Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
slaa atagombea tena mwaka huu?
Chadema wagombea Urais wenu wako wapi?
Anailalamikia serikali yake na chama huu ni ujinga angejiondoa kwanza huko ccm sasa wapinzani tunalalamika na watawala nao wanalalamika huu ni usanii tuuu
Nionavyo mimi mpaka sasa kama mmoja wa hawa waliotangaza nia akija kuwa raisi:
Lowassa: Masikini hawana lao, tutakua taifa lenye matajiri sana wachache na maskini sana wengi.
Wassira: Maendeleo katika sekta zote yataenda polepole mno hata kusimama. Sijamwona kama ni visionary leader mwenye uwezo wa kusukuma maendeleo yaendani na kasi ya maendeleo ya kisasa. Kabaki ki zama za kale sana.
Mwigulu: Akili anayo, uwezo anao ila uzoefu katika maswala ya international relations na diplomacy ambayo ni muhimu sana pia kwa maendeleo, je atachukuliwa seriously na the likes of Putin, Angela Merkel, Obama, Kagame, Uhuru e.t.c. Nahisi anaweza onekana bwana mdogo sana na kuwa side lined sometimes. Unajua hizo meetings status ya mtu ina matter sana.
Nilishawahi kuandika hapa kipindi ambako nilibahatika kukaa na Jeffrey Sachs kutokana na kum accompany ndugu yangu ambaye ni Prof. Ilikua informal meeting to kwenye lobby ya hotel, jumla tulikua watu 5 tu. Yani mimi nilbaki kukaa kimya na kusikiliza watu na taaluma zao wakishusha vitu. Hawakunionyesha dharau, lakini nilijiona kabisa huu sio uwanja wangu. Nina fikiri Mwigulu anaweza patwa na hili pia kimataifa kutokana na umri.
Thats my opinion.
Kwa Nondo hizi Padri slaa kamwe hagusi ikulu...labda akaombe kugombea Urais wa ma Padri wastaafu Tanzania....
Anailalamikia serikali yake na chama huu ni ujinga angejiondoa kwanza huko ccm sasa wapinzani tunalalamika na watawala nao wanalalamika huu ni usanii tuuu
Hakufoji,ila alienda kurudia shule kwa jina la mtu mwingine aliyekuwa kaacha shule,mimi namsifu maana alikuwa ana kiu ya Elimu,na yeye alitumia jina tu ila kila kitu mitihani alifanya mwenyewe,nashangaa watu wanamzonga mwigulu kwa kurudia darasa kwa jina la mtu aliyeacha shulekama alifoji vyeti vya darasa la 7 siyo yeye, ni wazazi wake labda kama alishazidi miaka 18. Yeye ni geniuos. Imagine ubongo wote ule ungeishia machungani.
The gay is smart.
sijui ugaidi wala ugoni wa mwigulu - ni siasa kama zingine lakini nikimtathmini kwa hotuba yake, Mwigulu amempita EL kwa kilomita nyingi sana. Kaka amepanga hoja zake vizuri. "Tone" na ujumbe vinashabihiana, kasema vipaumbele vyake na jinsi ya kuvitekeleza, hajanisomea neno moja baada ya jingine kana kwamba kaandikiwa - anajua anachokisema, ana upeo mkubwa (IQ). Mpaka sasa kwangu EL ana point 0, Mwigulu 1. Nachotaka kujua tu sasa ni nani mshika remote wake. Washika remote wa EL nawajua, na ndo maana nikifikiria kumpa kura vinywele vinanisimama. Tukio la Nchemba pia limenionyesha ni kwa kiasi gani mbwembwe na ufahari kwa EL vilitumika kufunika udhaifu binafsi wa EL kama mwanasiasa. Nchemba amevuta hisia zangu bila helikpta wala diamond platinum. Tukiwa chuo nilikuwa namchukulia poa tu, lakini kwa jinsi alivyoweza kuweka nia na juhudi katika maono yake ya kisiasa naona ni mtu anayeweza kujiongoza na kusimamia kile anachokiamua. Huo uwezo ni vigumu kuuona kwa watu hawa wagombea wazee. Kupanda kwao kisiasa hakukuhitaji bidii kubwa. Kuingia kwenye mfumo wa siasa wakati ule haikuwa kazi ngumu na walikuwa wachache kulingana na mahitaji ya nchi kwa wakati ule, lakini kwa rika la Nchemba si kazi rahisi kuwapiga vikumbo hawa wazee na kutoboza bila kujiamini. Kwangu mimi hii ni sifa ya kiongozi. Nawasubiri kina Membe ila katika hawa wawili Mwigulu ameamsha hamu ya kusikiliza wagombea kwa makini.
Anachekesha sana huyu. Mfumo mbovu lakini miaka yote hii amekaa kimya huku akifaidi nafasi ya juu ndani ya chama bila jitihada zozote zile za kubadili huo mfumo mbovu wa ndani ya chama. Amekuwemo ndani ya chama kwa miaka mingi sasa na na hadi kaingia Serikalini kama Naibu Waziri wa Fedha.
Miaka yote hii kimya hakutoa kauli ya kulaani mfumo mbovu hadi leo hii anapotaka kugombea urais ndio anauzungumzia mfumo mbovu ili kutuzuga Watanzania kama ilivyo kawaida ya MACCM. Mwigulu ulikuwa wapi 2005 kuzungumzia mfumo mbovu ndani ya MACCM na kuwashinikiza viongozi wa juu na wanachama kuuvunja mfumo huo na kuufanya uwe mzuri kama ambavyo wewe ungependekeza? Ulikuwa wapi 2010? Ulikuwa wapi 2012?
Hapana tumechoshwa na uongo wenu wa kukaa kimya huku nchini inaenda mrama miaka nenda miaka rudi kisha yale ambayo mnayajua kwamba ni mabaya kuja kuyazungumza pale mnapotaka kupata Urais ili mtuzuge Watanzania. Mkishaingia Ikulu speed ya kuendelea kuliangamiza Taifa inazidi kupamba moto.
Wewe ni Mojawapo ya madaktari wezi Ngariba mkubwa wewe