Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Mie huwa najua mwizi Ni mpiganaji ama mtafutaji ambaye anachukua risk kubwa ever ya kuuza maisha yake kwa Mali ama pesa. So ukielewana na mwizi Kama una pesa ya Mana na ukamuonyesha biashara ya Mana yenye faida kubwa mno nadhani mtapiga hela mno Mana jamaa hawaogopi wanajitoa.
Na Siri ya mafanikio ni kuwa fearless
 
Sehemu ya 17

Nilifika pale zilipo ofisi za Daqwa na ticket yangu nilishakatiwa nilikuwa na furaha sana isiyo na kifani kurudi Tanzania haswa nikijua nitaenda kuwaona wadogo zangu nijue maendeleo yao yakoje.

Basi lilishona haswa mpaka zile sehemu za watu kupita watu walikuwa wamejaa yaani sehemu ya kukanyaga hamna mi nilikaa siti ambayo siyo ya dirishani na dirishani alikaa faza mmoja ana kitambi na mkoba wake ameupakatia vizuri sana.

Tulianza kupiga stori na kuzoeana kabla safari haijaanza, na nilimgundua ana hela kwenye mkoba baada ya kutoa burungutu la hela kumpa mtu kwa nje. Nilimtamani sana yule faza na akili ilihama moja kwa moja na amani nilikosa haswa.

Yeye alikuwa amechangamka sana, basi liliondoka na tulifika eneo la kula msosi na kuchimba dawa, tulishuka na mimi kumwambia twende chooni. Tulienda nia na dhumuni langu kuu ni kummalizia huko huko chooni, lakini haikuwa hivyo kwani watu walikuwa wanaingia kwa wingi na kutoka hivyo nilishindwa zoezi langu na roho iliniuma sana.

Tulienda kwenye eneo la msosi nikatoa hela ninunue chakula, ila yeye alisema ataninunulia hivyo nisitumie pesa yangu. Aliniagizia chips na kuku mzima na yeye hivyo hivyo na juice kubwa ya box. Alifungua mkoba na kutoa tena hela kulipia ambapo alizidi kunichanganya kabisa, ikabidi niisihi akili yangu itulie na moyo utulie kwani naelekea mjini hivyo mambo yatakuwa mazuri. Lakini wapi nafsi inakataa kata kata.

Tulirudi kwenye basi na safari iliendelea njiani stori zilikuwa nyingi namimi nikuwa nimefura kwa hasira maana naona hela hizo hapo na sina cha kufanya.

Usingizi ulimpitia na kile kimkoba kilimtoka mikononi na kikawa sasa kama kimenilalia, niliona huu ndio muda muafaka sasa baada ya kama dakika 5 basi lilisimama kuna watu walikuwa wanashuka na kuna wengine wanataka kupanda na mimi wazo la kushuka likanijia hapo hapo.

Nilisimama kuangaza vizuri hayo mazingira kama yanafaa kushuka nikasikia akinisemesha vipi tumefika Kasumulo? Nikamjibu kwa hasira sana bado faza we endelea kupumzika. Safari iliendelea na tulifika boarder mapema kabisa ilikuwa lakini bado jua halijachomoza na adhana bado haijalia kwa muda huo.

Tulishuka pale na watu walikuwa wakisubiri ofisi za migration zifunguliwe kutapopambazuka. Nilikaa nje kule na yule faza na kulipopambazuka wale waliokuwa wanaenda kugongewa mihuri passport zao upande wa Malawi na kisha kwa upande wa Tanzania. Faza yeye aliondoka na aliniacha ambapo mimi nilitulia pale maana sina passport hivyo kwa maelezo niliyopewa ni kuwa kuna mtu atashughulikia suala langu. Alikuja afisa mmoja pale na kunikazia macho kidogo na mimi nikamkazia, akaniambia maswera? Na mimi nikamjibu maswera bonukaye! Muli bwanji? Na mimi nikamjibu ndili bwino kaya inu? Na yeye akajibu tena ndili bwino! Kisha akaniambia takulandirani achimwene! Na mimi nikamjibu zikomo!

Tuliondoka na kwenda kwenye mto pale boarder, ambako nakumbuka ulikuwa ni kwa upande huu wa Malawi ila jina siukumbuki kwa kweli ndio kwa mara ya kwanza na ya mwisho niliuona huo mto. Tulizungumza mengi sana huku akinisihi lazima nijitume kwenye kazi na niache kuendekeza huruma na mapenzi. Roho ya huruma itakugharimu katika maisha yako na mapenzi yatakupoteza na kukutoa kwenye reli ya mafanikio. Alinisihi sana na kuniambia mambo mazuri yapo mbele yangu ikiwa nitasimama kama mwanaume katika nafasi yangu nasio mvulana.

Tuliondoka na kuingia upande wa Tanzania ambapo kule alikutana na baadhi ya watu na mimi nilipita na kuingia rasmi Tanzania. Alinikabidhi kwa kijana mmoja mmoja wa makamu ambaye tuliongozana mpaka Kyela. Kutoka Kyela tuliondoka usiku na kuanza safari ndani ya gari private ambapo tulikuwa wawili tu. Mimi na huyo kijana.

Gari ilikuwa inatembea kwa mwendo sana, tulifika Mbeya na pale Mbeya hatukusimama tuliendelea na safari na majira ya alfajiri tulikuwa tupo Chalinze. Pale tulikaa kama nusu saa kisha tukaanza safari ya Dar ambapo tulifika salama kabisa. Mimi nilifikishwa moja kwa moja ofisini kwa mdosi ambapo alinipokea kwa mikono miwili na kunikaribisha. Mdosi yeye ni mtu wa Machame huko.

Aliniuliza uzoefu wangu kwenye kazi za kiume na mimi nikamjibu atoe shaka yeye anipe kazi hata sasa na hatojuta. Akaniuliza tena utaweza kweli mbona unaonekana kama mtoto wa mama? Nikamwambia mwonekano wa nje hauakisi muonekano wa ndani. Hivyo aliniambia kwa leo hamna majukumu hivyo niende nikapumzike na kulifurahia jiji la Dar kwa muda wa wiki moja.

Alivuta droo nakutoa kitita cha milioni 2 ambacho aliniambia hicho ni kwaajili ya kuburudika kwa hiyo wiki moja kisha ndio nitapangiwa jukumu langu la kazi.

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Njia ulizo pita sio rahisi ... Njia zako zote ngumu...nasoma huku nikiminya vidole kibaya kisikukute kama vile wewe sio msimuliaji hapa..... Nikutakie tu mema labda nikiamini mwisho mwema wa story bila ulemavu wa kudumu.
 
Aisee nimecheka mno izo hasira kwa hela za huyo mzee aliyekuwa analala. Ni kweli bana ukiwa unatamani kitu ukikiona akili inaenda mbali mno yaani mno. Mfano mwezi hujawahi Iona red so siku ukiona burungutu lazima akili ihame. Ni sawa na wale vit00mbi akiona paja akili inamhama,anabadilisha safari yaani alikuwa anaenda tegeta ila anaenda mbezi kimara
 
Wewe una roho ya kishetani tu na laana ya watu uliowaumiza na kuwaliza itakutafuna maisha yako yote. Kuondokewa na wazazi au kuishi kwenye umaskini sio justification ya wewe kufanya mauaji na kunyang'anya mali za watu. Kama intetion ilikuwa kufanya wizi kujikwamua kimaisha pesa uliyopata awali ilikutosha sana kufanya mishe zingine, ulaaniwe kulingana na watu wote uliowaumiza na kuwapora riziki zao walizozitafuta kihalali.
 
Sehemu ya 17
Nilifika pale zilipo ofisi za daqwa na ticket yangu nlishakatiwa nilikuwa na furaha sana isiyo na kifani kurudi Tanzania haswa nikijua ntaenda kuwaona wadogo zangu nijue maendeleo yao yakoje.
Basi lilishona haswa mpaka zile sehemu za watu kupita watu walikuwa wamejaa yaani sehemu y kukanyaga hamna mi nilikaa siti ambayo siyo ya dirishani na dirishani alikaa faza mmoja ana kitambi na mkoba wake ameupakatia vizuri sana. Tulianza kupiga na kuzoeana kabla safari haijaanza, na nilimgundua ana hela kwenye mkoba baada ya kutoa burungutu la hela kumpa mtu kwa nje. Nilimtamani sana yule faza na akili ilihama moja kwa moja na amani nilikosa haswa. Yeye alikuwa amechangamka sana, basi liliondoka na tulifika eneo la kula msosi na kuchimba dawa, tulishuka na mimi kumwambia twende chooni. Tulienda nia na dhumuni langu kuu ni kummalizia huko huko chooni, lakini haikuwa hivyo kwani watu walikuwa wanaingia kwa wingi na kutoka hivyo nilishindwa zoezi langu na roho iliniuma sana. Tulienda kwenye eneo la msosi nikatoa hela ninunue chakula, ila yeye alisema ataninunulia hivyo nisitumie pesa yangu. Aliniagizia chips na kuku mzima nayeye hivyo hivyo na juice kubwa ya box. Alifungua mkoba na kutoa tena hela kulipia ambapo alizidi kunichanganya kabisa, ikabidi niisihi akili yangu itulie na moyo utulie kwani naelekea mjini hivyo mambo yatakuwa mazuri. Lakini wapi nafsi inakataa kata kata. Tulirudi kwenye basi na safari iliendelea njiani stori zilikuwa nyingi namimi nikuwa nimefura kwa hasira maana naona hela hizo hapo na sina cha kufanya. Usingizi ulimpitia na kile kimkoba kilimtoka mikononi na kikawa sasa kama kimenilalia, niliona huu ndio muda muafaka sasa baada ya kama dakika 5 basi lilisimama kuna watu walikuwa wanashuka na kuna wengine wanataka kupanda na mimi wazo la kushuka likanijia hapo hapo. Nilisimama kuangaza vizuri hayo mazingira kama yanafaa kushuka nikasikia akinisemesha vipi tumefika kasumulo? Nikamjibu kwa hasira sana bado faza we endelea kupumzika. Safari iliendelea na tulifika boarder mapema kabisa ilikuwa lakini bado jua halijachomoza na adhana bado haijalia kwa muda huo. Tulishuka pale na watu walikuwa wakisubiri ofisi za migration zifunguliwe kutapopambazuka. Nilikaa nje kule na yule faza na kulipopambazuka wale waliokuwa wanaenda kugongewa mihuri passport zao upande wa malawi na kisha kwa upande wa Tanzania. Faza yeye aliondoka na aliniacha ambapo mimi nilitulia pale maana sina passport hivyo kwa maelezo niliyopewa ni kuwa kuna mtu atashughulikia swala langu. Alikuja afisa mmoja pale na kunikazia macho kidogo na mimi nikamkazia, akaniambia maswera? Na mimi nikamjibu maswera bonukaye! Muli bwanji? Na mimi nikamjibu ndili bwino kaya inu? Na yeye akajibu tena ndili bwino! Kisha akaniambia takulandirani achimwene! Na mimi nikamjibu zikomo!
Tuliondoka na kwenda kwenye mto pale boarder, ambako nakumbuka ulikuwa ni kwa upande huu wa malawi ila jina siukumbuki kwa kweli ndio kwa mara ya kwanza na ya mwisho niliuona huo mto. Tulizungumza mengi sana huku akinisihi lazima nijitume kwenye kazi na niache kuendekeza huruma na mapenzi. Roho ya huruma itakugharimu katika maisha yako na mapenzi yatakupoteza na kukutoa kwenye reli ya mafanikio. Alinisihi sana na kuniambia mambo mazuri yapo mbele yangu ikiwa nitasimama kama mwanaume katika nafasi yangu nasio mvulana.
Tuliondoka na kuingia upande wa Tanzania ambapo kule alikutana na baadhi ya watu na mimi nilipita na kuingia rasmi Tanzania. Alinikabidhi kwa kijana mmoja mmoja wa makamu ambaye tuliongozana mpaka kyela. Kutoka kyela tuliondoka usiku na kuanza safari ndani ya gari private ambapo tulikuwa wawili tu. Mimi na huyo kijana. Gari ilikuwa inatembea kwa mwendo sana, tulifika mbeya na pale mbeya hatukusimama tuliendelea na safari na majira ya alfajiri tulikuwa tupo chalinze. Pale tulikaa kama nusu saa kisha tukaanza safari ya dar ambapo tulifika salama kabisa. Mimi nilifikishwa moja kwa moja ofisini kwa mdosi ambapo alinipokea kwa mikono miwili na kunikaribisha. Mdosi yeye ni mtu wa machame huko.
Aliniuliza uzoefu wangu kwenye kazi za kiume na mimi nikamjibu atoe shaka yeye anipe kazi hata sasa na hatojuta. Akaniuliza tena utaweza kweli mbona unaonekana kama mtoto wa mama? Nikamwambia mwonekano wa nje hauakisi muonekano wa ndani. Hivyo aliniambia kwa leo hamna majukumu hivyo niende nikapumzike na kulifurahia jiji la dar kwa muda wa wiki moja. Alivuta droo nakutoa kitita cha milioni 2 ambacho aliniambia hicho ni kwaajili ya kuburudika kwa hiyo wiki moja kisha ndio nitapangiwa jukumu langu la kazi.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Leta vitu kijana,Ila naamini umesgabadilika kwa sasa
 
Wewe una roho ya kishetani tu na laana ya watu uliowaumiza na kuwaliza itakutafuna maisha yako yote. Kuondokewa na wazazi au kuishi kwenye umaskini sio justification ya wewe kufanya mauaji na kunyang'anya mali za watu. Kama intetion ilikuwa kufanya wizi kujikwamua kimaisha pesa uliyopata awali ilikutosha sana kufanya mishe zingine, ulaaniwe kulingana na watu wote uliowaumiza na kuwapora riziki zao walizozitafuta kihalali.
Ombea kizazi chako kupitia ulicho jifunza humu wasije pita aliko pita huyu... Mpaka amefikia kutuletea hapa jua ameacha anataka tupate kitu.
 
Wewe una roho ya kishetani tu na laana ya watu uliowaumiza na kuwaliza itakutafuna maisha yako yote. Kuondokewa na wazazi au kuishi kwenye umaskini sio justification ya wewe kufanya mauaji na kunyang'anya mali za watu. Kama intetion ilikuwa kufanya wizi kujikwamua kimaisha pesa uliyopata awali ilikutosha sana kufanya mishe zingine, ulaaniwe kulingana na watu wote uliowaumiza na kuwapora riziki zao walizozitafuta kihalali.
Hujawahi kuzini ama kufanya mapenzi kabla ya kuoa ama kuolewa,kumuonea mtu wivu,kumuongea mtu vibaya,kutamani. Tayari hizo Ni dhambi na Nina imani Moto wako Ni mkali na utashangaa jamaa anaenda peponi. Mungu huwa anafanya unapitia magumu ama unakuwa na madhambi makubwa ukisamehewa nadhani utakuwa na upendo mkubwa kuliko awali.
Sawa aliyesamehewa 1,10,100,100,1k,10k,100k,1M,10M,100M,1b,10bn,100bn,1t,10t,100t,1q,10q,100q unadhani Ni Nani atakayeshukuru zaidi unadhani
 
Wewe una roho ya kishetani tu na laana ya watu uliowaumiza na kuwaliza itakutafuna maisha yako yote. Kuondokewa na wazazi au kuishi kwenye umaskini sio justification ya wewe kufanya mauaji na kunyang'anya mali za watu. Kama intetion ilikuwa kufanya wizi kujikwamua kimaisha pesa uliyopata awali ilikutosha sana kufanya mishe zingine, ulaaniwe kulingana na watu wote uliowaumiza na kuwapora riziki zao walizozitafuta kihalali.
World is cruel.
 
Back
Top Bottom