Kutoka JamiiForums: Kliniki ya Kidigitali Maalum kwa Wanawake katika kumsheherekea Mwanamke

Kutoka JamiiForums: Kliniki ya Kidigitali Maalum kwa Wanawake katika kumsheherekea Mwanamke

Asha D Abinallah

Platinum Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
140
Reaction score
904
84CE69EF-6613-4973-A258-6FC56158D8CA.jpeg


Habari Wakuu,

Siku ya kusheherekea siku ya Mwanamke duniani, inahusu si wanawake tu, bali hata wanaume pia. Hii ni siku maalum ya kila mwanadamu kutambua umuhimu na nafasi ya Mwanamke kwa kumwangalia kama mwanadamu na si kwa vigezo vya sifa ya kuzaliwa Mwanamke. Na kwamba anastahili haki na usawa katika maisha yetu ya kila siku.

Ujumbe wa Kimataifa wa mwaka huu katika kuadhimisha siku hiyo mhimu ni “I am Generation Equality: Realising Women’s Right” Ikimaanisha “Mie ni Kizazi cha Usawa: Kutambua Haki za Wanawake”.

Siku ya wanawake duniani inaadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo mwaka huu kauli mbiu yetu Kitaifa ni “ Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadaye”

Jamii Forums katika kuhakikisha inasimamia lengo lake la kuhakikisha inachochea raia wa kidijitali uelewa na ufahamu imeamua kufanya “Digital Clinic” kwa wanawake wa Dar es Salaam.​
​
Clinic hii inalenga kusaidia wanawake wote wenye matatizo yoyote ya kidijitali, wanaotaka kujifunza namna ya kufanya jambo lolote la kidijitali na ambao wanafanya kazi zozote katika majukwaa ya kidijitali na wangependa msaada wa namna ya kuboresha wanakaribishwa.​
Mfano wa huduma zitakazotolewa​
  • Namna bora ya kutumia majukwaa ya mtandaoni ikiwemo JamiiForums, Twitter, Facebook, Instagram n.k
  • Namna ya kulinda kifaa chako na akaunti zako dhidi ya hatari za kidijitali
  • Namna ya kupata password ambazo umepoteza na zinakuzuia kutumia huduma mbali mbali mtandaoni
Tutakuwa Mlimani City siku ya Jumapili Tarehe 8 Machi kuanzia saa 3 asubuhi hadi 12 jioni mbele ya duka la game kwa ajili ya kukutana nanyi.​

​
​
Mnakaribishwa sana!​


Kwa niaba ya Uongozi na Team yote ya JamiiForums,
tunawatakia siku hii iwe nzuri kwenu
Happy International Women's Day 2020 #IWF2020
 
Ni wanawake tu ama na jinsia nyingine hawaruhusiwi kuhudhuria
Clinic hii inalenga kusaidia wanawake wote wenye matatizo yoyote ya kidijitali, wanaotaka kujifunza namna ya kufanya jambo lolote la kidijitali na ambao wanafanya kazi zozote katika majukwaa ya kidijitali na wangependa msaada wa namna ya kuboresha wanakaribishwa.

Special kwa ajili ya siku ya wanawake mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Ni Wanawake tu, ila ikitokea, upo hapo na hakuna Mwanamke hata mmoja wa kuhudumiwa, ndiyo kigezo pekee kinaweza kutumika Mwanaume kuhudumiwa.

Nisisitize tu kwamba, hatumaanishi Wanaume hawastahili huduma hiyo, bali tu katika kusheherekea nafasi ya Mwanamke, tumetoa kipaumbele.

Asante

Ni wanawake tu ama na jinsia nyingine hawaruhusiwi kuhudhuria
 
Mkuu,

Tafiti zinaonyesha kwamba Wanawake wa maeneo kama uliyotaja ni wachache mno waliojikita kwenye matumizi ya simu Kidigitali. Na hilo ni Wanawake kwa Waume.

Kwa maeneo ya mjini kama Dar es Salaam, Wanawake wamekuwa wakipata matatizo mengi sana kutokana na kutokuwa na maarifa ya kujidhatiti ili kuepukana na changamoto zinazoambatana na Digital Vulnerabilities. Tunatumia kesho kama fursa.


Vp wanawake wa misenyi, kolomije hko hii clinic ya kidigital itawahusu au wanawake wa mjinimjini

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Endapo wewe ni wa Arusha, na upo radhi kuandaa mazingira na walengwa kwa JamiiForums kuja kutoa Mafunzo hayo, tunaweza kujitolea siku 3 timu yetu ikaja, na ikalipia gharama zote za team yetu kufanikisha hilo, tupo tayari wakati wowote. Ni moja ya eneo la Mpango kazi. Ila Mkisubiri tupange, inawezekana ila inachukua muda zaidi.

Hivyo kazi kwako na Wana Arusha wote wanaoamini katika matumizi salama ya Kidigitali.

Vipi kwa Wana Arusha mkuu, lini tuwasubirie
 
Mkuu,

Endapo wewe ni wa Arusha, na upo radhi kuandaa mazingira na walengwa kwa JamiiForums kuja kutoa Mafunzo hayo, tunaweza kujitolea siku 3 timu yetu ikaja, na ikalipia gharama zote za team yetu kufanikisha hilo, tupo tayari wakati wowote. Ni moja ya eneo la Mpango kazi. Ila Mkisubiri tupange, inawezekana ila inachukua muda zaidi.

Hivyo kazi kwako na Wana Arusha wote wanaoamini katika matumizi salama ya Kidigitali.
Ok mamii ntacheki
 
Msaada Jinsi ya kuscreen shot massage za what’s up
 
Waste of money and resources, kwanini mnauwa mbu kwa gobole? Si mtengeneze documentary kuhusu mitandao ya kijamii then upload it on youtube na kila mtu afaidike,
 
Back
Top Bottom