Kutoka kitabu cha Kabendera: Mohamed Dewji alipotekwa alikuwa anapelekwa Benki jioni baada ya wafanyakazi wengine kutoka

Kutoka kitabu cha Kabendera: Mohamed Dewji alipotekwa alikuwa anapelekwa Benki jioni baada ya wafanyakazi wengine kutoka

Safari yeyote ya nje ilihitaji kibali cha magufuli mbona hii ilikua wazi
Kiilikuwa kibali cha serikali. Wafanyakazi tulikuwa tunaomba kibali kutoka utumishi (ofisi ya Rais). Agizo la kwamba tutasafiri kwa kibali ndio lililotolewa na Rais. Kama mimi mtumishi wa umma nilikuwa naruhusiwa kusafiri kwa kibali, yaani Mkapa ndio angekataliwa?
Hapa sipo kumtetea JPM au kumlaani, ila napendelea ukweli na mantiki.
 
Dah kusoma na kuelewa huwa ni vitu viwili tofauti, ni wapi ameongelea habari ya Mkapa kukosa hela ya kujitibu?

Umeambiwa alinyimwa kibali sio pesa,

Kipindi cha Magufuli kutoka nje ya nchi hii ni lazima upate kibali chake.

Na alifanya hivyo makusudi baada ya Mkapa kusema kwenye nchi hii hamna mtu ataongeza muhula mwingine zaidi ya miaka 10 akiwa hai

Aliyasema haya siku anazindua kitabu chake

Kwa roho ya korosho ya jiwe naamini kabisa alimnyima kibali
Hauna akili timamu,kama unaamini Rais mstaafu naye anahitaji kibali kama mkuu wa idara au mkurugenzi kuweza kwenda nje kupata matibabu.
 
Kabendera amenichekesha sana anaposema kuwa Mo alikuwa anapelekwa bank ili aweke finger print watoe pesa hahahahaha hakika Erick ni mwehu yani watu wenye mamlaka ya kufunga account ya pesa ya mtu na kuchukua pesa wahangaike na wewe kukupeleka bank ili wakatoe pesa hahahaha hakika hichi ni kituko
Hiki kitabu ni cha watu wenye low IQ.
 
Hicho kitabu ni kitamu kama unapenda rumors za corridor of power...

Hizo za Ben Saanane zimepigwa sana huku, hizo za Mo zimepigwa sana huku, mengine kaambiwa na washkaji zake aliowa mention kwenye kitabu..

Tusiamini kila kitu mkuu .. .ask questions.
Leta evidence kuzikanusha unazoita rummors, tafiti zinajibiwa kwa tafiti!!!

Acha kufanyia kazi SPECULATIONS!!
🤔🤔🚴🚴
 
Kiilikuwa kibali cha serikali. Wafanyakazi tulikuwa tunaomba kibali kutoka utumishi (ofisi ya Rais). Agizo la kwamba tutasfiri kwa kibali ndio lililotolewa na Rais. Kama mimi mtumishi wa umma nilikuwa naruhusiwa kusafiri kwa kibali, yaani Mkapa ndio angekataliwa?
Hapa sipo kumtetea JPM au kumlaani, ila napendelea ukweli na mantiki.
Mkapa hakuwa mtumishi wa serikali kipindi cha Magufuli.

Sasa ahitaji kibali cha nini?
 
###Kwa wale wavivu wa kusoma vitabu Matukio mbalimbali ndani ya kitabu cha kabendera yatakuwa huku kwenye huu uzi ###

Fedha zilikuwa zinatolewa kwenye account za kampuni, bank manager walikuwa wanapigiwa simu kusubiria bank jioni, kisha Mo anatokea akiwa na watu wa mfumo kutoa fedha. Mo bana kumbe anaficha vitu vya ajabu hivi kwa mujibu wa kitabu,

Mgogoro ulikuwa ni wa kikodi, baada ya kuchallenge Jiwe akamdaka na kushinikiza ile pesa ilipwe, ikalipwa cash akachukua Jiwe cash na haikuingia serikalini, wafanyabiashara wengi wamefanyiwa huu mchezo na ndio fedha baadhi alitumia kwenye uchaguzi huu

Nawakumbusheni msome kitabu
Hii ya Moo naweza kuamini maana niliangalia interview moja YouTube akihojiwa na waandishi akawa anaeleza namna alivyotekwa na mpaka kuachwa kwake halafu nikaangalia na sakata la jamaa aliyetuhumiwa nikahisi kabisa ile script iliandaliwa kizembe sana kiasi kwamba mtu anastukia tu nahisi MO alipigwa mkwara kwamba aongee hivi ili hii ishu ipite
 
Kwa hiyo unatuaminisha kuwa Mkapa alihitaji kibali cha Jiwe ili kusafiri?
Mbona wafanyakazi tu wa serikali walikuwa wanapata vibali vya kutoka utumishi na wakawa wanasafiri?

Mimi nafikiri mwandishi na sisi wasomaji, tungejikita kwenye kutafuta ukweli. Tusilazimishe vitu fulani vinavyofanya jiwe aonekane mbaya sana au mzuri sana kuliko alivyokuwa.
Kwa utawala wa Jiwe inawezeksna kabisa! Kwani hujui kuwa kuna Watu waliogopa kwenda kumuona Tundu Lissu akiwaHospitali!
 
Nadhani kuna kitu zaidi Kabendera ana Conspire

Kuna drama nyingi sana zimechezwa kwenye hicho kitabu
Mkuu kama huu ni uongo Mo yupo, si atakanusha!!

Au atamfungulia mashtaka Kabendera kwa kumchonganisha na serikali.

Inaelekea wewe ndiye umetengeneza drama na conspiracy theory kichwani mwako halafu unataka utupe taabu kuhangaisha bongo zetu.
 
Magufuli aliambiwa kuhusu ugonjwa wa Mkapa, ilikuwa Covid 19 ina msumbua na alikuwa na hali mbaya sana, madaktari na familia waliomba apelekwa Afrika ya Kusini kupata matibabu sahihi kutokana na hali yake kuwa mbayaMagufuli akakata kutoa ruhusa ya matibabu mpaka kifo kilimpomkuta wakasema ni homa ••IN THE NAME of the PRESIDENT: MEMOIRS of a JAILED JOURNALIST
Duh!
 
Nadhani kuna kitu zaidi Kabendera ana Conspire

Kuna drama nyingi sana zimechezwa kwenye hicho kitabu
Mohammed Dewji hakutekwa na Makonda na TISS? Wakati mwingine tumia akili kidogo. Dewji hakukutwa hapo maeneo ya Gymkhana na zile sarakasi zote za kutekwa na kupatikana za Mambosasa? Kitabu kinasema ukweli labda sehemu ndogo ndogo tu ameweka mawazo yake. Ukweli Magufuli ndiyo amesababisha nchi yetu iwe ya ovyo, ikawekwa kwenye level ya Syria, na Somalia. Haitatokea rais wa ovyo kama Magufuli. Huyu mwingine anaweza kumpita akiendelea na mtindo wake wa kuteka na kuua.
 
Mara paap mwisho wa mwaka upepo unabadilika, anaingia mwingine Giningi, huyo ni pro Jiwe, mara ka flag anasema hicho kitabu alishinikizwa kuandika na mtu flani..

Kumbe naota tu, ngoja nivute shuka nilale, huu mwaka una ndoto za ajabu
Umenifumbua ni "MKAKATI" !
 
M
Nadhani kabendera ame target wateja na hadhira yenye uwezo mdogo wa kufikiri na kupembua mambo.

Mythology aliyoitumia amefanikiwa sana, hasa humu jamiiforums ambamo panajulikana kama "The home of great thinkers".

Huwezi kuorodhesha mythical premises kama hizo zisizo na clear justifications halafu Kuna watu wana consume bila kujiuliza.

Kwamba Mo Dewji alitekwa Ili wakatoe pesa benki na maafisa wa serikali ya Magufuli? 🤣🤣🤣

Kwa taarifa yenu tu! Serikali inaweza kuchukua au ku freeze account yoyote ya pesa bila hata kumhitaji mhusika kwa kumteka.

Tumieni akili, simtetei Magufuli lakini pia siwezi kudanganywa kirahisi namna hii kwa sababu najua ninachokisema.

Hiki kitabu hakina tofauti na Ile "Takataka" Fulani ya bwana yericko.

Wataalamu wa mambo najua mnanielewa.
[/Nadhani kaflag katumika tu kuendesha " MKAKATI wa wanamkakati hao waliojificha nyuso zao ila wanaonekana haooooo.
 
Hivi unajua huku mwishoni kuwa Jiwe alitofautiana na Mkapa! ?
Okay, hata kama walitofautiana….

Kwa nini ahitaji [Mkapa] kibali toka kwa Magufuli cha kusafiri nje ya nchi?

Au labda mimi ndo sielewi. Hivyo nieleweshe.

Kila Mtanzania aliyetaka kusafiri nje ya nchi alihitaji kibali cha Magufuli?
 
Ichokitabu kitakuwa nicha dini mpya,tuambiwetu dini inaitwaje ilitukiulizwa tuseme sisi niwaumini wa dinigani.

Vitabu vya dini havihitaji udhibitisho ni mwendo wa kuaminitu nakutoa sadaka.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom