Kutoka kwa Mtanzania mwenzetu Twahir Abbas

Lakini watawala wengi huacha legacy na kukubukwa kwa MAWAZO mazuri yanayoishi, yenye manufaa ENDELEVU na UJENZI wa MIFUMO mizuri yenye tija kwa kizazi kimoja hadi kingine katika kupambana na UMASIKINI, UJINGA, MARADHI na DHULUMA.

Shukrani, mataga wasome bandiko lote hili murua kabisa hapa JamiiForums tukielekea 40 ya mwendazake.
 

nyumbu wana tabu mkuu,yaani bora uchunge mbuzi 10 kuliko kumwelewesha nyumbu mmoja.
 
[emoji38][emoji38]anasema hivyo si vitu vya kuacha legacy.

wakati asipotuma pesa ya matumizi nyumbani kwao kwa mwezi,roho yake haitulii.
Diaspora ni mafundi wa kukosoa. Ni burudani ya kipekee ukiwa nao katika group moja la whatsapp, huwa na maoni fulani ya ajabu.
 
Bibi yangu nilidhani alikuwa akithamini sana vitu....nilikosea sana, nilikuja kugundua.. yeye akithamini zaidi tendo la kupewa au kupata. Vitu vilimkumbusha tu watu, na matokeo ya jitihada na upendo wao kwake.

Vitu kwake vilikuwa alama tu ya jambo la muhimu zaidi (uhusiano) lilikokuwa likigusa moyo wake. Maneno matupu hayajengi... Mawazo mazuri ila matupu yasiyo na vitendo vya kuyadhihirisha ni ubatili.

Legacy au urithi wakati mwingine si wathamani kubwa.. ila moyo na jitihada za upendo za mtoaji huishi ndani ya zawadi hizi ndogo. Na wapokeaji wenye hekima hupokea hata ikiwa si cha thamani na watakitunza na kukithamini.



Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mantiki hiyo, tuihimize UNO hiyo pia imusifu Idd Amin na watu wa namna hiyo!

Kiongozi anapokanyaga haki za raia zake hayo mengine anayofanya hayana maana yoyote.

Watumwa waliochukuliwa hapa, hao waliofanya hivyo nao tuwashukuru kwa vile baadhi ya hao watumwa walipewa maisha mazuri?

Kuna mambo ya msingi yasiyotakiwa kwa kiongozi yeyote kuyakanyaga. Akifanya hivyo anaharibu kila kitu.

Kiongozi akanyage Katiba, aliyoapa kuilinda, halafu leo tuseme shilingi ina pande mbili?
 
Toka nimejiunga JF huu ndio uzi 100%
 
Busara tupu hizi. Mawazo huishi milele bali majengo ni ya muda.
 
Soma kitabu kinaitwa; War in Uganda and legacy of IDD Amin.
"By Tony Avirgan and Martha Honey."
Kiliandikwa na waandishi wamarekani walioshiriki kwenye vita ya Kagera mwanzo mppaka mwisho
 
Magufuli hata yale mazuri aliyofanya yaliharibiwa na mambo mabaya kupita kiasi aliyofanya. Kila nikikumbuka watu walivyofariki kwa corona kwa kukosa miongozo sahihi ya serikali huku yeye anakataza watu kuongelea kabisa hilo suala huwa naona akili zake zilikuwa zina hitilafu. Watu wanakufa kwa mateso makali na rais anajua lakini anajifanya hakuna shida yoyote?
 
Soma kitabu kinaitwa; War in Uganda and legacy of IDD Amin.
"By Tony Avirgan and Martha Honey."
Kiliandikwa na waandishi wamarekani walioshiriki kwenye vita ya Kagera mwanzo mppaka mwisho
"---waandishi wamarekani walioshiriki kwenye vita ya Kagera"? Kulikuwepo na 'mercenary' katika vita hivyo?

Siwezi kwenda kusoma kitabu kwa jambo kama hili.

Kwa hiyo waliandika nini, jinsi Idd Amin alivyoitumikia Uganda kwa uaminifu mkubwa na jinsi waganda walivyompenda kiongozi wao?
 
Reactions: BAK
Yote hii ni kuhangaika na marehemu,hakika wewe ni mwehu,hutoweza kumfuta
 
Hebu acha ujinga wako! Ni wapi ilipopigwa marufuku kumjadili magufuli akiwa hai au mfu!? Mbona yesu anajadiliwa mpaka kesho kutwa? 😳
Yote hii ni kuhangaika na marehemu,hakika wewe ni mwehu,hutoweza kumfuta
 
1.Hayati Mwl.J.K.Nyerere alifanikiwa kuwaunganisha watanzania wa makabila yote nchini kwa matumizi ya lugha ya kiswahili. Mtazania anawasiliana na mtanzania mwenzie vizuri popote pale nchini kitu ambacho in adimu kwenye nchi nyingine.

1.Mahtma Gandhi anakumbukwa kwa kudai Uhuru kutoka kwa waingereza kwa kuhamasisha uasi na mapambano ya kudai Uhuru bila kusababisha uharibifu wa mali na watu.(Non violent protracted peoples war) Hatimae akashinda vita na India ikapata Uhuru.

3.Nelson Mandera ;.
Huyu alifungwa miaka 27 na makaburu, alipoachiwa na kuchaguliwa kuwa rais wa Afrka ya kusini, aliunda tume ya ukweli na maridhiano ili kujenga taifa moja llilokuwa limegawanyika kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na kutawala muhula mmoja licha ya mateso yote ya miaka 27 gerezani.
Gereza alipokuwa amefungwa, kitanda alichokuwa akilala na vifaa vingine alivyokuwa anatumia ni vivutio vya utalii.

Wapo akina Winston Churchill , Franklin Roosevelt. Jerry Rawlings na wengine,
 
Usiwe mvivu wa kusoma, we soma kitabu utaelewa mkuu.
 
Mandele hajufungwa miaka 27 ni uongo mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…