Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Ndugu zangu, mambo ni mengi ambayo magufuli anataka kuyafanya.. anataka kuleta maendeleo ya kweli na Tanzania mpya ambayo itawafanya wananchi wote wafurahie Serikali yao kuliko sasa.

CCM OYEEE

Ama kweli mmeshikwa pabaya. Hadi wewe unakuja kujaribu kuokoa zari huku jukwaani? Wale vijana wa buku saba saba hawatoshi tena? Sasa nakubali taratiiiiibu miti yote imeanza kuteleza
 
12042847_1028492137171055_335016429244177346_n.jpg
 
Hii inashangaza kweli. sikudhani kama kuna watu watakuja kuongea ka wanamkataba na mungu. mungu hataniwi anaeeza nyofoa mmoja ili liwe fundisho
Mkuu, unajua mtu anayekebehi Mgonjwa hana huruma na wagonjwa; kwa maana hiyo anawakebehi hata wale ambao ndugu zao wanaumwa. mtu anawezaje kutumia ugonjwa kama kigezo cha kumnyanyasa mtu ? Hahala wanajinasibu kuwa wanajali haki za Binadamu !!!
 
Naona mnaiga kila kitu toka zile NEMBO ZA CHADEMA na kauli mbiu yao,sasa mmekuja hata kwa wimbo wa msanii.Kweli mmekosa ubunifu.

Ila mwambie Nape UHAI na UZIMA ni Mungu anatoa.

Hujamjua Nape mkuu, baada ya kuona wanaotabiria vifo wenzao wanapukutika Nape naye anatamani naye afe kama wao kwani atazikwa kwa heshima sasa hivi.
Kulingana na hali ya ccm sasa hivi na hali ya hatma yake baada ya octoba jamaa hana hamu ya kuishi tena maana utakuwa ulimwengu wa fedheha na mahangaiko sana. Bora akufuru na afe ndivyo anavyojiombea mkuda huyo.
Atatoswa na ccm kama alivyotoswa na familia. Maana kwa mzee Nnauye hawamtambui kama mwanafamilia na mzee Mwandosya na family yake nao hawana haja naye hasa kwa tabia zake. Nani atakubali tabia za kishenzi kuzileta kwenye familia?
Hilo ni chukizo
 
Hujamjua Nape mkuu, baada ya kuona wanaotabiria vifo wenzao wanapukutika Nape naye anatamani naye afe kama wao kwani atazikwa kwa heshima sasa hivi.
Kulingana na hali ya ccm sasa hivi na hali ya hatma yake baada ya octoba jamaa hana hamu ya kuishi tena maana utakuwa ulimwengu wa fedheha na mahangaiko sana. Bora akufuru na afe ndivyo anavyojiombea mkuda huyo.
Atatoswa na ccm kama alivyotoswa na familia. Maana kwa mzee Nnauye hawamtambui kama mwanafamilia na mzee Mwandosya na family yake nao hawana haja naye hasa kwa tabia zake. Nani atakubali tabia za kishenzi kuzileta kwenye familia?
Hilo ni chukizo

Kinachonisikitisha ni jinsi watanzania tulivyo wapumbavu ,hivi tunashangilia MATUSI,kweli???Halafu imeshindikana hata Mtu mzima mmoja tu kumwambia anyamaze,hata huyo Magufuli,hivi leo najiuliza kwanini nimpigie Magufuli kama anabariki Matusi na CHUKI za wenyewe kwa wenyewe,mbaya zaidi tuliowategemee waseme stop wanachekelea.

Hakika nimeshikwa nabutwaa hata wale waliokuwa wanashangilia sijawaelewa kama wanaakili timamu.
 
peopleeeees..
 

Attachments

  • 1443518847847.jpg
    1443518847847.jpg
    75.4 KB · Views: 122
Kinachonisikitisha ni jinsi watanzania tulivyo wapumbavu ,hivi tunashangilia MATUSI,kweli???Halafu imeshindikana hata Mtu mzima mmoja tu kumwambia anyamaze,hata huyo Magufuli,hivi leo najiuliza kwanini nimpigie Magufuli kama anabariki Matusi na CHUKI za wenyewe kwa wenyewe,mbaya zaidi tuliowategemee waseme stop wanachekelea.

Hakika nimeshikwa nabutwaa hata wale waliokuwa wanashangilia sijawaelewa kama wanaakili timamu.

Ndio unapopata tafsiri ya wimbo wao mashuhuri " CCM ni ile ile'
 
Kwa taarifa yake Nape watu wanaojua kuongea sana,si watendaji na hawana kitu kichwani kwani huwa wanafunika udhaifu wao kwa kupiga domo.Ila magufuli amejitahidi kwani UKAWA has nothing to loose kwa kuwa hawako madarakani
 
mahaba..
 

Attachments

  • 1443518939111.jpg
    1443518939111.jpg
    48.9 KB · Views: 217
Habari wakuu,

Leo ni muendelezo wa kampeni, mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli leo yupo uwanja wa Samora mjini Iringa. Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Iringa.
======
View attachment 292579
Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa waziri wa ardhi, ndugu William Lukuvi na anampigia chapuo mgombea anaewania ubunge jimbo la Iringa mjini ndugu Mwakalebela, pia anampigia chapuo mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli.

Nape: Siku moja UKAWA walikuwa wanazindua mkutano wao Dar, nikiwa pale wakaanza kubishana Magufuli ametumia muda mrefu sana kuongea, nikawaambia mgombea wa UKAWA akifikisha dakika kumi na tano natoa milioni tano na nikazitanguliza, nikaulizwa ulijuaje, nikawaambia tatizo Lowassa anadhani Ikulu ni wodi ya wagonjwa.

Watanzania hatutaki Rais wa majaribio, ambae tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi, tumchague tingatinga. Watanzania wameshaamua, hawawezi kupeleka fisadi Ikulu. Nakumbuka nilikuwa nahangaika na magamba, gamba namba moja Lowassa kashaondoka na chama kiko safi.

Kuna watu walikuwa wanakifanya chama chaka la kujifichia, wanaharibu katika serikali na kukimbilia katika chama wakiongozwa na Lowassa, tunaamini mabadiliko tunayoyataka ndani ya serikali na CCM tutayapata kwa ndugu Magufuli, katika orodha hakuna mtu alienistua kama Edward Lowassa. Nikasema na huyu fisadi anataka kwenda ikulu? Akasema hamuwezi kuzuia mafuriko, nikamwambia mafuriko yanazuiwa hata kwa kidole.

Mimi ni msemaji wa chama, kwanini hatukumpa nafasi mwizi? Hiyo habari ya ugonjwa anaijua yeye mwenyewe na tumuombee mungu tarehe 25 ashuhudie tunavyorudi Ikulu kwa kishindo!

Tunataka watuambie hata kazi moja tu ambayo Lowassa amefanya hakuiba, tulimpa uwaziri mkuu na miaka miwili tu Richmond, kazi gani ambayo tumempa Lowassa hakutumia madaraka yake vibaya na hakuiba? Mtu mwenye historia ya namna hii hatuwezi kumpeleka Ikulu, weka mbali na Ikulu.

Upande wa pili tunae Magufuli, nitajieni doa moja la Magufuli! Mbowe siku moja anasema vibaka wanachomwa moto, kibaka mkubwa Edward Lowassa yuko mtaani, leo amefika bei ya CHADEMA, wote kawatia mfukoni. Mzee Mtei kapigwa bilioni mbili, Mtei bilioni tatu na Msigwa ambae alisema atakaemuunga mkono Lowassa akapimwe akili. Sasa Msigwa tangulia mwenyewe ukapime akili yako mwenyewe.

Wakati wanajadili bei ya kuuzwa chama chao, Slaa alikuwemo ndani, nayajua mengi lakini leo nasema yanayomuhusu Msigwa, akaambie aende kufuta kauli akasema hawezi, akaambiwa basi nyamaza, akasema nipeni uji nishindwe kuinua mdopo, milioni 340 zikawekwa mezani ndio maana akipita anashindwa kumsema Lowassa na Magufuli, anabaki kusema nipeni kura. Uchungaji amesahau mtumishi huyu, tapeli mkubwa. Msigwa alisema watu wa Iringa msitumie bidhaa za ASAS, anaajiri vijana zaidi 400 Iringa na ndiye mlipa kodi mkubwa hapa Iringa. Anataka wale vijana 400 waje mtaani kuja kuwaandamanisha.

Tarehe 25 lazima tumwadhibu kwa kuhahakisha kura zote zinaenda kwa Mwakalebelela, wakati wa ujenzi wa barabara Iringa kwenda Dodoma, kambi ya Ujenzi ilitaka kuwekwa Iringa lakini ikabidi ikawekwe Dodoma akitaka eneo , kwanini! Msingwa. Sina mashaka Iringa tumemaliza, mwambieni pesa ziko wapi, pesa kidogo zilizobaki akale na mkewe, ya ubunge imeshaharibika.

Watanzania muombeeni mzee afya aone tunavyochukua nchi kwa kishindo, wanasema Nape alituambia bao la mkono, kelele watapiga sana lakini Ikulu inaenda kwa rangi za kijani, wenzetu wanahubiri mabadiliko, madadiliko ya kumuacha muadilifu tumpeleke mwizi, mabadiliko ya kumuacha mzima na kumpeleka marehemu. Kwa leo inatosha.

Magufuli
Anaeongea kwa sasa ni Magufuli na anawakosoa wale wanaosema serikali haijafanya kitu akiwemo mchungaji wa Iringa ambae aliamini anafata amri kumi. Anasema hata amani hamna chochote kilichofanyika! Anasema ni serikali hii hii ilileta vyama vingi 1992.

Sasa anaelezea kwanini ameomba urais ikiwemo kudumisha amani iliyopo na la pili ni kuafanya kazi na hatakuwa na blabla, analinganisha lami iliyoacha na mkoloni kwa miaka 76 na lami aliyojenga Kikwete kwa miaka 10. Pia anaelezea mipango yake ujenzi wa barabara njini Iringa ili magari makubwa yasikatishe Iringa mjini.

Anasema anafahamu hela ziko wapi na mapato hayo yatashuka chini kwa wananchi na anaeleza vipi atagharamia elimu bure mpaka kidato cha nne.






Magazetini,kama MATUSI NDIYO SERA KUBWA YA CCM basi watanzania hatuna sababu ya kuwapa KURA.Hata kama nilitaka kumpigia basi KURA yangu amekosa.

Jiulize kwa MATUSI haya amekosa KURA ngapi????Jamani mwambieni Magufuli, MATUSI siyo SERA.
 
Last edited by a moderator:
Kama ameshindwa kuiongoza tff sijui kama iringa mjini inamtosha.ila asubuh tupo wote usiku peeeopleessss....
 
Ndugu zangu, mambo ni mengi ambayo magufuli anataka kuyafanya.. anataka kuleta maendeleo ya kweli na Tanzania mpya ambayo itawafanya wananchi wote wafurahie Serikali yao kuliko sasa.

CCM OYEEE

Kama SERA ni zile za MATUSI duh,basi mnatukimbiza hata siye tuliyefikiri Magufuli anafaa lakini kumbe sera zake ni MATUSI,na anayafurahia,Nimemdharau,na KURA yangu na familia yangu hapati tena.
 
Iringa tumeshaamua kuifuta UKAWA bye byee Msigwa

Hakuwaletea Barabara na UWANJA akiwa waziri leo anasema akiwa RAIS mh!!!!!!!!!!!!Hongereni kama mnaamini ,maana amesema GAS imepewa MCHINA bure kwa MIAKA saba.
 
Nape jana kasema Lowasa alituibia kila alikowekwa, alianza kuiba akiwa mfanyakazi wa chama, akapelekwa AICC Arusha akiiba. Akahamishiwa wizara ya ardhi akajimegea maeneo kibao nchi nzima, akapelekwa wizara ya mifugo akajimilikisha ranchi nyingi za uma. Mwisho akapandishwa cheo na kuwa waziri mkuu, hapa ndio akatumaliza kabisa na Richmond.

Wameshindwa kumshitaki siku zote hizo sasa Nape anatuambia sisi ilitumhukumu. SASA WANANCHI TUMEAMUA KUMFUNGA MIAKA MITANO JELA YA IKULU NA KAZI NGUMU YA KUWATUMIKIA WATANZANIA.
 
Hela za richmond ni za watanzania kama ameiba tunamsamehe ili kuonyesha hatuna kinyongo tunamzawadia na urais

Hii ni nchi yetu wote na tunataka kuonyesha ni ya kila mtanzania
 
Watu wanasema mtoto yake NEPI kwa hiyo nguo inayovaliwa na kunyewa pamoja na kukojolewa na watoto ndio sababu yake.
Hivi nape anaweza kuelezea tsh.152,000,000/- ambazo zinalipwa hadi leo kwa RICHMOND ni nani anachukua? maana ule mkataba haukuvunjwa.
 
Back
Top Bottom