Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

mbona kashindwa kudibithi tuu shilingi yetu inaporomoka kila kukichaa yeye na yule mama.ivi akipewa nchii si ndio tutakua kama zimbabwe! !
 
Kuna uzi humu ulimuelezea vizuri sana, ila ninayokumbuka sasa ni:

1) hilo la kuwa amewahi kuwa mbunge wa arusha - jimbo ambalo linachukuliwa kuwa ni gumu kushinda kama hukubaliki, tena ukichukulia kuwa siyo mwana wa arusha

2) amekuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa mara kwa miaka 5

3) kwa sasa ni mbunge wa bunge la EAC

4) alithubutu kupinga hadharani vitendo vya ufisadi mwaka 2008 akishinikiza watu kujivua gamba


Nadhani 1-3 pia zinajibu swali lako kuhusu uzoefu wake ktk siasa za Tanzania

Ila nimegundua tunatofautiana kimtazamo kidogo. Tofauti niliyoiona kwako na mimi kuhusu Makongoro ni kwamba wewe unamwangalia kiushindani ziaidi, ndo maana unajaribu kumlinganisha na mwigulu au mbatia kiutendaji. Wakati mimi namuangalia katika mtazamo wa kuokoa chama na hii nguvu ya ukawa, ukizingatia ccm imeishachafuka sana usoni mwa watanzania kwa hizi skendo za ufisadi na rushwa.

kweli tunatofautiana kimtazamo. Mimi habari za chama sina kabisa. Ukawa wakileta mtu mzuri ndo watakuwa chama changu, ccm wakileta mtu mzuri ndo kitakuwa chama changu. Hakuna chama chenye sera bora ziadi ya kingine. Tunahitaji tu mtu wa kutupigisha kwata tubadilike tuweze kuendelea. Tuna shida sana ya uongozi.
 
kweli tunatofautiana kimtazamo. Mimi habari za chama sina kabisa. Ukawa wakileta mtu mzuri ndo watakuwa chama changu, ccm wakileta mtu mzuri ndo kitakuwa chama changu. Hakuna chama chenye sera bora ziadi ya kingine. Tunahitaji tu mtu wa kutupigisha kwata tubadilike tuweze kuendelea. Tuna shida sana ya uongozi.

BTW umeona uzi wa kilichojiri huko mwitongo, ngoja nikakumention kule maana sijakuona kabisa, hope hujauona
 
Yule MC katika shughuli ya Mhe. kutangaza nia pale Dodoma kwa kweli aliiwezea ile Shughuli maana aliichangamsha kupita maelezo, kwa kweli ilifana sana, je kuna mtu ana contact zake nataka nimtumie nami nikiwa natangaza nia kijijini kwetu LAELA, SUMBAWANGA
 
alijali muda sana alienda kumtoa yule askofu anayeomba bila kuzingatia muda
 
MC alipoozesha ile shughuli hafai yule bora Mr. Kibonde
 
MWIGULU NCHEMBA JEMBE LISILOVUNJIKA MPINI,MGOMBEA PEKEE ATAKAYE IVUSHA TANZANIA KIUCHUMI/MAENDELEO YA UHAKIKA.


"NITAWAVUSHA", "Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa".- Ni maneno mazito yaliyosikika masikioni mwa Watanzania siku Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mwigulu Nchemba alipotangaza rasmi nia ya kutaka kuteuliwa na chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisikika akipaza sauti na kusema "Nimetathmini vya kutosha, nimejiridhisha vya kutosha hivyo ahadi yangu kwa Watanzania nitawavusha … ninaomba mniamini na mniunge mkono kwani nitawavusha". Moja kati ya mambo aliyozungumza na kuwagusa wananchi ni pamoja na kuifanya nchi iwe katika kipato cha kati, kujenga taifa linalojitegemea pamoja na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wao, kukomesha rushwa sambamba na kuongeza ajira kwa vijana kwa kufufua viwanda vya zamani na kuanzisha viwanda vipya.

Baadhi ya wananchi walisikika wakipaza sauti zao huku wengine wakisema "tunaimani nawe Mwigulu" wakionesha kuridhishwa na utendaji kazi wake sambamba na hotuba aliyoitoa siku hiyo ya kutangaza nia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Mmoja wa wananchi waliopata nafasi ya kufika ukumbini hapo alisema ni wazi kuwa Mwigulu ndio chaguo jema kwa sasa kwani ana mambo mengi yanayombeba hasa ukizingatia hajawahi kukutwa na kashfa yoyote wala kukiuka maadili ndani ya chama chake.

Imani waliyoonesha wananchi hao kwa kijana machachari anayekubalika na wengi ambae amepata nafasi mbalimbali tena za juu ndani ya chama chake (CCM) zikiwemo Unaibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi pamoja na kuwa Naibu Waziri wa Fedha, hii ni kutokana na jitihada zake za kuwatetea wanyonge pamoja na kusimamia na kutekeleza ilani ya chama chake kikamilifu.

Wananchi wengi wamekuwa wakilalama ni kiongozi gani ambaye ataweza kusimama na kukomesha rushwa, ndipo Mwigulu alipojipambanua na kukemea vikali rushwa hata katika Sakata la Escrow lililosababishia serikali kukosa kodi kutoka katika bilioni 303 zilizochotwa kinyemela katika akaunti hiyo kijana huyu alitumia uwezo na nguvu zake kupingana na rushwa.

Nchemba hakuonesha unafiki kwa kumwonea mtu aibu hata kama ni wa chama chake (CCM), bali alisimamia ukweli katika jambo hilo na kuhakikisha haki inatendeka bila kumwonea au kumpendelea mtu yoyote mradi haki itendeke na kila mmoja aadhibiwe kwa makosa yake.

Alipotangaza nia akanukuliwa akisema "I will have zero tolerance on corruption" (sitavumilia rushwa) , haiwezekani rasilimali za taifa ziwanufaishe wachache wakati hospitali hazina madawa na shule zipo katika hali mbaya".

Kauli hiyo iliyotolewa na wananchi (tunaimani nawe) imezidi kupata mashiko baada ya kuona jinsi kiongozi huyu anavyoichukia rushwa na kusema waziwazi hatakuwa na uvumilivu hata kidogo na watu wanaotoa ama kupokea rushwa.

Akaongeza kuwa sheria iliyopo dhidi ya rushwa akiingia madarakani ataibadilisha mara moja ili kupambana kikamilifu na rushwa na ikibainika hakuna swalia mtume adhabu itakayotolewa ni kifungo kwani hakuna sababu ya wachache kunufaika kwa njia zisizo sahihi huku walio wengi wakiendelea kutaabika.

Alipokuwa akihutubia wananchi waliofurika ukumbini hapo kumsikiliza, Mwigulu alikuwa akiainisha na kufafanua agenda zake kwa umakini pasipo kusoma maelezo kwenye makabrasha tofauti na viongozi wengine waliotangaza nia wakitumia muda mwingi kutoa maelezo yaliyomo kwenye makaratasi, hii ikionesha umakini wa aina yake na namna alivyojipanga kuwatumikia Watanzania.

Nakumbuka kiongozi huyu alijinasibu akisema anafahamu vyema ajenda za Watanzania ndio maana ana dhamira ya dhati ya kuwavusha kutoka hapo walipo na kuwafikisha sehemu nzuri kwa kuwawezesha kumiliki uchumi wao.

Pasipo kupepesa macho wala kutikisa masikio Mwiguli alisema urais hauna uzoefu na kiongozi hapimwi kwa alichotenda hapo awali bali kwa anachoweza kufanya kwa wakati huu hivyo umri pamoja na uzoefu sio hoja za msingi na hazina mashiko.

Ni dhahiri kiongozi huyu anakubalika na makundi yoye yaani vijana, wazee na hata watoto kutokana na kuisimamia kikamilifu serikali na kuwa na shauku kubwa ya kuleta maendeleo kwa kasi katika taifa la Tanzania.


Chanzo:
 
MWIGULU NCHEMBA JEMBE LISILOVUNJIKA MPINI,MGOMBEA PEKEE ATAKAYE IVUSHA TANZANIA KIUCHUMI/MAENDELEO YA UHAKIKA.

Na Rachel Gabagambi
"NITAWAVUSHA", "Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa".- Ni maneno
mazito yaliyosikika masikioni mwa Watanzania siku Naibu Waziri wa
Fedha na Uchumi Mwigulu Nchemba alipotangaza rasmi nia ya kutaka
kuteuliwa na chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisikika akipaza sauti na kusema “Nimetathmini vya kutosha,
nimejiridhisha vya kutosha hivyo ahadi yangu kwa Watanzania
nitawavusha … ninaomba mniamini na mniunge mkono kwani nitawavusha”.
Moja kati ya mambo aliyozungumza na kuwagusa wananchi ni pamoja na
kuifanya nchi iwe katika kipato cha kati, kujenga taifa
linalojitegemea pamoja na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi
wao, kukomesha rushwa sambamba na kuongeza ajira kwa vijana kwa
kufufua viwanda vya zamani na kuanzisha viwanda vipya.
Baadhi ya wananchi walisikika wakipaza sauti zao huku wengine wakisema
"tunaimani nawe Mwigulu" wakionesha kuridhishwa na utendaji kazi wake
sambamba na hotuba aliyoitoa siku hiyo ya kutangaza nia katika ukumbi
wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Mmoja wa wananchi waliopata nafasi ya kufika ukumbini hapo alisema ni
wazi kuwa Mwigulu ndio chaguo jema kwa sasa kwani ana mambo mengi
yanayombeba hasa ukizingatia hajawahi kukutwa na kashfa yoyote wala
kukiuka maadili ndani ya chama chake.
Imani waliyoonesha wananchi hao kwa kijana machachari anayekubalika na
wengi ambae amepata nafasi mbalimbali tena za juu ndani ya chama chake
(CCM) zikiwemo Unaibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi pamoja na
kuwa Naibu Waziri wa Fedha, hii ni kutokana na jitihada zake za
kuwatetea wanyonge pamoja na kusimamia na kutekeleza ilani ya chama
chake kikamilifu.
Wananchi wengi wamekuwa wakilalama ni kiongozi gani ambaye ataweza
kusimama na kukomesha rushwa, ndipo Mwigulu alipojipambanua na kukemea
vikali rushwa hata katika Sakata la Escrow lililosababishia serikali
kukosa kodi kutoka katika bilioni 303 zilizochotwa kinyemela katika
akaunti hiyo kijana huyu alitumia uwezo na nguvu zake kupingana na
rushwa.
Nchemba hakuonesha unafiki kwa kumwonea mtu aibu hata kama ni wa chama
chake (CCM), bali alisimamia ukweli katika jambo hilo na kuhakikisha
haki inatendeka bila kumwonea au kumpendelea mtu yoyote mradi haki
itendeke na kila mmoja aadhibiwe kwa makosa yake.
Alipotangaza nia akanukuliwa akisema “I will have zero tolerance on
corruption” (sitavumilia rushwa) , haiwezekani rasilimali za taifa
ziwanufaishe wachache wakati hospitali hazina madawa na shule zipo
katika hali mbaya”.
Kauli hiyo iliyotolewa na wananchi (tunaimani nawe) imezidi kupata
mashiko baada ya kuona jinsi kiongozi huyu anavyoichukia rushwa na
kusema waziwazi hatakuwa na uvumilivu hata kidogo na watu wanaotoa ama
kupokea rushwa.
Akaongeza kuwa sheria iliyopo dhidi ya rushwa akiingia madarakani
ataibadilisha mara moja ili kupambana kikamilifu na rushwa na
ikibainika hakuna swalia mtume adhabu itakayotolewa ni kifungo kwani
hakuna sababu ya wachache kunufaika kwa njia zisizo sahihi huku walio
wengi wakiendelea kutaabika.
Alipokuwa akihutubia wananchi waliofurika ukumbini hapo kumsikiliza,
Mwigulu alikuwa akiainisha na kufafanua agenda zake kwa umakini pasipo
kusoma maelezo kwenye makabrasha tofauti na viongozi wengine
waliotangaza nia wakitumia muda mwingi kutoa maelezo yaliyomo kwenye
makaratasi, hii ikionesha umakini wa aina yake na namna alivyojipanga
kuwatumikia Watanzania.
Nakumbuka kiongozi huyu alijinasibu akisema anafahamu vyema ajenda za
Watanzania ndio maana ana dhamira ya dhati ya kuwavusha kutoka hapo
walipo na kuwafikisha sehemu nzuri kwa kuwawezesha kumiliki uchumi
wao.
Pasipo kupepesa macho wala kutikisa masikio Mwiguli alisema urais
hauna uzoefu na kiongozi hapimwi kwa alichotenda hapo awali bali kwa
anachoweza kufanya kwa wakati huu hivyo umri pamoja na uzoefu sio hoja
za msingi na hazina mashiko.
Ni dhahiri kiongozi huyu anakubalika na makundi yoye yaani vijana,
wazee na hata watoto kutokana na kuisimamia kikamilifu serikali na
kuwa na shauku kubwa ya kuleta maendeleo kwa kasi katika taifa la
Tanzania.
 
Mkuu huenda JokaKuu naye amehesabiwa na Lowassa? Uhuni wote wa Lowassa pale Amri Abeid bado Lowassa ni kielelezo kwa kulinganisha na wengine?

..LOL!!

..sijahesabiwa.

..hata UKAWA wakileta mgombea wao, nitampima kwa vigezo hivyo nilivyovieleza ktk post yangu ya awali.

..kuna makosa nimeyaona ktk mkutano ule wa Lowassa. sasa natagemea wagombea wengine wasirudie makosa yale.
 
Mwigulu kaeleweka vizuri sana, timu Lowassa mkajipange.Maana kumbe pesa haziwezi kununua hotuba nzuri, inahitaji pia uwezo wa mtoaji hotuba.Lowassa kwa hotuba ana F ndio maana mnahangaika saizi na hotuba wenzenu kwani kwa kasi hii mtaishiwa pesa bure.

duh mkuu mbona mkali hivi.. kwanza umenikosea sana kuniita timu lowasa i cant be team lowasa NEVER!!, Pili.. ah ngoja niache tu tusije tukaanza kubishana bila fact..
 
Back
Top Bottom