Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Na nyie muache kuiba dawa! Mnaua watanzania kwa tamaa zenu za kijinga.
 
Mtoa hoja huwezi geuza jiwe kuwa boflo...wewe msubiri kigwangala wenu...akimaliza Doctor kutia nia yake urudi tena humu kusifia.
 
Anailalamikia serikali yake na chama huu ni ujinga angejiondoa kwanza huko ccm sasa wapinzani tunalalamika na watawala nao wanalalamika huu ni usanii tuuu

Bonge la usaniii kabisaa ,miaka yote yuko humo leo 2015 ndo anaona mfumo mbovu?? Jamani hivi wanatuona sisi ni wajinga eeh?
 
Nionavyo mimi mpaka sasa kama mmoja wa hawa waliotangaza nia akija kuwa raisi:

Lowassa: Masikini hawana lao, tutakua taifa lenye matajiri sana wachache na maskini sana wengi.

Wassira: Maendeleo katika sekta zote yataenda polepole mno hata kusimama. Sijamwona kama ni visionary leader mwenye uwezo wa kusukuma maendeleo yaendani na kasi ya maendeleo ya kisasa. Kabaki ki zama za kale sana.

Mwigulu: Akili anayo, uwezo anao ila uzoefu katika maswala ya international relations na diplomacy ambayo ni muhimu sana pia kwa maendeleo, je atachukuliwa seriously na the likes of Putin, Angela Merkel, Obama, Kagame, Uhuru e.t.c. Nahisi anaweza onekana bwana mdogo sana na kuwa side lined sometimes. Unajua hizo meetings status ya mtu ina matter sana.
Nilishawahi kuandika hapa kipindi ambako nilibahatika kukaa na Jeffrey Sachs kutokana na kum accompany ndugu yangu ambaye ni Prof. Ilikua informal meeting to kwenye lobby ya hotel, jumla tulikua watu 5 tu. Yani mimi nilbaki kukaa kimya na kusikiliza watu na taaluma zao wakishusha vitu. Hawakunionyesha dharau, lakini nilijiona kabisa huu sio uwanja wangu. Nina fikiri Mwigulu anaweza patwa na hili pia kimataifa kutokana na umri.

Thats my opinion.

inawezekana anavyo ila hatujaviona kwa sababu mazingira ya kuvionyesha hayajatokea. Sasa ni bora kumpa membe kwa sababu ana uzoefu kwenye diplomasia? Hatuwezi kupata kiongozi mwenye sifa zote ila kama zile za msingi sana zipo na apewe tu hiyo nafasi, by the time anamaliza miaka mitatu atakuwa ameshapata uzoefu. Umenikumbusha Morgan Tzivangirai alivyoenda ulaya akaenda kuhutubia kwenye podium yenye bendera ya nchi mwenyeji! kalikuwa kaaibu ka aina yake lakini bado aliendelea kubaki na sifa ya kiongozi mahiri wa upinzani. alichokifanya pale hatakirudia tena, alijifunza.
 
Madaktari ni wezi sana wa dawa,,tena sio kufungwa tu INATAKIWA MNYONGWE KABISA,Mnasababisha vifo vya watu kwa kolukosa dawa mahospitalini.
 
Kwa Nondo hizi Padri slaa kamwe hagusi ikulu...labda akaombe kugombea Urais wa ma Padri wastaafu Tanzania....

Mkuu vivyo ndo vitu vya Dr, Mwigulu amedhilisha kua ccm ni chama cha majambazi na hawezi kutimiza anachokiamini ndani ya CCM.
 
Mwigulu yuko vyema kichwani. Lowassa ni show tu za mabraza meni, mission town na ma sista du. Halafu mafisadi papa wanadhamini event.... Pathetic
 
Anailalamikia serikali yake na chama huu ni ujinga angejiondoa kwanza huko ccm sasa wapinzani tunalalamika na watawala nao wanalalamika huu ni usanii tuuu

Ndo maajabu. Watu wanamsifia eti ndo kichwa!!!! Kichwa? Kwenye wizara muhimu alopewa amefanya nini???? Ukiwa mahiri wa kuongea tu cheo.

Anakuja kutupa historia ya familia yake na umaskini walopitia kwao... Utatusaidia nini sisi.. Baada ya kupata amewavusha wangapi kwa nafasi ya uwaziri alokua nao.
 
kama alifoji vyeti vya darasa la 7 siyo yeye, ni wazazi wake labda kama alishazidi miaka 18. Yeye ni geniuos. Imagine ubongo wote ule ungeishia machungani.
Hakufoji,ila alienda kurudia shule kwa jina la mtu mwingine aliyekuwa kaacha shule,mimi namsifu maana alikuwa ana kiu ya Elimu,na yeye alitumia jina tu ila kila kitu mitihani alifanya mwenyewe,nashangaa watu wanamzonga mwigulu kwa kurudia darasa kwa jina la mtu aliyeacha shule
 
So far Lowassa hazuiliki kimkakati wala kimvuto: Ilikuwa inajulikana kuwa Membe angewatanguliza Wassira, Nchemba, Makongoro ili wamsaidie ku-neutralise kasi ya Lowassa. well Wassira amejaribu kuwajengea baadhi ya watu kuwa Wala Rushwa watauza Magogoni wakati UKWELI ni kuwa yeye yuko pale na ESCROW waligawana mchana kweupee... as if haikuwa UFISADI wala Rushwa!!! Wassira ameshindwa kujibu maswali ya msingi na ya kina akaishia kupiga siasa kwenye mambo nyeti ya KATIBA, Kilimo na Ushirika, Uwajibikaji... amshindwa kuainisha vipaumbele vya maendeleo na jinsi gani atavisimamia... uongozi kwake anauchukulia kama styles tu!!!! Ameshindwa kujua kuwa Leadership ndo kila kitu na imeprove kuwa nchi zote zimeendelea si kwa mifumo tu bali utashi na dhamira wa viongozi wao!!! ... Nchemba bado sana, ujana si uhalali wa kupewa nchi; so far Comred Kinana anafanyakazi kubwa sana kuliko yeye mara 1000... anajaribu kutengeneza ugonvi kati ya wazee na vijana; hajui mambo muhimu katika uongozi wa nchi... amedesa nondo za UKAWA kupitia agizo la Chama Tawala aka ACT ndo maana uzi huu wamejaa wasaliti wa mabadiliko wakijaribu kumsupport... Kwa ujumla Membe hajafanikiwa kwani Wassira alikuwa na Nyambari Nyangwine, mnec wa Mbeya na mbunge mmoja wa kanda ya ziwa!!!! Nchemba alikuwa na nani kwenye kutangaza nia? .... Tunawajua walioko Nyuma ya Lowassa ambao ni Mastrategist wakubwa, wana-network yenye nguvu kubwa, wanainfluence hata ya kumtema JK wakitaka... Sioni namna ambayo Lowassa atazuiliwa maana products zake zinajulikana zinatamkika KASHWASA, UDOM, SHULE ZA KATA, aliweza kujiuzulu kwa kuonyesha kuwa cheo ni dhamana pamoja na kuwa hakula hata senti tano! Pinda, Membe et al ambao imethibitika kuwa ni beneficiaries wa ESCROW waligoma kujiuzulu, Sitta amethibitika kuwa ndo mla rushwa mkubwa na kwenye BMK wameharibu sana yeye na wassira ... So far Lowassa ndo pekee mwenye kukubalika ndani na nje ya CCM ...
 
Dawa zinaibiwa sana,usitake kutudanganya hapa,na hilo linajulikana,tena hata sehemu nyingine tunazijua...
 
sijui ugaidi wala ugoni wa mwigulu - ni siasa kama zingine lakini nikimtathmini kwa hotuba yake, Mwigulu amempita EL kwa kilomita nyingi sana. Kaka amepanga hoja zake vizuri. "Tone" na ujumbe vinashabihiana, kasema vipaumbele vyake na jinsi ya kuvitekeleza, hajanisomea neno moja baada ya jingine kana kwamba kaandikiwa - anajua anachokisema, ana upeo mkubwa (IQ). Mpaka sasa kwangu EL ana point 0, Mwigulu 1. Nachotaka kujua tu sasa ni nani mshika remote wake. Washika remote wa EL nawajua, na ndo maana nikifikiria kumpa kura vinywele vinanisimama. Tukio la Nchemba pia limenionyesha ni kwa kiasi gani mbwembwe na ufahari kwa EL vilitumika kufunika udhaifu binafsi wa EL kama mwanasiasa. Nchemba amevuta hisia zangu bila helikpta wala diamond platinum. Tukiwa chuo nilikuwa namchukulia poa tu, lakini kwa jinsi alivyoweza kuweka nia na juhudi katika maono yake ya kisiasa naona ni mtu anayeweza kujiongoza na kusimamia kile anachokiamua. Huo uwezo ni vigumu kuuona kwa watu hawa wagombea wazee. Kupanda kwao kisiasa hakukuhitaji bidii kubwa. Kuingia kwenye mfumo wa siasa wakati ule haikuwa kazi ngumu na walikuwa wachache kulingana na mahitaji ya nchi kwa wakati ule, lakini kwa rika la Nchemba si kazi rahisi kuwapiga vikumbo hawa wazee na kutoboza bila kujiamini. Kwangu mimi hii ni sifa ya kiongozi. Nawasubiri kina Membe ila katika hawa wawili Mwigulu ameamsha hamu ya kusikiliza wagombea kwa makini.

Hakuna jipya zaidi ya kucopy ya Dr na upinzani wanayosem kila siku.Zaida ameudhilisha uma kua CCM wanatuibia
 
Anachekesha sana huyu. Mfumo mbovu lakini miaka yote hii amekaa kimya huku akifaidi nafasi ya juu ndani ya chama bila jitihada zozote zile za kubadili huo mfumo mbovu wa ndani ya chama. Amekuwemo ndani ya chama kwa miaka mingi sasa na na hadi kaingia Serikalini kama Naibu Waziri wa Fedha.

Miaka yote hii kimya hakutoa kauli ya kulaani mfumo mbovu hadi leo hii anapotaka kugombea urais ndio anauzungumzia mfumo mbovu ili kutuzuga Watanzania kama ilivyo kawaida ya MACCM. Mwigulu ulikuwa wapi 2005 kuzungumzia mfumo mbovu ndani ya MACCM na kuwashinikiza viongozi wa juu na wanachama kuuvunja mfumo huo na kuufanya uwe mzuri kama ambavyo wewe ungependekeza? Ulikuwa wapi 2010? Ulikuwa wapi 2012?

Hapana tumechoshwa na uongo wenu wa kukaa kimya huku nchini inaenda mrama miaka nenda miaka rudi kisha yale ambayo mnayajua kwamba ni mabaya kuja kuyazungumza pale mnapotaka kupata Urais ili mtuzuge Watanzania. Mkishaingia Ikulu speed ya kuendelea kuliangamiza Taifa inazidi kupamba moto.

Hachekeshi huyu Bali anahuzunisha na kutia hasira anaendeleza unafiki tu,shangaa na wewe kwenda ikulu leo ndo anaona eti mabadiliko ni sasa? Alikuwa wapi kuwarekebisha hao wenye ari mpya, nguvu mpya na wenye safari za matumaini, wanafiki wakubwa hawa hawana jipya.......
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Simpendi huyu gaidi Mwigulu lkn nimpe pongezi kwa kusupport sera ya CDM ya kuhimiza domestic manufacturing of products eg. Textile and leather sectors...
 
Back
Top Bottom