Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Mtu anikumbushe akiwa naibu waziri amefanya nini hadi sasa
 
Nilivyomsikiliza Mwigulu Nchemba kaongea mambo mengi ya msingi ana uwezo wa kuongoza taifa letu anamzidi kwa mbali Dr.Slaa nawashauri UKAWA chaguo letu ni Mwigulu.
 
Last edited by a moderator:
Mi huku ccm bado hadi sasa hawajanishawishi nasubiri wajao
 
Hajazungumzia AFYA, ELIMU, UFISADI na RUSHWA, MIUNDO MBINU, USALAMA WA NCHI.

HAMNA RAISI HAPO. ABAKI TU AKAFUNDISHE UCHUMI UDSM.
 
Acha hizo bwana....weka akiba ya maneno nitakukumbusha siku moja.

Hahahahaha Lowassa akiwa Rais wa Tanzania nahama nchi.. Yule goigoi atatuaibisha aisee. Tutakuwa wajinga kuingiza jambazi Ikulu
 
Hivi vitu anavyoongea leo Mwigulu kila mwaka kambi ya uponzani inaishauri serikali kuvifanya..namshangaa mwigulu leo amekubali ile bajeti aliyoichanachana bungeni

Kweli nimeamini Tuwe na akiba ya maneno
 
Akitaka kunishawishi aniambie kinaga ubaga atadhibiti vp wala rushwa na ufisadi
 
Pics Tafadhali .........
image.jpg
 
Ha ha ha anaichamba serikali yake, huyu ni mwepesi sana
 
Wa mke wa Mwigulu.. Kumbe we humjui Juliana Shonza??

Namjua kidogo sana....ohooo kumbe unamzungumzia bibie?Kwahiyo nae kaolewa?
Inamaana alivyochoropoa za mtoa hotuba ndio maana hakuna kitu tena?
 
PLS usimlinganishe CAMARADE thomasi sankara na huyu...yule alikuwa zaidi ya huyu...pls..
Ndo maana nikasema kama idea zake akiziweka kwenye matendo kweli kwa mfano kupunguza matumizi,kuvaa vya pamba ya kwetu.Nimemsoma THOMAS SANKARA kiukweli sijaona mfano wake,maana mawaziri walipanda economy class kwenye ndege,na mengine kibao katika kupunguza matumizi
 
Huyu jamaa sasa anaonyesha ufala anaponda mfumo wa ukusanyaji kodi wakati yeye ndo alikuwa anahusika
 
Back
Top Bottom