Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron

Aaa wapi! kwa hili unajikosha na kutetea bihashara zenu chafu! kwani hatujui jinsi mnavyo fanya reparkaging? Acha kabisa!!!
 
Naunga mkono hoja hakuna aliye msafi CCM.....Nchemba ameipondea serikali,kapondea chama chake analalamika mfumo mbovu anamlalamikia nani wakati naye yumo ndani ya huo mfumo? Amefanya nini yeye kama yeye kuleta mabadiliko katika mfumo wao mbovu? Au anasafisha kikombe nje wakati ndani ni kichafu? Hana jipya naye ni wale wale.......
Anailalamikia serikali yake na chama huu ni ujinga angejiondoa kwanza huko ccm sasa wapinzani tunalalamika na watawala nao wanalalamika huu ni usanii tuuu
 
Ww ni mtanzania gani ambaye mtoto wako au mzazi wako anaumwa kisha unaenda hosp kwa matibabu unaambia dawa hakuna kanunue dawa hapo duka jirani na hosp then unakuta dawa ambazo zilistahili kuwepo hospitali?
 
Hahaha labdo ndo tez lilishaanza, el ameshauri wakapme japo majibu yatakuwa siri ya dr na mgonjwa
 
kuna jamaa mmoja anataka kugombea ubunge kupitia ccm nae anatumia kauli hii "NITAWAVUSHA" nishamshtukia kumbe team mwigulu

Wanataka kutuvusha kutupeleka wapi mkuu .watanzania wasitegemee mabadiliko au maendeleo yoyote chini ya utawala wa ccm tena wameshindwa kwa miaka 53 miaka 5 watafanya miujiza?
 
Tusiwe wajinga wa kufikri yeye alikuwa anazungumzia wizi wa dawa mahospitalini na kwamba dawa hizo hupelekwa kuuzwa kwe maduka ya nje hivyo amewalenga wale wanaoiba dawa na si wengine.
 
Jana na leo..!! Ndio maana watafungwa endapo watakachofanya sicho. Hakusoma hotuba iliyo haririwa alisema anayoyajua na kuyaishi kama mtanzania wa kawaida.
 
Wakati tu anaingia ulikuwa mbaya, kumbuka wakati JK anaingia na tatizo la majambazi japokuwa sio like for like lakini inawezekana kipimdi hiki ndio Dollar na Pound zimekuwa strong.

Ndio tuwape nchi wachumi watusaidie kwa kuweka mikakati ya muda huku wakiwa wanaset mipango ya muda mrefu, hatuna shida na wataalam wa sanaa kwani kina Diamond wanafanya vizuri kimataifa.

Yap ulikuwa mbaya na kwake yeye umekuwa mbaya zaidi na zaidi, si mwanauchumi yeye atleast ningetegemea angeokoa jahazi lisizame kabisa lakini kwake yeye tunaona ndo tunazidi kuzama kabisa, yeye ni msafi sawa unakumbuka majibu yake ya Escrow account pale bungeni zaidi ya kutupiga changa LA macho? yeye si mpiganaji wa rushwa mbona ameshindwa kushughulikia hayo machache kny utawala wake mdogo wa uwaziri ndo seuze nchi ataiweza?? Analalamika na mfumo mbovu wakati naye yumo ndani? Basi kifupi naye ni mbovu.......... Sera hizi hizi ndo zilimuingiza Kikwete matokeo yake leo tunalia tu....... Hakuna jipya kabisa wote ni wale wale.........
 
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.

'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.

Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.

Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni

Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.

Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu

Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa

Dr Kilawa the Iron
Dr hawa viongozi wetu hawajui hata regulations zinazoandaliwa na mawaziri wenyewe achilia mbali sheria zinazotungwa na bunge, ila si shangai kulisikia hili ni watu wengi tu hawafahamu mambo mengi sana kuhusu taratibu za nchi niliwahi kuhudhuria semina moja mtoa semina alikuwa mhadhili wa chuo kimoja hapa nchini alimimina matango ambayo hayapo popote hapa nchini japokuwa semina ilikuwa specific sana mpaka ikapoteza maana

kwahiyo Mwigulu kukurupuka sishangai ndiyo cream ya ccm iliyopo.
 
Wanataka kutuvusha kutupeleka wapi mkuu .watanzania wasitegemee mabadiliko au maendeleo yoyote chini ya utawala wa ccm tena wameshindwa kwa miaka 53 miaka 5 watafanya miujiza?

Slaa atagombea tena mwaka huu?
 
Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.

Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.

NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.

JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.

Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.

NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.

Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.

Pasco
wakati muda wote nasoma sikujua kuwa nasoma bandiko la pasco hadi nilipofika hapo ulipojitambulisha, ki ukweli mi naona mwigulu kaamua kutuvusha kikwelikweli, kikwazo ni kuwa ccm hawati mtu aina ya mwigulu, mama yangu kila siku analia akimkumbuka sokoine
 
Sasa ni zamu ya Mwigulu Nchemba na anatarajia kutangaza nia kuanzia saa 9 mchana wa leo na atafanya hivyo live kupitia star tv akiwa Chuo cha Mipango, Dodoma.
View attachment 255981
Muda: saa 9 Alasiri hadi Saa 12 Jion.
Mahali: Chuo cha Mipango Dodoma.
Ukumbi: Mwl. Nyerere Hall

KAULI MBIU YA MWIGULU: MABADILIKO NI VITENDO, WAKATI NI SASA

Mwigulu anadai alibeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.

Pia naona Mwigulu anamponda EL kiani kwa kusema watu wanajisifu kuwa wamekuwepo serikalini muda mrefu wakati huo huo wamelisababishia Taifa hasara kubwa katika muda huo mrefu waliokaa serikalini.

Inasikitisha kumuona analalamikia mambo mengi yanayoendelea chini ya serikali hii ya CCM wakati kila siku wanawakejeli wapinzani wanapolalamikia na kuhoji mambo hayo Bungeni.

Kwa kifupi,Mwigulu leo anaivua nguo CCM hadharani na zaidi leo anamponda kiana mh.sana na pia anaonyesha kuwa Mkulu na chama chake wamekuwa ni dhaifu.

kilichonishangaza kwa huyu jamaa ni kulalamika

wewe ni naibu waziri wa fedha alafu unalalalamika ......................................hawa ndio dizaini ya aliyopo madarakani

sina uhakika kama kawaeleza watanzania zile pesa za stanbink zilichuliwa katika mazingira gani amabyo kama naibu waziri wa fedha ameshindwa kujua hiiiiiiiii ndilo swali langu kwa huyu kijana na kama haikuwa rushwa je zililipiwa kodi haya mabo watanzania hatutakiwa kuyaacha yapite hivi
 
Yeye hajakaa mda mrefu serikalini msimfananishe na akina Lowassa isitoshe hata mda huo mfupi aliokaa madarakani hakuwa na maamuzi. Ila pale alipopata nafasi kidogo motto wake bungeni hata sisi wa upinzani tunamkubali. Kweli Lowassa amechemsha angesubiri wamalize wote apate cha kuongea.
 
Nadhani mwigulu kaeleweka kwa watanzania wa kawaida sana! Katika mazingira ya kawaida sana." Kama nyote mliokuja hapa mnataka kurudi mjini nauli ya daladala itapanda" ni lugha nyepesi inayoeleweka kwa Watanzania wengi.
 
Wanataka kutuvusha kutupeleka wapi mkuu .watanzania wasitegemee mabadiliko au maendeleo yoyote chini ya utawala wa ccm tena wameshindwa kwa miaka 53 miaka 5 watafanya miujiza?
mwigulu na huyo jamaa wako serious kwakweli tatizo mfumo wa chama chao ni shida
 
wakati muda wote nasoma sikujua kuwa nasoma bandiko la pasco hadi nilipofika hapo ulipojitambulisha, ki ukweli mi naona mwigulu kaamua kutuvusha kikwelikweli, kikwazo ni kuwa ccm hawati mtu aina ya mwigulu, mama yangu kila siku analia akimkumbuka sokoine
JK nadhani katika succession plan Huyo ni mmojawapo unadhani alipata unaibu Katiba Mkuu kwa bahati Mbaya?
Uliona alivyokuwa awekwa karibu na marais Wastaafu?
 
Nasikia mabasi mengi jana yalokuwa yakienda Arusha toka mikoa tofauti yalikodiwa na team Lowassa tax lodge etc. Who paid them where the find come from? Why they funded it...!!?
 
Back
Top Bottom