kabugira
JF-Expert Member
- May 14, 2014
- 1,186
- 659
TUTAWANYANG'ANYA LESENI, TUTAWAFUNGA JELA.
'Hakika usilolijua ni kama usiku wa giza" Nimeshangazwa sana na kauli ya Mh Mwigulu ambaye ni naibu waziri wizara ya fedha.
Ameonesha wazi hajui ni dawa gani zinazoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya madawa ya binadamu katika nchi yake.
Siwezi kushangaa sana japo kanisikitisha kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa hajui tofauti ya Dawa zinazokuwepo hospitalini na zile ambazo wamiliki wa maduka wanauza.
Kabla hajalizungumza hili kama mtia nia alitakiwa kujiuliza kwa wadau wa Afya wampe tofauti lakini pia hili jibu kuwa wao hawatibiwi hapa kwetu bali ni ughaibuni
Eti "Tutawanyang'anya leseni na kuwafunga" japo hao wamesomeshwa kwa kodi za wa Tanzania hawa si wengine ni madaktari, najiuliza huyu jamaa kala maharage ya wapi hadi anashindwa kuelewa dawa zinazomilikiwa na serikali zina nembo ya MSD na hizi haziuzwi katika la madawa kamwe.
Namshari afuatilie namna dawa hizi zinavyotolewa huko mahospitali na ajiulize kwanini madaktari wanawaonesha wagonjwa sehemu ya kununua kuliko kukurupuka.
Shame on u Mwigulu
Msema kweli haogopi kufungwa wala kufa
Dr Kilawa the Iron
Aaa wapi! kwa hili unajikosha na kutetea bihashara zenu chafu! kwani hatujui jinsi mnavyo fanya reparkaging? Acha kabisa!!!