Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Kwanini Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Kwahiyo hakuna Corona?
Khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee nani kakwambia hakuna Covid-19, hakuna dawa hivi sasa, tunaongelea hujuma, i.e. sio kila anayekufa ni kwa sababu ya Covid-19 pekee.
 
Wanabodi,

Kwa wale wenye nafasi, ifika saa 4:15 asubuhi hii, tujiunge na TBC kuangalia matangazo ya moja kwa moja ya live mubashara kutokea ikulu ya Chato.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Tweet ya Gerson Msigwa.

Pia leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa habari, huku Tanzania tukiwa kwenye hii vita ya kimataifa ya kupambana na janga la Corona, serikali ya Tanzania ikishutumiwa kuficha idadi ya kweli ya vifo vya Corona, hivyo tufuatilie kwa makini tukimsikiliza rais Magufuli atazungumza nini.
P

==========

View attachment 1438587

BAADHI YA NUKUU:

Rais Magufuli: Miaka ya nyuma ulikuwa ukienda kutembela sehemu ukaambiwa kuna Surua unaogopa. Leo ugonjwa huo umeonekana wa kawaida na hofu imeondoka. Ni hivyo kwa magonjwa mengi ambayo tumekuwa tukiyaona kama nchi kama TB na Ukoma. Hofu hiyo imeondoka hata kwa Ebola

Rais Magufuli: Niwaombe watanzania hili tatizo (#COVID19) litaondoka na tuendelee kuchukua tahadhari zinazotakiwa tusihusishe na uchumi wa nchi yetu.

Nchini waajiriwa zaidi ya 49% ni walimu ila tumelipa mishahara shule zikiwa zimefungwa na tutaendelea kulipa.

Rais Magufuli: Waziri Mwigulu nimekuapisha leo, itabidi mkafanye uchunguzi kwenye masuala fulani ktk maabara ya Kitaifa inayohusika kupima #Corona

Nimeona walikuwa wanatoa tu matokeo watu wameathirika tu. Nilitoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakaangalie.

Rais Magufuli: Namshukuru Katibu Mkuu mpya, wameenda na kufanya yafuatayo; Tulichukua sampuli ya Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari na kupeleka maabara bila wao kujua

Sampuli ya oil kwa mfano tuliipa jina la Jabri Hamza mwenye miaka 30, ile ilileta “negative”

Rais Magufuli: Sampuli ya Fenesi iliyopewa jina la Sara Samweli matokeo yake yalikuwa 'inconclusive'

Sampuli ya Papai tukaipa jina ya Elizabeth Anne, majibu yakawa Positive kwamba lina Corona kwamba maji ya ndani ya papai yana #COVID19

Rais Magufuli: Sampuli ya ndege Kware imekuwa ‘positive’, ya Sungura ikawa ‘indeterminate', ya Mbuzi ikawa ‘positive’, ya Kondoo ikawa ‘negative’

Sasa ukiona ya binadamu ikawa positive maana yake na mapapai yote yaweke isolation au mbuzi na fenesi wote wawe isolated.

Rais Magufuli: Ukigundua kitu hiki lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika katika maabara hii na katika nchi hii.

Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, au hawana utaalamu; kitu ambacho si kweli au vifaa maana hadi vipamba vinatoka nje.

Rais Magufuli: Kama hadi mapapai yana #CoronaVirus basi WHO inatakiwa ifanye kazi kubwa ktk haya, na kama hadi Mbuzi wana Corona basi wanasayansi hawajafanya kazi ya kutosha

Kutokana na hizi taarifa lazima kuna watu wameambiwa ‘positive’ wakati si wagonjwa wa #COVID19

Rais Magufuli: Kuna wengine si ajabu wakafa kwa hofu. Papai halijafa lipo tu linaiva, Mbuzi yule yupo tu wala hajafa hata fenesi lipo

Natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu. Wale ambao hawajachoka wala kuumia kwanini uwe na hofu? Mafua yamekuwepo ila haya ni advanced.

Rais Magufuli: Kitendo cha kukuta hata papai lina #COVID19 mule ndani wala sio juu, kwasababu ingekuwa juu wangesema labda aliyegusa ana #CoronaVirus. Wametoa specification vizuri kabisa, walichoma ndani wanachukua sampuli. Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Rais Magufuli: Kuna vitu vingi vya kujiuliza, huenda kuna kitu hakijaeleweka kwa wanasayansi lakini hata dunia hawajakielewa

Natoa wito kwa wanaotumia vifaa hivi hasa Afrika, wachukue sampuli ya kitu chochote hata ukuta, mjusi watakuja kuthibitisha haya.

Rais Magufuli: Tuendelee kuchapa kazi, uzalishaji uendelee maradufu, tusitishane. Wanasiasa waache kuitumia #COVID19 kama agenda, haitasaidia

Mtu anasema funga Dar, funga Tanga, sifungi nilishasema. Ni lazima Watanzania tuchape kazi na kuendelea kuchukua tahadhari.

Magufuli: Inawezekana fenesi, papai lingekuwa linasikia kuwa lina #COVID19 lingekuwa limeshaoza kabisa. Lakini kwa vile halisikii, lina #CoronaVirus na bado lipo

Sasa wewe kama Waziri (Nchemba) mkashirikiane na Wizara ya Afya mkaangalie hiyo Maabara ya Taifa kuna nini?

Rais Magufuli: Mbeleni ninafikiria hata kuruhusu ligi iendelee ili watu wawe wanacheza tukiangalia kwa TV. Tuweke utaratibu mzuri.

Ninaelewa hata walioathirika na #COVID19 sijaona mwanamichezo aliyedhurika sana. Hii ni wazi kuwa wanaofanya michezo #Corona inawakwepa.

Rais Magufuli: Kama tunazuia hata kucheza mpira maana yake tunawaambia wapate #Corona. Najaribu kusubiri wataalamu wanishauri vizuri

Inawezekana tunaishi na huu ugonjwa kama watu wenye UKIMWI, TB, Surua na maisha yakaendelea. Tuache kuogopana na kutishana.

Rais Magufuli: Ninajua wapo wengine wangependa kuzungumza kuhusu #Corona. Naona na vyombo vingine vya habari wao ni corona tu, tena vya nje na huko vinapotangazia ndio imeua watu wengi

Lazima mjiulize kwanini havizungumzii ya kwao wanaongelea ya #Tanzania?

Rais Magufuli: Natoa wito kwa hasa vijana ambao kila siku wakimuona mtu amekufa ni #COVID19

Jaji Mkuu (Augustino Ramadhani) tumehangaika naye hapa kwa mwaka mzima, si vizuri kutaja matatizo yake. Baba yangu kafariki kwa saratani kama Jaji Mkuu ila watu wamebadili maneno ya ajabu.

Rais Magufuli: Si kila anayekufa ni #Corona. Malaria inaua, ajali inaua. Juzi Mkuranga wamekufa watu 21 kwa ajali, roho zao Mungu azipumzishe kwa amani

Siku hizi mtu hata akijifia chumbani kwake wanapoenda kuchukua ile maiti ni Corona. Ninawaomba Watanzania tubadilike.

Rais Magufuli: Nawapongeza madaktari, manesi na watendaji wa Wizara ya Afya kwa kuendelea kuhudumia Watanzania ktk kipindi hiki.

Kuna mengi ya kushangaza nchini. RC wa Mtwara nikamsikia kwenye vyombo vya habari eti "DC huyu hawezi kusafirishwa kwenda kwao", inasikitisha.

Rais Magufuli: Kama madaktari wanaenda kuwaona wagonjwa wakiwa na PPE. Walishindwaje viongozi wa Mkoa wa Mtwara chini ya RC kuifunga maiti PPE na kuipeleka Moshi?

Niwaombe viongozi wenzangu tusichukue hili kwa papara, tuwatumie wataalam kupata ushauri utakaosaidia.

Rais Magufuli: Ninaamini #CoronaVirus ipo ila si kwa 'extent' hiyo. Katika siku 2-3 zilizopita tulikuwa na watu 16 waliofariki kwa #COVID19

Sasa tafuta uwiano wa watu 16 na idadi ya watu karibu mil. 60 na uwiano wa nchi nyingine na idadi yao ya waliokufa halafu utaona.

Rais Magufuli: Tunawatisha Watanzania wanaogopa hata kwenda kufanya kazi au sokoni

Nilisoma kwenye WhatsApp mtu anasema “funga masoko”. Nikajiuliza huyu ana akili za kawaida? Hapo alipo hana shamba wakifunga masoko atapata wapi chakula? Tena yupo Dar, ni “shortsighted”

Rais Magufuli: Ukizuia soko la Kariakoo, watu milioni 6 wa Dar watakula wapi? Wabaya wetu wanataka tuingie kwenye ujinga huo.

Nchi zilizofunga mnaona matokeo yake. Sitaki kuzitaja ila kuna nchi watu wamekufa zaidi ya elfu 50 na zina uwezo wa kila kitu.

Rais Magufuli: Tuchukue tahadhari na kuwapuuza wanaojaribu kututisha, hawana maana. Tuendelee kumuomba Mungu.

Kuna Viongozi wengine wa dini wamemsahau Mungu, wameanza kuyumba na wameanza kuweka ubinadamu mbele. Wanasema tuache kuomba ili tujiokoe. Ni mambo ya ajabu!

Rais Magufuli: Hali si mbaya kama tunavyotishwa, sisi tupo vizuri na biashara zinaendelea ndio maana hata tunaweza kulipa mishahara.

Hata hao wanaosema tufunge huku anaendeshwa na gari limeandikwa STK, mafuta anawekewa na Serikali, amesahau alichokalia ndicho kinamlisha.

Rais Magufuli: Ninawasiliana na Madagascar na wameandika barua wanasema kuna dawa imepatikana. Tutatuma ndege ili ziweze kuletwa nchini.

Serikali tunafanya kazi usiku na mchana. Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa sitakiwi kuwa huku? Huku si ndiko nitazikwa?

Rais Magufuli: Tunatakiwa kusimama pamoja. Nampongeza Mbatia (James) ni mwanasiasa mzuri. Wakati wa vita ni vita wote tushikamane twende mbele

Mpaka ananiandika SMS " Uwe na moyo mkuu, tuendelee kuchapa kazi". Ni wa Upinzani ila ni muelewa unajua yupo kwa ajili ya nchi.

Rais Magufuli: Kuna mwingine anazungumzia Dar wala hayupo Bungeni "Leo tumeahirisha kwenda Bungeni". ACHA!

Nimetoa maelekezo hakuna kuwalipa posho. Utalipwaje wakati huifanyii kazi? Usipoenda watakulipa hao mababeru wanaokutumia kuzungumza hayo unayotaka kuzungumza.
Ushauri wangu wa bure tu kwa Mwigulu ni kuwa azingatie sheria,utwala bora na si amri au mihemuko.
 
Hivi sampuli ya kupima corona huwa nini? Kama ni damu papai pia lina damu?
kwa kawaida sample collection inaweza kuwa damu,mate,mafua pia ila hapo hakuwa na mana iyo.ujue ata kwa akili ya kawaida tuuh Ni ngumu virus wa corona kumultipley in plant cell na papai kuadhirika
Kwaiyo unadhani alimanisha kuwa papai Ni halali kuwa na corona? open your mind Apo ana manisha Kuna tatizo in our laboratory test iyo ndio mana halisi huwenda Kuna upikaji wa samples report
 
Dah! yaani wamepeleka sampuli za hovyo hovyo badala ya kupeleka za binadamu, mtaalamu atapima kile alichopelekewa na kusoma majibu. Ukimpotosha kwa kumpa kitu tofauti apime linakuwa siyo tatizo lake.....ina maana unataka afanye kazi ya ziada ya forensic ili aweze kugundua kama hiyo sampuli ni genuine na hilo linaweza kufanywa na maabara tofauti au na wataalaamu tofauti, huna haja ya kufuata mlolongo wote huo....kuna namna bora ya kuthibitisha majibu ya vipimo hasa kama utakuwa umefanya 'rapid test' itabidi ufanye 'confirmatory test' hasa kwa zile sampuli ambazo ni positive au zile ambazo una mashaka na majibu yake......ila chonde chonde usipeleke sampuli ambazo hazikukusudiwa kwa lengo la kuwalaghai wapimaji...
Hahahaaaaa wasomi wa Mahabara yaani usigundue. Sample ya mwanadamu na tunda! Mimi Furaha yangu ni moja tu!

Mbowe na waliomtuma wamegonga Mwambasi, Their dirty game has been revealed!

I am very sorry with opposition members of parliament, ambao wanaburuzwa! Halafu hi si ndiyo bunge la mwisho kuelekea uchaguzi eheee! Hahaaa mtakosa hata hela za kuwawekea Vocha wapiga kura wenu.

Your boss is having a deal na watu Fulani! Yeye Anapiga pesa ndefu, nyie mnafuata Mkia.
 
Kweli kifo kinaogopwa jamani, yaan mzee kaukimbia mji mazima! Daah, we Corona toka baba yetu arudi mjini! R.I.P Mahiga huwezi amini Maderu ndio karithi cheo chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilichopima leo toka kwenye ile hotuba inaonekana JPM ni member wa Jf maana mambo yote ya kipuuzi ambayo huwa mnaandika huwa anayasema. Mfano hili la kujichimbia Chato.
 
Mzee Paskali acha kutuongopea, Ikulu-chato?? Msigwa mwenyewe kasema tu Chato mkoani Geita. Chato hakuna Ikulu. Rais yuko kwenye self isolation, hii ni karne ya 21 hauwezi kuwadanganya watu kwa propaganda.
Kama ni self isolation aide de camp angekuwa nyuma yake wakati anahutubia? Au self isolation mimi inanichanganya?
 
Wewe ndyo umeenda shule na ukaelimika!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na huo ndio utaratibu, validation iki fail maana yaje hiyo machine au chemicals in question hazifai kutumika kufanya any human testing.
Errors needs to be investigated and corrected siyo kudhalilishana hadharani. So far hatujui kosa liko wapi, ni machines au chemicals au wataalam walio husika. Sasa anapolaumu anatakiwa awe specific kwa kueleza, what was wrong.
Ni kweli uchunguzi ufanyike tufahamu tatizo liko wapi.
 
Na pengine labda walistuka nao wakaamua kujifanya machizi zaidi kwa kumpa positive. Na mtu kama huyu ili kumfanya asizidi kuwa mwenye michezo ya kitoto unampima naye unampa positive
Mimi nadhani hizo positives kama zipo zilitokana na hao watu wa rais waliohusika kuaandaa hizo specimens... Akiwemo na yeye mwenyewe!
Kwa jinsi alivokuwa akikohoa bila shaka sampuli yake ilirudi na majibu positive na hataki kuyakubali!
To be honest tunaye rais ambaye ni muongo kuliko waongo ninaowafahamu...

Kwa akili zangu zitamamu niliona akisoma kwenye kikaratasi na kila alipokuwa akitaja sample majibu yaliyorudi yalithibitisha kuwa mashine wa haina shida...
Alisoma maneno kama "inconclusive", "unidentified" n.k alipoona atauumbuka akaacha kusoma kimemo...

Nadiriki kusema kuwa kwa sasa ni kama Magufuli kama amejisogeza Chato asubirie kifo cha namna yoyote ile!!
 
1. Kuna wanaosema niifunge Dar sababu ya Corona, siifungi nilishalisema. Watanzania waache uoga wachape kazi. Wanasiasa waache maneno maneno.
2. Wengine wanasema nimekimbia nipo Chato. Kwani Chato sitakiwi kuwepo? Hapa ndipo nilipozaliwa na nikifa nitazikwa hapa. Ningeenda Moshi wangesema nimekimbilia Moshi. Ili uonekane hujakimbia sijui wanataka uwepo wapi? Tuache siasa za ajabu.
3. Mambo ya kucopy na kupaste nchi hii hatuwezi kufanya. Wapo waliofunga mipaka na shughuli za kiuchumi mnaona wanavyoteseka. Sisi tuchape kazi.
4. Nafikiria kufungulia hata ligi ya mpira iendelee maana mpaka sasa sijaona mchezaji yeyote mwenye corona. Ligi iendelee watu watizame hata kwenye TV.
5. Nilimuona Mkuu wa mkoa wa Mtwara akisema DC Mmanda amefariki hatuwezi kusafirisha atazikwa hapahapa. Ilinisikitisha sana. Kama madaktari wanawahudumia wagonjwa wa corona kwa kuvaa PPE, walishindwaje kuivisha maiti ya Mmanda PPE na kuisafirisha kwenda Moshi akazikwe kwao kwa heshima?
6. Wengine wapo Dar wanasema watu wasiende bungeni. Nimeagiza wasilipwe posho maana utalipwa kwa kazi uliyofanya. Kama umekimbia kazi unategemea kulipwa nini?
7. Inawezekana hivi vipimo vyenyewe sio salama, vimetengenezwa kwamba vikipima watu 30 anayefuata lazima akutwe na Corona. Mimi ni mwanasayansi naelewa ninachosema. Natoa wito kwa nchi za Afrika zianze kufanya uchunguzi kuhusu hivi vipimo (test kits) maana hatujui nia ya waliovitengeneza.
8. Tulifanya mambo kadhaa ili kujua ubora wa Maabara tukapeleka sampuli za wanyama, ndege na vitu vingine bila wao kujua, tukazipa majina ya watu, tumepeleka sampuli ya mbuzi akawa positive, kondoo Negative, mapapai nayo positive, maana yake mbuzi na mapapai yote yana corona. Inawezekana wafanyakazi wa Maabara zetu wanatumika na Mabeberu ili ugonjwa huu uonekane ni tishio.
9. Sina imani na Mkuu wa maabara ya taifa maana haiwezekani tupeleke sampuli za papai, mbuzi na kware zionekane zina Corona
10. Huu ni wakati wa kuwapima imani hata viongozi wetu wa dini. Unawazuiaje watu kwenda kanisani au msikitini wakati hujajenga wewe?
 
Yeye
Wanabodi,

Kwa wale wenye nafasi, ifika saa 4:15 asubuhi hii, tujiunge na TBC kuangalia matangazo ya moja kwa moja ya live mubashara kutokea ikulu ya Chato.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Tweet ya Gerson Msigwa.

Pia leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ya uhuru wa habari, huku Tanzania tukiwa kwenye hii vita ya kimataifa ya kupambana na janga la Corona, serikali ya Tanzania ikishutumiwa kuficha idadi ya kweli ya vifo vya Corona, hivyo tufuatilie kwa makini tukimsikiliza rais Magufuli atazungumza nini.
P

==========

View attachment 1438587

BAADHI YA NUKUU:

Rais Magufuli: Miaka ya nyuma ulikuwa ukienda kutembela sehemu ukaambiwa kuna Surua unaogopa. Leo ugonjwa huo umeonekana wa kawaida na hofu imeondoka. Ni hivyo kwa magonjwa mengi ambayo tumekuwa tukiyaona kama nchi kama TB na Ukoma. Hofu hiyo imeondoka hata kwa Ebola

Rais Magufuli: Niwaombe watanzania hili tatizo (#COVID19) litaondoka na tuendelee kuchukua tahadhari zinazotakiwa tusihusishe na uchumi wa nchi yetu.

Nchini waajiriwa zaidi ya 49% ni walimu ila tumelipa mishahara shule zikiwa zimefungwa na tutaendelea kulipa.

Rais Magufuli: Waziri Mwigulu nimekuapisha leo, itabidi mkafanye uchunguzi kwenye masuala fulani ktk maabara ya Kitaifa inayohusika kupima #Corona

Nimeona walikuwa wanatoa tu matokeo watu wameathirika tu. Nilitoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakaangalie.

Rais Magufuli: Namshukuru Katibu Mkuu mpya, wameenda na kufanya yafuatayo; Tulichukua sampuli ya Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari na kupeleka maabara bila wao kujua

Sampuli ya oil kwa mfano tuliipa jina la Jabri Hamza mwenye miaka 30, ile ilileta “negative”

Rais Magufuli: Sampuli ya Fenesi iliyopewa jina la Sara Samweli matokeo yake yalikuwa 'inconclusive'

Sampuli ya Papai tukaipa jina ya Elizabeth Anne, majibu yakawa Positive kwamba lina Corona kwamba maji ya ndani ya papai yana #COVID19

Rais Magufuli: Sampuli ya ndege Kware imekuwa ‘positive’, ya Sungura ikawa ‘indeterminate', ya Mbuzi ikawa ‘positive’, ya Kondoo ikawa ‘negative’

Sasa ukiona ya binadamu ikawa positive maana yake na mapapai yote yaweke isolation au mbuzi na fenesi wote wawe isolated.

Rais Magufuli: Ukigundua kitu hiki lazima ujue kuna mchezo wa ajabu unafanyika katika maabara hii na katika nchi hii.

Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, au hawana utaalamu; kitu ambacho si kweli au vifaa maana hadi vipamba vinatoka nje.

Rais Magufuli: Kama hadi mapapai yana #CoronaVirus basi WHO inatakiwa ifanye kazi kubwa ktk haya, na kama hadi Mbuzi wana Corona basi wanasayansi hawajafanya kazi ya kutosha

Kutokana na hizi taarifa lazima kuna watu wameambiwa ‘positive’ wakati si wagonjwa wa #COVID19

Rais Magufuli: Kuna wengine si ajabu wakafa kwa hofu. Papai halijafa lipo tu linaiva, Mbuzi yule yupo tu wala hajafa hata fenesi lipo

Natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu. Wale ambao hawajachoka wala kuumia kwanini uwe na hofu? Mafua yamekuwepo ila haya ni advanced.

Rais Magufuli: Kitendo cha kukuta hata papai lina #COVID19 mule ndani wala sio juu, kwasababu ingekuwa juu wangesema labda aliyegusa ana #CoronaVirus. Wametoa specification vizuri kabisa, walichoma ndani wanachukua sampuli. Mbuzi, papai, fenesi na Kware wawe na Corona?

Rais Magufuli: Kuna vitu vingi vya kujiuliza, huenda kuna kitu hakijaeleweka kwa wanasayansi lakini hata dunia hawajakielewa

Natoa wito kwa wanaotumia vifaa hivi hasa Afrika, wachukue sampuli ya kitu chochote hata ukuta, mjusi watakuja kuthibitisha haya.

Rais Magufuli: Tuendelee kuchapa kazi, uzalishaji uendelee maradufu, tusitishane. Wanasiasa waache kuitumia #COVID19 kama agenda, haitasaidia

Mtu anasema funga Dar, funga Tanga, sifungi nilishasema. Ni lazima Watanzania tuchape kazi na kuendelea kuchukua tahadhari.

Magufuli: Inawezekana fenesi, papai lingekuwa linasikia kuwa lina #COVID19 lingekuwa limeshaoza kabisa. Lakini kwa vile halisikii, lina #CoronaVirus na bado lipo

Sasa wewe kama Waziri (Nchemba) mkashirikiane na Wizara ya Afya mkaangalie hiyo Maabara ya Taifa kuna nini?

Rais Magufuli: Mbeleni ninafikiria hata kuruhusu ligi iendelee ili watu wawe wanacheza tukiangalia kwa TV. Tuweke utaratibu mzuri.

Ninaelewa hata walioathirika na #COVID19 sijaona mwanamichezo aliyedhurika sana. Hii ni wazi kuwa wanaofanya michezo #Corona inawakwepa.

Rais Magufuli: Kama tunazuia hata kucheza mpira maana yake tunawaambia wapate #Corona. Najaribu kusubiri wataalamu wanishauri vizuri

Inawezekana tunaishi na huu ugonjwa kama watu wenye UKIMWI, TB, Surua na maisha yakaendelea. Tuache kuogopana na kutishana.

Rais Magufuli: Ninajua wapo wengine wangependa kuzungumza kuhusu #Corona. Naona na vyombo vingine vya habari wao ni corona tu, tena vya nje na huko vinapotangazia ndio imeua watu wengi

Lazima mjiulize kwanini havizungumzii ya kwao wanaongelea ya #Tanzania?

Rais Magufuli: Natoa wito kwa hasa vijana ambao kila siku wakimuona mtu amekufa ni #COVID19

Jaji Mkuu (Augustino Ramadhani) tumehangaika naye hapa kwa mwaka mzima, si vizuri kutaja matatizo yake. Baba yangu kafariki kwa saratani kama Jaji Mkuu ila watu wamebadili maneno ya ajabu.

Rais Magufuli: Si kila anayekufa ni #Corona. Malaria inaua, ajali inaua. Juzi Mkuranga wamekufa watu 21 kwa ajali, roho zao Mungu azipumzishe kwa amani

Siku hizi mtu hata akijifia chumbani kwake wanapoenda kuchukua ile maiti ni Corona. Ninawaomba Watanzania tubadilike.

Rais Magufuli: Nawapongeza madaktari, manesi na watendaji wa Wizara ya Afya kwa kuendelea kuhudumia Watanzania ktk kipindi hiki.

Kuna mengi ya kushangaza nchini. RC wa Mtwara nikamsikia kwenye vyombo vya habari eti "DC huyu hawezi kusafirishwa kwenda kwao", inasikitisha.

Rais Magufuli: Kama madaktari wanaenda kuwaona wagonjwa wakiwa na PPE. Walishindwaje viongozi wa Mkoa wa Mtwara chini ya RC kuifunga maiti PPE na kuipeleka Moshi?

Niwaombe viongozi wenzangu tusichukue hili kwa papara, tuwatumie wataalam kupata ushauri utakaosaidia.

Rais Magufuli: Ninaamini #CoronaVirus ipo ila si kwa 'extent' hiyo. Katika siku 2-3 zilizopita tulikuwa na watu 16 waliofariki kwa #COVID19

Sasa tafuta uwiano wa watu 16 na idadi ya watu karibu mil. 60 na uwiano wa nchi nyingine na idadi yao ya waliokufa halafu utaona.

Rais Magufuli: Tunawatisha Watanzania wanaogopa hata kwenda kufanya kazi au sokoni

Nilisoma kwenye WhatsApp mtu anasema “funga masoko”. Nikajiuliza huyu ana akili za kawaida? Hapo alipo hana shamba wakifunga masoko atapata wapi chakula? Tena yupo Dar, ni “shortsighted”

Rais Magufuli: Ukizuia soko la Kariakoo, watu milioni 6 wa Dar watakula wapi? Wabaya wetu wanataka tuingie kwenye ujinga huo.

Nchi zilizofunga mnaona matokeo yake. Sitaki kuzitaja ila kuna nchi watu wamekufa zaidi ya elfu 50 na zina uwezo wa kila kitu.

Rais Magufuli: Tuchukue tahadhari na kuwapuuza wanaojaribu kututisha, hawana maana. Tuendelee kumuomba Mungu.

Kuna Viongozi wengine wa dini wamemsahau Mungu, wameanza kuyumba na wameanza kuweka ubinadamu mbele. Wanasema tuache kuomba ili tujiokoe. Ni mambo ya ajabu!

Rais Magufuli: Hali si mbaya kama tunavyotishwa, sisi tupo vizuri na biashara zinaendelea ndio maana hata tunaweza kulipa mishahara.

Hata hao wanaosema tufunge huku anaendeshwa na gari limeandikwa STK, mafuta anawekewa na Serikali, amesahau alichokalia ndicho kinamlisha.

Rais Magufuli: Ninawasiliana na Madagascar na wameandika barua wanasema kuna dawa imepatikana. Tutatuma ndege ili ziweze kuletwa nchini.

Serikali tunafanya kazi usiku na mchana. Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa sitakiwi kuwa huku? Huku si ndiko nitazikwa?

Rais Magufuli: Tunatakiwa kusimama pamoja. Nampongeza Mbatia (James) ni mwanasiasa mzuri. Wakati wa vita ni vita wote tushikamane twende mbele

Mpaka ananiandika SMS " Uwe na moyo mkuu, tuendelee kuchapa kazi". Ni wa Upinzani ila ni muelewa unajua yupo kwa ajili ya nchi.

Rais Magufuli: Kuna mwingine anazungumzia Dar wala hayupo Bungeni "Leo tumeahirisha kwenda Bungeni". ACHA!

Nimetoa maelekezo hakuna kuwalipa posho. Utalipwaje wakati huifanyii kazi? Usipoenda watakulipa hao mababeru wanaokutumia kuzungumza hayo unayotaka kuzungumza.

Yeye kajificha lakini Watanzania wanakufa na wateendelea kufa kama hatatabadilika. Watafute suluhisho la mapungufu badala ya kujilaumu wenyewe nani kanunua vifaa? Hakuna nchi kwa wakati huu mgumu yenye muda wa kutaka Watanzania wafe hakuna na wala si kweli. Je ni vipimo vingapi kama ni hivyo ambayo vimeonyesha watu hawana kumbe wanao. Kuna wrong positive na wrong negative sasa tusiangalie upande mmoja vyote vinawezekana na inawezekana hata wrong negative ikawa kubwa zaidi
 
Jina ni utambulisho na una weza kubalisha mara nyingi tuu mradi iwe kisheria,
Ndio unaweza kubadilisha ila kwa yeye hajabadili jina bali alitumia jina la mtu mwingine kama unajua mambo ya elimu tena mtu akifaulu kama hajaja shule unaonga mwalimu unatumia jina la huyo mtu.
 
Kitu pekee ninachokijua ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Mtwara hana muda mrefu katika hiyo Nafasi na ajiandae tu Kisaikolojia.
 
Arudi Ikulu anafanya nini huko kwa muda wote huu anaonyesha wananchi kama anaogopa . Vilevile wasijaribu kila kitu kuwaingiza wapinzani kwenye hili wamakuwa kama Watanzania wengine tu. Inamaana hata wabunge hakuna uhakika wa vipimo vyao hivyo huwezi kuwalaumu
 
Back
Top Bottom