Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

CHADEMA

Political Party
Joined
Apr 13, 2013
Posts
495
Reaction score
2,540
Habari wakuu,

Leo ni uzinduzi wa kampeni kwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambazo zinafanyika leo Jumamosi tarehe 29 Agosti 2015 katika viwanja vya Jangwani. Kampeni hizi zitaungwa mkono na umoja wa vyama vilivyo chini ya UKAWA vinavyojumuisha NLD, NCCR na CUF.

Tuwe pamoja hapa (kwenye hii thread) kujuzana yatakayojiri kwenye kampeni za leo.

KWA MATUKIO: PICHA UZINDUZI WA KAMPENI CHADEMA

​

============

View attachment 281775


​
Kwa sasa ni burudani kwa wasanii mbalimbali kutumbuiza na kwa sasa aliemaliza kuimba ni Singo na anaefata ni Juma Nature akiwa na msaga sumu.

9:18 Mchana: Kilichopo kwa sasa bado ni burudani na Sasa inatumbuiza bendi

9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.

9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.

9:48 Mchana: Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.

9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa

Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye UKAWA.

Imani yenu kamwe haitapotea bura, mnaiweka mahali sahihi na sisi tutaisimamia. Natangaza rasmi sasa mkutano wetu umezinduliwa na tusubiri nondo zenye hoja.

Lawrence Masha: Waheshimiwa viongozi, watanzania wenzangu, sisi sote ambao tumehama CCM tuna akili timimu, sio wapumbavu, sio makapi. Kutokana na mambo yaliyotutokea mimi na vijana, wale wote wanaofanya kazi katika serikali yetu, magereza, polisi mahakama kuu, niwapongeze wote waliofata maadili yao ya kazi lakini wapo wachache wasiofata maadili yao ya kazi. Mabadiliko yanakuja na ndugu zangu msiogope na tarehe 25 mpige kura tuingize serikali mpya ya UKAWA.

Mdee(10:10):
Niseme mambo machache, kwa kipindi kirefu wanawake wa nchi tumekuwa wateja wa chama cha mapinduzi, kwa kipindi kirefu sana sisi ambao ni wahanga kwenye huduma za afya, tunaojifungulia chini. 2010 CCM waliahidi kununua bajaji kwa ajili ya wanawake wajawazito, Kikwete amejitengea bilioni 50 kwenda mamtoni, pesa hizo pekee zingetosha kununulia ambulance 300, wakati ni huu, imetosha. Tumalizie kwa kupiga kibwagizo.

Nimeambiwa niombe kura za Kawe, wanakawe mpoo, mtanipaa, asanteni sana

Mama Regina: Wakinamama mpo! Kwangu Mungu ametenda, mimi juzi nimeongea na wanawake wenzangu Tanzania nzima kupitia wanawake wa Dar, matatizo ya mwanamke nayafamu japokuwa sio yote. Nachowaomba wanawake wenzangu tushirikiane, mabadiliko haya tutayaleta sisi kwa umoja wetu. Mungu awabariki sana.

Mbowe(10:18): Dar es Salaam Oyeee, DJ tafadhali naomba utupe utulivu. Kwa sababu ya muda nizungumze kwa kifupi sana, ukiona hicho kidude kinaruka juu ni mtambo wa kupigia picha. Kwa sababu ya muda niende kwenye tukio la kuzindua Ilani. Tunazindua ilani kama CHADEMA lakini ilani hii pia ni ilani ya CUF, NLD na NCCR. Niwatambulishe wagombea wetu wa ubunge kwa Dar es Salaam. (Sasa ni tukio la kukabidhi ilani na nakala za ilani zinakabidhiwa Lowassa Lowassa, Duni na Hamad Sharif)

Sasa ni zoezi la kutambulisha wabunge watakaowania ubunge katika majimbo ya Dar es Salaam kasoro majimbo mawili ya Segerea na Kigamboni yana wagombea wawili wa UKAWA kila moja

Mbowe: Majimbo yote tunasema tunasimamisha mgombea mmoja, lakini majimbo mawili bado taratibu hazijakamilika lakini naamini yatakamilika

Wanaowania ubunge Dar es Salaam
Mtulia Said, Mwita Mwaitabe, Said Kubenea(Ubungo) Halima Mdee(Kawe) Julius Mtatiro(Segerea ushind Shaaban Nkumbi Kigamboni John Mnyika Kibamba Naotrapia (CHADEMA jimbo la Segerea) Kondo (Mbagala) na Asanali (Lofa wa Ilala)

Makaidi(NLD): Zamani mimi nilikuwa mwanamichezo mpiga mpira na mwenyekiti wa SImba kwa miaka mingi, Simba huu ndio mwaka wao na Yanga, mpira hauwezi kuwa mzuri kama siasa ni mbaya, tuhakikishe tunachague sera nzuri ya UKAWA, hivi haiwezekani kutengeneza picha yenye sura ya Lowassa, sura yake nzuri yenye nywele nyeupe. Miaka 50 iliyoputa nilisema ipo siku TANU itapata jambajamba, mwaka huu TANU na CCM yake imepata jambajamba.

Taslima(CUF): Kinachosemwa hapa ni mabadiliko, tunatoka mahali pabaya, tunaingia mahali pazuri. Mabadiliko hayazuiliki isipokuwa waliodhani mabadiliko yanaweza kuletwa na CCM peke yake, hayo mawazo wayaondoe.

Mbatia(NCCR): Lowassa amesomea digrii ya pili Uingereza, degree ya maendeleo. Serikali atakayoiunda tutashirikiana kwa pamoja. Lowassa tunahakikishia umma wa watanzania utakulinda. Biblia inasema pasipo na kuni hakuna moto, pasipo na uchochezi hakuna vita. Wao wanachochea vurugu, sisi tunaleta matumaini yenye heri kwa watanzania, matusi na uchochezi huo kuna maandikwa kwenye bibilia unasema heri kijana masikini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambae hasikii tena maonyo na Mtume amesema ukiona uovu kemea, ukiona huwazi basi weka chuki. (Anamalizi kwa kuimba wimbo)

Mbowe(CHADEMA): Asanteni sana Dar es Salaam, nitaongea kifupi sana kwa sababu ya muda, leo hii tunazindua rasmi kampeni za mgombea wa Urais, mgombea mwenza na wagombea wote wa UKAWA kwa nchi nzima.

Tunataka mabadiliko haya yakalete maisha mapya, nawashukuru sana viongozi viongozi wenzangu na zaidi waliopata ujasiri wa kuondoka CCM wakiongozwa na Lowassa, akafatiwa na mzee Sumaye na wengine ambao sitawataja kwa sababu ya muda.

Mzee Warioba umasikini sio sifa, wala sisi katika umoja wa UKAWA hatuutamani umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. Tunataka Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.

Nimalizie kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10 amekuwa muhanga wa propaganda za CCM. Nawashukuru sana Dar, niwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu, hataibiwa mtu simu, sadaka ya mabadiliko itafanywa katika kampeni nyingine. Nimkaribishe mheshimiwa Sumaye.

Sumaye: Kwa ajili ya muda nitasema kwa kifupi sana, nimetoka chama cha mapinduzi, katibu mkuu alisema sisi ambao hatukuteuliwa hatukuwa na maadili, mimi nasema kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana, mimi nitakuwa mtakatifu, CCM wamekuwa wakiongoza siasa ya chama kimoja kwa ngozi ya vyama vingi, mmekunjika kwa miaka yote. Tulitaka kufanya mabadiliko kulekule, kukawa na tatizo ndani ya CCM, ukitaka kufanya lolote wanakuzingira. Wanawajaza watanzania uoga wa usilolijua, mkiwapa wapinzani wataharibu nchi, kila binadamu ana uoga wa asilolijua.

Lowassa kwa kuliona hilo, kwa kuwa watanzania wanamfahamu aliona uoga wa aina hiyo haitakuwepo, na mimi nimekuja kwa sababu hiyo. Watanzania leo elimu yetu inashuka sana, tunashusha alama za kufaulu wanafunzi ionekane wamefaulu wengi, pia ukienda katika afya. Tunataka tubadilishe hali hiyo.

Leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni KIkwete aliemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni LOwassa huyuhuyu ndie aliemuingiza KIkwete Ikulu, Kwamba watanzania wanampenda Lowassa, halina mjadala.

Mmewasikia kwenye kampeni zao, fisadi mkubwa huyo amechukua fedha za matajiri, Lowassa amechukua ustaarabu wa kuwajibika. Waziri anachukua mzigo ili kumuokoa Rais na serikali yake. Asanteni sana.

Nyerere wakati anastaafu, kwenye kikao kimoja nafikiri cha halmashauri kuu. Alisema hajaona mtu mvumilivu kama Kawawa, alibeba mizigo aliyostahili kubeba yeye, ndiyo kazi aliyofanya Lowassa. Vichwa vya treni vinavyonunuliwa, Lowassa alikuwepo? Wajenzi wa barabara nchi hii wanaidai serikali trilioni 1.4, kudai si tatizo katika hizo bilioni 900 ni pesa za adhabu, huo si ufisadi, mbona hawasemi? Serikali hii ni dhaifu sana na alituthibitishia katibu mkuu, mwenyewe kusema kuna mawaziri mizigo.

Mwisho wanalomsema nalo, Escrow Lowassa alikuwepo, kile kipande cha Lugemalira tulijua waliokula, kila kipande cha Habinder ni nani aliekula, tangu lini benki ikaruhusiwa kutoa cash kwa mabilioni. Wamejenga kibr, hawajali tena maumivu ya wananchi, naomba mwaka huu msikubali, watanzania mfurahie mabadiliko ya ndani ya vyama vingi.

Wanasema mgonjwa, mimi nataka niwaulize, kwani Magufuli mzima? Wanaenda kufanya nini Ulaya kama ni wazima, mtu yeyote ukishavuka miaka 50 hauwezi kuwa wazima kwa asilimia 100, hivi Rais mkapa alipokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa operashi Ulaya, nchi ilidorora? Alienda akarudi akaikuta nchi usalama.

Kwani KIkwete alivyokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa upasuaji mkubwa Markani, Rais si kazi ya kubeba zege Ikulu, anatakiwa kuwake timu nzuri ya kazi, yeye ni meneja tu, naomba sana tumchague itakapofika tarehe 25 Oktoba. Asanteni sana, nawashukuru. Nimkaribishe ndugu Maalim Seif.

Maalim Seif(11:20): Kwa sababu ya muda mimi sitaki nizungumze leo, namkaribisha babu Duni ili azungumze na nyinyi

Duni(11:21): Na mimi kwa kuzingatia muda sina haja ya kusema sena, mimi natakiwa kumsaidia Lowassa atakapokuwa Ikulu. Katika mambo ambayo yametokea kwa miaka 50 ni watanzania kuonewa, Tanzania hakuna haki, tangu 95, wanaoonewa ni wapinzani tu, wanafunguliwa kesi za jabu ajabu, kuanmajitu yanayoitwa mijanja weed, kuna majitu yanaitwa zombi, huku bara TV zinazuiliwa, mazikoni hatutakiwi, G/Mboto tabu. Unapoonea watu wanajenga chuki, pamoja na kuambiwa ina amani haina amani, wenye amani ni wanyonge kwa ajili ya stahamala zao, tumeonewa vya kutosha, sasa tunasema basi, tunataka mageuzi.

Nini tutafanya tukiwa IKulu, Hakuna kitu muhimu kama kuwa na katiba ya wananchi wote, miaka hamsini hatujawahi kuwa na katiba yenye ridhaa kwa pande mbili. Lazima tufanye kama Afrika kusini, tutaunda tume kama ya Afrika kusini, tume ya maridhiano tusameheane na tutafunga kitabu cha uhasama mabadiliko yatakapotoke

Mdee amekuja kuzungumza matatizo ya kina mama, umma wote hapa huu umezaliwa na mwanamke, kitu muhimu tunachohitaji kufanya ni kuwaheshimu wakina mama. Sasa ni Lowassaaa.

Tambwe Hizza: Peoples, kwanza naomba mnisamehe, mwenzanu nilienda kuongeza ulofa kwenye kiwanda cha ulofa. Watu wazito wameamua kukiacha chama cha mapinduzi, na mimi nimeamua na wapo wengi wameogopa eti watasema ana tamaa, hivi nani hana tamaa, hata Magufuli aliacha ualimu.

Napenda sana Lowassa na Sumaye, juzi nilimuona Rais akifanya utani na bosi wake, Kikwete akiwa waziri, Sumaye alikuwa waziri mkuu, eti anasema hajamuelewa, hivi ukishindwa kumuelewa bosi wako utaweza kuwaelewa watanzania.

Mwakyembe wakati akiwa mwenyekiti wa NBC, Mkapa alipotaka kuuza benki, Mwakyembe kwa mdomo wake alisema sikubali, leo anatumiwa kuja kumchafua mheshimiwa Lowassa.

Edward Lowassa(11:41): Peoples, Bwana Yesu asifiwe, tumsifie yesu Kristo, kuna tatizo kidogo muda umeenda wasije kupata sababu... Hotuba ipo kwenye maandishi, kwenye tovuti ya chama.

Niwashukuru waliopita kwa kunisemea, niliahidi kampeni safi lakini wameanza lakini wakianza ndio hivyo watavyopata. Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu. Maneno haya nimeyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa gharama ya serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha.

Tatu tumeweka umuhimu sana kwenye afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo. Wanokwenda nje ya nchi ni watu wakubwa, eneo jingine ni mawasiliano, ni muhimu sana tuwekeze. Kwa hio jambo la kwanza nitakalofanya ni kujenga upya reli ya kati iende Kigoma na Mwanza. Tutafufua Air Tanzania, nisme mambo matatu ya mwisho.

Mashehe wa Zanzibar wako jela muda mrefu sasa, nasikia habari ya babu Seya, nimeisikia. Naelewa hisia zenu kuhusu babu Seya, Tutatumia utawala bora kuwatoa muda ukifika.

Kuna bango hapa, mzee ukifika Ikulu tuletee Balali, ana pesa zetu huto, nimewasikia. Nakumbushwa hapa, katika vipaumbele vya ilani, kipo maji vijijini na vyuo vya ufundi lakini nimalizie kwa kuwaomba, naomba kura, hebu watakaonipatia kura wanyooshe mkono. Watu wanasema hivi, kura tutapata nyingi sana lakini zitaibiwa, kwahiyo, Rais peke yake haitoshi, ni kuhakikisha mtaenda kupiga kura. Lakini nimeulizwa na rafiki yangu mmoja, kwanini sijaenda mikoani bado, nakwenda kwenye daladala, nakwenda wapi. Nimebaki hapa Dar es Salaam maana hapa ni .. group, naomba watu wa Dar es Salaam mnitafutie kura kwa watu wa bara, kwa mke wako, kwa mume wako, kwa rafiki yako ili hata wakiiba, wataiba nyingi lakini zitabaki nyingi za kutosha kutushindisha.

Nimalizie, ninawashukuru sana kwa mapokezi, haijapata kutokea hata mkutano wa wakubwa zetu wa CCM, hongereni sana, nimependa mapenzi yenu, rafiki yango mmoja mzanzibar aliniambia, haya si mapenzi, ni mahaba lakini nawaomba mahaba haya yaonekane katika sanduku la kura. Ndugu zangu ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.

11:52: (Wimbo kwa Lowassa unaongozwa na Salum Mwalimu),

Mshehereji: Mkutano wetu tunaufunga saa 11:55 jioni, tunaitaka tume ya taifa ya uchaguzi itueleze, kwanini mikutano ya CCM inaisha usiku wa manane hawatoi hata onyo, mkutano wetu tumeshafunga. Nawashukuru wana Darisalama.
 
Matukio katika picha yatawekwa hapa:

===============

View attachment 281703View attachment 281704View attachment 281623
View attachment 281705
Shamsa Ford,Aunty Ezekiel,Jacq Wolper,Joyce Kiria na Halima Mdee
View attachment 281768
View attachment 281708
View attachment 281717
View attachment 281740View attachment 281741View attachment 281742View attachment 281743
View attachment 281766View attachment 281767
View attachment 281776
4.jpg
5.jpg
 
Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :

1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.

2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.

3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.

UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.

1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.

CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.

Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.

2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.

3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.

4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.

Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.

Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al
 
Kwa niongeza lowassa atueleze kwa nini aliua kitengo cha tourism ndani ya shirika la AICC?
Na hatimaye kupelekea kukua kwa kampuni bonafsi kama vile leoparsds tours ambayo inashutumiwa na vijana madereva kwa unyanyasaji...na pia inasemekena hawa leoprds tours ndio wanao mpa fedha za kampeni.

Pia tujulishwe kuhusu ranchi za taifa na mustakabali wake.
 
There is nothing like 50 years. Dirty propaganda

Mchambue mtu kama msomi.Discuss on both sides of the coin.His positive&-ve contributions
Umezaliwa lini?.Unakumbuka enzi za Prime minister Edo.Alipokuwa an ziara wilayani?.Matumbo yalikuwa moto tangu DC hadi mkurugenzi....



Post yako ni ya kikada na sio kisomi.Wewe ni Kada wa CCM.
 
Mvua iliyo anza kunyesha asubuhi ya leo mkoa wa Dar es salaam imeharibu mkutano wa UKAWA.
 
Back
Top Bottom