Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Jamaa kajitahidi kwa kweli lakini tatizo ndani ya ccm ni ngumu sana kutekeleza anayoyasema. Wasubiri Moto utakaowashwa na UKAWA watajuta kuufahamu upinzani nchi hii.
 
Baada ya yeye kuingia MOF hebu cheki dola inavyotugaragaza
Hhahahaha yeye siyo Rais,labda anatoaga views zake halafu hazifuatwi sasa atafanya nini?Wampe Rungu ili AIVUSHE TANZANIA
 
Hahahaha,hizi ligi zenu huku siziwezi.Nisijetia neno bavicha wakaniletea kigodoro bure!

Teh Teh Bavicha wana muunga mkono Mwigulu wamechoshwa na Profesa Mbowe...
 
Maneno meeeengiiiii........ Sifa kibaaaaoooooo..... Kwa nafasi yake ya uwaziri kafanya nn??????

Fedha inashuka thamani kwa ajili ya utegemezi ,kwamba tunanunua kuliko kuuuza.. Serikali anayo iongoza si ndo imetufikisha apa ? Si wao ndo wameua viwanda vyote ? Si wao ata madini na ifadhi zetu wameshindwa kuendeleza ....anamlalamikia nani sasa?.

Cabinet ndio yakulaumiwa sio Mwigulu pekee.. Labda yeye anatoa mawazo mazuri huko lakini yanapuuzwa.
 
Sio wao tu, mi nilipofika Mzumbe Un. Watu wa BBA BPA BAF wote tulisoma ECO 100 chini ya injini moja inaitwa Kuzirwa, Prof.

Well! Kinachosumbua hapa ni BOT kutokuweka akiba ya kutosha ya dola ili kukabiliana na upungufu wa dola unapotokea nchini. Demand na supply ndo hapo zinapofanya kazi. Huu ni uhuni wa mafisadi ili yapate faida kubwa kutoka kwenye sh.yetu. piga kelele kataa wezi kwenda ikulu.
 
Maneno meeeengiiiii........ Sifa kibaaaaoooooo..... Kwa nafasi yake ya uwaziri kafanya nn??????

Fedha inashuka thamani kwa ajili ya utegemezi ,kwamba tunanunua kuliko kuuuza.. Serikali anayo iongoza si ndo imetufikisha apa ? Si wao ndo wameua viwanda vyote ? Si wao ata madini na ifadhi zetu wameshindwa kuendeleza ....anamlalamikia nani sasa?.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mwigulu haongozi serikala wala wizara. Yeye ni naibu waziri tu.

Alikuwa anatoa maoni yake as mchumi na changamoto alizoziona Serikalini.

Kaongea vizuri tumpe hongera yake.
Cha kujiuliza je ataweza kutekeleza?? Kwa sababu sio mara ya kwanza kusikia maneno ya kutia moyo kama hayo.

Maoni tu.
 
Teh teh napenda unavyozicheza karata zako.. Wewe unasubiri mgombea ateuliwe ndio uanze kuunga mkono
Unajua muda huu niwakuwa makin kuwa sikiliza na kuwapima bado wanatangaza nia kwahio wacha wagombea watakapo subiria mikasi ya wananch hapo ndipo penye kujiweka sawa
 
Mleta mada timu lowasa nini maana aliyosema lowasa jana yamekufurahisha lkn aliyosema Mwigulu yanakuchoma. Songa Mwigulu tupo nyuma yako
 
Back
Top Bottom