Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Hayo ndio mnayaweza kukebehi na kupinga
Mwigulu kaambiwa afuatilie mambo ya kisheria,muda wa kusikiliza hotuba hamna mnakuja humu kupoozana stress tu
Kuna hotuba ya kusikiliza?
 
Yawezekana kabisa kuwa Magufuli ni "akili kubwa"..
Ndiyo... Amewazidi Watanzania wengi akili... Na amewashika vizuri...

Kati kati ya janga la #Covid_19 yeye kajificha kijijini kwake lakini wafuasi wake kawasisitiza waendeleee kuchapa kazi kwa bidii...

Kwa wafuasi wake neno lake ni zaidi ya maagizo...

Lakini wachache wanaomzidi akili wanahoji (nikiwemo na mimi)... Ni kwa nini asijitokeze mstari wa mbele kuungana na wafuasi wake kwenye mapambano...??

Ni kwa nini yeye ajifungie ndani huku akiendelea kuwahimiza wengine wachape kazi...
 
Hayo ndio mnayaweza kukebehi na kupinga
Mwigulu kaambiwa afuatilie mambo ya kisheria,muda wa kusikiliza hotuba hamna mnakuja humu kupoozana stress tu
Yule Rais wa Russia iliyosemekana amepandikizwa na nchi zingine ili Urusi uvurugike na ikavurugika alianza namna hii. Tusipochukua hatua mapema tutajikuta pabaya; jamaa ni pandikizi kabisa.
 
Inawezekana kuna kitu kimegundulika nyuma ya Ugonjwa huu, tuwe makini sana.
Kama wamechunguza, kuna uwezekano wa mengi kutokusemwa wazi na shirika la afya dunia.
Kama ilivyoaminika Iran, China na Marekani katika utafiti wao wa Kijasusi, vipi hapa ?
Safi kabisa umejenga hoja kuntu mkuu,ningependa wote tungejikita katika maswali ya namna hii pengine wataalamu waliomo humu wangepata vya kujibu lakini "vitoto" vya chuo vinabwabwaja mambo ya ajabu siasa siasaaaaaaaa siaaaaaaasa tu tunaboa sana na saaaaana yaaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya kupima mapapai?
Ndio mana nasema hukusikiliza hotuba
Huwa mnasubiri Rais aseme mpate sababu ya kuondoa stress
Mapapai ni sampuli ilipelekwa kwa siri bila ya wao kujua,ili kupima accuracy ya maabara
Na hawapeleki kipande cha papaj,wanachukua ute tu na kuandika Daudi Mchambuzi,ngoma inarudi na postive
 
Wanabodi
Kwa wale wenye nafasi, ifika saa 4:15 asubuhi hii, tujiunge na TBC kuangalia matangazo ya moja kwa moja ya live mubashara kutokea ikulu ya Chato.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Tweet ya Gerson Msigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Mei, 2020 atamuapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Tukio hilo litarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari kutoka Chato Mkoani Geita, kuanzia saa 4:15 asubuhi. Gerson Msigwa on Twitter

Karibuni mshuhudie
Pia leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa habari, huku Tanzania tukiwa kwenye hii vita ya kimataifa ya kupambana na janga la Corona, serikali ya Tanzania ikishutumiwa kuficha idadi ya kweli ya vifo vya Corona, hivyo tufuatilie kwa makini tukimsikiliza rais Magufuli atazungumza nini.
P

UPDATES

MAGUFULI: PAPAI LILIKUTWA NA #CORONA KATIKA ‘KUTEST’ MABARA KUU

Katika kuwatoa hofu watanzania Rais Magufuli amesema kuna uwezekano watu wasio na #CoronaVirus wakaambiwa wana #CoronaVirus kwa kuwa katika kuwajaribu watu wa maabara waliwapelekea sampuli ya Oil, Papai, kondoo, mbuzi na fenesi

Papai, ndege aina ya Kware na Mbuzi walikutwa na #CoronaVirus. Rais Magufuli amesema inawezekana hawa walioko maabara wamenunuliwa na mabeberu. Kwa kuwa sampuli ya papai ilikuwa ni ya ndani ya tunda na sio nje kusema kuwa mtu aliye na #CoronaVirus aliligusa

Pia amesisitiza hatofunga mkoa wowote, na anafikiria pia kuruhusu ligi ya mpira wa miguu iendelee, kwa kuwa hakuna mwanamichezo ambaye ameathirika katika hili

Magufuli anasema inawezekana wanaofanya mazoezi hawaguswi na #CoronaVirus kwa hiyo kuwazuia mazoezi ni kutaka wapate korona

Tunaweza kuishi na #CoronaVirus kama tunayoishi na Surua, UKIMWI

Mkuu nilichofurahi ni kujua kumbe Hata raisi unaweza kuwa hana taarifa za kutosha za mambo mengi tuu!

Wataalamu kwa sisi wapenda kusoma na watafiti wametuambia corona virus wanaweza kuwa kwenye: kiti cha daladala, kitasa cha mlango, nguo tunazovaa, sakafu, kwenye viatu, kwenye wanyama tunaofuga provided vitu vimekuwa exposed kwa corona virus.

Nimaamini hata fenesi, embe, ugali nk vikiwa exposed kwa corona virus vitakuwa contaminated, sijaelewa Mwalimu wa chemistry hajui hilo au anafanya maksudi kwa mambumbumbu!

Najua mtukufu sio msomaji kama wewe na Mimi, naweza tambua hili mosi, uwasilishaji hoja, mbili, ubishani shindanishi, tatu kushindwa kuconnect maada, unfortunately here in Tanzania we have leaders who aren't readers, sio kama mataifa mengine, leaders are knowledgeable! Here leaders are dumps!!
 
Ndio mana nasema hukusikiliza hotuba
Huwa mnasubiri Rais aseme mpate sababu ya kuondoa stress
Mapapai ni sampuli ilipelekwa kwa siri bila ya wao kujua,ili kupima accuracya ya maabara
Na hawapeleki kipande cha papaj,wanachukua ute tu na kuandika Daudi Mchambuzi,ngoma inarudi na postive
Comrade leo mmepima mapapai mangapi?
 
Yule Rais wa Russia iliyosemekana amepandikizwa na nchi zingine ili Urusi uvurugike na ikavurugika alianza namna hii. Tusipochukua hatua mapema tutajikuta pabaya; jamaa ni pandikizi kabisa.
Hatua gani?
 
Mkuu nilichofurahi ni kujua kumbe Hata raisi unaweza kuwa hana taarifa za kutosha za mambo mengi tuu!

Wataalamu kwa sisi wapenda kusoma na watafiti wametuambia corona virus wanaweza kuwa kwenye: kiti cha daladala, kitasa cha mlango, nguo tunazovaa, sakafu, kwenye viatu, kwenye wanyama tunaofuga provided vitu vimekuwa exposed kwa corona virus.

Nimaamini hata fenesi, embe, ugali nk vikiwa exposed kwa corona virus vitakuwa contaminated, sijaelewa Mwalimu wa chemistry hajui hilo au anafanya maksudi kwa mambumbumbu!

Najua mtukufu sio msomaji kama wewe na Mimi, naweza tambua hili mosi, uwasilishaji hoja, mbili, ubishani ahindanishi, tatu kushindwa kuconnect maada, unfortunately here in Tanzania we have leaders who aren't readers, sio kama mataifa mengine, leaders are knowledgeable! Here leaders are dumps!!
"Nimaamini hata fenesi, embe, ugali nk vikiwa exposed kwa corona virus vitakuwa contaminated, sijaelewa Mwalimu wa chemistry hajui hilo au anafanya maksudi kwa mambumbumbu!"

Japo umesema wewe msomaji ila kupitia hiki kitu wewe husomi mkuu

Kaelezea yote hayo hebu fuatilia usipende kusikia habari toka kwa kina kigogo mkuu,,,,

Mapapai,fenesi nk kasema sample walizochukua hazikuwa exposed na virus,halafu wewe nae hata bila kufikiri tu usiwe unaona mtu kuitwa Rais ni jambo dogo, to Rais ni taasisi hawez akaongea kama unavyotaka kutuaminisha hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom