Mimi naelewa kwa nini Rais Magufuli anaweza kuwa frustrated sasa hivi, hata ungekuwa wewe nadhani hata ungepata uchizi.
Imagine umetumia miaka minne, umepambana we, ukatumia nguvu zote hadi za ziada kufanya kila utakacho, umefanya miradi mikubwa, wakati mwingine umeumiza hata wengine huku ukisema ni kwa maslahi mapana ya taifa, leo hii kanakuja ‘kaugonjwa’ tu kanataka kupukutisha yale yooote uliyotaka kufanya. Niambie kati yenu, nani asingekuwa frustrated?
Anyway, nimeona picha hii ya leo ya kuapishwa kwa Bwana Nchemba, nikasema hii ni social distance kabisa ya kiwango cha 5G!
Na tena nasikia shughuli imefanyika hotelini, pembeni tu ya jiko, hakutaka hata mgeni afike nyumbani kusalimia? Anyway, mgeni mwenyewe alikuwa Bungeni juzi, hatujui atakuwa amebeba nini, nadhani tahadhari ni muhimu kuliko hatari. Hata mimi ningefanya hivyo, je wewe?
Watanzania, kusikia hamsikii, hata picha hamuoni?