo, nan Msuya wamemkimbia baada ya kugundua hatashughulikia mafisadi kama walivyomshauri, wakaona ni vema wajitenge naye. Ukisoma stori hii sambamba na Makala ya MASWALI MAGUMU ya Ngurumo utagundua kuna jambo hapa. Ila inaonekana kuna ambayo wameogopa kuandika kwani kwenye blogu ya Ngurumo kuna breaking news ambayo ndiyo ilipaswa kuwa hasa habari yenyewe...sijui tofauti hizi za uandishi zimetokanana na nini. Ngja tuendelee kutafakari.

na Masamaki, Dar, Tanzania, - 30.03.08 @ 10:36 | #4129

ccm siyo chama Mkapa,Mwinyi auSumaye,kwani wakifa wao maamuzi haya fanyika?KIkwete kaza buti.achana nao wezi hao kwanza ukikaa nao wawatakuambukiza tabia zao chafu

na akim makukungumahafu, iringa tanzania, - 30.03.08 @ 10:52 | #4131

Hallo,hallo Kikwete,CCM na Watanzania wenzangu wapenda haki na wachuk

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:13 | #4135

Hallo,hallo Kikwete,CCM na Watanzania wenzangu wapenda haki na wachuk

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:19 | #4136

Hallo,hallo Kikwete,CCM na Watanzania wenzangu wapenda haki na wachuk

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:19 | #4137

Hallo,hallo Kikwete,CCM na Watanzania wenzangu wapenda haki na wachuk

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:20 | #4138

CCM-Chama Cha Mafisadi,hatimaye kisambaratikana mikononi mwa Kikwete.EPA na Richmond vitawahukumu.

na Masalakulangwa ng'hulu, Mwanza.Tz, - 30.03.08 @ 11:32 | #4139

hiyo ni laana unadhani mtawadhulumu watanzania mpaka lini? kila kitu kina mwanzo na mwisho, huu ni mwisho wa mafisadi kamwe Kikwete usiogope tupo nyuma yako kaza buti baba!!!

na ndorobo, belgium, - 30.03.08 @ 11:56 | #4157

Ndiyo dawa chungu lazima inyweshwe hata kama ni kwakufunga pua na kubana midomo kama wafanyiwavyo wattoto. Viongozi wa zamani kama wameamua kutohudhulia kikao hicho ni hiari yao, na hilo lisimzuie Kikwete kuendesha kikao. Kua Rais wetu, yatima ndio maisha yao ya kila siku wajikutapo hawana wazazi, hupaswa kufikia maamuzi mazito kwa maslahi ya watooto na wadogo zao. Kaza buti askari vitani. Ila tukumbuka iatabidi kuwavua pia hao waliokaribu yako na maswahiba ambao mwenendo wao ni wa mashak. Ndiyo mmekutana Butiama, kumbuka Mwalimu ilipobidi alimtosa bestman wa Harusi yake, Bw. O Kambona, nakuweka maslahi na mtizamo na maamuzi ya chama mbele.
No one is indispensable. Tanzania Kwanza.

na Mtukwao, TZ, - 30.03.08 @ 13:23 | #4166

WEWE SHIJA HAPO JUU MPUMBAVU SANA, KIKWETE TANGU LINI ANAPAMBANA NA MAFISADI??? AMEKUPA NINI ?? USITAKE KUTUKANWA JUMAPILI HII!!

na imani - 30.03.08 @ 13:40 | #4167

KIKWETE ANACHEZEA MOTO, MAFISADI HUWA HAWALINDWI, MWAMBIENI KIKWETE HAO JAMAA WALIOKOSEKANA SI WAJINGA, HAIWEZEKANI KWA MAMLAKA YA KIKWETE ALISEMEE SWALA LA EPA BUTIMA!!!! KITU KIKO WAZI, INA MAANA ANATAKA AMWITE MKAPA AKAMSUTE MBELE YA WANACHAMA LUKUKI HUKO BUTIMA???? THIS IS IMPOSSIBLE.

JE KIKWETE NCHI HII ANAWAULIZA HAO WAZEE??

SIJUI ANAJIAMINI VIPI MTU HUYU, NADHANI ATAPATA WANAWAKE WENGI WA KUMPIGIA KURA UCHAGUZI UJAO, NA WALE WANAUME WALIOKAMA WANAWAKE(i mean ambao hawajaui maisha na kutafuta ni nini)

HIVI ANATAKA SALIM AHED SALIM AMSHAURI NINI, NYUNDO,MSUMARI KILA KITU ANACHO??

HIVI MWINYI ATAVUMILIA KUONA MKAPA ANASUTWA IS THIS MAKES SENSE???

ANACHEZA NA MOTO HUYU BROTHER, UKIWALINDA MAFISADI, HUWA WANAKURUDI, NA HII NI KUWA YEYE MWENYEWE NI FISADI SO ANAANGALIA FUTURE YAKE, KUWA NA YEYE AJE KULINDWA

NYERERE NA MWINYI NDIO WALIKUWA MARAIS NCHI HII!!!!!!!!!!!!!!!!

na imani, USA, - 30.03.08 @ 13:47 | #4168

Hao waliokosekana hawana tija ktk nchi hii zaidi ya kuwa ni wezi wanaolindwa na sheria haswa mkapa na mkewe anna.

na Dawa chungu, Dar, - 30.03.08 @ 13:49 | #4169

Kutowasili mkutanoni kwa MKAPA, SALIM, SALMIN, SUMAYE ni baraka kwa Taifa kwani matatizo yote ya ufisadi yametokea wakati wao. Ningeshangaa kama MKAPA NA SUMAYE wangekwenda Butiama. Kutajwa kwa mara kwa mara kwa MKAPA NA SUMAYE ktk ufisadi ni jambo lisiloweza kuepukika hasa ukizingatia kuwa yote hayo yametokea wakati wao wakiwa madarakani na hawakuweza kuchukua hatua yeyote.

CCM haiwezi kushika hatamu kwa kuwatetea wezi, eti kwa vile ni VINGUNGE. Ni lazima tukumbuke kuwa SUMAYE amehusishwa na ufisadi hata bado akiwa madarakani. La ajabu ni kwamba hakuruhusu uchunguzi ufanywe ktk maeneo yale ambayo ameshutumiwa. Machoni mwa watanzania Sumaye atabaki kuwa ni FISADI. Na ndio maana hakuchaguliwa CC. MKAPA hajatokea ktk vyombo vya habari na kujibu tuhuma- naye ni muovu na ndio maana hakwenda Butiama kwani hana la kujitetea na anajua wazi kuwa JK hatamtetea.

Ili CCM ibadilike ni lazima ichukue DIRA mpya- DIRA YA UTEKELEZAJI NA KUWANYOSHEA KIDOLE MAFISADI HATA KAMA WAO NI MAKADA. Umaarufu wa JK usitegemee ushikaji bali itegemee utendaji. Hilo haliwezekani ikiwa akina GETRUD MONGELA watatetewa ktk CCM japo wamekula pesa ya AU, au MKAPA asiguswe kwavile ni mjumbe wa kudumu CC.

CCM imara itajengwa kwa kuondokana na TAMADUNI ZA MAADILI YA CHAMA ZILIZOPITWA NA WAKATI. Ni vyema kutokuwa maarufu kwa CCM lakini uwe maarufu kwa wananchi. TUMUUNGE MKONO RAIS WETU ILI TUWAFUNJE MOYO MAFISADI. JK CHAPA KAZI!!!!!!!!!!

na Zawadi Ngoda, Dar es salaam/ Tanzania, - 30.03.08 @ 13:57 | #4171

Ndugu Waadnishi wa Habari naomba muwe makini katika kuandika Kiswahili fasaha na kutochafua lugha ya Kiswahili, kichwa cha habari mumeandika ( JK alemewa Butiama ) na iliyosahihi ni ( JK aelemewa Butiama ) neno: elemea na elemewa inamaana tafauti na wasojua kiswahili Fasaha wanachanganyikiwa katika ufahamu wa neno na kulibeba kimakosa katika maengezi na maandishi :

elemea - ku-elemea , elemea : ameelemea. ( ni kitendo cha mtu kumuelemea mwengine ).

lakini aelemewa : elemewa - ku -elemewa , elemewa .( ni kitendo cha mtu kuelemewa na mwengine ).

kuna maneno mengi nakuta yanaandikwa vibaya na kuharibu lugha ya kiswahili Fasaha : mfano neno : Serekali huandikwa ; Serekari . Askari huandikwa Askali n.k

Lugha ya Kiswahili Fasaha ni moja kwa hiyo kusikuweko na uandishi wa aina mbili na kuharibiwa Kiswahili.

Kusiwe na kasumba ya Uzanzibari na Ubara kuwa Wazanzibari watamke li na ndio ngeli sahihi na Bara wakawa wanatamka na kuandika ri , Kiswahili Sanifu Kilichotamkwa na Wazee tokea Enzi na kuandikwa kwa ufasaha kwa hivyo kusije Kiswahili Chengine Kichafu Kisiojulikana mizizi yake.

dumtum alaa kheir

na Mzanzibari, Zanzibar, - 30.03.08 @ 14:07 | #4173

MZee Mwinyi yuko nje akipata matibabu. Anaheshimika kwa kuwa hakufisidi nchi ila alitoa ruksa kwa kila mtu ajiendeleze. Aliefuatia akaifuta ruksa kwa kila mtu akawapa wachache kuchimba mafuta, gesi, dhahabu, almasi, makaa ya mawe na kuikamua TANESCO kwa TANPOWER, Songas,Net Solutions, Richmond na zingine lukuki. Hao waliombeza kwa kutoa ruksa sasa tumejua siri yao walijipa ruksa kuuza kila kitu bei poa kwa mradi wa PSRC.

na BITs - 30.03.08 @ 14:26 | #4176

Aina gani ya uandishi hii? Mbona mwandishi unalalama ooh mbona Mwinyi, Mkapa, Sumaye, Salmin hawapo? Je idadi ya wajumbe wa kufanya maamuzi haijakamilika? Mwandishi hatakiwi kupendelea upande wowote kama unavyofanya wewe mpaka unafikia kudhani kuwa maamuzi hayatakuwa na nguvu kwa sababu tu ya kukosekana watu wako hao.Hayo tuachie sisi wasomaji?
Kwenu wajumbe we NEC (CCM), Tanzania ya leo ni ya kuchambua mambo, sio kila anachosema mwenyekiti ni sahihi, kama amekosea mumwambie hapa mkuu spidi imezidi au mwelekeo sio sahihi na sio kuwa wanafiki kupiga makofi kila anachosema.
Nasema hivi kikao kiendelee na fanyeni kazi iliyowapeleka hapo, wenye akili zetu tutachambua kujua ukweli ni upi. Waliokosekana watajulishwa kilichoendelea. Kikwete usiyumbishwe na mtu. Maamuzi ya kupambana na ufisadi ni magumu na ya kujitoa mhanga ila matunda yake watafaidi mengi na ka muda mrefu ujao.
Kwenu watanzania hakuna njia ya mkato katika maisha, ni nidhamu ya kufanya kazi tuu. Kwenu viongozi tunataka uwajibikaji katika nafasi zenu, hatutaki masihara, maneno yenu na matendo yaendane sio yatofautiane. Kwenu watu wa system mnahitaji kubadilika. Inasikitisha nchi inaoza na nyie mliokula viapo mpo kama hampo. Sitaki kusikia visingizio vyenu. Hakikisheni nchi inakuwa na utawala wa haki na sheria sio kwa watawala tu, pia kwa watawaliwa. Haki ni pamoja na kutooneana katika mambo yanayohusu ustawi wa kila mwananchi. Lindeni misingi ya nchi, misingi ya siasa zetu na sio watu. Mtu akikiuka hafai huyo, hata kama Rais anampenda. Narudia tena mtu asijaribu kukiuka, anayekiuka hatufai. Hivyo viapo vina maana sana. Sio kuwa wanafiki kama askari wa Zombe, siku ya siku kila mtu atawajibika kivyake.
Ushauri wangu wa bure kwa Serikali, wekezeni katika elimu ndio mambo yatanza kubadilika na si vinginevyo. Jengeni vyuo na wawezesheni vijana kujiunga na vyuo hivyo sio kuweka vikwazo. Kiongozi mzuri ni yule ambae anaona mbali na matunda ya kazi yake yanaonekana baada ya muda mrefu. Sio vitu vya muda mfupi kama kujenga uwanja wa taifa wa Kisasa au kuleta kocha Mbrazili ili twende Ghana. Hayo ni mambo ya muda mfupi.Kwa hayo machache natumaini kila mmoja ataanza kubadilika katika sehemu yake ya kazi.

na cadet culture son, dsm, tz, - 30.03.08 @ 14:50 | #4181

wewe mdebwedo unayejifanya unatakasha kiswahili mwenyewe unaandika kilugha...hakuna serekali katika kiswahili kuna serikali, hakuna kiswahili chengine kuna kiswahili kingine. situletee lugha zako za mchambawima za maji ya bomba kuwa maji ya mfereji,shule kuwa skuli,mazishi kuwa maziko hizo mmezoea wenyewe huko sababu ya mlivyomdebwedo mdomoni msitake kutuambukiza mdebwedo wenu sisi huku.

na bandarini, unaposhukia ukija tanzania, - 30.03.08 @ 15:04 | #4183

Bwana dumtum alaa kheir,
Tunashukuru kwa kiswahili ulichorekebisha. ila umeongea sana. Nadhani wengi wetu tumemwelewa. hapa tunataka issues zijadiliwe zaidi mambo ya kiswahili nenda hiko wizara za elimu za CCM ambazo wameshindwa kusimamia na kutoa elimu bora. Jadili ufisadi maswala ya lugha naomba hapa tusiyape nafasi tutakuwa tunapoteza mda right?

na shapu, Uganda, - 30.03.08 @ 15:08 | #4184

SISIEMU wamekalia moto. Kwani Mkapa hasipohudhuria hivyo vikao kutakuwa na upungufu gani???????? Hawezi kuhudhuria wakati akijijua yeye ni FISADI na anajua kuwa UFISADI ni moja ya ajenda ambazo zingejadiliwa. Nafikiri sasa ni wakati Muafaka wa kumshughulikia kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni za Katiba yetu. Haoni umuhimu wa chama ambacho kilimpa nafasi ya kudokoa alichoweza. Yeye na Sumaye wanatakiwa kutueleza what happened huko EPA pamoja na kizunguzungu cha KIWIRA.

na Indume Yene, Dsm, Tz, - 30.03.08 @ 15:21 | #4185

KUTOKUHUDHURIA KWA VIONGOZI WASTAAFU WA CCM KWENYE CC , NEC,NI KIELELEZO TOSHA KWAMBA ***** YEYOTE HAWEZI KUJISALIMISHA MPAKA ABANWE KISAWASAWA.KUNA WEZI WA MALI NA WEZI WA FADHILA HAPO.
MKAPA ALISEMA WAZI KUWA ATATUMIA NGUVU ZA KIJESHI KUHAKIKISHA CHAMA CHAKE KINASHINDA ZNZ .
2.SALMINI ALITOA KAULI KAMA HAKUNA MSETO WA MAWE NA KOKOTO , BORA WATU WALE DONGO ,MPEMBA KUINGIA IKULU NI SAWA NA MBWA KUINGIA MSIKITINI.
MZEE MSOMI WA DINI YA KIISLAMU NA ALIEPATA KUHESHIMIKA KWA MKUBWA NA MDOGO ,ALITOA KAULI MBAYA SANA ETI HATA KAMA WATU WATAOGELEA KWA DAMU, LAKINI NCHI HATUTOI .
4.SALIM A.SALIM, KATIKA MAISHA YAKE YOTE HAJAPATAPO KUITETEA ZNZ PAMOJA NA NYADHIFA ZOTE ALIZO KUWA NAZO.
MH. SHEIN,ANASABABU ZA MSINGI NA TUNAMTAKIA MAMA YETU MALEZI MEMA NA KAULI THABIT INSHAALLAH.WAFIWA M/MUNGU AWEPE MOYO WA SUBRA.YEYE NI WA M/MUNGU NA SOTE TUTAREJEA KWAKE.
KWA MAELEZO HAYA SIFIKIRII KAMA WATU HAWA WANAWEZA KUHUDHURIA KWENYE KIKAO CHOCHOTE CHENYE MASLAHI KWA ZANZIBAR NA WAZANZIBAR, TANGU WALIPOKUWA VIONGOZI WA JUU WALIONYESHA UADUI WA DHAHIR SHAHIR KWETU ,HAWA SIO WATU WEMA NI MAADUI ,MAFISADI ,DHAIFU WANAFSI ZAO NA NI MAADUI WA JAMII YA WATANZANIA,TUWAPUUZE TUWABEZE NA IKIWEZEKANA WADHARAULIWE.
KAMA HII SIO MIPANGO YA CCM BASI NINAIMANI HAWA HAWAZIMI ,HAWAWASHI, LAKINI NINA WASIWASI KUWA INAWEZEKANA PIA IKAWA NI MBINU ZA CCM KUPOTEZA WAKATI NA KUPIMA PRESSURE YA UPINZANI .
HAIWEZEKANI WATU WAZIMA WENYE AKILI TIMAMU KILA SIKU KUGEUZWA MATAAHIRA.
ONYO
SIKU WAZANZIBARY NA WATANGANYIKA TUTAKAPOJUWA KAMA MNATUONA SISI ****** , MABWEGE, NA MAMBUMBUMBU , MOTO WA KIZALENDO UTAKAPO FUMUKA NA SHIDA ZA MAISHA ZITAKAPO SHINDIKANA KUVUMILIKA BASI NDIO MTAKUJA JUTA ,MTAJUTA HATA KUJA DUNIANI .
MNASHEREHEKEA MAASI MNAPALILIA MAASI MNAWAPA WATU WENU UWEZO WA KUAMUA LIKIJA LIKIAMULIWA SIO JESHI WALA POLISI WATAKAO PAMBANA NA NGUVU ZA RAIA .
TAFADHALINI MSITUONE WAJINGA KIASI HICHO ,

na ik, uk, - 30.03.08 @ 15:34 | #4187

ndug zetu raha ya ccm ina katiba na wote smbao hawakuwaili sio mitume wala miungu, hapo ukweli wajumbe wanaotimiza idadi ya kuendeshakikao imefika, mwacheni jk acheze mchezo wake. msiwapelekee wa tz hoja ambazo hazipo na kwa mtindo huu hatutafika na sioni zaidi ya kusema tusitengeneze habari bali tuandike habari za uhakika na ukweli. aidha tunaamini waliopo wataangalia maslahi ya taifa kwani kwa ccm hakuna aliye maarufu bali chama ndiyo maarufu na ushahidi upo muangalieni leo lowasa yuko wapi, jee nani maarufu ni yeye au chama, ukweli yeye ameondoka na ccm iko pale pale na hivyo ndivyo ilivyo.

na ikram, tz, - 30.03.08 @ 16:22 | #4193

Damn if you do, Damn if you dont ndio JK alipo...Sasa,Maoni mengi huwa yana consensus yakuwa Ben Mkapa ni "alledge" Fisadi...Sasa, inakuwaje Fisadi Mkapa (alledge) kukwepa Mkutano NEC inakuwa mapungufu kwa JK sasa?..it does make sense..

Kati mazingira ya kawaida and for sake ya fairness,Kukimbia kwa Mkapa kungeweza kutafisiriwa kama ushupavu wa JK kupromote good governance,ndio maana wanakimbia, lakini wapi..Mkapa angeenda Butiama, JK angekuwa anaambiwa anakumbatia mafisadi by virtue ya mahudhurio,au ingekuwa stori kama hii.... ___________fisadi wafanya________ Butiama!!! Fill in the blanks tu..

Yaani hapatii hata afanyeje huyu JK...Zamani mtu akikimbiwa kivita ndio mahiri, sasa Standards zetu ni moving target!!

Kiuandishi, JK is stuck between a rock and a hard place..or Damn if do, Damn if you dont!!! Yaani alichaguliwaje sasa, eti Hapatii kitu
 
Huyu ndiye anajiita mwandishi na mchambuzi wa siasa na ICT .Ndiyo watanazania hawa na sasa wamesha lamba pipi wanajaribu kuja na mambo yao hapa kutufanya sote wajinga.Ignore the boy anatafuta kula huyu hana majukumu ana waya waya.Dogo anataka mkutega ili wamjue yupo apewe kula maana hajiamii ila anaamini kuishi kwa mgongo wa CCM.Anajilengesha Rostam amunone na CCM wampe nafasi ya kuandikia Uhuru .Miaka chini ya 30 unakuwa na mawazo mgando namna hii lazima mtu ujiulize .Tujikite kwenye issue yenyewe kwamba matumaini ya Watanzania Butiama yame enda na maji ya mtoni kama mnyama achinjwae mtoni hutaweza kujua maana hata damu itaenda na maji ya mtoni .

KWAHIYO WEWE UNACHOOTA HAPO NI SIKU MOJA TANZANIA ITAKUWA NCHI YA ASALI NA TENDE WATU WAKAECHINIYA MITI WALE NAWASHIBE BILA KUFANYA KAZI ,NA SIKU HIYO NDIO SISIEM ITAKUWA HAIKO MADARAKANI

BWANA MDOGO WACHA KUDANGANYA UMMAH

NAAMINI MTU KAMA WEWE UKO TAYARI KUJITOA MHANGA ILI MRADI CCM WASIWE PALE WALIPO ILI MARADI CCM IONEKANE IMEBORONGA

DUH WALAHI

KAZIIPO KAMAUPINZANI WENYEWE NDIOHUU
 
Damn if you do, Damn if you dont ndio JK alipo...Sasa,Maoni mengi huwa yana consensus yakuwa Ben Mkapa ni "alledge" Fisadi...Sasa, inakuwaje Fisadi Mkapa (alledge) kukwepa Mkutano NEC inakuwa mapungufu kwa JK sasa?..it does make sense..

Kati mazingira ya kawaida and for sake ya fairness,Kukimbia kwa Mkapa kungeweza kutafisiriwa kama ushupavu wa JK kupromote good governance,ndio maana wanakimbia, lakini wapi..Mkapa angeenda Butiama, JK angekuwa anaambiwa anakumbatia mafisadi by virtue ya mahudhurio,au ingekuwa stori kama hii.... ___________fisadi wafanya________ Butiama!!! Fill in the blanks tu..

Yaani hapatii hata afanyeje huyu JK...Zamani mtu akikimbiwa kivita ndio mahiri, sasa Standards zetu ni moving target!!

Kiuandishi, JK is stuck between a rock and a hard place..or Damn if do, Damn if you dont!!! Yaani alichaguliwaje sasa, eti Hapatii kitu

You must be joking! kukimbia kwa Mkapa ni good governance? 😕
What did Kikwete do to make Mkapa run away from that meeting? 😕

What about those EPA, Radar, Richmonduli Mafisadis who are still at large? is that good governance too? You've to think before writing your thoughts.
 
Kikao bado kinaendelea muda huu lakini wamepumzika kidogo kwa ajili ya chakula cha usiku, hivyo sitashangaa kikao kitaendelea hadi usiku sana, na taarifa yoyote ya kikao hicho itatolewa mapema kesho asubuhi...
 
Mtanzania, mheshimiwa sitaki kuweka kifungu hicho cha Katiba hapa ili watu wao wenyewe waende waisome. Narudia tena, kwa mujibu wa Katiba ya CCM mwanachama wa CCM jukumu lake la kwanza ni kwa CCM na si kwa nchi. Someni Katiba inapatikana hapa: http://www.ccmtz.org

Mwanakijiji,

Mimi nimeisoma na sijaona hicho kipengere na ndio maana nikaomba msaada kwa anayejua hicho kipengere.

Naona toka jana kila mtu anasema katiba inasema hivyo, kwanini hamtaki kukiweka kipengere kamili?
 
Kweli Yameshafanyika Sasa Nyie Mnaamuwa Nini?

Mtagoma Kushirikiana Na Bot Au Tanesco Na Tra ?/

Ole Wenu
 
You must be joking! kukimbia kwa Mkapa ni good governance? 😕
What did Kikwete do to make Mkapa run away from that meeting? 😕

What about those EPA, Radar, Richmonduli Mafisadis who are still at large? is that good governance too? You've to think before writing your thoughts.

Bubu angalia jina la mtetea hoja .Je halina uhusiano na wale wa EPA ? Unajua mambo mengine ni kusoma alama za nyakati.
 
Ndio Tuangalie Alama Zanyakati

Maoni Yametoka Upande Mmoja Wa Upinzani Yaani Chadema

Sasa Unategemea Nini ??
 
Bubu angalia jina la mtetea hoja .Je halina uhusiano na wale wa EPA ? Unajua mambo mengine ni kusoma alama za nyakati.

Judge all your books by it cover, OK..Uko sahahi, alama za Nyakati ni fisadi________? fisadi that___________?

Utumbo ndio huu, common sense will prevail at all means necessary, na tanzania kuna mambo mengi zaidi ya siasa za matukio, upevu mdogo wa wachangaji lazima uwe scrutinized, kama unataka kuwa personal nimetoa mpaka anwani na Jina langu: Twalipo, checking in as the beautiful Ngorongoro Hotel ya Ngurudoto,nimefika...we EPA tu, huna lolote na alama za nyakati!!!
 
Mwanakijiji,

Mimi nimeisoma na sijaona hicho kipengere na ndio maana nikaomba msaada kwa anayejua hicho kipengere.

Naona toka jana kila mtu anasema katiba inasema hivyo, kwanini hamtaki kukiweka kipengere kamili?

kwa sababu tukikiweka tutakuwa tunawafanyia watu kazi ambayo wanaweza kuifanya, kama wangesoma Katiba wasingepata hilo shaka. Yawezekana ni kweli ndugu yangu umeisoma lakini nakushauri urudie tena ili uweze kuona lakini ukweli bado uko pale pale kwamba Katiba ya CCM imeweka jukumu kwa CCM kuwa ni kitu cha kwanza kabisa kabla ya nchi na siyo kwa maneno yenye utata ambayo mtu anaweza kuyatafsiri tofauti bali kwa maneno ya wazi kabisa ambayo kwa mtu aliyesoma katiba hiyo hatapata shida ya kuyatambua.

Naomba urudie tena kusoma lakini kama kweli utakuwa umeshindwa kabisa kukiona hicho kipengele (siyo kwa vile hakipo) basi with pleasure nitajitolea kukuonesha kilipo.
 
You must be joking! kukimbia kwa Mkapa ni good governance? 😕
What did Kikwete do to make Mkapa run away from that meeting? 😕

What about those EPA, Radar, Richmonduli Mafisadis who are still at large? is that good governance too? You've to think before writing your thoughts.

Bubu huwa unaongea lakini kusema bado, kuongea na kusema ni vitu viwili tofauti..

Soma, kwanza....I went through lenghts to explain hypothetical kuwa ingekuwa mazingira ya kawaida, absense ya Mkapa ingeweza kuwa chochote, bubu kasema Mkapa kakimbia, I didnt say that...Point ni tunalishwa habari za hivi hivi sababu ya kiu iliyopo ambayo haiongezi maendeleo.
.Sasa unachojua wewe siyo ndio matatizo yote ya Tanzania, wewe unajua skendo zote, nadhani hata ukiamshwa usiku wa manane, mtiririko huo utautaja kirahisi tu...
 
Mwanakijiji,

Mimi nimeisoma na sijaona hicho kipengere na ndio maana nikaomba msaada kwa anayejua hicho kipengere.

Naona toka jana kila mtu anasema katiba inasema hivyo, kwanini hamtaki kukiweka kipengere kamili?

wameongeza maji ili hali unga robo ! kama wanaweza, waweke ! simpo !
hoja hujibiwa kwa hoja !
 
Kikao bado kinaendelea muda huu lakini wamepumzika kidogo kwa ajili ya chakula cha usiku, hivyo sitashangaa kikao kitaendelea hadi usiku sana, na taarifa yoyote ya kikao hicho itatolewa mapema kesho asubuhi...

mkuu samahani lakini si tulishatoa report ya ndani ya CC?? Therefore NEC won't have any news since they will just deal with what was decided during CC meeting ie CUF/CCM and blah blah rhetoric nyingi tu kuhusu hali ya siasa na uchumi.
 
Back
Top Bottom