Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Lowasa kila siku muda haumruhusu kuongea, Lini utamruhusu.!
ELIM ELIM ELIM!!!!!
RELI YA KATI
AIR TANZANIA
KATIBA MPYA
WAKULIMA
ULIKUA Unataka nn na MASHEHE,BABUSEYA,,BALALI ET KAFA KUMBE YUKO ULAYA HII SERIKAL DHAIFU MWIZ HUYU RAIS KIWETE!!!!!nakwakifup dar wafanya biashara wakiwemo boda na mama ntilie walisha zungumza haha leo tumewafichulia uchaf wenu kwi kwi
 
nimemsikiliza kwa dk 10 alizoongea sijasikia Sera zake ni zipi zaidi ya kuomba kura, kuahidi kumuachia babu Seya na Masheikh wa Zanzibar pamoja na Balali, then akishafanya yote hayo maisha bora yanapatikanaje, halafu sera yake ni elimu, elimu, elimu..ha ha mwaka huu mtaisoma namba, mtu mwenyewe hana hata stamina hawezi kusimama dk 30.
 
Taarifa za ndani ya serikali zinasema kwamba Magufuli amekuwa akienda kubadilisha damu Ulaya kutokana na kuugua ugonjwa mkubwa ulio maarufu. Hatua hiyo ya kubadilisha damu kila mwezi inagharimu fedha nyingi ambazo analipiwa na serikali anayoongoza Rais Kikwete.
 
hiyo tuataichapisha na kuisambaza sie wenyewe:
a)tutajitolea muda
b)tutajitolea uwezo wetu wote
c)tutajitolea elimu ya tehama(it) ktk kuichapisha,kuifafanua na kuisambaza ilani hii kw wale ambao hawana elimu na exposure ya tehama
d)tujitolee kuichapisha ktk vibooktet vidogovidogo vya rangi
 
Mm nashabikia mwanzo mwishooooo Nina hakili sio kama wale majambazi wajingaaa
 
Kwa ujumla katuangusha, a veritable anti-climax. Nikifikiria alisema nini hasa najikuta kukumbuka Babu Seya na Mashehe wa Zanzibar, halafu elimu elimu elimu mara tatu kama punguani vile eti aliambiwa na Tony Blair. Mwenziye Babu Duni kasema yeye kipaumbele ni Katiba ya Muungano, na pili wataunda Kamati ya Maridhianao kama ile alifanya Mandela baada ya Ubaguzi wa Rangi kuisha, sijui sisi nani alikuwa anambagua nani. Kasema spichi yako iko website wala haipo, hata Ilanin yenyewe haijawekwa hata kwenye website ya NLD wala ya CUF William Marconi

Wewe ni miongoni mwa watz wanaopenda kudanganywa na ilani 100 ambazo hazitekelezwi

Je ni lowassa au watu waliokuwepo jangwani ndio walimtaja babu seya ?

Binafsi nimeambua
1. Elimu ,elimu ,elimu
2,kilimo
3,afya
4,reli
5,shirika la ndege
6, katiba

Kuhusu babu seya na balali ni wananchi ndio walikua wanapga kelele ,yy akajibu nimesikia na nitayafanyia kazi nikipata nafasi.
 
Wakuu salaam. Nikiwa mtanzania wa kawaida kabisa ambaye napima mambo ya kisiasa kwa vigezo vya msingi kuliko ushabiki, hatimaye nimejiwekea mambo machache tu na ya kawaida kabisa ambayo UKAWA na Lowassa wanatakiwa kuyafafanua leo ili nijenge imani kwao. Mambo haya ni :

1. Kwa kuwa Lowasa kati ya mwaka 1997 na 2000 alikuwa akiiongoza wizara ya kuondoa umasikini, alifanya nini kinachompambanua kwamba anachukia umasikini? Hapa mfumo si hoja yenye tija sana kwa sababu mifumo mibovu ina kawaida ya kuwajenga viongozi bora kwani hujipambanua wazi wazi.

2. Kati ya mwaka 1993 na 1995 Lowassa alikuwa akiiongoza wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi, alifanya jambo gani la kumtofautisha na watendaji wengine? Wananchi wamkumbuke kwa lipi katika wizara hiyo ambayo ilikuwa maalum kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora na kuondoka katika dimbwi la umasikinttti.

3. Mwaka 2000 - 2005 huyu mheshimiwa aliongoza wizara ya maji na mifugo. Ninachotaka kujua ni kwa nini katika kipindi chake cha uongozi migogoro ya wakulima na wafugaji ilizaliwa. Ni dhahiri kuwa ni wakati huu wafugaji walipata nguvu ya kuvamia maeneo ya wakulima na kusababisha tatizo ambalo limekuwa sugu hata leo.

UKAWA kwa upande wao naomba watueleze ni kwa nini tuendelee kuwaamini iwapo wamerudi kukanusha yale waliyotuaminisha hata tukawapenda.

1. Vita dhidi ya ufisadi. CHADEMA walijipambanua kama wapiganaji wa kweli dhidi ya ufisadi. Hii ndio sera ambayo bila ubishi iliwapatia umaarufu mkubwa.

CHADEMA wasimame na kukiri hadharani leo kwamba yale waliyotuaminisha kwa muda mrefu juu ya ufisadi ni uongo. Haitoshi tu kusema Lowassa hakuwahi kutueleza ukweli kuhusu Richmond. Hii ni ushahidi kuwa Chadema si chama makini hata kidogo. Kinaendesha siasa za kitapeli kwa malengo binafsi.

Tena msamaha huu uende mbali zaidi kukiri kuwa yale mliyokuwa mkijidai kuwa ni ushahidi mzito mlionao ulikuwa uongo ili kupata huruma ya wananchi.

2. CHADEMA ikiri na kuomba radhi kwa watanzania kwa kitendo chake cha kukiuka misingi kiliyojiapiza kuisimamia na kukanyaga demokrasia. Msamaha uombwe dhidi ya dharau na kejeli walizofanyiwa waliokipigania chama hata kukifikisha hapo kilipo. Mchakato wa kupata wagombea katika ngazi za urais na ubunge umegubikwa na sintofahamu kiasi cha kusababisha mgawanyiko wa kisiasa. Intelijensia ya CHADEMA imekuwa juu ya matakwa ya wananchi.

3. CHADEMA iombe radhi kwa utapeli wa kisiasa ilioufanya dhidi ya mauaji ya Olasiti. Ule mkanda unaoonyesha wauaji wakitekeleza mauaji hayo umeota mbawa. Hizi ni siasa za kitapeli. Kutafuta huruma za wananchi kwa hila.

4. CHADEMA wafafanue mipaka ya mashirikiano yao na CUF hasa linapokuja suala tata na nyeti kwa maslahi ya nchi la sera ya ULIBERALI. Watanzania tumeaminishwa na CHADEMA kwamba CUF wanasimamia ushoga na wanauunga mkono. Naomba CHADEMA waelezee msimamo wao, ama waombe radhi kwa kuwazushia uongo CUF.

Haya ni baadhi ya masuala ya msingi sana ambayo natarajia mkutano wa leo wa UKAWA utayatolea ufafanuzi.

Tujadili kwa hoja, matusi mwiko. Lizaboni, RIZ1, et al

Tatizo ni mfumo
 
Dah watu tangu asubuhi tumejazana pale, njaa na kiu! vyote mali yetu, kwa ajili ya kumsikiliza jamaa kumbe anakujakutuambia tukatafute internet.
 
Hajaongea juu ya

1.Barabara
2.Umeme
3.Maji
4.Uvuvi
5.Viwanda
6.Watumishi
7.Rushwa/Ufisadi
8.n.k

Kaongelea
Babu seya, Balali,ATC, Utalii n.k alafu katumia sekunde 2 kwa kila jambo

subiri utavisikia kwenye kampeni muda haukuwa rafiki hayo unayosema ya kina babu seya alikuwa anajibu mabango ya watu mzee umebugi anza upya
 
Leo kasahau wataja bodaboda na mama ntilie. Nlikua naskia pipoz pipos pipos pipos.. Mzee huyu akapumzike .
 
kwa kifurushi gani cha mb8 embu Lowasa aache utani watu tumekaa kusubiri sera anakuja kuuza sura tu jangwani.

kaka kwa miaka 50 mmekua mkiletewa mihotuba mireeefuuuuuu, isiyotekelezeka,

sasa huyu anakuja kisomi kwa hotuba fupi yenye tija mnataka nini?

Mlitaka ahotubie masaa 2 ndio mmwamini?

Watanzania ni lalazima tuondokane na ujinga, kwamba kuzani mtu anayejua kuongea kama kasuku ndiye kiongozi,

uho ni ujinga wa hali ya juu sana. Ccm wamekua mabingwa wa kujieleza na kutoa marundo ya ahadi lakini kutekeleza ni hadithi.

Tujifunze kwa wenzetu, mfano mzuri alikuwa rais wa marekani, alitumia staili ihi ya maneno kidogo kazi kubwa,
 
Hajaongea juu ya

1.Barabara
2.Umeme
3.Maji
4.Uvuvi
5.Viwanda
6.Watumishi
7.Rushwa/Ufisadi
8.n.k

Kaongelea
Babu seya, Balali,ATC, Utalii n.k alafu katumia sekunde 2 kwa kila jambo

Bora wewe ulikua makini kusikiliza
 
Sasa nimeanza kuamini lengo la mbowe kumsajili sumaye.kumbe mzee mamvi hajiwezi kabisa yeye naona abaki kutoa fedha tu.

Kuwa mahiri jukwaani si uthibitisho wa kuwa kiongozi bora. Lowassa anazo sifa nyingi na tunazifahamu lakini ntakupa sifa moja tu ambayo hamna kiongozi yeyote wa CCM anayo. UTHUBUTU.
 
Back
Top Bottom