Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Exactly.....umenena vyema kabisa mkuu....!Nakubaliana na wewe mkuu, wapo pia wenye imani n Lowasa, Membe, Wassira,Sumaye.....nk. Mwisho october atapatikana raisi mmoja tu. Sasa hivi kila mtu ana haki ya kuwa na imani na yeyote anayemtaka.
Yani alitaka amwangamize yeye na familia pia kwa mapenzi ya kijinga zidi ya chama chake cha mafisadi, alafu huyu mwonevu anaomba ridhaa ya kutuongoza wakati ana chuki nyingi moyoni, akipewa upinzani utapata tabu, kwani mbinu nyingi za kigaidi alizojifunza china ni hatari.kwa unyama aliomfanyia lwakatare sitamsamehe asilani .
...
Angalia hapa akiomba ridhaa kupokea kijiti kutoka kwa JK kwa mama yetu maria Nyerere, hapo sijui yeye na mwanae ampe ridhaa nani
![]()
Tukiwa tunaenda kuhitimisha zoezi la kutafuta wadhamini ndani ya chama changu chama cha Mapinduzi - CCM, nimeona ni vema na busara nami kuchukua muda na kufanya tathmini japo kwa ufupi kwa zoezi hili ndani ya chama changu pendwa. Nami nitajikita katika mambo mawili au matatu tu.
Ni hakika chama changu, CHAMA tawala kimeteka mjadala mzima wa uchaguzi huu mkuu wa 2015 sio tu kwa kuvunja rekodi ya watia nia kuwa wengi bali pia matukio na vituko tulivyovishuhudia.
Mijadala mingi ya kisiasa kwa sasa imetawaliwa na mchakato wa utafutaji wa wadhamini pamoja na mchakato wa uteuzi wa chama ulioanza kwa wagombea kutangaza nia, walikijisifu kwa rekodi zao nzuri,
kujitetea kutokana na tuhuma za ufisadi na kuonesha wanaelewa matatizo ya Watanzania, wana mikakati, uwezo, nia ya dhati na ari mpya ya kuyatatua.
Wapo walioenda mbali zaidi na kutoa vipaumbele na hata mwelekeo wa sera, wakiponda mikakati ya serikali ya sasa, ingawa kwa kawaida mwelekeo wa sera za seriklai ijayo huamuliwa na ilani ya chama, Lakini ni vema mgombea hasa wa Urais kuwa na maono juu ya wapi atatupeleka, na kwa namna gani atatufikisha huko.
Wapo waliosema, Elimu, Elimu, Elimu Kwanza kinyume na sera ya sasa ya kilimo kwanza.
Katika waliotangaza nia, tumeona kila aina ya mbwembwe. Wapo waliotangaza nia majimboni mwao wakafanyiwa matambiko na kuvishwa uchifu, wapo waliofanya katika kumbi za kisasa za Dar es Salaam au Mwanza na wapo waliotangaza nia katika viwanja vikubwa vya mpira wakajaza wafuasi kwa maelfu, Na hapa tumeshuhudia uvunjwaji na upuuvwaji wa wazi wa taratibu na kanuni tulizojiweka ndani ya chama.
Wengine hapa kwa makusudi kabisa wakijua wamekuwa wakikiuka taratibu na kanuni hizi wamezidi kufanya kampeni na mikutano ya hadhara ndani ya kipindi cha kutafuta wadhamini, huku wakijaribu kuwaaminisha umma kuwa wanakubalika na kudhani chama kitawaogopa kuwawajibisha kama kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya chama zinavyoelekeza.
Nasisitiza kuwa CCM ni chama makini kilichojengwa katika misingi ya haki na ukweli, na kimekuwa kikitenda haki Daima, Haki itatendeka hakuna mkubwa zaidi ya chama.
Lakini wapo wale walioamua kuachana na utaratibu ya kutangaza nia na badala yake wakaenda Dodoma moja kwa moja, kimya kimya, kuchukua fomu na kuanza kutafuta wadhamini kimya kimya.
Nikienda mbali zaidi binafsi nimeguswa na kupendezwa na mtia nia ambaye ni mbunge wa Iramba na pia naibu waziri fedha wa JMT, ndugu Mwigulu Nchemba, anayeongozwa na Uadilifu, Uchapakazi, Uzalendo na Uajibikaji.
Moja, Hakika huyu ni kiongozi wa mfano na kuigwa maana kabla ya kutangaza nia rasmi aliamua kujiuzulu nafasi yake Unaibu katibu mkuu ili kuweka mazingira ya haki kwa wote maana kwa kujua kwamba kwa nafasi hiyo naye angeshiriki katika vikao vya maamuzi katika kupata wagombea watakao pelekwa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura ili apatikane mmoja tu wa kupeperusha bendera ya chama.
Pili, ni ile hotuba yake ya kutangaza nia pale Dodoma, ilikuwa ni hotuba iliyobeba ndoto nyingi na maono hai kwa kila Mtanzania wa tabaka zote, Ni hotuba iliyogusa makundi yote ya jamii ya Watanzania, kuanzia watoto, wakina mama, wazee na kwa Kiasi kikubwa kundi la Vijana na changamoto zinatukabilii na kwa namna gani zitatatuliwa.
Hotuba ile imetoka mwangaza na picha halisi inayoakisi turning point ya kuitafuta miaka 50 mingine ya taifa letu toka tupate Uhuru wetu wa bendera,
Ni hotuba iliyolifanya taifa lisimame hasa pale mikakati ya kupata Uhuru wa kiuchumi ilipokuwa ikizungumziwa na kwa jinsi gani itatekelezeka, mfano, vijana kufanya kazi kwa shift.
Hotuba imetupa uhakika wa kutupeleka kuwa wananchi wa kipato cha kati na kujijengea uwezo wa kumiliki Uchumi wetu wenyewe.
Tatu, na hapa nimethibisha kuwa Mwigulu Nchemba ni kiongozi tunayepaswa kumwamini kwa kauli zake na matendo maana amekuwa akiheshimu na kufuata taratibu na kanuni za chama na serikali kwa ujumla.
Upande wa Serikali hajawahi kutumia gari ya serikali kwa shughuli zake binafsi au za chama.
Nadhani mtakumbuka walipokuwa wakiwasiliana na Katibu mkuu wa chama kama bosi, alimwambia Mikutano yako ya kujenga chama ina kama mlengo wa kujipigia kampeni naye aliacha mara moja.
Vivyo hivyo katika zoezi hili la kutafuta wadhamini, amekuwa akitimiza masharti ya fomu ya udhamini kwa kufuata na ku observe taratibu na kanuni tulizojiweka ndani ya chama chetu.
Mwigulu amedhihirisha kuwa ni kiongozi anayeishi katika kauli zake na matendo pia na amesadifu kauli mbiu yake ya "Mabadiliko Ni Vitendo, Wakati Ni Sasa"
Mwigulu Nchemba Tunakuamini Utatuvusha 2015-2025
Hatimaye CCM tumepata Kiongozi Atakayepeperusha Bendera yetu
Ahsante sana[/QUOTE
Sawa