Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kweli umeghafirika kichwani mwako, nahisi unajipunguza akili. Hivi nini maana ya hotuba? Au hujui na kama hujui si uulize!!
 
hizo picha kikwete hataamani atajua ni computer, na pressure itaongezeka
 
Tunataka hotuba ya kusikia kutoka kinywani mwa mtu. Sio kupitia mitandao sijui nini. Kila mtu anaweza kuandika hotuba akaipitisha mtandaoni kwani kuna kazi gani. Hotuba ni mkataba wa kiongozi na anayeongozwa. Tunamthibitisha mgombea kwa kumsikia na sio kupitia mtandao. Kwani yeye ni disable? ? Msirudie tena kutujazia simu zetu na madudu yenu

hakika mkuu watz watakuwa vichwa maji kma watampa kura jamaa ndani ya mwaka mmoja na nusu tu watalia na kusaga meno na nchi itageuka kuwa ugiriki ya pili...hatakuwepo wa kumlaumu m2 muda huo cuz mliyataka wenyewe
 
Acha uoga wako, ndio umetumwa kuandika uoga wa akili yako na hao waliokutuma? Sikia ndugu yetu, uoga ni kifo na hofu ni zambi, kwahiyo hatukubaliana na uoga wako. Je huyu tuluemtegemea kwa miaka 10 amekusaidia nini? Huu ni muda wa mabadiliko, tuwe kama Ugiriki au China tunamuachia Mungu. Na hukatujuza kipindi hiki unatufananisha na nchi gani?
 
Waziri mkuu mstaahafu Fredrick Sumaye ndiye alikuwa kivutio kikubwa katika kampeni za mgombea uraisi kwa tiketi ya vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA.Mheshimiwa Sumaye kila alichokisema wananchi walikuwa wakimshangilia na kumpigia makofi kwani alidhiirisha ccm imechokwa na wananchi.Jambo alilofurahisha pale aliposema na kumtetea raisi wa awamu ya tano kutoka ukawa Eduard Ngoyayi Lowassa kwamba mtu mzima unapofikia umri wa miaka ( 50) maradhi kukupata ni jambo la kawada.Akasema mbona wao wanatibiwa ulaya watu hawawasemi wakirudi wanakuta nchi iko salama?? shangwe zililipuka hadi raha,Mh.Sumaye aliendelea kusema waliotafuna escrow Lowassa alikuwepoo?? mambo mengi aliyasema huku watu wakimshangilia kiukweli aliinogesha kampeni ya ukawa.
 
Dah! Nilikuwa jangwani. Kwa kweli palipendeza; na watu wamehamasika kumuondoa mkoloni mweusi - chama cha majambazi.
 
hakika mkuu watz watakuwa vichwa maji kma watampa kura jamaa ndani ya mwaka mmoja na nusu tu watalia na kusaga meno na nchi itageuka kuwa ugiriki ya pili...hatakuwepo wa kumlaumu m2 muda huo cuz mliyataka wenyewe

Kama tulivyo yataka kwa kumchagua Kikwete sio.
 
Kule kwetu ngopyolo, mpaka uende kusikiliza itv hakmashauli kule ndo madish mengi yapo, baada ya hapo unarudi nyumbanii. Hiayo uliyoyaandika atayasoma wapi kama si mimi na wewe wa hapa tulipo. muulize hata ndugu yako yoyote aliyepo kijijini kwenu kama ulichokileta hapa amekiona. CCM mnayoiikataa mjini , inakubalika sana vijijini. Sasa huo usanii wenu wa leo mtaufikishaje vijijni, kwa website? Amkeni Tanzania ya leo si ya vibaka, madereva wa bodaboda na mama ntilie mliowakusanya leo pale jangwani, Tanzania ya leo inataka umakini hasa kule (site) viijini ambako hawana umeme, maji safi na salama, madawa kwenye dispensari na huduma za msingi ambazo zinapaswa kuwafikia. Mgombea anapanda daladala mjini wakati vijijini wanatembea mpaka kilometa 10 kwa miguu na mkungui wa ndizi kichwani ili akauze arudi na sabuni, sukari, chumvi na vitu vitakavyotosha kufuatana na alichopata. kama kweli anataka akae na watu wa hali ya chini, akatembee nao kule kijijini kwake angalau hata kiolometa 5 ingawa najua hawezi maana yale matembezi ya kuishia TCC chang'ombe alishindwa. Amkeni acheni siasi siasa nyepesi kiasi hicho watz wa leo sio wapumbavu na malofa kama mnavyodhani.

Sasa nani lofa kama si wewe? Hapa unakiri kama baada ya miaka zaidi ya 50 ya CCM hakuna dawa, maji, elimu na miundo mbinu vijijini, halafu unaita wapinzani malofa.

Kwa taarifa yako, ukisikia ilani kwenye TV mara moja ndio inakuwa hadithi, lakini ikiwepo kimaandishi, wakati wote unayo. Sisi vijana tutachukuwa jukumu LA kuwafikia wazee vijijini Na tutawasomea. Hiyo ya CCM ushaisikia kwa miaka 50, na nini kimekuwa? Don't be a fool anymore. Amkaaaaaa. Sijui hiyo title ya Dr umeipataje, kwa utumbo unaouongea hapa, siamini kama ni Dr either way
 
Sumaye anaijua CCM, anaijua serikali na anawajua wanaccm hivyo kuwajibu ni rahisi sana kwake
 
Hatuhitaji maneno mengi yasio na tija tunahitaji vitendo kumbuka maneno matupu hayavunji mfupa

Well said mkuu, watu wanataka ngonjera na kudanganywa wajisikie amani..huu umasikini wa fikra unaliangamiza taifa
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    11.4 KB · Views: 235
Acha uoga wako, ndio umetumwa kuandika uoga wa akili yako na hao waliokutuma? Sikia ndugu yetu, uoga ni kifo na hofu ni zambi, kwahiyo hatukubaliana na uoga wako. Je huyu tuluemtegemea kwa miaka 10 amekusaidia nini? Huu ni muda wa mabadiliko, tuwe kama Ugiriki au China tunamuachia Mungu. Na hukatujuza kipindi hiki unatufananisha na nchi gani?

Watz wengi wana hofu ya wasichokijua, wamekaririshwa! Sumaye kafafanua vyema sana
 
Sumaye ana fahamu kila uhuni wa Kikwete na CCM yake. Nani hapa JF alikuwa ana fahamu kwamba Magufuli ana kwenda nje kutibiwa kila mwezi kwa fedha ya serikali.
 
Mate yalikuwa hakuna kwa kutemea niliduaa nilipoona maelfu kwa mamilioni ya watu waliofurika au hata tuseme kugharikishwa na wana UKAWA nikaamini nguvu ya umma ni nooooma.Nilikuwa nasoma kwenye mitandao ya kijamii mara oooh! picha za kuunga,mara oooh! picha zile za kutengeneza bali tarehe 29/08/015 historia imejidhihirisha wazi na msemo wa mwenye macho haambiwi tazama kiukweli umeonekana na Watanzania wanaohitaji mabadiliko.
 
Ungeona magari yaliyoleta watu toka mikoa yote ya karibu pamoja na pemba usingebetua mdomo wako kuongea ubwabwa bibie.
 
Sema maneno yake yananitia hofu kuhusu usalama wake hawakawii kumuundia tume mzee wa watu...
 
Back
Top Bottom