Kutoka kwa Mtanzania mwenzetu Twahir Abbas

Anaandika mtanzania mwenzetu Twahir Abasi (kutoka Chuo kikuu cha Sayansi na teknolojia cha Huazhong, huko Wuhan, China).
______
Legacy ya watawala haipo sana kwenye ujenzi wa vitu labda vitu hivyo viwe ni VIKUBWA SANA, vya muhimu sana au vya kipekee sana. Kwa mfano Great wall ya China au Pyramid za Misri.

Lakini watawala wengi huacha legacy na kukubukwa kwa MAWAZO mazuri yanayoishi, yenye manufaa ENDELEVU na UJENZI wa MIFUMO mizuri yenye tija kwa kizazi kimoja hadi kingine katika kupambana na UMASIKINI, UJINGA, MARADHI na DHULUMA.

Thomas Jefferson wa Marekani hakumbukwi kwa visima vya maji alivyochimba, bali anakumbukwa kwa Tamko la Uhuru wa Marekani (Declaration of Independence).

Abraham Lincoln hakumbukwi kwa barabara alizojenga huko New York na Michigan, bali anakumbukwa kwa tamko la kishujaa la kuachia huru watumwa (Emancipation declaration) na Falsafa ya demokrasia (Philosophy of democracy).

Yeye ndiye aliyesema "democracy is a government of the people, by the people, for the people" definition ambayo vizazi na vizazi vimeikariri duniani pote. Mtoto wa form one kule Tunguu (Zbar) au Lutindi (Korogwe) ukimtajia Abraham Lincoln hatakumbuka barabara alizojenga huko Maryland, bali atakumbuka "government of the people, by the people, for the people." Hii ndiyo legacy.

Hata Mwalimu Nyerere hatumkumbuki kwa kujenga viwanda vya nguo vya MWATEX na URAFIKI, au kiwanda cha nyama cha TANGANYIKA PACKERS, bali tunamkumbuka kwa MAWAZO yanayoishi ya kudai UHURU, HAKI, UMOJA na HESHIMA ya MWAFRIKA.

Kizazi kijacho hakitakumbuka Stendi za mabasi, wala madaraja ya juu yaliyojengwa miaka 20 au 50 iliyopita, maana hata chenyewe kitajenga yao. Tena ikibidi hizi flyover za sasa watazivunjilia mbali ili wajenge nyingine zenye ubora zaidi, nyingi zaidi na za kisasa zaidi.

Kizazi kijacho kitaona legacy ya watawala wa sasa kikikuta nchi yenye HAKI na UHURU kama vichocheo vya MAENDELEO YA WATU. Kwa hiyo KATIBA bora ni msingi wa LEGACY imara, Sheria nzuri ni kuta za LEGACY imara, na MIPANGO thabiti ni Paa la Legacy Imara. Legacy sio madaraja au stand za mabasi.

Muhimu zaidi Legacy hailindwi, inajilinda. Legacy haitetewi, inajitetea yenyewe. Asomaye na afahamu.!
 
Hoja siyo muda aliotumikia kifungo, hoja ni legacy alioiacha.
Mandela alifungwa miaka 27 mkuu.Miaka 18 kwenye jela iliyokuwepo Robben Island.Anayekanusha aje na ushahidi mwingine.
 
Naona kama anajifunza kuota. Nadhani huyu anajifunza kutumia ile dhana ya kuku na yai nani alianza. Kwa leo hajapatia bali aendelee kujifunza kuhoji na hojaji bila kupotosha.
 
Kwa waliomulewa WAMEMUELEWA na kumpigia makofi mengi sana kwa umahiri wake.
Naona kama anajifunza kuota. Nadhani huyu anajifunza kutumia ile dhana ya kuku na yai nani alianza. Kwa leo hajapatia bali aendelee kujifunza kuhoji na hojaji bila kupotosha.
 
Lazima tutofautishe changamoto za USA na Tanzania.
Wao changamoto yao ilikuwa ni hiyo slavery , wakati sisi tumekuwa na shida ya ufisadi na maendeleo ya physical structure ambayo ilikuwa inadumaza mazingira ya Maisha yetu na biashara pia.
Hivyo maono ya mtanzania juu ya "legacy" ya kiongozi ita focus huko.
Nakumbuka enzi za "boys to men" watu humu kwenye jf waliwekapicha za barabara zenye flyover Na spaghetti, ikiwa ni matarajio yao kwamba ndipo tunakopelekwa.
Bahati Mbaya haikuwa hivyo.
Legacy ya mjerumani ingawa ilikuwa kwa force labour n.k lakini hadithi za wazee wetu juu ya maendeleo fulani ilikuwa ni Yule mjerumani Bwana, hana mchezo mchezo katika kutekeleza kwa jambo au kitu. Ni Bahati Mbaya ndio hivyo, lakini hatujui, ingekuwaje ange weza kuongoza kwa hiyo miaka 10.
Kuhusu legacy yake kuishi au kutokuishi, kwa Sasa bado ni mapema sana kwani bado kuna miradi haija isha, kama hiyo sgr, na hydropower.
Kinacho tokea sasa hivi ni siasa za kutoka utawala wa tano kwenda wa sita , bila kufanya uchaguzi , bali kufuata katiba endapo jambo kama hilo linatokea na pia kupata nafasi kwa mafisadi kupumua Kidogo, baada ya aliyewathibiti kutokuwepo.
Na jambo kama hilo tunaliona USA na issue kama Obama care ilivyotaka kutenguliwa na Trump
 
Sasa kwa maelezo hayo ya huyo Msomi wetu, watu kama akina magufuli watakumbukwa kwa lipi! Kwa kutuletea udikteta na mataga, au!!

Mtangulizi wake JK nae alianza vizuri kwenye mchakato wa Katiba Mpya, lakini mwisho wa siku akakengeuka!
Shida ya viongozi na wanachama wa ccm wao wanawaza kutawala tu. Hawana muda wa kufikiria juu ya Tanzania ya wajukuu zao itakuwaje.

Yaani wakati majira na nyakati zinabafilika wao bado wanawza kushika madaraka tu hata kwa njia haramu lakini mradi watawale.
 
Mwl. Nyerere (Aendelee kupumzika kwa Amani Shujaa) hakuita watu chini ya mti kuwaunganisha... Alitumia vitu vya serikali ikiwemo fedha magari, watumishi majengo nk.. na kwa wakati wake we needed that.. twas a new country lazima tuunganishwe kwanza..

Mahatma Gandi its a story for another day .. there is what you have been fed and what's true. Read about Subash Chandra Bose. Gandi divided people and broke India in pieces for English Interests. So was Mandela.

Mzee Mandela, we can debate, his move ilitengeneza illusion ya usawa ila ukweli halisi huo usawa na maridhiano haukuja.. na kufungwa miaka 27 don't make you a hero no kumsamehe mtu aliyekufunga miaka 27 kupigania haki yako hakukufanyi Masiha

Bottom line the causes they tried to pursue was good and just.. ninachojihoji where did they use their money/resources to do that. Na walifanya for who!? How do you separate mahitaji ya watu na ndoto za kiongozi!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
[emoji108]Maneno kuntu
 
Twahir Abasi anaongelea tofauti katika ya legacy ya Statesman na Populist.
Tufafanulie kama alivyofafanua mwenzio Twahir Abasi, hoja yake imetulia na inaeleweka tena kwa kiswahili hiyo "Legacy ya Statesman" na hiyo "Polulist" ndio ushuzi gani sijui

Yaani hata 40 bado mnashindwa kutetea aliyo aliyoyasimami huyo muuaji ambayo wenyewe mnaita LEGACY sasa badala ya kukienzi Kiswahili mnacho dai alikipeleka SADC unaletea kingereza uchwara humu

Mxieusssszzzz shuwani kweli nyie [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mnaopinga kwa nguvu nanyinyi what ia ze bigidili?[emoji16]
 
Better than mwandishi wa China...
The home of fakes[emoji16]
 
Hata kumuongelea ni kumsifia pia.
Endelea kuandika boss.

Ukiona hafai ignore him wala usiandike.
Otherwise kivuli chake kitaendelea kukutesa...

Haters made him powerful[emoji16]
 
Kwa maana mkataba was better before Magufuli intervention?

Accounting my left foot[emoji16][emoji16]
 
You don't need a lot of energy and time advocating for ones legacy, let's remind our leaders to do good deeds for public interest and the legacy will come calling.
 
Hoja za Kitoto Sana ,alafu zimetolewa na Dr
 
Hata kumuongelea ni kumsifia pia.
Endelea kuandika boss.

Ukiona hafai ignore him wala usiandike.
Otherwise kivuli chake kitaendelea kukutesa...

Haters made him powerful[emoji16]
Ametutesa sana huyu shetani, let him rest in hell forever. Na kama unampenda you can equally follow him and be buried with him at Chato.. Nitatesekaje wakati mtesi analiwa na funza na minyoo sasa hivi? Unadhani Mungu ni wa Wasukuma pekee?? Katenda tuliyomuomba baada ya kupiga kila goti
 
Kwa maana mkataba was better before Magufuli intervention?

Accounting my left foot[emoji16][emoji16]
Magufuli alichofanya ni kututoa kwenye mrahaba wa 6% alizoziacha JK na kwenda 16%. Naye Kikwete alitutoa kwenye 3% aliyoiacha BWM hadi 6%. Hayo ndiyo majukumu ya u-Rais, na hayamfanyi leo hii tuanze kumtukuza, sisi tulimchagua na tukamwauajiri afanye kazi hizo.

Vile vingine vinaitwa 50/50 economic benefits, na fact ya kuwa sisi ni class 2 shareholderskwenye Twiga Mining Company hazina any meaningul or incremental benefits. Transfer pricing will absorb all profits
 
Yuko vizuri.. ..

Raisi wa sasa Mama samia atafanya mambo makubwa, na yenye kufurahisha sanaa.. .. na nchi huenda ikaingia kwenye top ten ya nchi zenye furaha duniani.. mpo hapo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…