NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Za jioni.
Jpm akaenda kwenye usingizi wa milele, Rais Samiah akashika hatamu katika kipindi kigumu sana, akatuvusha na Amani ikatawala Hadi sasa!
Leo maandamano ya upinzani na mabango yao kila kona nchini, Lissu anaunguruma yote, nadhani kapata nafasi ya kisiasa ya kutosha sana tangu aanze siasa zake kwa muda mrefu!!
Maandamano sio kuvunja Sheria lakini kwa awamu zote hadi za Rais wa kizazi cha vijana kufanikiwa Rais kikwete bado yalionekana ni haram na kosa kisheria na walishughulikiwa kweli kweli!!
Ni huyu Rais pekee alieruhusu haya kutokea na ikawa kawaida sana kuona upinzani sio uhaini bali ni walipakodi wenzetu!
Mafanikio ya Rais Samia siyo kujenga miundombinu Wala mashule na mahospitali kwani yote hayo watangulizi wake walifanya, lakini hili la maandamano ndio mafanikio makubwa pekee yanayomtofautisha na watangulizi wake!!
Kwenye hili Mimi binafsi nampa maua yake, sio rahisi kuwa Rais mwanamke halafu ukaruhusu maandamano sidhani kama angekua mwanamme mwenzangu angeruhusu hata kutokea nchini!!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais Samia amalize awamu yake hii salama na atimize matakwa ya jamhuri na sio yale binafsi!!