Dawa ya Mjinga
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 382
- 145
Mimi nikisikia mtu anamkashifu na kumtukana mtu mwingine mwenye umri sawa na baba yake huwa najua ana matatizo makubwa sana kichwani.
Si wote wanaowafahamu baba zao. Wengine hawakuwa na bahati hata ya kuwa na baba wa kufikia wa kuwakanya namna ya kuishi duniani. Waswahili wanasema ukikosa la mama hata la mbwa. Sasa sehemu nyingine mbwa wenyewe hawapo la mbwa angelipata wapi? Mhurumieni maana asiyefunzwa na mamaye, dunia itafanya shughuli hiyo kwa ukamilifu wake.
Kuna walimtangulia kuleta dhihaka na kejeli za namna hiyo, leo wamefutwa kabisa kwenye uso wa dunia. Dunia hadaa, ulimwengu shujaa!