Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hivi huyu makongoro ni yule aliyewahi kuishi arusha? mwanasheria? sijui aliwahi pia kuwa mbunge? kama ndo huyo basi mwigulu ni bora mara 20
Nimeitoa paala
Leo taifa letu linapita katika historia nyingine , historia hiyo ni ile ambayo wengi wetu tunaisubiri hatma yake 25.October , pale Tanzania itakapo apisha Rais MPYA wa awamu ya5 kuelekea miaka 50 NYINGINE
Na katika mchakato huu kwa sasa tupo katika hatua muhimu , hatua ya kuwapima viongozi wanao jitokeza kuomba ridhaa hiyo
Kwa sasa tumeanza Na ccm Na tunazidi kuwaona wale wenye nia ya kutaka kuliongoza taifa wakijitokeza na kujinadi
Kwa sababu ni taifa langu Na Rais anayetafutwa ni Rais wa nchi yangu siwezi kujitenga nyuma juu ya kuwaongelea wale wanao ongelewa kuwa marais wetu
Jana nimesikia Mh Lowassa Leo nimemsikia Mh Mwigulu Na bahati mbaya sikimsikia Mh Wasira
Nasimama hapa kwanza kuwapongeza wote ambao wanajitokeza kulibeba hili gudulila la Tanzania .Make nikikiria ni sio swala la MTU kukurupuka .
Kwa namna nilivyo Pima wote ambao wamejitokeza wanaonesha wanao uwezo tena uwezo mkubwa kuwaza kuluongoza taifa letu nawapongeza
Nasimama kidogo kuchambua kidogo iliyokuwa hotuba ya Mwigulu Leo
Mwigulu ni kijana aliyo Na maono na moyo juu ya kuisaidia Tanzania ,
Lakini katika hotuba YAKE ya Leo sivyo nilivyo tarajia , haijanigusa niseme ukweli hata mkunipiga mawe
Hotuba ya Leo ya Mh Mwigulu sio ya "presidential material " ilikuwa ni hotuba ya kawaida mno na ya mambo Yale Yale yanayozungumzwaga na watu Hawa wale wale yasoyotendeke
Hotubu ya Mh Mwigulu ilikuwa na mapungufu haya niliyouaona Mimi
Ukizingatia ukubwa na unyeti wa nafasi aliyokuwa akiomba kwa chama chake
1.Hotuba yake haikuwa na kipa umbele au vipa umbele .... Mh Hamisi kigwangwala yeye amejitanabaisha Kama kipa umbele chake ni ajira kwa vijana
Sisi Kama wasomi unapo taja vipa umbele vyako ndipo unapo tupa nafasi ya kujadili kuwezekana na kutokuwezekana kwa vipa umbele hivyo
Taifa letu tumekwama kwa kuwa ni taifa lisilo na vipa umbele na taifa lilo na vipa umbele visivyojadilika na mwisho haviwezi kutendeka
Mh Hamisi katika ajenda yake hiyo tunamuuliza utatekelezaje ajira katika taifa ambalo 56% ya vijana na watu wazima hawana Elimu? Kigwanomics amejikita kusema mfumo wake wa ajira utalenga formal education na informal Education ambapo ataongeza nguvu kwenye mfumo wa ajira rasimi na zisizo rasimi
Mh Lowassa yeye amejielekeza kwa kusema vipa umbele vyake Vya kwanza mpaka cha NNE ni "Elimu"
Kosa la pili
2.Hotuba ya Ndugu Mwigulu Nchemba haijazungumzia kabisa mambo ambayo ni national core Mfn hajazungumizia muungano in content and contest, hajazungumzia amani umoja na mshikamano wa watanzania in content and contest as a presidential contests, hajazungumzia Tanzania na nchi za nje Sera Zake ambalo ni muhimu Sana kwa diplomasia ya nje na ambalo nadhani mataifa mengi kwa sasa yatakuwa yanaliangazia hilo
Kosa la 3
3.Ametulimia mda mwingi kuilamu serikali iliyopo as if yeye sio sehem ya serikali hii! Analaumu makampuni makubwa na matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi wakati yeye ndo ndo mkusanya kodi na mtunga Sera
..sasa Kama yeye analalamika nani ni responsible? .Mambo haya angeyazungumza Dr Slaa au Lipumba ni sawa ila sio Waziri
4.kuna wakati amesema yeye ni mjumbe wa kamati ya ushauri ya uchumi Na Sera hivyo wizara hiyo anaijua Sana ,lakini akashindwa kuja Na njia mbadala juu ya mporomoko wa shilingi yetu unao simamiwa na idara hiyo ambayo yeye ni mjumbe Na umekuwa akifanya hapo kabla ya naibu Waziri wa wizara
Pamoja na hyo machache niliyo yataja Mh Mwigulu anaweza kuwa hazina na president material kwa Siku zijazo...!
jana sikupata bahati ya kusikiliza kwa makini hotuba ya Lowasa, lakini leo asubuhi nimesikiliza hotuba ya wasira.. ki ukweli sikutarajia kama wasira angeweza kuja na hotuba nzuri (imekaa kiproffessional) so nikajua nchemba kwa kuwa yeye ni msomi wa kisasa, kijana na ameshaona makosa ya wenzake angekuja na hoja za maana na nzito kwa hiyo nikawa nasubiri kwa hamu sana na nikamsikiliza kwa makini.. but sikutarajia nilichokisikia... ameonesha udhaifu mkubwa kabisa hasa ukizingatia yeye ni msomi na kijana
1. Jambo la kwanza nililoliona toka mwanzo yule mc wake anaanza ni kuwa inaonekana nchemba hana kitu tangible cha kujivunia alichokifanya katika utendaji wake serikalini.. ndio maana wakawa wanazungumzia historia ya umasikini wake akiwa mdogo
2. kosa kubwa sana aliloanza nalo hakua amefocus kwenye sera na hoja zake.. akatumia muda mwingi kuwajibu wakosoaji wake kuwa hana uzoefu, na umri wake mdogo. nk
Kwa marafiki zaoHawa Jamaa wametoa hela wapi ya kurusha matangazo live kwenye channels kibao?
Mkuu hotuba ya EL ilikuwa nzuri kuliko ya Mwigulu na Wasira? Au umati?..kampiga bao Lowassa kwa kutangaza nia huko vichochoroni?
..Lowassa has set the standard ya kutangaza nia.
..wagombea wote watakaotangaza baada ya Lowassa wanapaswa kufanya vizuri kuliko alivyofanya Lowassa.
..wanatakiwa kupata umati mkubwa zaidi. wanatakiwa kutoa hotuba nzuri na ya kusisimu kuliko ya Lowassa. wanatakiwa kuwa more organized and disciplined ktk mkutano wao. zaidi wanatakiwa wa-articulate a better vision kuliko ile aliyotoa Lowassa.
cc Pasco, Lizaboni, Ritz, Chademakwanza, Tumaini Makene, Mag3, Nguruvi3, Kimbunga, Mohamedi Mtoi, Kapwela
Simba wa Yuda ni Mwina Kaduguda, huyo photocopyLowasa ni simba wa yuda
Vyama vyote haviwapi nafasi vijana wagombea wa CUF ni Maalim Seif na Lipumba,ukija CHADEMA ni Dr Slaa hawa wote wameshafikisha miaka 60.Bado mfumo wa vyama vya siasa za Tanzania hauwapi nafasi vijana kugombea nafasi nyeti
Hayo ni mawazo yako kijana, Ccm ndo baba na mama wa maendeleo yote uyaonayo hapa nchini wengine hao watasubiri sana, kaeleweka sana wewe tu umetumwa kwa mambo yenu binafsi, angalia njaa itakuua kijana.mwigulu ameongea mambo mazito na mazuri.bahati mbaya utekelezaji wake ndani ya ccm ni ndoto.
Rock spider,laki si pesaHotuba ya Mwigulu itakuwa imemzimisha Lowassa ndiyo maana Team Lowassa hawaonekani hapa watakuwa kwenye kazi ya kumzindua msukule wao.
Kwa hiyo kila jema likiongelewa na CCM ni idea ya upinzani?
Mwigulu ni jembe na ni kiboko ya upinzani, lazima mpanick..
yes ndo huyo aliyewahi kuwa mbunge wa arusha, na sasa ni mbunge ktk bunge la EAC
No usimjaji hivyo hapo kwa red, naona umesahau ulichoandika khs mwigulu uliyemjua mwanzo huko nyuma, kwamba he is not the same now!!