Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Ritz,

I beg to correct you, they dont really love Nyerere and they dont have blind love for him. They use his name and legacy falsely and especially when they are connered with Truth like the truth TL dared to speak openly in that sacred place in Dodoma on live National TV.

IF THEY LOVE HIM THEY WOULD NOT THROW AWAY HIS LEGACY OF ARUSHA DECLARATION AND LEADERSHIP ETHICS, WHAT THEY ARE DOING IS CHERRY PICKING HIS POLICIES WHEN AND WHERE IT FITS THEIR PURPOSE.
Punjab Singh,

Najua nyie wasia mlipata tabu sana wakati wa Nyerere, mlidhulumiwa sana mali zenu pole sana, nyumba zenu, hospitali, mashule, na pesa zenu.
 
Last edited by a moderator:
Chamviga,
Mimi bahati yangu ni kuwa walionizaa ndiyo walioasisi harakati hizi.
Mtu yoyote angekuwa kwenye nafasi yangu na yeye angeyajua
haya pengine hata kunishinda.

Mfano, kuwa Karume alilala nyumbani kwa mmoja wa wazee wangu
siku ya kuamkia mapinduzi kwa wakati ule 1964 wala haiukuwa siri na
wala hakuna aliyedhani hili jambo litakuja kuwa muhimu kiasi hiki siku
zijazo.
Acha kulewa sifa mzee mzima
 
Wanaukumbi,
Imekuwaje leo Uislam wa Zanzibar unakuwa neno miaka 50 baada ya muungano? Kuna kitu hapa hakisemwi kwa kuwa kinatisha. Dunia nzima hivi sasa Uislam unakuja juu na huu ni ukweli usiopingika. Hapa kwetu Tanganyika Uislam umechukua sura nyingine pia. Kuna kitu Ulaya na Marekani wanakifahamu nacho ni ''Militant Islam.'' Hili ni somo tosha linalojitegemea lakini hapa hatuwezi kuingia ndani ila itoshe tu kusema kuwa kuna Waislam wananyanyua silaha kuilinda dini yao. Kama hivyo ni sawa au si sawa hilo tuwaachie maulamaa waamue.

Ili mtu aweze kuelewa kwa nini leo uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika umefika hapa ulilipofika ni muhimu sana akaijua historia ya kweli ya muungano. Vinginevyo mtu atakuwa anatapatapa hana mahali pa kushika.

Mwaka 1964 wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar, Tanganyikahaikuwa kama hivi sasa ilivyo. Suala la ''udini'' halikuwapo katika siasa za Tanganyika. Uislam ulikuwa umetumika vilivyo kupigania uhuru wa Tanganyika bila ya kuuathiri Ukristo na hakuna aiyekuwa hajui nguvu ya Uislam. Nyerere mwenyewe aliingia madarakani mwaka 1961 na kuishika nchi akiwa amekaa juu ya mabega ya Waislam. Siasa zilizotamalaki wakati ule zilikuwa siasa za uzalendo wa Kiafrika. Dini katika uendeshaji wa nchi haikuwa na nafasi. Hii leo mambo yamebadilika sana.

Uislam Tanganyika ulianza kupigwa vita vya chini kwa chini mara baada ya uhuru hatimaye kufika mwaka 1968 vita hii ilikuwa ishafika kileleni katika mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuundwa kwa BAKWATA. Si siri tena kuwa Nyerere na Kanisa Katoliki walihusika sana na hatimae nguvu ya Waislam katika siasa za Tanganyika zikapotea kabisa pamoja na historia ya Uislam katika kupigania uhuru wa Tangayika. Hadi leo mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika historia yao imefutwa. Imekuwa mwiko hata kuwataja katika vitabu vya historia.

Hivi sasa hisia za Uislam katika nchi yetu zinafukuta chini kwa chini na ndiyo maana tumekuwa na mauaji ya Mwembechai, Picha ya Ndege, na Kilindi na vijiji vya pembezoni mwake hivi karibuni na majuma mawili yalopita tu Waislam wamingiliwa msikitini (staili ya Mwembechai) na kupigwa na polisi. Kesi za masheikh zimekuwa maarufu Zanzibar na Tanganyika. Shuhudia hapa JF hamaki za kidini na wakati mwingine matusi baina ya Waislam wa Wakristo. Hizi ni dalili tosha kuwa mambo si shwari tena. Kitu cha kushangaza ni kuwa viongozi wetu wanajifanya hakunajambo, tuna amani.

Hii leo Zanzibar Karume akitajwa baadhi ya watu wanamlaani na halikadhalika Tanganyika Nyerere akitajwa baadhi ya Waislam wanamlaani. CCM Zanzibar katika chaguzi zote toka 1995 wamekuwa wakishindwa na hili linafahamika dunia nzima. Zanzibar wanachukua serikali kwa mtutu wa bunduki. Kitu cha kujiuliza ni hiki. Ni nani hawa wanaowanyima CCM Zanzibar kura? Jibu ni kuwa hawa ni wananchi na wengi wao wamezaliwa baada ya mapinduzi.

Wazanzibari asilimia 99 ni Waislam. Hii asilimia 99 leo inajua kuwa nchi yao imeungana na Tanganyika mbayo viongozi walioshika madaraka ni Wakristo na wana chuki kubwa na Uislam. Wazanzibari hawajasahau sakata pale walipojiunga na Organisation of Islamic Conference (IOC) mwaka 1993 na wala hawajasahau Aboud Jumbe alivyotolewa madarakani Dodoma kwa kuidai Zanzibar. Viongozi wa leo wa Tanganyika hawa hawapendezi Zanzibar kama walivyopendeza kwa wazee wao wakati wa muungano mwaka wa 1964. Viongozi hawa ndiyo hawa katika kundi la akina William Lukuvi wanaoingia kanisani na bila hofu kusema kuwa hawataki kuiona Zanzibar inakuwa nchi ya Kiislam. William Lukuvi alipopewa nafasi ndani ya Bunge Maalum la Katiba kujieleza bila hofu na kwa kibri cha hali ya juu akarudia maneno yale yale na kusema yeye si mnafiki atasema kile kilicho katika nafsi yake kuwa hawawezi kuiachia Zanzibar iwe huru isimamishe Uislam. Ile picha iliyozoeleka Zanzibar na Tanganyika hapo zamani ya kuwaona Karume na Nyerere wote wamevaa kofia za mkono (kofia za Kiislam) leo haipo.

Labda kitu cha kujiuliza leo ni kwa nini Nyerere aliacha kuvaa barghaishia iliyokuwa ikimkaa vyema? Viongozi wa Tanganyika leo wanaingia Zanzibar wamening'iniza misalabamizito ya dhahabu shingoni. Ilikuwa Wazanzibari watanabahi siku nyingi sana. Naomba nihitimishe kwa kunukuu maneno ya Dk. Harith Ghassany katika kitabu chake maarufu kuhusu Zanzibar, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru’’:

‘’Inavoonyesha, bado haijawadhihirikia Tanganyika watawala kuwa baada ya miaka 50 kuwa ipo haja kubwa kwa Tanganyika kuubadilisha mtizamo wake juu ya Zanzibar na kuupinduwa msimamo mkongwe wa kuinyanganya na kuinyima Zanzibar haki zake kwa kukhofia kuwa ikiwachiwa huru Zanzibar itakuwa ni tatizo la kimataifa kwa Tanganyika. Au Zanzibar itakuja kutumiliwa au kutumika kama ni mlango wa kuuingiza ubeberu wa Kiarabu na wa Kiislamu Tanganyika na Afrika ya Mashariki na ya Kati. Wako wengi wenye kuhadaika na udogo wa Zanzibar ingawa athari zake wanaziona lakini wameamuwa kuukataa ukweli huo. Anasema Jalaluddin Rumi “Yatizame macho yako. Ni madogo lakini yana uwezo wa kuyaona mambo makubwa.”

Nyie wazee bora mfe mmalizike wote maana mnatuchafulia hali ya hewa na historia zenu za kuunga unga. Kila mwenye miaka 60 na kuendelea anajifanya anaijua historia. Historia zenyewe ni za kuwagawa watanganyika na wazanzibar. Kufeni tubaki wenyewe tusiojua historia lakini tumeishi kwa amani
 
Punjab Singh,

Najua nyie wasia mlipata tabu sana wakati wa Nyerere, mlidhulumiwa sana mali zenu pole sana, nyumba zenu, hospitali, mashule, na pesa zenu.

Na wewe kinda la juzi tu bado unanuka maziwa mdomoni umeahaathiriwa na wachochezi kina Mohamed Said?
 
Last edited by a moderator:
WildCard,

Unataka kuniambia hakuna ukabila wala udini kwenye taasisi na idara za serikali.

Kuhusu Tundu Lissu, hakumtukana Nyerere kaeleza ukweli.

Kwani ni uongo hakuwapoteza kina Aboud Jumbe na Dourado walipohoji muungano.

Tatizo mna mahaba sana na Nyerere mpaka mnasahau kama alikuwa binadamu.

Wewe allah akikujalia kufika miaka 50 utakuwa LICHAWI namba moja. Umri huo unawaza ukabila na udini? Zama hizi ndo za kuwaza hayo?! Mbulumundu mkubwa we!
 
Last edited by a moderator:
Segwanga,
Hapana kulewa kitu katika hilo la Karume.

Yapo makubwa ya kihistoria kama kulewa ningelileweshwa na hayo.

Mimi nimeeleza historia tu kama niijuavyo.
 
Kitabu cha "Kwaheli Ukoloni Kwaheli Uhuru" cha Dr.Harith Ghassany, kumbe kilipigwa marufuku Zanzibar, juzi kwenye bunge la katiba nilimuona mjumbe mmoja akifanya reference kupitia kitabu hicho.

Soma makala za Joseph Mihangwa uelimike kuhuzu Zanzibar. Achana na vitabu vya kigaidi kama hivyo
 
Nyie wazee bora mfe mmalizike wote maana mnatuchafulia hali ya hewa na historia zenu za kuunga unga. Kila mwenye miaka 60 na kuendelea anajifanya anaijua historia. Historia zenyewe ni za kuwagawa watanganyika na wazanzibar. Kufeni tubaki wenyewe tusiojua historia lakini tumeishi kwa amani
Unaonekana una upeo mdogo sana kwa akili yako unadhani vifo vipo kwa ajili ya wazee tu.
 
Soma makala za Joseph Mihangwa uelimike kuhuzu Zanzibar. Achana na vitabu vya kigaidi kama hivyo
Wewe kauzu kweli, yaani Joseph ndiyo anifundishe historia mimi? wakati wazee wangu ndiyo walimpokea Nyerere, mjini mwaka 1954 walikuwa mstari wa mbele kwenye kutafuta uhuru, soma wewe wakuja.

Isinipasue mbavu zangu..
 
Wewe allah akikujalia kufika miaka 50 utakuwa LICHAWI namba moja. Umri huo unawaza ukabila na udini? Zama hizi ndo za kuwaza hayo?! Mbulumundu mkubwa we!
Leo utaongea yote lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
 
Uislam Tanganyika ulianza kupigwa vita vya chini kwa chini mara baada ya uhuru hatimaye kufika mwaka 1968 vita hii ilikuwa ishafika kileleni katika mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuundwa kwa BAKWATA. Si siri tena kuwa Nyerere na Kanisa Katoliki walihusika sana na hatimae nguvu ya Waislam katika siasa za Tanganyika zikapotea kabisa pamoja na historia ya Uislam katika kupigania uhuru wa Tangayika. Hadi leo mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika historia yao imefutwa. Imekuwa mwiko hata kuwataja katika vitabu vya historia.

Hii article imejaa uongo na uchochezi mwingi. Mwandishi ametumia porojo za gengeni na kuzifanya kuwa ni facts. Hili la EAMWS ni moja ya uongo na uchochezi uliozagaa mitaani. EAMWS ilikufa kutoana na migogoro ya ndani hasa ule wa Bukoba kulikokuwa na mgongano kati ya wahindi/waarabu (mabepari) vs waislamu wazawa waliokuwa wana-support ujamaa (TANU & ASP). TANU hawakuanzisha mgogoro wa EAMWS ingawa viongozi wake wa kiislamu walishiriki kwenye usuluhishi. Tuachane na fitina/uchochezi kwani hata maandiko nayo yanakemea fitna.
 
Tatizo JF siku hizi mambo ya dini flani yanazungumzika lakini ukiweka yale ya dini nyingine hayatakiwi kabisa wanasema ni uchochezi!!
 
sioni haja ya kuwepo huu uzi...mod vipi mbona umeuacha hewani sana.
 
WildCard,

Unataka kuniambia hakuna ukabila wala udini kwenye taasisi na idara za serikali.

Kuhusu Tundu Lissu, hakumtukana Nyerere kaeleza ukweli.

Kwani ni uongo hakuwapoteza kina Aboud Jumbe na Dourado walipohoji muungano.

Tatizo mna mahaba sana na Nyerere mpaka mnasahau kama alikuwa binadamu.

Makasuku wenzio wa CCM Wanasema nyerere ni mtakatifu hakufanya makosa. So Tundu lisu alimtukana wewe unasemaje
 
Last edited by a moderator:
Hii article imejaa uongo na uchochezi mwingi. Mwandishi ametumia porojo za gengeni na kuzifanya kuwa ni facts. Hili la EAMWS ni moja ya uongo na uchochezi uliozagaa mitaani. EAMWS ilikufa kutoana na migogoro ya ndani hasa ule wa Bukoba kulikokuwa na mgongano kati ya wahindi/waarabu (mabepari) vs waislamu wazawa waliokuwa wana-support ujamaa (TANU & ASP). TANU hawakuanzisha mgogoro wa EAMWS ingawa viongozi wake wa kiislamu walishiriki kwenye usuluhishi. Tuachane na fitina/uchochezi kwani hata maandiko nayo yanakemea fitna.

Kubwajinga,
Hayo ulosema ya migogoro ya ndani katika EAMWS ndiyo ''official
version,'' iliyotengenezwa na Usalama wa Taifa na ndiyo iliyodumu
kwa miaka yote.

Marehemu Rashid Kayugwa aliyekuwa Usalama wa Taifa ndiye
aliyepewa jukumu la kuongoza propaganda hizi.

Mwisho wa maisha yake alieleza yote na Kayugwa alijuta sana
alitubia na kuomba msamaha kwa Allah amsamehe.

Lakini nitakuongezea jingine labda hulijui katika sakata ile ya EAMWS.

Uongo ulitengenezwa kuwa Sheikh Hassan bin Amir alikuwa
anataka kupindua serikali ya Nyerere.

Haya yalidumu kwa kipindi kirefu hadi pale nilipofanya utafiti na
baadae kuandika ''paper,'' ''Islam and Politics in Tanzania,''
(Al Haq International (Karachi) Vol. 1 No. 3 August- December
1993)
.

Lakini kabla ya kuchapwa kwa hii ''paper,'' Pakistan mwaka 1993
niliitoa kwenye mkutano wa East Africa Study Circle, Nairobi mwaka
1989.

Kwa mara ya kwanza ikawa kisa cha mgogoro wa EAMWS kinaelezwa
na upande wa pili na mkono wa Nyerere na Kanisa Katoliki ukawa kwa
mara ya kwanza umewekwa kweupe.

Huu ndiyo ukweli ambao Waislam leo wanaujua.

Vitabu vilivyofuatia vya P van Bergen na John Sivalon kuonyesha
fitna za Kanisa dhidi ya Uislam Tanzania.

Ikawa kama vimekuja kunisadikisha yale ambayo nilikuwa nimeandika
siku nyingi.

Hayo si uchochezi wala si fitna ni ukweli mtupu wa yale yaliyotukumba
Waislam na yanaendelea kututaabisha hadi leo.

Kubwajinga,
Umeniita mie muongo.

Nakuthibitishia kuwa yote niliyosema ni kweli na kama una uwezo
fanya utafiti wako yote nilliyosema yatakudhihirikia.

Zentrum Moderner Orient (ZMO) ni taasisi kubwa ya historia
duniani iko Berlin.Walinialika hapo kwa mwezi mmoja na tulielezana
mengi katika maandishi yangu.

Kama wewe na wao walikuwa na shaka na baadhi ya mambo.

Hadi hivi sasa nimepokea watafiti watatu kutoka Ujerumani na USA
na wote haowanatafiti kile nilichoandika wakiakisi yale nilohadhiri
Ujerumani.

In Sha Allah tusubiri matokeo ya tafiti hizo.

Picha hiyo hapo chini nikiwa ofisini kwangu Zentrum Moderner Orient,
Berlin, Ujerumani mwaka 2011.
 
Attachments

  • SAM_2015.JPG
    SAM_2015.JPG
    701.5 KB · Views: 70
Makasuku wenzio wa CCM Wanasema nyerere ni mtakatifu hakufanya makosa. So Tundu lisu alimtukana wewe unasemaje
Hivi wewe unamjua Ritz au unakurupuka kujibu, unadhani mimi nashikiwa akili na Mbowe au Dr.Slaa kama wewe, Nyerere alikuwa dikteta tu, muongo, mdanganyifu.
 
Last edited by a moderator:
Mi nahofu tukiwa na serikali 3 Tanganyika itakuwa nchi ya kikristo. Teh teh teh!
 
Back
Top Bottom