Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Mimi amenishangaza mwingulu kuongea kama kiongozi wa kambi ya upinzania while yeye ni waziri

ama kweli dunia iko na vichekesho
 
hivi huyu makongoro ni yule aliyewahi kuishi arusha? mwanasheria? sijui aliwahi pia kuwa mbunge? kama ndo huyo basi mwigulu ni bora mara 20

yes ndo huyo aliyewahi kuwa mbunge wa arusha, na sasa ni mbunge ktk bunge la EAC

No usimjaji hivyo hapo kwa red, naona umesahau ulichoandika khs mwigulu uliyemjua mwanzo huko nyuma, kwamba he is not the same now!!
 
Nimeitoa paala

Leo taifa letu linapita katika historia nyingine , historia hiyo ni ile ambayo wengi wetu tunaisubiri hatma yake 25.October , pale Tanzania itakapo apisha Rais MPYA wa awamu ya5 kuelekea miaka 50 NYINGINE

Na katika mchakato huu kwa sasa tupo katika hatua muhimu , hatua ya kuwapima viongozi wanao jitokeza kuomba ridhaa hiyo

Kwa sasa tumeanza Na ccm Na tunazidi kuwaona wale wenye nia ya kutaka kuliongoza taifa wakijitokeza na kujinadi

Kwa sababu ni taifa langu Na Rais anayetafutwa ni Rais wa nchi yangu siwezi kujitenga nyuma juu ya kuwaongelea wale wanao ongelewa kuwa marais wetu

Jana nimesikia Mh Lowassa Leo nimemsikia Mh Mwigulu Na bahati mbaya sikimsikia Mh Wasira

Nasimama hapa kwanza kuwapongeza wote ambao wanajitokeza kulibeba hili gudulila la Tanzania .Make nikikiria ni sio swala la MTU kukurupuka .

Kwa namna nilivyo Pima wote ambao wamejitokeza wanaonesha wanao uwezo tena uwezo mkubwa kuwaza kuluongoza taifa letu nawapongeza

Nasimama kidogo kuchambua kidogo iliyokuwa hotuba ya Mwigulu Leo

Mwigulu ni kijana aliyo Na maono na moyo juu ya kuisaidia Tanzania ,

Lakini katika hotuba YAKE ya Leo sivyo nilivyo tarajia , haijanigusa niseme ukweli hata mkunipiga mawe

Hotuba ya Leo ya Mh Mwigulu sio ya "presidential material " ilikuwa ni hotuba ya kawaida mno na ya mambo Yale Yale yanayozungumzwaga na watu Hawa wale wale yasoyotendeke

Hotubu ya Mh Mwigulu ilikuwa na mapungufu haya niliyouaona Mimi
Ukizingatia ukubwa na unyeti wa nafasi aliyokuwa akiomba kwa chama chake

1.Hotuba yake haikuwa na kipa umbele au vipa umbele .... Mh Hamisi kigwangwala yeye amejitanabaisha Kama kipa umbele chake ni ajira kwa vijana

Sisi Kama wasomi unapo taja vipa umbele vyako ndipo unapo tupa nafasi ya kujadili kuwezekana na kutokuwezekana kwa vipa umbele hivyo

Taifa letu tumekwama kwa kuwa ni taifa lisilo na vipa umbele na taifa lilo na vipa umbele visivyojadilika na mwisho haviwezi kutendeka

Mh Hamisi katika ajenda yake hiyo tunamuuliza utatekelezaje ajira katika taifa ambalo 56% ya vijana na watu wazima hawana Elimu? Kigwanomics amejikita kusema mfumo wake wa ajira utalenga formal education na informal Education ambapo ataongeza nguvu kwenye mfumo wa ajira rasimi na zisizo rasimi

Mh Lowassa yeye amejielekeza kwa kusema vipa umbele vyake Vya kwanza mpaka cha NNE ni "Elimu"

Kosa la pili

2.Hotuba ya Ndugu Mwigulu Nchemba haijazungumzia kabisa mambo ambayo ni national core Mfn hajazungumizia muungano in content and contest, hajazungumzia amani umoja na mshikamano wa watanzania in content and contest as a presidential contests, hajazungumzia Tanzania na nchi za nje Sera Zake ambalo ni muhimu Sana kwa diplomasia ya nje na ambalo nadhani mataifa mengi kwa sasa yatakuwa yanaliangazia hilo

Kosa la 3

3.Ametulimia mda mwingi kuilamu serikali iliyopo as if yeye sio sehem ya serikali hii! Analaumu makampuni makubwa na matajiri wakubwa kukwepa kulipa kodi wakati yeye ndo ndo mkusanya kodi na mtunga Sera
..sasa Kama yeye analalamika nani ni responsible? .Mambo haya angeyazungumza Dr Slaa au Lipumba ni sawa ila sio Waziri

4.kuna wakati amesema yeye ni mjumbe wa kamati ya ushauri ya uchumi Na Sera hivyo wizara hiyo anaijua Sana ,lakini akashindwa kuja Na njia mbadala juu ya mporomoko wa shilingi yetu unao simamiwa na idara hiyo ambayo yeye ni mjumbe Na umekuwa akifanya hapo kabla ya naibu Waziri wa wizara

Pamoja na hyo machache niliyo yataja Mh Mwigulu anaweza kuwa hazina na president material kwa Siku zijazo...!

Timu Lowassa wamepanick.Sasa kama kaisikiliza ya Mwigulu na ya Lowassa atashindwaje kuzifananisha hizo mbili?maana ya Mwigulu ya kuongea binafsi na ya lowassa pamoja na kuandikiwa ni kama usiku na mchana.Ya Lowasaa ipo chini ya kiwango ata cha kusikilizwa.
 
jana sikupata bahati ya kusikiliza kwa makini hotuba ya Lowasa, lakini leo asubuhi nimesikiliza hotuba ya wasira.. ki ukweli sikutarajia kama wasira angeweza kuja na hotuba nzuri (imekaa kiproffessional) so nikajua nchemba kwa kuwa yeye ni msomi wa kisasa, kijana na ameshaona makosa ya wenzake angekuja na hoja za maana na nzito kwa hiyo nikawa nasubiri kwa hamu sana na nikamsikiliza kwa makini.. but sikutarajia nilichokisikia... ameonesha udhaifu mkubwa kabisa hasa ukizingatia yeye ni msomi na kijana

1. Jambo la kwanza nililoliona toka mwanzo yule mc wake anaanza ni kuwa inaonekana nchemba hana kitu tangible cha kujivunia alichokifanya katika utendaji wake serikalini.. ndio maana wakawa wanazungumzia historia ya umasikini wake akiwa mdogo

2. kosa kubwa sana aliloanza nalo hakua amefocus kwenye sera na hoja zake.. akatumia muda mwingi kuwajibu wakosoaji wake kuwa hana uzoefu, na umri wake mdogo. nk

Mwigulu kaeleweka vizuri sana, timu Lowassa mkajipange.Maana kumbe pesa haziwezi kununua hotuba nzuri, inahitaji pia uwezo wa mtoaji hotuba.Lowassa kwa hotuba ana F ndio maana mnahangaika saizi na hotuba wenzenu kwani kwa kasi hii mtaishiwa pesa bure.
 
..kampiga bao Lowassa kwa kutangaza nia huko vichochoroni?

..Lowassa has set the standard ya kutangaza nia.

..wagombea wote watakaotangaza baada ya Lowassa wanapaswa kufanya vizuri kuliko alivyofanya Lowassa.

..wanatakiwa kupata umati mkubwa zaidi. wanatakiwa kutoa hotuba nzuri na ya kusisimu kuliko ya Lowassa. wanatakiwa kuwa more organized and disciplined ktk mkutano wao. zaidi wanatakiwa wa-articulate a better vision kuliko ile aliyotoa Lowassa.

cc Pasco, Lizaboni, Ritz, Chademakwanza, Tumaini Makene, Mag3, Nguruvi3, Kimbunga, Mohamedi Mtoi, Kapwela
Mkuu hotuba ya EL ilikuwa nzuri kuliko ya Mwigulu na Wasira? Au umati?
 
Mwiguru sio sili hotuba yako ni bora kipita hotuba zote za watangaza nia kupitia chama chako.....lowassa anachokuzidi ni kukodi mabodaboda njaa nchi nzima na kuwapeleka arusha lengo na madhumuni ni kuudanganya umma.binafsi nimeshuhudia vijana wenzangu wakipanda mabasi kwenda arusha si kwamba wanamkubali bali ni kuudanganya umma kwamba wanakubali kwa kuwarundika arusha.....poleni sana enyi vijana mlio laaniwa
...maana ukishiki ibada ya shetani na wewe ni shetani na hukumu yenu ni moja.
 
Vyama vyote haviwapi nafasi vijana wagombea wa CUF ni Maalim Seif na Lipumba,ukija CHADEMA ni Dr Slaa hawa wote wameshafikisha miaka 60.Bado mfumo wa vyama vya siasa za Tanzania hauwapi nafasi vijana kugombea nafasi nyeti

Tatizo langu ni mfumo wa sasa chini ya CCM....

Sina tatizo na wazee walio nje ya mfumo wa sasa....kwani naamini hafikiri na kuwaza kama wazee ama vijana walio chini ya mfumo wa sasa.

Suala la vijana tusitumie kama buzzword tu...kuwa kijana haina maana ndiyo sifa ya kuwa kiongozi bora. Na kuwa mzee haina maana ndiyo sifa ya kutokuwa kiongozi bora.

Tatizo la Tanzania hii ni mfumo. Tubadili mfumo ili wazee na vijana tuweze kulipeleka mbele taifa hili.
 
nadiriki kusema hujachambua vizuri....hotuba iliyokuwa nampangilio na wasilishaji mzuri ni ya wasira......huyu nchemba anashika namba mbili kisha yule wa tamasha la jana hata namba tatu hashiki..siwezi kumuweka namba tatu hafai nafasi hiyo
 
mwigulu ameongea mambo mazito na mazuri.bahati mbaya utekelezaji wake ndani ya ccm ni ndoto.
Hayo ni mawazo yako kijana, Ccm ndo baba na mama wa maendeleo yote uyaonayo hapa nchini wengine hao watasubiri sana, kaeleweka sana wewe tu umetumwa kwa mambo yenu binafsi, angalia njaa itakuua kijana.
 
yes ndo huyo aliyewahi kuwa mbunge wa arusha, na sasa ni mbunge ktk bunge la EAC

No usimjaji hivyo hapo kwa red, naona umesahau ulichoandika khs mwigulu uliyemjua mwanzo huko nyuma, kwamba he is not the same now!!

sawa kaka. unajua nimekulia arusha na sifa za huyo baba nilikuwa nikizisikia nikiwa mdogo kuwa "...mtoto wa nyerere mlevi sana.....hajiheshimu ...hapendezi kuitwa mtoto wa JK..." lakini kipindi kile akagombea kwa tiketi ya nccr akapata kwa sababu aligombea kwa chama cha jembe la wakati huo - mrema. baada ya nccr kupoteza umaarufu na yeye akapotea kwenye masikio yangu. wenzie kama kina mbatia baada ya kupoteza ubunge kutokana na kudhoofika kwa chama bado waliendelea kuwa active mpaka leo wapo na legacy yao inaonekana. Sasa huyu makongoro ananitia shaka kidogo. Anajitokeza wakati wa mgao tu? uongozi wa mwigulu niliuona toka tukiwa chuo ila hakuwa maarufu kama kina zitto na msando, ila nilipomuona anapanda kisiasa ndo nikasema kumbe yule kaka alikuwa serious na siasa??

Mwigulu ana faida ya kutokuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu kwa hiyo nguo yake itakuwa na matobo kidogo ukilinganisha na hao wagombea wengine akiwemo makongoro. nakubali tayari nina prejudice kwa makongoro. kama anafaa kuwa rais basi na mimi awamu ijayo natangaza nia.
 
Back
Top Bottom