Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Nimeshtuka sana leo katika uzinduzi wa kampeni za CHADEMA/UKAWA katika viwanja vya Jangwani Dsm umati wa watu kupiga kelele kwamba wanamhitaji Daudi Balali pamoja na fedha za Akaunt ya madeni ya nje maarufu kama EPA zilizoibiwa benki kuu kati ya mwaka 2009 na 2010 na mgombea Urais wa CHADEMA/UKAWA Mh Edward N. Lowassa kusema amelichukua hilo na atalifanyia kazi ikiwemo kesi ya Shekhe Ponda na wenzake pamoja na mwanamziki maarufu Babu Seya na wanae kwamba atatumia utaratibu wa kisheria kuhakikisha wanakuwa huru.

Hili la Balali ndo limeniacha hoi zaidi kwa sababu nilijiuliza inawezekanaje kumrudisha mtu ambaye tayari alisha kufa?

Je, inawezekana Daudi Balali hakufa yupo some where? Si tuliambiwa na kuaminishwa na serikali ya CCM na Kikwete kuwa huyu bwana amekufa na kuzikwa huko Marekani? Kwa nini umati ule umtake Balali ambaye ni marehemu?

Hapana!.. Mbona hili jambo si la kawaida? Huu uchaguzi wa mwaka unaonekana kuja na mambo ya kipekee na yasiyo ya kawaida maana hata Edward N. Lowassa ambaye ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA nilivyomwona anaonekana naye kuelewa na kujua kitu flani kuhusu hili.

Hebu CCM na Jakaya Kikwete Na serikali kwa ujumla, tuambieni tena Balali alikufa? Alizikwa wapi? Kwa nini mazishi yake yalikuwa kama ya Osama Bin laden? Huyu (Balali) alikuwa mtu mkubwa aliyekuwa anaongoza taasisi kubwa ya serikali, ni kwa nini kuugua kwake, kifo chake na mazishi yake yawe ya siri vile na hasa baada kashfa ya EPA??

amekufa lakn yupo!
 
Mi najiuliza hv kwanini watu kama Dk slaa na Lipumba wameamua kukaa kushoto dhidi ya UKAWA mimi nikiwa kama mwanaukawa naanza kuona chembechembe za hatari kwa watu hawa wawili kuamua kukaa kimya nahic wameamua kutuonesha watanzania ubovu wa UKAWA kwa sababu hawa ndio waasisi
 
Lipumba alishajua Born Town Mbowe kawazidi akili ndo maana kaondoka Kistaarabu, hakutukana wala kulaumu Mtu kaondoka Kimya kakiri nafsi inamsuta hajasimama popote kukiponda Chama chake Kaamua Kustaafu siasa. NCCR itapata jimbo moja tu la Vunjo, yale ya Kigoma watagawana Ccm na ACT, CUF yale majimbo mawili ya Lindi yote yanarudi Ccm. HONGERA MBOWE
 
Wameongea wengi katika mkutnao wa leo jangwani, lakini wengi wa walioomgea walikua wa ukanda wa, Mbowe, Mbatia, Sumaye,Luwassa, Tambwe Hiza Duni Haji na Maali Seifu.
 
Habari wadau!

Akihutubia mamilioni ya watanzania katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi mh.James Mbatia pamoja na mambo mengine amenitoa machozi kwa kuimba wimbo wa tenzi namba 116.

Wimbo huo umenikumbusha mazishi ya baba yangu yaliyofanyika tarehe 13/ 05/2014 wilayani Rungwe katika mji wa tukuyu kijiji cha itagata baada ya kufariki mikononi mwangu tarehe 12/05/2014 Mjini Sumbawanga.

Wimbo huo uliimbwa wakati maiti ya mzazi wangu huyo ikiingizwa kaburini na baadaye kutupiwa udongo,nimesikitishwa sana na wimbo huo,ninaamini baba yangu alifariki kwa kukosa huduma bora za afya na nimekata shauri sitaichagua CCM maishani mwangu mpaka nakwenda kaburini kama baba yangu,nawaomba watanzania wote kuacha kuchagua CCM mpaka mwisho wa maisha yenu!
 
SIjaona Bendera zenu, sijawaona viongozi wenu wakitoa hata neno moja. Sijawaona mkiwa mmevaa sare zenu. Sijawaona na vipeperushi vya vyama vyenu.
NLD sijaona nembo ya chama chenu kwenye vipeperushi vya Wagombea wa UKAWA, nembo ya Chadema, CUF na MCCR zipo.

Ww acha uongo unataka kick au
 
[h=2]Haijawahi kutokea...Lowassa Kavunja Rekodi...!![/h]
9:13 PM No comments
1.jpg

2.jpg

3.jpg


Tupe maoni yako hapo chini​
 
Nimeisikiliza hotuba ya Lowassa leo jangwani ameahidi mengi sana na mojawapo kasema akiingia ikulu atamuachia babu seya na wale mashehe wa uamsho

Naomba niwajulishe tu kuwa, katika wale mashehe, Sheikh Farid ambae ndie kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha uamsho ndio mtu alieagiza mauaji ya Father Mushi na ushahidi mkubwa polisi wanao, muda si mrefu mtasikia na atasomewa mashtaka mahakamani.

Babu Sea inasemekana alikua analawiti na kubaka watoto wadogo na ndio maana kafungwa jela.

Sasa kitendo cha kuwabeza Polisi kusema utawaachia huru ina maana polisi ni waongo na mahakama nao ni waongo

Hii desparate ya kura kutoa ahadi za kipumbavu mwisho wake ni kuhatarisha usalama wa taifa letu

Sitashangaa siku akituambia na wale walioua askari pale stakishari nao atawaachilia huru na wauaji wa albino

Kwa kifupi anachofanya ni kufurahisha baadhi ya watu bila kusahau anaanza kututia hofu wapenda amani

Mungu ibariki Tanzania
 
Sasa mkuu kwani UKAWA hawakujua leo wanakujakufanya nini? hawakujua kama mgombea wao anaitaji muda wa kutosha kuwaambia wananchi nini atawafanyia?
Ndio siasa zetu zilivyo mkuu....Na mi nikuulize kwani CCM hawakujua walikwenda jangwani kufanya nini?...kama magufuli asingevunja sheria akapitiliza muda mpaka zaidi ya saa 1830 unafikiri angesema kitu pale?...by the way nilimuona Lowassa ITV mida ya saa tatu na ushee hivi akiwa anazungumza aliyokuwa amepanga kuyasema leo kwa kirefu jangwani ambayo kama angeamua na yeye kupitiliza muda angeweza kuyasema yote kwa mtiririko walokuwa wamepanga!
 
Habari wadau!

Akihutubia mamilioni ya watanzania katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam mwenyekiti wa NCCR
sasa unasema nini. Umelia ili iweje. Kasema nini cha kukutoa machozi. Au ndo mwanzo wa kupagawa na pepo unahitaji kuombewa
 
atujakuelewa mkuu...ameongea kipi cha kukuliza kiandike na sie tulie
 
Nimeisikiliza hotuba ya Lowassa leo jangwani ameahidi mengi sana na mojawapo kasema akiingia ikulu atamuachia babu seya na wale mashehe wa uamsho

Naomba niwajulishe tu kuwa, katika wale mashehe, Sheikh Farid ambae ndie kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha uamsho ndio mtu alieagiza mauaji ya Father Mushi na ushahidi mkubwa polisi wanao, muda si mrefu mtasikia na atasomewa mashtaka mahakamani.

Babu Sea inasemekana alikua analawiti na kubaka watoto wadogo na ndio maana kafungwa jela.

Sasa kitendo cha kuwabeza Polisi kusema utawaachia huru ina maana polisi ni waongo na mahakama nao ni waongo

Hii desparate ya kura kutoa ahadi za kipumbavu mwisho wake ni kuhatarisha usalama wa taifa letu

Sitashangaa siku akituambia na wale walioua askari pale stakishari nao atawaachilia huru na wauaji wa albino

Kwa kifupi anachofanya ni kufurahisha baadhi ya watu bila kusahau anaanza kututia hofu wapenda amani

Mungu ibariki Tanzania
Tulia soma kisha elewa then njoo hapa uanze kucomment acha kutafuta cheap popularity, kasema hatafuata misingi ya utawala bora au ulikuwa na haraka na haujaelewa?Shirikisha kidogo na ubongo na fikiri kama great thinker then come up na something concerete
 
Back
Top Bottom