Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Namie nimesoma hapo hapo,kumbe wewe Ni mboyzia mwenzangu. Nimelala kimweri dormitory miaka yote minne.
Hata mimi, henzi hizo maadui wetu wakubwa ni Milambo, hahahaah can't forget those moments. Tulikuwa na mademu(Tabora girls) karibu lakini hawatutaki, si mchezo enzi hizo
 
T
Good afternoon brothers and sisters 👋

Based on a true story!
Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivo fuatana nami mpaka mwisho.

Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni mchaga wa rombo useri na mama ni mchaga wa marangu kirua. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa hapa jijini Arusha wa vitambaa maeneo ya kilombero na mama yeye alikuwa mtumishi yaani mwalimu katika shule ya Arusha Secondary School kifupi Arusha sec. Tulikuwa tukiishi sakina maeneo ya silentini ndipo wazazi walipojenga.

Maisha yetu kwa kweli yalikuwa mazuri sana hapakuwahi kuwa na shida nyumbani upendo ulitawala na ndugu walitupenda sana na kila tukifunga shule basi bibi wa huko kijijini wa pande zote kila mmoja alikuwa anang'ang'ania tukakae kwake. Shule tulisoma nzuri mimi nakumbuka nilisoma st. Constantine iliyopo Arusha, shuleni tulienda kwa school bus na kurudi kwa school bus. Hata shuleni kulikuwa na tour za kwenda mbuga za wanyama mbali mbali na vivutio vingine nchini.

Kwa kweli shida sikuwahi kuzijua maana nyumbani tulikuwa hatuli maharage na dagaa maana mama alikuwa na vidonda vya tumbo. Nakumbuka hata nguo nlikuwa nafuliwa na dada wa kazi ambaye alikuwa mwenyeji wa Singida. Asubuhi ilikuwa lazima tule cornflex na maziwa. Nilikuwa mtoto wa geti kali hata kucheza ni ndani kwa ndani tu.
Mwaka 1995 nakumbuka nikiwa shule alikuja mjomba shule hivyo niliitwa ofisini kwa mwalimu mkuu nakuambiwa nirudi nyumbani. Tuliondoka na mjomba kwenye gari aina pegeout mpaka nyumbani ambapo kulikuwa na watu wengi tayari, sikujua nini kinaendelea kwa hiyo mimi na wadogo zangu tulikuwa na mjomba muda wote, ndipo baadae alipokuja baba mkubwa na kutuambia baba na mama hawapo tena! Mdogo wangu aliuliza wamesafiri watarudi lini? Alijibiwa hawatarudi tena na sasa ninyi ni jukumu letu.

Mimi sikuielewa na hakuna ambaye pia alielewa tukazidi kuhoji na tuliambiwa tu wameenda mbinguni kwa Mungu. Bado kwetu kuamini na kuelewa ilikuwa ngumu lakini tulienda kuzika Rombo na huko tulilia sana ila mdogo wetu wa mwisho Agness yeye wala hakulia ni kama alikuwa haelewi kinachoendelea. Mazishi yalikamilika hakuna aliyekuwa na nawasi wasi sana ila ndio hivo tulishabaki yatima bila kujijua.

Kilichobaki hapo ni mgawanyo wa mali na kwa mila zetu mimi ndio nilimikishwa mali zote za Mzee ikiwemo mashamba huko Rombo na nyumba hapo sakina. Na huko Rombo pia mzee alijenga nyumba yake. Kule kwa mama kirua pia napo mzee alimjengea mama mkwe wake nyumba.

Basi baba mkubwa ambaye alikuwa akiishi dar kwa wakati huo alisema angetuchukua tukaishi kwake huko dar na kwamba angetusomesha mpaka tutakapokuwa. Ile nyumba baba mkubwa alisema isiuzwe bali waishi ndugu zetu nayeye pia akiwa anakuja arusha aweze kufikia huko.

Sikuwahi kujua kuhusu hati ya nyumba, mafao yoyote ya mama maana alikuwa mtumishi na wala kujua kama mzee alikuwa na hela benki au akiba yoyote. Mzee alikuwa na magari 3 pegeout ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kupeleka abiria namanga, defender 110 ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kubeba abiria kutoka mererani kaza moyo kupitia mbuguni mpaka arusha mjini na staut nyeupe ambayo ndio alikuwa akiiendesha yeye katika shughuli zake ilikuwa ikimsaidia sana. Ila baba na mama walipata ajali ndani ya hiyo staut maeneo ya mto nduruma na umauti kuwafika hapo hapo!

Pegeout alibaki nayo mjomba akiendelea na ruti za namanga na ile defender 110 baba mkubwa aliipeleka kijijini ikafanye kazi ya kubeba maziwa na kuleta moshi mjini. Statut ilibaki imekaa juu maye na ilichinjwa ikauzwa.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatilia mkasa huu wa maisha ya kweli unaosisimua na kutoa machozi.

Yakwanza tayari bora kama ni fupifupi hivi ntawahi kuzimaliza
 
Sehemu ya 2
Tulienda dar es salaam na usafiri binafsi wa baba mkubwa nakufika, ambapo alikuwa akiishi kurasini karibu kabisa na mizani. Miasha ndani ya jiji ya dar hayakuwa mazuri sana maana joto lilikuwepo na mbu kwa wingi, haswa ukizingatia arusha hali ya hewa haswa ukanda wa sakina una baridi kwa kweli. Ndani ya wiki mbili 2 niliugua Malaria na kwa wakati huo dawa iliyokuwa ikitumika sana ni chloroquine. Ila dada zangu wao hawakuugua Malaria.

Tulikaa dar na baba mkubwa akatutaftia shule huko moshi ambayo ni ya bweni yaani kulala ili tusijihisi upweke pale nyumbani. Hivyo tulienda kusoma shule moja inaitwa Moshi Academy maeneo ya ushirika kibosho. ( Kwa watu wa moshi watakubaliana nami ushirika na kcmc zote zipo ndani ya kibosho).

Kwa maisha ya pale shule tulisoma na mimi nilifaulu ijapokuwa nilipata wakati mgumu sana haswa kwenye kubadili mtaala maana ukumbuke pale arusha shule tulisoma kwa mfumo wa Cambridge na sio huu wa Tanzania. Nilimaliza darasa la 7 mwaka 1998 nikawaacha wadogo zangu shule ambao nao walilia sana kuwa hawawezi kusoma hapo kama sipo. Lakini walibaki kusoma hapo hapo. Mimi nakumbuka baada ya hapo baba mkubwa alinipeleka tabora kwa shemeji yake ambaye alikuwa akikaa maeneo ya bachu. Nilifika tabora na nilifanyiwa mpango wa kujiunga na Tabora boys.

Nilianza kidato cha kwanza mwaka 1999 na mwaka huo ndio ulikuwa ni kama mwanzo wa mateso yangu. Baba mkubwa alikuwa amechukua mikopo hivyo mambo hayakuenda vizuri na duka lile la vitambaa pale kilombero lilokuwa la mzee aliliuza pamoja na ile nyumba iliyokuwa halali yangu kwa kisingizio cha elimu yetu ni kipaumbele kumbe alitumia kulipa madeni yake. Hivyo mambo yalianza kwenda kombo mimi nikiwa busy na shule baba mkubwa mambo yalizidi kuyumba sana baada ya hapo mke wake ambaye alikuwa ni mwenyeji wa tabora maeneo ya isikizya alimwambia sisi ndio chanzo cha mikosi na mabalaa yanayomkumba hivyo atuache turudi kwa bibi kijijini.

Baba mkubwa alijaribu kukaza shingo akiwa na nia thabiti ya kutusaidia ila shinikizo la mwanamke ukizingatia na hali inazidi kudorora kiuchumi, rasmi mrija wa misaada ulikata kwangu na kwa wadogo zangu, mimi pale nilipokuwa nikikaa nilihama mwenyewe kwasababu ya manyanyaso, kipindi hiko maji tabora yalikuwa ya shida hivyo unaeza tumwa kwenda kisimani unachota maji na baiskeli ukirudi unaambiwa uende upeleke mchele wa vitumbua mashineni hapo hujala chochote.

Ukirudi unaambiwa uwashe moto na kwenda kutafta kuni za kupikia ukirudi unakuta wameshakula wamekuachia ugali kidogo na kisamvu cha karanga. Ukishakula hapo ndio basi tena mpaka kesho tena. Mi kiujumla hayo maisha yalinishinda yamanyanyaso haswa ukizingatia sikuyazoea kabisa, nikaomba kuondoka kurudi nyumbani, nilipandishwa basi la nbs na kurudi dar. Dar napo nikapokelewa mzobe mzobe kwa kisingizio kwamba nimewatukana mama zangu wadogo na mkwe wa baba mkubwa hivyo nikafungashiwa virago na kupandishwa basi la ngorika kurudi moshi ambapo ntaenda kijijini Rombo kwa bibi.

Kweli nilifika mida ya 8 mchana njia panda ya himo nikashushiwa hapo na mizigo yangu. Nilikaa sana nikimsubiri mtu wa kuja kunipokea ndipo kijana mmoja ndugu naye alipokuja na kurudi na mimi mlimani. Kule nilikutana na wadogo zangu na kwa kweli walifurahi sana kuniona nami pia nilifurahi sana kuwaona faraja zilirejea mioyoni yetu kwa muda huo.

Maisha ndani ya Rombo hayakuwa mazuri, bali yalikuwa ni ya shubiri kukata majani ya ng'ombe, kutafta kuni, kusafisha hori la ng'ombe na fimbo kwa wingi sana yaani ukifanya kosa dogo ni fimbo haswa! Tulikosa mtetezi na ni kama tulitengwa na hilo lilikuwa linaonekana wazi wazi maana hata kuku akichinjwa sisi tutaishia kupewa vikwaru kwaru yaani miguu, kichwa au kibawa kile ambacho hakina nyama. Na hata wakipika nyama basi wengine wanafichiwa katikati ya wali na pale juu inawekwa moja au mbili kama geresha.

Mwaka 2000 niliamua kwenda tarakea kwa shangazi alipoolewa nikakaa huko ili nijaribu kufungua ukurasa mpya wa masha yangu!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Kweli Maisha ni kama gwaride!!

Naendelea ya 3🙇
 
Sehemu ya 4

Nilifika Arusha na maisha yangu yalianza rasmi ambapo nilikuwa nakaa maeneo ya Ngarenaro Oysterbay na geto jingine lilikuwa Ungalimited. Hiyo nakumbuka ilikuwa mwaka 2002 ambapo shughuli kubwa pale chuga ilikuwa ni wizi.

Hao ambao nilikuwa nao mmoja ni Mmeru na wawili ni Waarusha. HivYo kwa kipindi hicho kwa sababu mimi nilikuwa mdogo nilikuwa napewa kazi ya unyokaa. Yaani kuchumpa dirishani na kuzama ndani kuangalia vya maana nakuiba.

Nyakati za mchana tulikuwa tuderee maeneo ya Kilombero na kuwapiga watu finga kuchomoa wallet zao mfukoni. Hayo ndio yalikuwa maisha ukishtukiwa mtu akiita mwizi basi sisi tunakimbilia kule mtoni hakuna anayekuja na hupati msaada maana kipindi hicho kwa pale maeneo ya Kilombero mgeni ukiibiwa wenyeji hawakusaidii.

Biashara hiyo ikaendelea nikaanza kuuza bangi na mirungi ambayo ilikuwa inalipa sana maana kama gomba wachanjaji walikuwa wengi. Na stimu zetu ilikuwa lazima utumie kuberi au ugoro unachanganya kwenye mbege.

Siku ya Jumapili mchana nikiwa maeneo ya soko mjinga naangalia mamangulo nimkware mmoja, nilifatwa na jamaa wawili wakaniambia wana maongezi na mimi na mimi bila hiyana nilikubali. Hivyo tuliondoka hapo na kuelekea Mianzini ukiwa unataka kutokea Sakina.

Huko niliwakuta wale wenzangu hivo tukapewa msuko na ramani nzima ya kwenda kupiga tukio kwa Bensonii tajiri mmoja wa vifaa vya simu maredio tv camera n.k

Sisi tulikuwa 4 kundi letu na wale jamaa kundi lao walikuwa watatu. Msuko wa hiyo ramani ni lazima mmoja ajifanye ni mteja ile mida ya jioni, mwingine atakuwa na pikipiki aina ya baja akiangalia uelekeo wa kwenda mawingu na mwingine atakuwa na gari ambayo itakuwa uelekeo wa kwenda Kilombero na wa mwisho yeye atakuwa na pikipiki nayo baja yeye uelekeo wake na mjini kati. Kumbuka tuko 7 waliobaki watatu kazi yao ni silaha tu.

Kutokana na umbo langu kuwa dogo niliambiwa niwe mteja na kwakuwa English najua hivo nitavaa nipendeze siku ya tukio na hela ntakuwa nayo ya shopping. Wengine waliingia kwenye mazoezi ya kupigwa msasa namna ya kuchezea pikipiki na gari. Mafunzo yakiendelea huku pia namimi nikiendesha shughuli zangu za kimagendo na uwizi.

Ilipita miezi miwili siku ya Alhamisi tulikubaliana kuwa leo ndio ile siku ya kuushinda umasikini, hivyo tulipeana moyo na kwa mtu mwenye uwoga maana ulikuwepo tulitumia bangi na kuberi ili kuondoa uwoga. Tulikaa pamoja tukikumbushana majukumu yetu na kiongozi ambaye tulimuita jombaa, yeye alikuwa ana imani sana huku akisema hakuna kushindwa jambo.

Muda ulienda na ilipotimu saa 8 tulianza kujisogeza eneo la tukio taratibu huku wale wa vyombo vya usafiri wakikagua njia na kuangalia mapai wamekaa eneo gani foleni ya magari ikoje na mizunguko ya watu.

Majira ya sa 9 tulipewa vidonge aina ya benzodiazepine kwaajili ya kutuliza wenge kichwani. Nilitoka kwenye gari nimevaa jeans na tshirt nikaingia ndani kwa muhindi kwa nia ya kununua camera. Ile nikiwa nachagua chagua naonyeshwa na ufanisi wake nilisikia mlio wa bunduki hapo ndani paa! Wote laleni chini!

Je, Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Kuvuta bangi na kuberi!!
Naendelea..🙇
 
Back
Top Bottom