Mtu wa Kwao
JF-Expert Member
- Jan 15, 2008
- 258
- 21
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imeanza kikao chake mchana huu hapa Butiama. Salaam kutoka kijijini Butiama.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imeanza kikao chake mchana huu hapa Butiama. Salaam kutoka kijijini Butiama.
Ohh Halisi,
how we missed you our dear brother.
Mungu akuongoze na kukuonesha njia.Jitahidi kivuli cha Mwalimu kikufunike upitwe mbali na kikombe kile walichokunnywa kina Lowassa,Mkapa,Rostam,Mramba,Mgonja,Chenge,Balali mmhh majina hayaishi tu...sijui na Kiwete?
Kwa kifupi wasikuambukize ufisadi.
ccm chama changu na daima nitakipenda
kidumu chama cha mapinduzi
taratibu ulijuaje kama halisi brother?
naam mambo yameanza na mara hii tena ccm imewapa kitendawili watanzania hakuna anaweza kutabiri nn kitatokea.
ccm ni chama pekee mpaka sasa kilichoonesha demokrasia ya kweli]
chama ambacho viongozi wao wako tayari kuwajibika kwa wanayoyafanya na kuwajibishana.
ni chama ambacho kiko tayari kukosolewa, kusoma kutoka kwa wengine,kwenda na wakati na kujipanga upya kuendana na mahitaji ya jamii.
ccm chama changu na daima nitakipenda
kidumu chama cha mapinduzi
True that, kiache kiendelee kudumu hivyo hivyo maana kubadilika ni kazi!
Mkuu wangu, kwanza ninataka kuamini kuwa wewe ni mbongo mwenzangu, maana haiwezekani ukawa mbongo ukashindwa kujua kuwa kustaafu mapema kwa Mahita, ex-Police Chief, hoja ilianzia NEC na baadaye CC, kwamba Mbilinyi waziri wa zamani wa hazina hoja ya kumpuzisha ilianzia NEC, kwamba majuzi kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri watatu, hoja zimetokea NEC na CC, I mean kamati ya CCM ya ulinzi na usalama kazi yake ni nini? kamati ya uchumi ya CCM kazi yake ni nini?
Ni pamoja na kufuatilia ishus za uchumi za taifa, kukutana na gavana na waziri at their call, kwa hiyo kama kuna ishu wanatakiwa kuifikisha kwenye NEC, ni lazima wawaite waziri na gavana, ili kuwasilisha their side of the professional story inayowakilishwa na kamati kwa NEC, bunge hufanya hivyo pia kumbuka kuwa hiyo professional Nduulu ameipata baada ya kuchaguliwa na rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, ambaye taifa tumempa nafasi kisheria kutekeleza sera za CCM, ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi,
Hivi kweli haya yanahitaji kuwa professor kuelewa, hivi mkuu kweli unaaamini kuwa mkuu wa majeshi na wa polisi sasa hivi hawako Butiama tayari!
Go east,Go West ;Nyerere was the best ever.Hta mafisadi wanajua hilo
Pamoja na kuendeleza juhudi kubwa za kutetea chama chako bado mnachemsha BIG TIME.
Katiba ya nchi imempa madaraka makubwa sana Rais. Na kwa madaraka haya yenye ndio CEO wa nchi na maamuzi yake yana impact kubwa kwa nchi.
Kinachosumbua ni kuwa Rais anashindwa kufanya kazi kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba. Na anachofanya ni kuwa na mikutano ambayo inatoa collective decisions ambazo zinamuondoa yeye kwenye lawama.
Hivyo akiulizwa atajitetea kuwa ni maamuzi ya NEC au CC. Na hii yote inatokana na ukweli kuwa anaowachagua ni watu wanaomfahamu, waliomdhamini au anaogopa kulogwa.
Watendaji wanaoteuliwa na rais wanafanyakazi kwa ridhaa yake na yeye anaweza kuwaondoa madarakani bila kusubiri vikao vya NEC au CC.
Na mtindo wa kutumia NEC, CC tuliiga kutoka katika nchi za Ulaya mashariki na sasa hivi mtindo huo ni PRE-HISTORIC. Nendeni na wakati.