Mahondaw
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 67,252
- 168,563
Sehemu ya 5
Watu walilala ila yule muhindi akawa naye hajalala na mimi nilikuwa nimesimama nikijua kazi imeanza, nilisikia sauti ikisema mkate wenge mejaa, ghafla nilishtukizwa na kofi moja matata sana nyuma ya kichogo na kusindikizwa na mtama chini nilianguka mzima mzima mpaka chini na wenge lilikata kweli.
Muhindi yule bwana Bensonii naye hakutaka kukubali hivi hivi ila alitoa pesa haswa wenyewe wakisisitiza na kauli yao usitujazie nzi hapa. Na sisi wateja pia tuliibiwa na watu wakasepa.
Mimi nimeenda kuiba ila nikaibiwa kwa kweli jiji la Arusha nyakati hizo lilikuwa na ubabe sana sio mtoto, sio mwanamke, sio mzee kila mtu ni mbabe na hataki kuonewa. Polisi nao sio haba haswa kipindi hicho tukio likitokea mtakaa hadi nusu saa ndio muwaone. Mi nilitoka na sikuwaona wale jamaa zangu, ikanibidi nipige ngoko mpaka kule kambi niliwakuta na kuwahoji kulikoni?
Wao walisema mpango umefeli kuna watu wameuza ramani yao kwa genge lingine kukawa na mvutano wa hapa na pale kisha tukaachana kwa ahadi tutakutana tena siku nyingine.
Niliondoka Arusha nakwenda Rombo tena nikawakuta wadogo zangu na kuwapa zawadi kidogo kidogo, nakutaka kujua maisha yanaendaje kwa kweli malalamiko yalikuwa ni mengi haswa ukizingatia wabibi wakizeeka wanakuwa na maneno sana.
Niliwaahidi naenda mjini nakirudi basi ntawachukua twende wote mjini nao walifurahi na kuonyesha tabasamu lao ambalo kwangu lilinipa moyo sana na faraja.
Hii ilikuwa ni mwaka 2003 nakumbuka nilikuwa na moto sana wakutoboa kwenye maisha na kuwasaidia wadogo zangu hivyo dili za magendo ndio zilikuwa zina unafuu na chanel nilikuwa nishaanza kuziona.
Nyakati hizi niliungana na Mroso wa Matejoo na Palangyo wa Tengeru tuliungana na kuwa kundi moja hivo lengo letu lilikuwa ni kuendesha matukio ya ujambazi hii njia ya Arusha na Moshi haswa tukiwatarget wafanyabiashara wa madini maana walikuwa na fujo sana mjini kipindi wamepata hela na ilikuwa rahisi kuwagundua.
Tulijua kuwavizia huko Mererani ni risky sana maana nao huwa wako rafu mno katika uendeshaji na wengi wamejipanga hivyo tulibidi tujiongeze kwa kutafta wadada wawili mmoja kwa jina Mankah wa Machame Nronga na mwingine Adela Mrombo wa Mashati wote walikuwa weupe na wanalipa.
Hapa sasa tulimtafuta Kicherema yeye ni Mkenya mtaalam sana wa mambo ya madawa haya kizungu na alitupatia maji ambayo anasema ni kemikali sumu na inaweza kumzimisha mtu. Alitwambia ni nitrous oxide kwahyo hata sisi tuwe nayo makini. Tulianza kuwawinda haswa huko huko Mererani kwenye nyumba za wageni na 🍺🍻. Mara nyingi hawa wakishapiga mishondo wanakuwa na wapambe saivi ndio chawa ila kipindi hicho ni wapambe.
Nakumbuka aliingia Ima akiwa na wapambe wake akamwita meneja wa bar na kumpa hela acheze wimbo mmoja tu aliuchagua mpaka achoke. Kutokana na watoto wale wakichaga nimekaa nao pale wanaita jamaa alituma wapambe wake waje na sisi tulikuwa 5 jumla wanaume 3 na warembo 2. Hivo sisi hatukubana nao wakasema hawana hela hawa miyeyusho hivyo wakatuhama nakuhamia meza kuu ya hela.
Hapo tuliona mambo yanaenda kama tulivyopanga. Sisi tuliondoka na kwenda eneo letu kutulia tukisubiri ishara.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
"Mkate wenge mejaa"😂
kumbe akili zenyuu sio kosa lenu ni kawaida huko bange kubeli miraa bado pombe karee😎!!