Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Jana kupitia taarifa ya habari K24 nimesikisia Al shaabab wakiimba "Nairobi tutafikaaaaa Al Shaabab tunasemaaaaa" Wakenya matumbo moto saa hizi! Tuache mawazo ya udini tusivuruge nchi.
 
Wanaukumbi,
Imekuwaje leo Uislam wa Zanzibar unakuwa neno miaka 50 baada ya muungano? Kuna kitu hapa hakisemwi kwa kuwa kinatisha. Dunia nzima hivi sasa Uislam unakuja juu na huu ni ukweli usiopingika. Hapa kwetu Tanganyika Uislam umechukua sura nyingine pia. Kuna kitu Ulaya na Marekani wanakifahamu nacho ni ''Militant Islam.'' Hili ni somo tosha linalojitegemea lakini hapa hatuwezi kuingia ndani ila itoshe tu kusema kuwa kuna Waislam wananyanyua silaha kuilinda dini yao. Kama hivyo ni sawa au si sawa hilo tuwaachie maulamaa waamue.

Ili mtu aweze kuelewa kwa nini leo uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika umefika hapa ulilipofika ni muhimu sana akaijua historia ya kweli ya muungano. Vinginevyo mtu atakuwa anatapatapa hana mahali pa kushika.

Mwaka 1964 wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar, Tanganyikahaikuwa kama hivi sasa ilivyo. Suala la ''udini'' halikuwapo katika siasa za Tanganyika. Uislam ulikuwa umetumika vilivyo kupigania uhuru wa Tanganyika bila ya kuuathiri Ukristo na hakuna aiyekuwa hajui nguvu ya Uislam. Nyerere mwenyewe aliingia madarakani mwaka 1961 na kuishika nchi akiwa amekaa juu ya mabega ya Waislam. Siasa zilizotamalaki wakati ule zilikuwa siasa za uzalendo wa Kiafrika. Dini katika uendeshaji wa nchi haikuwa na nafasi. Hii leo mambo yamebadilika sana.

Uislam Tanganyika ulianza kupigwa vita vya chini kwa chini mara baada ya uhuru hatimaye kufika mwaka 1968 vita hii ilikuwa ishafika kileleni katika mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuundwa kwa BAKWATA. Si siri tena kuwa Nyerere na Kanisa Katoliki walihusika sana na hatimae nguvu ya Waislam katika siasa za Tanganyika zikapotea kabisa pamoja na historia ya Uislam katika kupigania uhuru wa Tangayika. Hadi leo mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika historia yao imefutwa. Imekuwa mwiko hata kuwataja katika vitabu vya historia.

Hivi sasa hisia za Uislam katika nchi yetu zinafukuta chini kwa chini na ndiyo maana tumekuwa na mauaji ya Mwembechai, Picha ya Ndege, na Kilindi na vijiji vya pembezoni mwake hivi karibuni na majuma mawili yalopita tu Waislam wamingiliwa msikitini (staili ya Mwembechai) na kupigwa na polisi. Kesi za masheikh zimekuwa maarufu Zanzibar na Tanganyika. Shuhudia hapa JF hamaki za kidini na wakati mwingine matusi baina ya Waislam wa Wakristo. Hizi ni dalili tosha kuwa mambo si shwari tena. Kitu cha kushangaza ni kuwa viongozi wetu wanajifanya hakunajambo, tuna amani.

Hii leo Zanzibar Karume akitajwa baadhi ya watu wanamlaani na halikadhalika Tanganyika Nyerere akitajwa baadhi ya Waislam wanamlaani. CCM Zanzibar katika chaguzi zote toka 1995 wamekuwa wakishindwa na hili linafahamika dunia nzima. Zanzibar wanachukua serikali kwa mtutu wa bunduki. Kitu cha kujiuliza ni hiki. Ni nani hawa wanaowanyima CCM Zanzibar kura? Jibu ni kuwa hawa ni wananchi na wengi wao wamezaliwa baada ya mapinduzi.

Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam. Wazanzibari hawajasahau sakata pale walipojiunga na Organisation of Islamic Conference (IOC) mwaka 1993 na wala hawajasahau Aboud Jumbe alivyotolewa madarakani Dodoma kwa kuidai Zanzibar. Viongozi wa leo wa Tanganyika hawa hawapendezi Zanzibar kama walivyopendeza kwa wazee wao wakati wa muungano mwaka wa 1964. Viongozi hawa ndiyo hawa katika kundi la akina William Lukuvi wanaoingia kanisani na bila hofu kusema kuwa hawataki kuiona Zanzibar inakuwa nchi ya Kiislam. William Lukuvi alipopewa nafasi ndani ya Bunge Maalum la Katiba kujieleza bila hofu na kwa kibri cha hali ya juu akarudia maneno yale yale na kusema yeye si mnafiki atasema kile kilicho katika nafsi yake kuwa hawawezi kuiachia Zanzibar iwe huru isimamishe Uislam. Ile picha iliyozoeleka Zanzibar na Tanganyika hapo zamani ya kuwaona Karume na Nyerere wote wamevaa kofia za mkono (kofia za Kiislam) leo haipo.

Labda kitu cha kujiuliza leo ni kwa nini Nyerere aliacha kuvaa barghaishia iliyokuwa ikimkaa vyema? Viongozi wa Tanganyika leo wanaingia Zanzibar wamening'iniza misalabamizito ya dhahabu shingoni. Ilikuwa Wazanzibari watanabahi siku nyingi sana. Naomba nihitimishe kwa kunukuu maneno ya Dk. Harith Ghassany katika kitabu chake maarufu kuhusu Zanzibar, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru’’:

‘’Inavoonyesha, bado haijawadhihirikia Tanganyika watawala kuwa baada ya miaka 50 kuwa ipo haja kubwa kwa Tanganyika kuubadilisha mtizamo wake juu ya Zanzibar na kuupinduwa msimamo mkongwe wa kuinyanganya na kuinyima Zanzibar haki zake kwa kukhofia kuwa ikiwachiwa huru Zanzibar itakuwa ni tatizo la kimataifa kwa Tanganyika. Au Zanzibar itakuja kutumiliwa au kutumika kama ni mlango wa kuuingiza ubeberu wa Kiarabu na wa Kiislamu Tanganyika na Afrika ya Mashariki na ya Kati. Wako wengi wenye kuhadaika na udogo wa Zanzibar ingawa athari zake wanaziona lakini wameamuwa kuukataa ukweli huo. Anasema Jalaluddin Rumi “Yatizame macho yako. Ni madogo lakini yana uwezo wa kuyaona mambo makubwa.”

wewe sasa ndio unataka Wakristo waliokuwa wameanza kuwaunga mkono Ukawa warud nyuma. ndio maana huwa wakat mwingine mnadharaulika hv huwez kukaa nyuma ili Waislam na Wakristo walivyokubaliana watusaidie kuitoa CCM madarakan? tambua kuwa cku Chadema na Cuf kwa nia ya dhat wakiungana kwa jina la Tanzania Ccm inapigwa chin plz ucwe kama ccm uctugawe tena. ficha udin wako
 
wewe acha kujidanganya, wakristo hasa wakatoliki Wwa Tanganyika mna chuki Sana na uislam na waislam, hivi zile pumba aizoomwaga #Lukuvi Ni nini kama SI chuki na uislam??

Mimi mtizamo wangu ni kuwa ccm haipendi wakristo na waislamu wawe na maelewano ili wasije kuioji juu ya maendeleo wameamua kuwagawa. Hakuna mkristo anamchukia muislamu au muislamu anamchukia mkristo isipokuwa wachache wanaotumika kisiasa kwa manufaa yao binafsi
 
wewe acha kujidanganya, wakristo hasa wakatoliki Wwa Tanganyika mna chuki Sana na uislam na waislam, hivi zile pumba aizoomwaga #Lukuvi Ni nini kama SI chuki na uislam??

Acha ku- generalize mambo. Aliyosema Lukiuvi yamepingwa na watu wa dini zote na wala hakuna ushahidi wowote kama alitumwa na wakatoliki. Lazima tumwandame mtu kwa upofu wake binafsi.
 
jackline, nimepita tu baada ya kuliona jina langu limetajwa na sitasumbuka kusoma zaidi yaliyomo ndani ya thread hii for that would be stooping and I choose never to stoop. Mohamed Said? Ndio nani huyo tena? Hilo jina nililifuta kabisa katika orodha ya...ooops, I had promised myself not to ever stoop...! Samahani jackline, nakitoa, huo muda wa kupoteza sina! Kwa sasa tunajadili namna ya kujenga msingi imara wa taifa...Katiba inayoitambua Tanganyika.

Mohamed Said ni mwandishi mahiri Afrika na duniani kwa ujumla, wewe unam-blacklist kirahisi rahisi tu? Hebu funguka zaidi mkuu Mag3 tuuone upande wa pili wa MS
 
Last edited by a moderator:
Umesema, nanukuu "Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam" . Hi statement ni matusi kwa viongozi wa wa nchi yetu waliopo na waliong'atuka. Je Mzee Mwinyi na Kikwete ambao wamekuwa au ni viongozi wakuu wa dola la Tanzania nao wanachuki na wananchi wenzao? Acha kuandaki mambo kwa hisia.
 
wewe acha kujidanganya, wakristo hasa wakatoliki Wwa Tanganyika mna chuki Sana na uislam na waislam, hivi zile pumba aizoomwaga #Lukuvi Ni nini kama SI chuki na uislam??

Wewe ndo hujui unachoongea kwani Lukuvi ni Mkatoliki?
Hebu tupia mfano mmoja unaoonyesha chuki za wakatoliki dhidi ya uislam.
 
Kinachonikere ni "ushujaa" wa Lukuvi.

Kulikuwa na kafir wa Makkah aliyevuka handaki lililochimbwa na Waislamu na kuingia upande wa Waislamu watupu, kitu cha kwanza alichofanya kafiri yule alipoingia upande wa Waislamu ni kumkata miguu ngamia wake ili kufuta fikra yoyote ile ya kukimbia na kurudi nyuma, kwa maana nyingine alikwenda pale kupigania ukafiri wake mpaka afe!

Mpaka siku Lukuvi atakapoamua kwenda Zanzibar na kusema maneno yake yale mbele ya mhadhara wa Waislamu basi hapo ndipo nitakapomuona si mnafiki lakini kusema maneno kama yale katika "kona nne" za bunge na kujiita si mnafiki huo kwangu mimi ni ubabaishaji wa hali ya juu.
 
Amma kwa hakika hakuna kilichonifariji bungen(BMK) kama maneno ya William Lukuvi alipokuja "kupangua" hoja ya Ibrahim Lipumba.

Katika "kupangua" kwake hiyo hoja ameudhihirishia ulimwengu kuwa kilio cha Waislaam wa Tanzania si cha bure.

Cha kushangaza, amerudia zaidi ya mara tano neno "hofu".

Nauliza, ikiwa leo ana "hofu" ya Zanzibar kuwa nchi ya Kiislaam, jee, Waislaam wana haki ya kuwa na hofu kuwa Tanzania inafanywa, kuanzia kwa Nyerere na mpaka leo hii kwa William Lukuvi, kuwa nchi ya Kikristo?

Hivi Nyerere ana heri ipi ya kuwa "mwenye heri" kuelekea "utakatifu" ilhali aliongoza Serikali isiyo na dini?
 
Uislam zanzibar ni 93% ukristo 5% wasio waslam wala wakristo 2%. Twakimu ya mleta mada ya 99% ni uongo
 
Umesema, nanukuu "Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam" . Hi statement ni matusi kwa viongozi wa wa nchi yetu waliopo na waliong'atuka. Je Mzee Mwinyi na Kikwete ambao wamekuwa au ni viongozi wakuu wa dola la Tanzania nao wanachuki na wananchi wenzao? Acha kuandaki mambo kwa hisia.

William Lukuvi ana "hofu" kuwa Zanzibar itakuwa nchi ya Kiislaam. Jee, wewe huna hiyo "hofu"?
 
Umesema, nanukuu "Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam" . Hi statement ni matusi kwa viongozi wa wa nchi yetu waliopo na waliong'atuka. Je Mzee Mwinyi na Kikwete ambao wamekuwa au ni viongozi wakuu wa dola la Tanzania nao wanachuki na wananchi wenzao? Acha kuandaki mambo kwa hisia.

Wapuuzi hawa. Kwa muda mrefu, Rais, Makamu wa Rais, Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Intelijensia, Mkuu wa Mahakama, Waziri wa Fedha walikuwa waislamu kwa wakati mmoja lakini bado wanawalaumu wakristu kwa matatizo yao! Amekuwepo Rais Mwinyi kwa miaka kumi baada ya Mwalimu na sasa tuna Rais Jakaya Kikwete anayetimiza mwaka wa 9 madarakani lakini bado wanaona kama vile ni makafir wanaombana Jumbe huko Kigamboni. Wanashindwa kukubali kuwa ni chaguo lake kuishi Tanganyika na sio Zanzibar kama vile wanavyofanya viongozi wastaafu lukuki kutoka nchi hiyo iliyoneemeka.

Amandla.....
 
Mzee Mohamed Said ,leo hii wapingaji na wenye kebehi dhidi yako wamekaa kimya. Ukweli unapodhihiri uongo hauna nafasi,wanajitia kibri kukutukana na kukubeza na hali wanatumia 'nondo' zako kama references kwa kazi zao. Kibaya zaidi wanaona haya kuku-acknowledge!

Ninakuonea tamaa na wivu wa elmu yako kwa upande mmoja,na ninaona faraja na fahari kwa upande mwingine kwa namna tu ulivyo mtu muhimu katika historia ya nchi yetu. Furaha yangu inaongezeka pale unapotumia lugha ya kuelimisha zaidi hasa kwa makusudi kabisa mtu anapokutukana. Allah akuongezee hekma zaidi na maisha marefu,na akujaalie mwisho mwema In Shaa Allah.
 
Last edited by a moderator:
Amma kwa hakika hakuna kilichonifariji bungen(BMK) kama maneno ya William Lukuvi alipokuja "kupangua" hoja ya Ibrahim Lipumba.

Katika "kupangua" kwake hiyo hoja ameudhihirishia ulimwengu kuwa kilio cha Waislaam wa Tanzania si cha bure.

Cha kushangaza, amerudia zaidi ya mara tano neno "hofu".

Nauliza, ikiwa leo ana "hofu" ya Zanzibar kuwa nchi ya Kiislaam, jee, Waislaam wana haki ya kuwa na hofu kuwa Tanzania inafanywa, kuanzia kwa Nyerere na mpaka leo hii kwa William Lukuvi, kuwa nchi ya Kikristo?

Hivi Nyerere ana heri ipi ya kuwa "mwenye heri" kuelekea "utakatifu" ilhali aliongoza Serikali isiyo na dini?

Kwa hiyo wewe unataka Tanganyika nayo iwe nchi ya Kiislamu? Una hofu gani na Ukristu?

Amandla.....
 
Back
Top Bottom