Kutoka kwa Mtanzania mwenzetu Twahir Abbas

Ideas tena sio ideas tu yaani useme watu wazae bila mpango wa kujua wataleaje watoto tukukumbuke haiwezekani, only constructive ideas ndio tutazikumbuka, Newton, hakujenga hata banda lakini tunamkumbuka suala la mabarabara halitupi pressure
 
Wale mnaodhani flyovers au interchange ni bigdeal mjue kabisa sisi sio mapoyoyo kiasi hicho ile sio hisani ni pesa na kodi ya mtanzania, hakuna kiongozi aliyetoa pesa yake mfukoni kujenga reli, kujenga hospital, kujenga madarasa ile ni kodi ya watanzania na ndio hata kama ni mkopo wao wanalipa sasa awamu ya tano mlisahau hamtumii pesa zenu isipokua ni fedha ya watanzania wote wa dini na vyama vyote sasa mlivyoanza kuwabagua kwa vyama vyao tena wazi wazi hivi unatarajia umbague mtu kesho akeshe anakusema vizuri haipo hiyo
 
Binadamu lazima aongee. JK alikuwa anawashawishi watanzania wa ughaibuni warudi nyumbani ili wajenge nchi yao.

Kama vitu vinavyojengwa na kuonekana havina umuhimu JK asingehangaika kama alivyofanya angeridhika tu kuona MOI inabakia duni.

Angeridhika na tulivyokuwa wakati anaingia ikulu.

Ni upuuzi kuongelea legacy wakati kijijini kwa huyo jamaa aliye huko nje hakuna maji na umeme wa REA haujafika.

Diaspora huwa wamejawa na nadharia nyingi zisizo na mashiko kwa Tanzania.
 
Mtazamo wa mwanasayansi huyu unamchanganya mwenyewe ,anatuelezea matokeo ya Legacy kama ndio Legacy yenyewe.

Legacy ni Imani Kiongozi aliyonayo kwamba itatoa nchi hatua moja kwenda nyingine.Ikiwa imani yake haina matunda chanya Legacy yake inakufa kimyakimya,lakini kama ilikuwa inaleta matokeo yanayoonekana mtatamani kaburi lake lisionekane,kama wanavyoangaika na Mzimu wa Gadaf

Legacy ya Kiongozi ikiwa ni kupata uhuru wa kiuchumi kwa kuboresha miundo mbinu mikubwa na matunda yakaonekana Legacy hiyo itaishi .

Si kila kitu unabuniwa na wengine na kikapigiwa kampeni ukakiita Legacy.
Toka umeambiwa definition ya democracy kwamba ni Government of the people by the people basi ni mwendo wa kukariri tu.The Question is how? hapo ndipo kila kiongozi anaweza akaja na Legacy yake ya kufanya definition ya Demacracy iwe na maana.
Gadafi alikuja na Legacy yake mkaichafua na kuiita udikiteta leo baada ya kumuondoa kinyama kwa Legacy za kukopi walibya wamililia tena.
 
Binafsi sina shaka na aliyepo sasa ,hasa ikizingatiwa kuwa ndiye aliyekuwa Makamu wa Mwenyekiti wwa Bunge la Katiba; mchakato ulioishia njiani.
Tumpe muda.
Au nasema uongo ndugu zangu?
Wasiwasi wangu ni kwamba alipokuwa kwenye kamati ya bunge la Katiba hakuwa ameonja hiyo nafasi.

Mtu ambaye ameonja nafasi ya urais kwenye taifa lenye Katiba mbovu hawezi kukubali aibadili labda mpaka atakapoona anakaribia kuondoka kama hayakuwa mroho wa madaraka.

Nachokiona ni labda ataachana na huo mchakato wa Katiba mpya au atauleta mchakato huo kipindi anaondoka ili yasimkute yatakayokuwepo kwenye Katiba mpya
 
Hebu acha kupotosha maana ya neno Legacy.


 
Umemaliza mkuu. Magu hana legacy yoyote zaidi ya kuua watu kwa wingi ili kuficha madhaifu yake
 
Niongeze na Nelson Mandela anakumbukwa kwa kupigania uhuru wa Africa kusini na kuleta utangamano kwa taifa. Flyover za Afrika kusini zilijengwa na makaburu lakini hawakumbukwi.
 
Hebu nisaidie Kiongozi... Ni kiongozi gani duniani aliwapa urithi taifa lake kutoka mikononi mwake au mfukoni mwake.. na alifanya mambo ambayo wananchi hawakumtuma awafanyie!?

Kama hayupo chukua Rais au Mfalme yeyote ambaye ni relevant kwa maisha yetu leo, unipe mifano ambayo amefanya kwa watu anaowaongoza kwa fedha yake na leo tunai-recognize kama Legacy ya Kiongozi huyo.

I would love to learn, ili wenye nia ya kujifunza tujue zaidi juu ya "Legacy/Urithi" wa viongozi.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwa maelezo hayo ya huyo Msomi wetu, watu kama akina magufuli watakumbukwa kwa lipi! Kwa kutuletea udikteta na mataga, au!!

Mtangulizi wake JK nae alianza vizuri kwenye mchakato wa Katiba Mpya, lakini mwisho wa siku akakengeuka!

sio mbaya nyumbu mkimsahau.
 


.
 

sasa anapaswa rais afanye kipi ionekane ni alama ya pekee ameweka!!!maana akiwa kama rais kila anachofanya ni kile anachotakiwa kufanya.

wewe ukijenga nyumba bora tukupuuze tu maana ni baba anayetimiza wajibu wake,unadhani mababa wazembe watajipima wapi???
 

kwani angefanya lissu angetoa hela mfukoni!!!
 

[emoji38][emoji38]anasema hivyo si vitu vya kuacha legacy.

wakati asipotuma pesa ya matumizi nyumbani kwao kwa mwezi,roho yake haitulii.
 
BAK huyu Twahir Abbas mwambie aende duka lolote lile aka chukue nguo za Idd nitalipa.
Naunga mkono hoja, jamaa kaongea vizuri sana kuhusu legacy, ni virtues na sio material things. Nilidhani utamtafuta umpe kitu kitamu kitamu, chenye thamani, kama kumpa kitu kitamu kama tunda ale, afurahi, mfano mpe tunda kama apple, wewe umege kidogo na kumpa na yeye amege, akipendezewa, mpe yote!. Zile apples nyekundu za South Africa zingefaa sana
P
 
Dah! Nilitaka kukomenti, lakini baada ya kuona picha ya mwandishi, nimeghairi!
 
Sasa mtoto wa Tunguu huko Zanzibari angejuaje habari za Abrahamu kama amejenga barabara wakati alitoshelezwa na kuambiwa habari za maana ya Demokrasia kisha jambo likaishia hapo,ila huko kwao watoto wa huko huenda hata hawajui habari za maana ya Demokrasia aliyoitoa Ahrahamu ila wanajua kuhusu ujenzi wa barabara.
 
Niongeze na Nelson Mandela anakumbukwa kwa kupigania uhuru wa Africa kusini na kuleta utangamano kwa taifa. Flyover za Afrika kusini zilijengwa na makaburu lakini hawakumbukwi.

hawakumbukwi na wewe,sababu kwanza unawataja kama makaburu makusudi kabisa.

ila SA leo ndio nchi iliyopiga hatua kuliko zote africa sababu ya hao makaburu,sio huyo mandela na uhuru wa 1992.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…