Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Amemaliza, bado mtu mmoja ambaye macho na masikio ya watanzania wanasubili kujua anatangazia nia wapi,ukipiga simu kusini, mashariki magharibi na kasikazini wanauliza ni lini anatangaza nia, nae si mwingine ni JOHN POMBE MAGUFULI,
ili kuamini haya fanya utafiti mwenyewe piga simu pote tz utapata majibu,timuyake hii hapa

1, MWAKYEMBE
2, FILIPO LUNJOMBE
3, MWIGULU NCHEMBA
4, JAJI RAMADHANI
5, HUSSENI MWINYI
6, MZEE WA SIMANJORO
7, ANNA KILANGO
8, MZEE ZUNGU
9, MZEE WALIOBA (MZEE MSHAURI)
10, MKAPA (KIJANA WAKE POMBE)
11, mama wa sheria

na wengine wengi chini ya kapeti,
 
Hatuwezi kupata rais bora ndani ya ccm kwani kama wanamachungu na nchi hii wasingeunga mkono katiba mbovu kiasi hicho huku wakiwakejeli wapinzani!
 
..mimi nataka kuona mambo yafuatayo:

1. umati wa kumshinda Lowassa.

2. presentation nzuri na oratorical skills kuliko Lowassa.

3. better articulated vision for the country, inayoendana na rekodi ya mhusika.

4. halafu nidhamu na mpangilio mzuri wa mkutano.

..mtangaza nia akifanya yote hayo, then nitamkubali kwamba yuko serious, na anafaa kufikiriwa kwa nafasi hiyo.

Kwa kile alichokifanya Lowasa Sheikh Amri Abeid juzi, chama makini kingempa automatic disqualification.

Yetu macho
 
leo nimeamini inzi akiacha mambo ya kijinga anaweza kutengeneza asali. mwigulu akiacha mambo ya kipuuzi kama kupenda madem za watu , pombe anaweza kuwa kiongozi mzuri sana
 
Amemaliza, bado mtu mmoja ambaye macho na masikio ya watanzania wanasubili kujua anatangazia nia wapi,ukipiga simu kusini, mashariki magharibi na kasikazini wanauliza ni lini anatangaza nia, nae si mwingine ni JOHN POMBE MAGUFULI,
ili kuamini haya fanya utafiti mwenyewe piga simu pote tz utapata majibu,timuyake hii hapa

1, MWAKYEMBE
2, FILIPO LUNJOMBE
3, MWIGULU NCHEMBA
4, JAJI RAMADHANI
5, HUSSENI MWINYI
6, MZEE WA SIMANJORO
7, ANNA KILANGO
8, MZEE ZUNGU
9, MZEE WALIOBA (MZEE MSHAURI)
10, MKAPA (KIJANA WAKE POMBE)
11, mama wa sheria

na wengine wengi chini ya kapeti,

CCM inahitaji mtu anayechukia rushwa,nguvu ya pesa ya baadhi ya wanaogombea kupitia CCM si kigezo cha uongozi bora.
 
Yeye ni CCM kimwili lakini kadhihirisha kwamba kiroho ni UKAWA. Kwakuwa ana sura mbili hafai. CCM lazima ulinde ufisadi, utetee uzembe, uponde hoja za upinzani. Sasa unapojinadi kwa hoja za upinzani na kuponda yanayofanywa na kusimamiwa na CCM hapo kweli wewe unatekeleza ilani ya CCM? Mwigulu usichanganye mada. Kama vipi hama kambi tukuelewe.
 
Sasa ni zamu ya Mwigulu Nchemba na anatarajia kutangaza nia kuanzia saa 9 mchana wa leo na atafanya hivyo live kupitia star tv akiwa Chuo cha Mipango, Dodoma.
View attachment 255981Muda: saa 9 Alasiri hadi Saa 12 Jion.Mahali: Chuo cha Mipango Dodoma.Ukumbi: Mwl. Nyerere Hall
KAULI MBIU YA MWIGULU: MABADILIKO NI VITENDO, WAKATI NI SASAMwigulu anadai alibeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.Pia naona Mwigulu anamponda EL kiani kwa kusema watu wanajisifu kuwa wamekuwepo serikalini muda mrefu wakati huo huo wamelisababishia Taifa hasara kubwa katika muda huo mrefu waliokaa serikalini.Inasikitisha kumuona analalamikia mambo mengi yanayoendelea chini ya serikali hii ya CCM wakati kila siku wanawakejeli wapinzani wanapolalamikia na kuhoji mambo hayo Bungeni.Kwa kifupi,Mwigulu leo anaivua nguo CCM hadharani na zaidi leo anamponda kiana mh.sana na pia anaonyesha kuwa Mkulu na chama chake wamekuwa ni dhaifu.
project ACT imekufa sasa Mwigulu anakusanya watu na kuandaa choo ya kwenda vaa vazi la kimasai na kupandisha mori..kwamba El ni nguli.Nashukuru mlitusikilza ushauri wetu..kuendelea itunza ACT ni kuwaambia wapinzani kwamba Safari ya matumaini haina matumani ktk CCM .
 
Ulitegemea akiwa Bungeni akubali Serikali yake kuangushwa? kumbuka pale ni naibu waziri hana mamlaka zaidi ya kumtetea aliyemwezesha kuwa pale. Nani hasa alisema agenda za upinzani hazifai? kwa sasa mwingulu anachotaka ni kuwa na mamlaka ya kusimamia ukweli juu ya umaskini wa mtazania, kumiliki uchumi na kupunguza utegemezi. Kama ulimsikiliza Wasira ambaye alikuwa Waziri Ikulu utaona kuwa walichokuwa wanaongea na mapungufu ya Serikali iliyopo madarani hasa katika suala la ufisadi na namna mafisadi wanavyoshugulikiwa. Ili bidi hadi mwandishi mmoja amuulize mbona kama anachukua rasimu ya ilani ya uchaguzi ya ccm na kuitangaza taking advantage kuwa yeye ni m/kiti ya kuandaa rasimu husika. To be fair Mwingulu alikuja na hotuba yenye mashiko na mtiririko wenye matumaini kuliko waliomtagulia. Sina sababu ya kumtetea ila huo ndiyo ukweli.
Heshima iwe kwenu wadau.

Baada ya kumsikiliza mtangaza nia namba 3 kutoka CCM ndugu Mwigulu Nchemba nimeingiwa na wasiwasi kidogo.

Kwa wale waliofuatilia na kumsikiliza mh. naibu waziri mtagundua kuwa Mwigulu alikuwa anaongea kama vile yeye si sehemu ya serikali.

Lakini cha ajabu zaidi mtakumbuka kuwa Hoja alizokuwa anaziongelea leo ni zile zile zilizokuwa zikiongelewa na wapinzani bungeni na yeye kuamka kuzipinga kwa kuwakejeli.

Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kuwa Mwigulu katumia hoja za wapinzani kujinadi wakati ndye aliyekuwa mstari wa mbele kuzicrash hadi akasifiwa na Mwenyekiti wa chama na kupewa unaibu katibu mkuu bara pamoja na unaibu waziri kwa hiyo kazi.

Kwa lugha yepesi Mwigulu Nchemba tunaweza kumuita Chichidodo (Ndege mnafiki anayechukia kinyesi wakati chakula chake kinatokana na kinyesi)

Na hapa ndipo ninapopata wasiwasi kujua hasa nimwamini Mwigulu Nchemba yupi?!

1) Yule aliyekuwa anazipinga hoja za wapinzani?!

Au

2) Huyu aliyetumia hoja za wapinzani kutangaza nia?!
 
Nikikuambia kua hayo ya kuhusu viwda vya nguo niliishayaongelea miaka mitatu iliyopita utaniambia wakisema sawa na mimi wanakosea kwa sababu nimewahi kuyasema?

Mwigulu ni mjanja tu. Ameona alama za nyakati akadandia Sera za Ukawa ila ccm haiwezi kuzitekeleza kwa kuwa kimejaa mafisadi. Kwa mfano fedha za escrow ni haramu lkn amezihalalisha kwa kuzitoza kodi badala ya kuwalazimisha wazirejeshe na sheria ichukue mkondo wake kwa kuanza upya mchakato.
 
Chilisosi umefufuka? Twambie ile ahadi yako ya kumtoa Msigwa Iringa mjini. Me simpingi ila nashangaa huyu Mwigulu aliyekuwa kinara kukebehi wapinzani leo anaongea hayohayo ya wapinzani tumwamini kama tulivyomwamini Maisha bora kwa kila mtanzania, Kasimpya na Ari Mpya?
 
Nimemsikiliza Mwigulu vizuri ninachoona na hasira aliyonayo kitu kinachoitwa utawala wa sheria na haki ya kusikilizwa kabla ya kukutwa na hatia kwake ataiweka pembeni katika msimu wa utawala wake.
 
Hayo ni mawazo yako kijana, Ccm ndo baba na mama wa maendeleo yote uyaonayo hapa nchini wengine hao watasubiri sana, kaeleweka sana wewe tu umetumwa kwa mambo yenu binafsi, angalia njaa itakuua kijana.

bado narudia.mwigulu kaongea mambo mazito na mazuri. lakini bahati mbaya kwa ccm utekelezaji wake ni ndoto za mchana kweupe.mfano mwigulu anapinga sherehe wakati ni sera ya chama chake kuendekeza sherehe kama za wakati wa mbio za mwenge na sherehe za uhuru ambako mamilioni hutumika. mbaya zaidi wapinzani wamezungumza sana hayo.
 
Hayo ni mawazo yako kijana, Ccm ndo baba na mama wa maendeleo yote uyaonayo hapa nchini wengine hao watasubiri sana, kaeleweka sana wewe tu umetumwa kwa mambo yenu binafsi, angalia njaa itakuua kijana.
Maendeleo gani unayoweza kijigamba hapa? deni la nchina kushuka thamani ya shilingi? Jiji lisilokuwa na master plan? Ufisadi? kuanguka kwa elimu?
 
Hufuatilii Siasa Za Nchini Mkuu. Mwigulu Leo Alikuwa UKAWA kwa hotuba yake. Amerudia Yaleyale Yanayosemwa Na Wapinzani, Hasa Katika Bunge Hili La Bajeti.

mkuu huo ndo ukweli. nimegundua wapinzani ndo hueleza mambo halisia..
 
Sera ipi ya upinzani aliyotumia? Huyu ndio jembe la ccm hana makundi na anauwezo wa kukemea jambo lolote baya bila aibu

mkuu tatizo hamfuatilii siasa za nchi yetu vizuri. kwa mfano mwigulu anapinga mambo ya masherehe. hiyo ni sera ya wapinzani kila anayefuatilia bunge anayajua hayo. pia anazungumzia kufilisi wala rushwa na kuwafunga hayo kina lisu wanayasema kila siku bungeni na hata kwenye sakata la escrow walipiga kelele sana. tuache ushabiki mwigulu jana kaichana live serikali ya jk.
 
Mnaweza kufanana malengo mkatofautiana ni jinsi gani ya kufikia hayo malengo. Acha wivu wa kike wewe hamna mtu kama mwigulu huko Ukawa wewe

mkuu kama kusingekuwepo hayo mawazo angepata vipi? nilikuwa na kiongozi mmoja wa ccm wakati tunasikiliza hotuba ya mwigulu, kasema kwa hotuba hii nwigulu anawaongezea sifa wapinzani waliokuwa wanazungumzia hayo yote bungeni.
 
Back
Top Bottom