Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Sehemu ya 16
Tulielekea pale boarder mwami na gari ndogo, tukiwa watu wanne. Mchongo ulikuwa kuna wafanyabiashara watatu wa kutoka ndola, Zambia ambao walikuwa wanaelekea malawi kwaajili ya biashara zao. Tulikaa almost lisaa na hatukufanikiwa kuwaona, kwa taarifa ni kwamba wameshaondoka na wako nchini malawi.
Sasa malawi kuingia ni mtihani hivyo ilibidi sasa mdosi kwa connection zake atufanyie mpango na tuingie malawi. Gari lilibaki na sisi tulitafta usafiri wa hadi lilongwe kule Malawi. Kule tulifanikiwa kukutana na mdosi mwingine wa kitanzania ambaye alitufanyia mpango wa gari dogo kwaajili ya kutekeleza adhma yetu. Hao wafanyabiashara hawakukaa sana lilongwe nawenyewe walikuwa wanaelekea maeneo ya mzuzu huko Malawi. Tuliendelea na safari na kutoka lilongwe mpaka mzuzu kuna ka kipande kidogo. Wote tulifika mzuzu na hapo walichukua lodge nasisi pia tulichukua. Kulikuwa hakuna kulala kila mtu ana kazi ya kumsikilizia mwenzie. Walitoka na kuanza safari yao nasisi tulisubiri dakika 10 tukafata nyuma yao, safari ilianza kutoka mzuzu kuelekea eneo la karonga, ambako njiani kuna milima kama ile ya kitonga. Wao walikuwa mbele yetu kwa magari kama sita na sisi ndio tuko nyuma. Ghafla gari yao ilisimama kama vile inatatizo na wakashuka kupanda milimani huko kutafta nini mimi sijui na kuna nyani sana ilo eneo. Tukikaribia walianza kulishambulia gari ambalo lilikaribia kulikwepa lakwao likitokea karonga kuelekea mzuzu kumbuka na sisi tunatoka mzuzu tunaelekea karonga.
Dereva alisimamisha gari na site ambayo sio yake wale waliokuwa kwenye lile gari lingine ilibidi wapige breki za ghafla sana. Hivyo mashambulizi pale yalianza moja kwa moja na kukawa na sintofahamu. Iko hivii wale hawakuwa wafanyabiashara wa ndola bali majambazi kama sisi na wale wengine waliokuwa wanatoka karonga walikuwa ndio wafanyabiashara. Hivo sisi tulikuwa tunajua tumeshtukiwa na kuona gari imepaki na ile paniki tulianza kurushiana risasi. Nao wafanyabiashara walikuwa si haba wamejizatiti.
Katika ile ya piga ni kupige na risasi za bila mpangilio wenzetu wawili waliuwawa pale pale na wale wafanyabiashara wote wawili walifia pale pale pia. Ukimya ulitawala kidogo kisha tukaenda kwenye gari la wale majambazi ambako kulikuwa hakuna kitu, tukaenda kwenye lile gari la wafanyabiashara nako pia hamna kitu tukaamua kuondoka na gari tukirudi huko huko mzuzu na wale waliokufa basi tuliwaacha pale pale.
Karibia na mzuzu gari tuliliteketeza na hivyo kupanda bas pale mzuzu mpaka lilongwe Malawi. Kufika kule ikabidi tueleze yaliotokea na hivyo tuliambiwa tukae tusubiri kwanza ripotinza wadau zinasemaje isije kuwa tumebeba hela au madini alafu tunajifanya mchongo umebuma.
Ni kweli kumbe tulienda kucheza ngoma ambayo siyo ya kwetu na hatuijui. Wale jamaa walitumwa kwenda kuwamaliza wale wafanyabiashara na hawakwenda kuiba kitu. Sisi tuliwafuatilia kwanzia Zambia tukijua ni wafanyabiashara kumbe hola. Kulikuwa na msako mkali na sisi tulikaa hapo kwa kujificha na ukimya mwingi sana. Na kule Zambia mdosi akawa amemind sana kuwa sisi ni wazembe na hawezi kurisk kufanya kazi na mimi tena. Hivyo yule mwenzangu mambo yakitulia arudi Zambia na mimi nitajua mwenyewe kule kwake nisirudi tena. Lilikuwa ni pigo kubwa sana na huyo mdosi wa hapo lilongwe aliniambia nisubiri kwa wiki nyingine moja anitaftie mchongo mwingine. Nilikaa wiki, ikawa miezi hatimaye aliniambia kuna mdosi yupo kariakoo na anataka watu wa kazi kwaajili ya kazi.
Ilikuwa ni fursa ya kipekee kwangu haswa nikifurahia kurudi tena Tanzania. Safari ilianza pale lilongwe ya kurudi Tanzania ndani ya basi la daqwa, ambapo mimi ntakapokuwa boda kule kasumulo kuna mtu atanipokea hivyo nisiwe na wasiwasi ukumbuke hapo sina passport wala nini!
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Dah, kweli bhana huo mlima unaitwa chiweta
GARI kinaitwa Taqwa
 
Ila kuondokewa na wazazi c ndo guarantee ya kufanya maovu ili kujikwamua...ni wangapi wameondokewa na wazazi wao ila wamefanya shughuli halali na kujikwamua?kwa maana hyo anataka kufundisha jamii inayotuzunguka kwamba ukizaliwa na ikatokea bahat mbayaa ukaondokewa na wazazi njia nzur ya kufikia malengo ni kujihusisha na uhalifu?
Sio kwamba tunafurahi swala la wizi lkn tunapata story namna maisha watu waliopitia .
 
Kuna jamaa kwenye ule uzi wa rikiboy wa kula kimasihara alimtafuna kichaa baada ya lile tukio hakuwahi kumuona tena yule kicha,aliposimulia ile story hapa alifuatwa PM akaambiwa futa haraka sana hujipendi
Kwanini hao watu walimshauri afute mkuu?..unahisi ni kwanini?
 
Back
Top Bottom