Kutoka kitabu cha Kabendera: Mohamed Dewji alipotekwa alikuwa anapelekwa Benki jioni baada ya wafanyakazi wengine kutoka

Sijuwi wewe ila mimi maadam sikuwepo kwenye inner cycle ya Magufuli naweza kudadisi vitu kadhaa kutumia kitabu cha kabendera
Mfano kupotea kwa Ben saanane.....kama hakuhusika kwa nini asingeamuru uchunguzi wa kina ufanyike? Hajawahi kuzungumzia popote wakati alijua fika ilimuharibia image ya serikali yake?
Kupigwa risasi Lissu tena kwenye makazi ya serikali....huyo mungu wako mbona alijikausha kama hajui lolote zaidi ya tweet moja ya kinafiki?
Halafu umeambiwa kufreeze mali za mtu kama MO ambaye ni internationally recognised business mogul unahitaji calculation za hali ya juu na siyo kama unavyofikiri wewe kichwa maji.
Kuhusu watoto mimi na wewe pia hatuwezi jua exactly anao wangapi labda kama wewe ulikuwa mke mwenza wa mama Janeth.
 

Sijawahi kuwa fan wa Jiwe ila siwezi kujazwa ujinga kama mtoto. Mimi simtetei jiwe bali nasema hizi story ni za kitoto na kijinga. Kwahiyo ukitaka kumtukana jiwe naweza kukuunga mkono as well ila siwezi kuamini story za kipumbavu kama nyumbu it's an insult to my intelligence.

Watu walipotea before na hata sasa bado wanapotea does that mean rais anahusika moja kwa moja? Wote wanaotekwa sasa ni sababu ya Samia au jiwe bado anaendelea kuwateka? Ripoti ya mzee kibao imetoka?

Kama kumteka MO na kuwithdraw pesa cash kirahisi hivyo tu ndo akili kubwa basi mfumo wa bank Tanzania na duniani kote kwa ujumla ni mfumo wa hovyo sana. Mtu yeyote wa bank akisikia hii scenario atacheka sana. Nashindwa kujua nani mjinga zaidi kaflag au nyie mnaoamini hii pumba!

Kama wewe sio mama Janeth hujui watoto wake, kaflag ni mama Janeth? Iweje awajue yeye tu nchi nzima watu 27? Hao watoto wamejificha hadi leo bado wanamuogopa jiwe kuendelea na maisha yao? Kiwango chenu cha ujinga kinashangaza.
 
Akuletee wewe ushahidi? Amesema kulingana na taarifa zake na ushahidi wake. Ukiona shida nenda mahakamani wao ndio wanaweza kumtaka atoe ushahidi. Ukiona uzushi chapa lapa acha sisi wajinga tuamini.

Ila mngetusaidia mfano Ben Saanane hakupigwa risasi kichwani na jiwe; sawa yuko wapi na uchunguzi wa kupotea kwake ulifanywa lini? Waliomshambulia Lissu nani amekamatwa na uchunguzi wake ulifanywa lini?

Tuacheni wapenda uzushi tuamini Magufuli was a cool blooded murderer
 
he had a severe insanity
 
Unaweza nipa source ya uhakika zaidi ya "Trust me bro nawajua watu nyeti". Kila mtu anawatu nyeti hii nchi na kila mtu ni usalama hadi vichaa.
Siwezi kukutajia watu kwa sababu za kiusalama, ila ni habari za uhakika tupu. Muulize Ridhiwani kama anaruhusiwa kukanyaga China na vitongoji vyake utajua ukweli.
 
Dogo nii mjinga, alishauriwa na wenzake wasimuhusishe baba yake maana kontena lilikuwa kubwa. In short, dogo hana faida na hii nchi angeachwa tu anyongwe.
 
Kauli hii ilikuwa inamlenga Kikwete moja kwa moja na ndiyo maana jamaa anakula mirungi na bangi mpaka muda huu.
 
Siwezi kukutajia watu kwa sababu za kiusalama, ila ni habari za uhakika tupu. Muulize Ridhiwani kama anaruhusiwa kukanyaga China na vitongoji vyake utajua ukweli.

Hizo ndo source za trust me Bro πŸ˜‚πŸ˜‚

Kaflag nae kaandika pumba akiulizwa source atasema trust me bro.
 
Eti kwny kitabu cha kabendela siwezi amini hizo tamthiliya kama zingine tuu,huyu mwandishi uvivu wa kulima tuu unamsumbua
 
Sasa hapo kosa ni nini? Mbona kuna wazee wa kimasai wana watoto 90 mkuu?
Sio wao wote mkuu. Hata wewe unaweza kuzaa na mke wa mmasai ila mtoto anabaki kuwa ni wa mmasai. Wana mambo ya kingese sana wale jamaa
 
Ebu mda mwingine tuwe tunashirikisha akili zetu vizuri alizotujaalia Mwenyezi Mungu,hivi kweli late Mkapa kwa pesa alizokuwa nazo alishidwa kwel kwenda south kwa matibabu kwa vile magu alikataaa yeye kwenda soutg
Unajua protocol ya kutibu viongoz ikoje mkuu?
 
Kama mtu unaweza kununua kitabu cha Yerico Nyerere, ccm inahitaji mtutu wa bunduki wa nini kuendelea kubaki madarakani?

Kama una akili za kununua kitabu cha Yerico basi ccm hawana sababu ya kutafta mtutu, hata manati haihitajiki, labda makofi.
Kwenye kujifunza kitu hutakiwi kuweka mipaka au kuchagua mwl. Unaweza kujifunza hata kwa kumuangalia kichaa chief. Na hapo ndio wazungu wanatuacha, tunaishi kwa kuchagua ya kujifunza kumbe dunia ni kama bahari elimu iko popote. So nakushauri sio vitabu vya yeriko tu usome. Hata vya wale unaowadharau sana hutakosa cha kujifunza na hawataandika ujinga 100% .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…