Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 13,332
- 7,406
Kwani shoga huwa anaoa?Wewe pitia shanga zako mkuu, sitaki unigombanishe za mke wangu
Kwani shoga huwa anaoa?Wewe pitia shanga zako mkuu, sitaki unigombanishe za mke wangu
simuoni Dk Slaa wala Lipumba!watu wanataka kusikiliza Sera na Ilani badale yake wanahubiri taarabu kwa KIKWETE!kampeni za kuchafuana bado zinaendelea Ukawa
Mbowe ameshindwa kabisa namna gani amsafishe fisadi mamvi
tulia dozi ikuingie
![]()
Sawa mkuu lakini unaweza linganisha hii nyomi na ile ya CCM juzi maana wale pia walikaa kwenye viti
Habari wakuu,
Leo ni uzinduzi wa kampeni kwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambazo zinafanyika leo Jumamosi tarehe 29 Agosti 2015 katika viwanja vya Jangwani. Kampeni hizi zitaungwa mkono na umoja wa vyama vilivyo chini ya UKAWA vinavyojumuisha NLD, NCCR na CUF.Kwa sasa ni burudani kwa wasanii mbalimbali kutumbuiza na kwa sasa aliemaliza kuimba ni Singo na anaefata ni Juma Nature akiwa na msaga sumu.
Tuwe pamoja hapa (kwenye hii thread) kujuzana yatakayojiri kwenye kampeni za leo.
KWA MATUKIO: PICHA UZINDUZI WA KAMPENI CHADEMA
9:18 Mchana: Kilichopo kwa sasa bado ni burudani na Sasa inatumbuiza bendi
9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.
9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.
9:48 Mchana: Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.
9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa
Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye UKAWA.
Imani yenu kamwe haitapotea bura, mnaiweka mahali sahihi na sisi tutaisimamia. Natangaza rasmi sasa mkutano wetu umezinduliwa na tusubiri nondo zenye hoja.
Lawrence Masha: Waheshimiwa viongozi, watanzania wenzangu, sisi sote ambao tumehama CCM tuna akili timimu, sio wapumbavu, sio makapi. Kutokana na mambo yaliyotutokea mimi na vijana, wale wote wanaofanya kazi katika serikali yetu, magereza, polisi mahakama kuu, niwapongeze wote waliofata maadili yao ya kazi lakini wapo wachache wasiofata maadili yao ya kazi. Mabadiliko yanakuja na ndugu zangu msiogope na tarehe 25 mpige kura tuingize serikali mpya ya UKAWA.
Mdee(10:10): Niseme mambo machache, kwa kipindi kirefu wanawake wa nchi tumekuwa wateja wa chama cha mapinduzi, kwa kipindi kirefu sana sisi ambao ni wahanga kwenye huduma za afya, tunaojifungulia chini. 2010 CCM waliahidi kununua bajaji kwa ajili ya wanawake wajawazito, Kikwete amejitengea bilioni 50 kwenda mamtoni, pesa hizo pekee zingetosha kununulia ambulance 300, wakati ni huu, imetosha. Tumalizie kwa kupiga kibwagizo.
Nimeambiwa niombe kura za Kawe, wanakawe mpoo, mtanipaa, asanteni sana
Mama Regina: Wakinamama mpo! Kwangu Mungu ametenda, mimi juzi nimeongea na wanawake wenzangu Tanzania nzima kupitia wanawake wa Dar, matatizo ya mwanamke nayafamu japokuwa sio yote. Nachowaomba wanawake wenzangu tushirikiane, mabadiliko haya tutayaleta sisi kwa umoja wetu. Mungu awabariki sana.
Mbowe(10:18): Dar es Salaam Oyeee, DJ tafadhali naomba utupe utulivu. Kwa sababu ya muda nizungumze kwa kifupi sana, ukiona hicho kidude kinaruka juu ni mtambo wa kupigia picha. Kwa sababu ya muda niende kwenye tukio la kuzindua Ilani. Tunazindua ilani kama CHADEMA lakini ilani hii pia ni ilani ya CUF, NLD na NCCR. Niwatambulishe wagombea wetu wa ubunge kwa Dar es Salaam. (Sasa ni tukio la kukabidhi ilani na nakala za ilani zinakabidhiwa Lowassa Lowassa, Duni na Hamad Sharif)
Sasa ni zoezi la kutambulisha wabunge watakaowania ubunge katika majimbo ya Dar es Salaam kasoro majimbo mawili ya Segerea na Kigamboni yana wagombea wawili wa UKAWA kila moja
Mbowe: Majimbo yote tunasema tunasimamisha mgombea mmoja, lakini majimbo mawili bado taratibu hazijakamilika lakini naamini yatakamilika
Wanaowania ubunge Dar es Salaam
Mtulia Said, Mwita Mwaitabe, Said Kubenea(Ubungo) Halima Mdee(Kawe) Julius Mtatiro(Segerea ushind Shaaban Nkumbi Kigamboni John Mnyika Kibamba Naotrapia (CHADEMA jimbo la Segerea) Kondo (Mbagala) na Asanali (Lofa wa Ilala)
Makaidi(NLD): Zamani mimi nilikuwa mwanamichezo mpiga mpira na mwenyekiti wa SImba kwa miaka mingi, Simba huu ndio mwaka wao na Yanga, mpira hauwezi kuwa mzuri kama siasa ni mbaya, tuhakikishe tunachague sera nzuri ya UKAWA, hivi haiwezekani kutengeneza picha yenye sura ya Lowassa, sura yake nzuri yenye nywele nyeupe. Miaka 50 iliyoputa nilisema ipo siku TANU itapata jambajamba, mwaka huu TANU na CCM yake imepata jambajamba.
Taslima(CUF): Kinachosemwa hapa ni mabadiliko, tunatoka mahali pabaya, tunaingia mahali pazuri. Mabadiliko hayazuiliki isipokuwa waliodhani mabadiliko yanaweza kuletwa na CCM peke yake, hayo mawazo wayaondoe.
Mbatia(NCCR): Lowassa amesomea digrii ya pili Uingereza, degree ya maendeleo. Serikali atakayoiunda tutashirikiana kwa pamoja. Lowassa tunahakikishia umma wa watanzania utakulinda. Biblia inasema pasipo na kuni hakuna moto, pasipo na uchochezi hakuna vita. Wao wanachochea vurugu, sisi tunaleta matumaini yenye heri kwa watanzania, matusi na uchochezi huo kuna maandikwa kwenye bibilia unasema heri kijana masikini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambae hasikii tena maonyo na Mtume amesema ukiona uovu kemea, ukiona huwazi basi weka chuki. (Anamalizi kwa kuimba wimbo)
Mbowe(CHADEMA): Asanteni sana Dar es Salaam, nitaongea kifupi sana kwa sababu ya muda, leo hii tunazindua rasmi kampeni za mgombea wa Urais, mgombea mwenza na wagombea wote wa UKAWA kwa nchi nzima.
Tunataka mabadiliko haya yakalete maisha mapya, nawashukuru sana viongozi viongozi wenzangu na zaidi waliopata ujasiri wa kuondoka CCM wakiongozwa na Lowassa, akafatiwa na mzee Sumaye na wengine ambao sitawataja kwa sababu ya muda.
Mzee Warioba umasikini sio sifa, wala sisi katika umoja wa UKAWA hatuutamani umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. Tunataka Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.
Nimalizie kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10 amekuwa muhanga wa propaganda za CCM. Nawashukuru sana Dar, niwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu, hataibiwa mtu simu, sadaka ya mabadiliko itafanywa katika kampeni nyingine. Nimkaribishe mheshimiwa Sumaye.
Sumaye:
Kwani shoga huwa anaoa?
Hana jipya huyolafudhi ya sumaye haina mvuto kabisa,hivi ni mhazbe nini huyu,,,,
lafudhi ya sumaye haina mvuto kabisa,hivi ni mhazbe nini huyu,,,,
Kwani shoga huwa anaoa?
Andika tu lugha ya Taifa,hii ya Malikia waachie wengine