Unaweza ukawa na sababu kusema hivyo lakini pia idara inaonekana imezidi kuwa bora siku hadi siku,kuteteleka kupo kwa taasisi yoyote ile ila mpaka sasa idara imepiga hatua sana.
Hata nchi zilizo na nguvu za kijeshi duniani tumeona ni namna gani idara zao za kijasusi zilivyoyumba mara kwa mara na kutoa mwanya kwa maadui kutekeleza yao.
Mfano shambulio la WTC miaka ile NY na PENTAGON idara za ujasusi hasa CIA walikuwa na taarifa za kutokea kwa mashambulio nchini mwao ila kwa sababu walizozijua wenyewe viongozi wa CIA na FBI hawakuwa wakishea taarifa za kijasusi hadi dakika za mwisho wakapigwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app