Kutoka kuwa Mkurugenzi wa TISS na kuwa IGP hii imekaaje?

Kutoka kuwa Mkurugenzi wa TISS na kuwa IGP hii imekaaje?

Kabla ya mwaka 1996 TISS (UWT) kuanzishwa ilikuwa chini ya Wizara ya Mambo ya ndani na mpaka leo wengi wa maafisa waliokuwa huko ni POLISI mishahara na masurufu yako huko,
kuna mdau kaelezea vizuri lkn uelewa wa member

Pale Ikulu kwenye ulinzi wa Rais kuna aina tatu za Walinzi, wengi wanawaita TISS lkn kuna JWTZ makomandoo, inner circle wakifuatiwa na TISS na POLISI na hata mavazi silaha na escort vinajionesha kabisa,
cc Evarist Chahali
Chai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kizuri humu ndani kila mtu mjuaji, kuna wanaojua wamekaa kimya na kuna wasiojua wanaonesha kujua. Sitaki kubishana ila nataka kuwasaidia kidogo. TISS ndicho chombo kikuu cha kukusanya taarifa,kuzichambua na kushauri. Taarifa zote kutoka kila sehemu iwe ni jeshini, bungeni, nje ya nchi, sokoni nk. Narudia tena taarifa zote wanatakiwa kuwa aware nazo baadaye wanazifanyia screening na kuchukua za maana tu.

Kwa mantiki hiyo TISS wanashauri uteuzi wa nafasi nyeti ndani ya serikali, from no where mtu hawezi kupewa cheo cha CDF aongoze jeshi bila kufanyiwa vetting. No lazima wajiridhishe then wampitishe. Vivyo hivyo kwa IGP nk

TISS wapo kila mahali, iwe kanisani (kapilimba alikua mchungaji) msikitini, ikulu, shuleni nk. Kila penye watu wapo!

TISS imegawanyika sehemu kuu mbili. Kurugenzi ya mambo ya nje na ndani. Huko nje tuna mawakala kibao kamwe hatutowajua kwa macho!

TISS members wanapatikana kwa ujuzi wa hali ya juu sana, vetting huchukua hadi mwaka mzima. Nilipokua chuo yalinikuta haya... Kama isingekua.... Leo hii ningekua huko.
TISS ndo wanaratibu hata aina ya siasa na uongozi wa nchi, ndio wanaochezesha hata michezo michafu kama ile ya kina Zit...
TISS wanacheza sana na saikolojia za watu, propaganda kwao ni somo kule chuoni, kuna watu maalumu wapo kwenye vyombo vya habari, mitandaoni nk wakileta habari wanazotaka tusikie kwa malengo yao... Amini nakuambia!

TISS ni dubwana kubwa! Usidanganywe na neno 'idara' kisheria hawaruhusiwi kuendesha any operation lakini.... Pia wao kwa wao hawajuani maana kule unafanya kazi kwa amri na maelekezo kama utapewa kazi ya udukuzi utaifanya tu hata kama kwa mke wa rais

Sitaki nilinganishe vyeo vyao... Nataka ujue majukumu ya kazi zao.. Wengi hatumjui rais ajaye Ila miongoni mwao wanajua mda mrefu. Pia depo yao ile ya Siri pale ba... Sio mchezo! Pale ndo wanatoka PSU kwa ajili ya ulinzi wa viongozi, snipers wa kazi maalumu na wale wasiojul...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kidogo umejitahidi kuelezea, asieelewa hapa hatokuja kuelewa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itifaki ina mambo lukuki sana,kwanini Rais wa JMT akienda kwenye sherehe za mapinduzi Zanzibar huingia uwanjani mapema kabla ya Shein ni kwamba kiitifaki Rais wa Znz ni mdogo kwa wa JMT ila linapokuja suala la maadhimisho kama haya yanayohusu kwa mfano sherehe za mapinduzi ya Znz basi hii shughuli mgeni rasmi atakuwa Rais wa Znz kwa kuwa yeye ndiyo kiongozi wa Znz na shughuli nzima ni ya Wazanzibar na ndiyo maana hata kwenye lile gari la wazi analopanda Rais kuwasalimia wananchi waliojitokeza uwanjani huwa Rais wa Znz anapanda na Mkuu wa Jwtz kwa upande wa Znz na siyo CDF wa JMT hiyo ni kuuonesha umma kuwa shughuli husika inamhusu Mzanzibar na kwa kuwa wana Rais wao basi ni Rais wao ndiyo atakuwa mgeni rasmi ktk sherehe zile ila linapokuja suala la JMT basi senior ni Rais wa JMT.

Unyeti wa majukumu ya TISS unatokana na dhima nzima ya kuianzisha idara ile lakini hauipi uhalali wa idara kuwa kubwa kimamlaka kuizidi JWTZ au Polisi Tanzania,hata sheria haiko hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sijui ila huwa nafikiria kuwa TISS ni kitengo ambacho ni cross-cutting kati ta taasisi za kijeshi na za kiraia pia. Kwa hiyo Mkurugenzi wa TISS anaweza kuwa ni mkubwa kwa BAADHI ya walio chini ya taasisi hizo, lakini hawezi kuwa mkubwa kwa wakubwa wa Taasisi zile ambazo ni za kijeshi. Anaweza kuwa mkubwa kwa wakubwa wa taaisi zile ambazo ni za kiraia tu basi!
 
Hilo dubwana unalolisema mkuu ukimaanisha system siyo TISS tu mkuu ni pamoja na hao unaowaona ni wadogo kwa mkurugenzi wa tiss,ukitaka tubishane juu ya hili tutabishana sana mpaka mwisho wa dunia ila elewa tu IGP ni mkubwa sana kuliko huyo wa TISS.

Alafu mkuu kwenye haya mambo ya uongozi wa wakuu hawa usibabaike sana na aina ya majukumu waendayo kuyafanya huko naona hapa ndiyo panakuchanganya sana na kumuona IGP ni mdogo sana kwa DGTISS.

Hivi kwa mfano mkuu wa sasa wa TISS ana cheo gani cha kijeshi? Si ametoka Polisi akiwa ACP? Hapa tu unaweza kuona ni vipi ni mdogo kwanza kicheo tu na Insipekta Jenerali wa Polisi tena kwa mbali sana,hao kina Mzena,Kitine,Kombe na Apson walikuwa na vyeo wengine ni Kanali tu wa Jeshi kwahiyo usibabaike sana na aina ya majukumu anayoyafanya na kudhani yeye ndiyo kila kitu.

Kama unaona kushauri moja kwa moja kwa Rais masuala ya usalama ndiyo ukubwa pekee basi tambua hata huyu IGP kila siku iendayo kwa Mungu anaingia kwa Rais kumpa taarifa za masuala ya kiusalama wa Nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kombe alikuwa Major General ndo akaingia Tiss na Apson alikuwa Colonel
 
Sujui tukuelezaje uelewe, TISS inatambulika kama idara lakini ni "dubwana" kubwa sana Diwani kabla hajawa DGIS alikua huko polisi nani alifahamu? Kipilimba alikua BOT nani alifahamu ni Tiss? Imran kombe alitoka jeshini, kitine alitoka jeshini... Huwez kua TISS member bila kupita kule kwenye shule zao.... Wao wanakupangia sehemu ya kwenda kufanya kazi kulingana na mahitaji yao, unaweza kwenda jeshini, bungeni kama akina membe, polisi, boda boda nk. Pia unaweza kua hata mkuu wa jeshi. Usifuate sana itifaki na sheria kuangalia muundo wa TISS kwani ni very complicated kuung'amua. Wanasema idara ipo chini ya waziri wa utawala bora ukienda kwenye idara za utawala bora huwaoni.

Kwao wao rais ni "sponsor" ndiye mlaji mkuu wa taarifa zao. Wanashauri nani awe nani, na nani akae wapi!! Kiufupi wao ndo Wana control serikali ikiwemo na kuhakikisha usalama ni wa uhakika. Kwa majukumu hayo DGIS anaweza kua sawa IGP? Tumieni ubongo kidogo

Pili TISS wanahusika na mambo ya nje,( kurugenzi ya mambo ya nje) wana watu wanaokusanya taarifa,kuzichambua na kuchukua hatua kwa masuala ya kimataifa, hapo kwenye kuchukua hatua wanavaa koti la ubalozi, uwaziri nk... Huwezi kuwajua tu kwa macho... Wote hawa wanaripot kwa DGIS, unapata picha ya ukubwa wa huyo bwana? Braza kaka yangu ni OCS kituo Fulani hp temeke hata nilivyomuambia kuhusu huu mjadala kaishia kucheka... IGP ana deal na polisi tu, polisi wanaopewa oda hata na mwenyekiti wa mkoa wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumedhajadili sana hilo, ila huyu bwana ameamua kuwa mbishi tu. DGIS wasimuone amekaa pale wakamchukulia ni mtu wa kawaida huyu bwana ndio amewapa mkate hao wakina CDF na IGP kwa hiyo huwezi beza ukubwa wake...

Hata kwenye recruitment ya URAIS yeye ndio ana mchango mkubwa pia...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijui ila huwa nafikiria kuwa TISS ni kitengo ambacho ni cross-cutting kati ta taasisi za kijeshi na za kiraia pia. Kwa hiyo Mkurugenzi wa TISS anaweza kuwa ni mkubwa kwa BAADHI ya walio chini ya taasisi hizo, lakini hawezi kuwa mkubwa kwa wakubwa wa Taasisi zile ambazo ni za kijeshi. Anaweza kuwa mkubwa kwa wakubwa wa taaisi zile ambazo ni za kiraia tu basi!
Tiss ni civilian agency
 
JWTZ wana idara yao ya usalama ikiitwa Military Intelligence nao wanafanya kazi kama wafanyayo TISS na kabla CDF wa sasa hajawa CDF amewahi kuiongoza MI,lakini pia PT wana idara yao ya usalama wakifanya kazi kama TISS na wote wakiripoti kwa mtu mmoja sasa kuipaisha juu TISS sana ni kupotosha tu mambo.
Hata vikao vya ulinzi na usalama vya taifa muundo wa ukaaji ni ule ule TPDF ni top,akifuatiwa na IGP.

Na ndiyo maana kwa nchi nyingine nyingi Idara ya Usalama kama TISS yetu unakuta iko ndani ya Jeshi kama la JWTZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
British Agent James Bond 007 under MI6 (Military Intelligence 6), with his Boss, Mr. M....... In one occasion katika scenerio moja, M anamwambia Bond

...................."this damn thing could break out into a full scale war, and that's why I'm out here myself,..., so you need to move faster double O seven!

Hawa watu wanavyofanya kazi zao huwa wananifurahisha hadi akili yangu inasikia maumivu. Kabisa yaani!
 
Kwa hili la Rais nakataa Pascal Mayalla hakupatia km upo uzi weka au aweke hapa
Nakumbuka Pasco alikuwa kwa Mamvi
mpaka Jamaa anaongea na Waandishi wa Habari bado Pasco hakua kwake
IGP bado ni mkubwa kicheo kuliko DG wa TISS
Masuala ya Muungano yaache yalivyo na bendera, wimbo wao nk, lkn Amiri Jeshi na Mkuu wa Majeshi hawabadiliki hata km Rais wa Zanzibar atakagua Gwaride
Ujio wa JPM haukupangwa na TISS wala hawakumuambia akachukue fomu ila wao wanathibitisha kuwa atafaa kuwa Rais baada ya Kamati na wajumbe wa Chama kutumia Kura, kwani ndani ya Chama UWT (TISS) wapo
Kwanini TISS hawakumpitisha Membe jamaa yao au kumuongezea kura hata amkute J Makamba?
Uzi upo Pasco aliwahi kuandika hata mimi nilikuja kuusoma baadaye sana hata Rais tayari akiwa madarakani, nilishangaa sana. Pasco yuko safi namuaminia, ila naona kama siku hizi naye kuna baadhi ya vitu vimeshaanza kumpita, maana unaona anauliza swali ambalo ni dhahiri kuwa halikutakiwa kuulizwa na mtu kama yeye!
 
Comrade Makanyaga
Umenifurahisha Sana

We chukua tu, uchangie maendeleo ya ya Chama na Nchi

Kiuhakika, Wazee wa Makoti (kule juu) wanajua nani anafata baada ya Mzee wa sasa.

Ndio maana AJAYE yuko protected ili asichafuke kwa namna yoyote hata vyombo vya habari viko well directed kumlinda bila hata wao kujua.

Wazee wa Makoti ndio Engine ya Gari letu linaloitwa TANZANIA

Yaani wewe hapa sasa umenikatisha tamaa kabisa. Maana nilikuwa na mpango wa kuchukua fomu ya kugombea mwaka huu, lakini kwa namna ulivyoandika hapa, umenipa uhakika kabisa kuwa siwezi kuwa mimi. Nimeahirisha kuchukua fomu, lakini pia nashukuru kwamba umenisaidia ku-save hiyo Shillingi million moja ya kuchukulia fomu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Comrade Makanyaga
Umenifurahisha Sana

We chukua tu, uchangie maendeleo ya Chama na Nchi

Kiuhakika, Wazee wa Makoti (kule juu) wanajua nani anafata baada ya Mzee wa sasa.

Ndio maana AJAYE yuko protected ili asichafuke kwa namna yoyote hata vyombo vya habari viko well directed kumlinda bila hata wao kujua.

Wazee wa Makoti ndio Engine ya Gari letu linaloitwa TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazee hawa wa makoti bahati mbaya wakati mwingine wanalaumiwa sana, lakini ukiwaangalia walivyo fair, wako almost next to God. Wangekuwa wanafanya kazi kwa kutoa Press Release, naamini baadhi ya watu wangefanya makosa hata ya kuwaabudu! Mungu awabariki, tuko pamoja nao sana tu. Maendeleo ya Nchi nitachangia kwa namna nyingine, fomu nimeahirisha!
 
Haaaaahhhahh
...jiandae kupiga kura 2025
2020 achana napo, Siku ya kupiga kura nenda zako shamban tukalime

Huku tukisubiri MZEE aapishwe pale Taifa
Wazee hawa wa makoti bahati mbaya wakati mwingine wanalaumiwa sana, lakini ukiwaangalia walivyo fair, wako almost next to God. Wangekuwa wanafanya kazi kwa kutoa Press Release, naamini baadhi ya watu wangefanya makosa hata ya kuwaabudu! Mungu awabariki, tuko pamoja nao sana tu. Maendeleo ya Nchi nitachangia kwa namna nyingine, fomu nimeahirisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tiss ni civilian agency
Unamanisha nini hapa sijaelewa? You mean kuna civilian agencies ambazo zina uwezo wa ku-operate beyond civilian borders, muundo wake ukawa umeingia hadi ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, JW, PT, MT, n.k.?
 
Mkuu asiyetaka kueleweshwa muache abaki na ujinga wake.
MG ni Jeshi la Akiba pamoja waliopitia JKT na kimsingi mafunzo yao wanafundishwa mafunzo ya msingi ya kijeshi kama ulengaji shabaha nk sasa yeye kubisha kuwa hawafundishwi mafunzo ya kivita sijui labda atuambie wanafundishwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Usibishane na MTU ambae haelewi kitu

Majeshi ya akiba yote yanpitia mafunzo ya kivita ingawa tu tofauti ni basic sio advanced sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sujui tukuelezaje uelewe, TISS inatambulika kama idara lakini ni "dubwana" kubwa sana Diwani kabla hajawa DGIS alikua huko polisi nani alifahamu? Kipilimba alikua BOT nani alifahamu ni Tiss? Imran kombe alitoka jeshini, kitine alitoka jeshini... Huwez kua TISS member bila kupita kule kwenye shule zao.... Wao wanakupangia sehemu ya kwenda kufanya kazi kulingana na mahitaji yao, unaweza kwenda jeshini, bungeni kama akina membe, polisi, boda boda nk. Pia unaweza kua hata mkuu wa jeshi. Usifuate sana itifaki na sheria kuangalia muundo wa TISS kwani ni very complicated kuung'amua. Wanasema idara ipo chini ya waziri wa utawala bora ukienda kwenye idara za utawala bora huwaoni.

Kwao wao rais ni "sponsor" ndiye mlaji mkuu wa taarifa zao. Wanashauri nani awe nani, na nani akae wapi!! Kiufupi wao ndo Wana control serikali ikiwemo na kuhakikisha usalama ni wa uhakika. Kwa majukumu hayo DGIS anaweza kua sawa IGP? Tumieni ubongo kidogo

Pili TISS wanahusika na mambo ya nje,( kurugenzi ya mambo ya nje) wana watu wanaokusanya taarifa,kuzichambua na kuchukua hatua kwa masuala ya kimataifa, hapo kwenye kuchukua hatua wanavaa koti la ubalozi, uwaziri nk... Huwezi kuwajua tu kwa macho... Wote hawa wanaripot kwa DGIS, unapata picha ya ukubwa wa huyo bwana? Braza kaka yangu ni OCS kituo Fulani hp temeke hata nilivyomuambia kuhusu huu mjadala kaishia kucheka... IGP ana deal na polisi tu, polisi wanaopewa oda hata na mwenyekiti wa mkoa wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa unazingua kufanga vetting ya MTU haimaanishi ndo unakua makubwa kwake,

Wewe mwenyewe unajipinga kwa logic yako. Maana Umesema wanafanya hadi vetting ya rais je inafanya DG-TISS kuwa mkubwa zaidi ya raisi????

Seniority jeshini ndo kila kitu.ukiuliza nani makubwa tunaangalia chain of command na protocol.

Wanavojipanga kwenye mkutano ndo ukubwa wao hivo hivo

Cdf-IGP- (DG-TISS)-----

Sent using Jamii Forums mobile app
 
British Agent James Bond 007 under MI6 (Military Intelligence 6), with his Boss, Mr. M....... In one occasion katika scenerio moja, M anamwambia Bond

...................."this damn thing could break out into a full scale war, and that's why I'm out here myself,..., so you need to move faster double O seven!

Hawa watu wanavyofanya kazi zao huwa wananifurahisha hadi akili yangu inasikia maumivu. Kabisa yaani!
Teh [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom