Mkuu wangu, kwanza ninataka kuamini kuwa wewe ni mbongo mwenzangu, maana haiwezekani ukawa mbongo ukashindwa kujua kuwa kustaafu mapema kwa Mahita, ex-Police Chief, hoja ilianzia NEC na baadaye CC, kwamba Mbilinyi waziri wa zamani wa hazina hoja ya kumpuzisha ilianzia NEC, kwamba majuzi kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri watatu, hoja zimetokea NEC na CC, I mean kamati ya CCM ya ulinzi na usalama kazi yake ni nini? kamati ya uchumi ya CCM kazi yake ni nini?
Ni pamoja na kufuatilia ishus za uchumi za taifa, kukutana na gavana na waziri at their call, kwa hiyo kama kuna ishu wanatakiwa kuifikisha kwenye NEC, ni lazima wawaite waziri na gavana, ili kuwasilisha their side of the professional story inayowakilishwa na kamati kwa NEC, bunge hufanya hivyo pia kumbuka kuwa hiyo professional Nduulu ameipata baada ya kuchaguliwa na rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM, ambaye taifa tumempa nafasi kisheria kutekeleza sera za CCM, ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi,
Hivi kweli haya yanahitaji kuwa professor kuelewa, hivi mkuu kweli unaaamini kuwa mkuu wa majeshi na wa polisi sasa hivi hawako Butiama tayari!