Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Unachosha watu,uliishiaga darasa la ngapi?
Uliesoma ngumbaru ndo unaona wengine hawajaenda shule...kwa uandishi wako tu naweza kujua level Yako ya elimu pamoja na uwezo wako mdogo wa kupambanua mambo
 
Nimeisoma yote. Naikosoa sasa. Nalaani yule jamaa alivyomcharaza panga girlfriend wake baada ya kumfumania.
Treachery,usaliti,kapewa lifti lwenye boda boda,kamwelekeza bodaboda porini halafu amempiga na kumpora hela.
Mshangao. Diazipum ni vallium,kama sikosei,(dawa ya usingizi),iweje watu wanakwenda kwenye mission wanatumia sopoforic?
Iweje wanavuta bangi kujitayarisha kwa mission?
Haujakosoa lolote.Umeshangaa tu.Ungejua...!
 
Sehemu ya 2
Tulienda Dar es Salaam na usafiri binafsi wa baba mkubwa na kufika, ambapo alikuwa akiishi Kurasini karibu kabisa na mizani. Maisha ndani ya jiji ya Dar hayakuwa mazuri sana maana joto lilikuwepo na mbu kwa wingi, haswa ukizingatia Arusha hali ya hewa haswa ukanda wa Sakina una baridi kwa kweli. Ndani ya wiki mbili 2 niliugua Malaria na kwa wakati huo dawa iliyokuwa ikitumika sana ni chloroquine. Ila dada zangu wao hawakuugua Malaria.

Tulikaa Dar na baba mkubwa akatutaftia shule huko Moshi ambayo ni ya bweni yaani kulala ili tusijihisi upweke pale nyumbani. Hivyo tulienda kusoma shule moja inaitwa Moshi Academy maeneo ya Ushirika Kibosho. ( Kwa watu wa Moshi watakubaliana nami ushirika na KCMC zote zipo ndani ya Kibosho).

Kwa maisha ya pale shule tulisoma na mimi nilifaulu ijapokuwa nilipata wakati mgumu sana haswa kwenye kubadili mtaala maana ukumbuke pale Arusha shule tulisoma kwa mfumo wa Cambridge na sio huu wa Tanzania. Nilimaliza darasa la 7 mwaka 1998 nikawaacha wadogo zangu shule ambao nao walilia sana kuwa hawawezi kusoma hapo kama sipo. Lakini walibaki kusoma hapo hapo. Mimi nakumbuka baada ya hapo baba mkubwa alinipeleka Tabora kwa shemeji yake ambaye alikuwa akikaa maeneo ya Bachu. Nilifika Tabora na nilifanyiwa mpango wa kujiunga na Tabora boys.

Nilianza kidato cha kwanza mwaka 1999 na mwaka huo ndio ulikuwa ni kama mwanzo wa mateso yangu. Baba mkubwa alikuwa amechukua mikopo hivyo mambo hayakuenda vizuri na duka lile la vitambaa pale Kilombero lilokuwa la mzee aliliuza pamoja na ile nyumba iliyokuwa halali yangu kwa kisingizio cha elimu yetu ni kipaumbele kumbe alitumia kulipa madeni yake. Hivyo mambo yalianza kwenda kombo mimi nikiwa busy na shule baba mkubwa mambo yalizidi kuyumba sana baada ya hapo mke wake ambaye alikuwa ni mwenyeji wa Tabora maeneo ya Isikizya alimwambia sisi ndio chanzo cha mikosi na mabalaa yanayomkumba hivyo atuache turudi kwa bibi kijijini.

Baba mkubwa alijaribu kukaza shingo akiwa na nia thabiti ya kutusaidia ila shinikizo la mwanamke ukizingatia na hali inazidi kudorora kiuchumi, rasmi mrija wa misaada ulikata kwangu na kwa wadogo zangu, mimi pale nilipokuwa nikikaa nilihama mwenyewe kwasababu ya manyanyaso, kipindi hiko maji Tabora yalikuwa ya shida hivyo unaeza tumwa kwenda kisimani unachota maji na baiskeli ukirudi unaambiwa uende upeleke mchele wa vitumbua mashineni hapo hujala chochote.

Ukirudi unaambiwa uwashe moto na kwenda kutafuta kuni za kupikia ukirudi unakuta wameshakula wamekuachia ugali kidogo na kisamvu cha karanga. Ukishakula hapo ndio basi tena mpaka kesho tena. Mi kiujumla hayo maisha yalinishinda yamanyanyaso haswa ukizingatia sikuyazoea kabisa, nikaomba kuondoka kurudi nyumbani, nilipandishwa basi la NBS na kurudi Dar. Dar napo nikapokelewa mzobe mzobe kwa kisingizio kwamba nimewatukana mama zangu wadogo na mkwe wa baba mkubwa hivyo nikafungashiwa virago na kupandishwa basi la Ngorika kurudi Moshi ambapo nitaenda kijijini Rombo kwa bibi.

Kweli nilifika mida ya 8 mchana njia panda ya Himo nikashushiwa hapo na mizigo yangu. Nilikaa sana nikimsubiri mtu wa kuja kunipokea ndipo kijana mmoja ndugu naye alipokuja na kurudi na mimi mlimani. Kule nilikutana na wadogo zangu na kwa kweli walifurahi sana kuniona nami pia nilifurahi sana kuwaona faraja zilirejea mioyoni yetu kwa muda huo.

Maisha ndani ya Rombo hayakuwa mazuri, bali yalikuwa ni ya shubiri kukata majani ya ng'ombe, kutafuta kuni, kusafisha hori la ng'ombe na fimbo kwa wingi sana yaani ukifanya kosa dogo ni fimbo haswa! Tulikosa mtetezi na ni kama tulitengwa na hilo lilikuwa linaonekana wazi wazi maana hata kuku akichinjwa sisi tutaishia kupewa vikwaru kwaru yaani miguu, kichwa au kibawa kile ambacho hakina nyama. Na hata wakipika nyama basi wengine wanafichiwa katikati ya wali na pale juu inawekwa moja au mbili kama geresha.

Mwaka 2000 niliamua kwenda Tarakea kwa shangazi alipoolewa nikakaa huko ili nijaribu kufungua ukurasa mpya wa masha yangu!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
ULIVYO SIMULIA MAMBO YA TABORA HAKIKA NI UHALISIA KABISA KABISA!!!!!!! POLE SANA ILA NATUMAINI KWA SASA UKO VIZURI SANA NA UMEIMARIKA KIUCHUMI!!!!!
 
Nimeisoma yote. Naikosoa sasa. Nalaani yule jamaa alivyomcharaza panga girlfriend wake baada ya kumfumania.
Treachery,usaliti,kapewa lifti lwenye boda boda,kamwelekeza bodaboda porini halafu amempiga na kumpora hela.
Mshangao. Diazipum ni vallium,kama sikosei,(dawa ya usingizi),iweje watu wanakwenda kwenye mission wanatumia sopoforic?
Iweje wanavuta bangi kujitayarisha kwa mission?
Sasa unakosoa nini bhuda? Hizo madawa kama wewe zinakufanya usizi yaani udevele au umbwele na kunyenta nakushauri Acha,wenzio walikua wanatumia kukata wenge kifupi ni imani ya kazi..
Nb:-VIPO VITU KWA AJILI YA WATU,LAKINI SIO KILA MTU KULA KITU...
 
Sehemu ya 16

Tulielekea pale boarder Mwami na gari ndogo, tukiwa watu wanne. Mchongo ulikuwa kuna wafanyabiashara watatu wa kutoka Ndola, Zambia ambao walikuwa wanaelekea Malawi kwaajili ya biashara zao.

Tulikaa almost saa na hatukufanikiwa kuwaona, kwa taarifa ni kwamba wameshaondoka na wako nchini Malawi.

Sasa Malawi kuingia ni mtihani hivyo ilibidi sasa mdosi kwa connection zake atufanyie mpango na tuingie Malawi. Gari lilibaki na sisi tulitafta usafiri wa hadi Lilongwe kule Malawi.

Kule tulifanikiwa kukutana na mdosi mwingine wa kitanzania ambaye alitufanyia mpango wa gari dogo kwaajili ya kutekeleza adhma yetu. Hao wafanyabiashara hawakukaa sana Lilongwe na wenyewe walikuwa wanaelekea maeneo ya Mzuzu huko Malawi. Tuliendelea na safari na kutoka Lilongwe mpaka Mzuzu kuna ka kipande kidogo.

Wote tulifika Mzuzu na hapo walichukua lodge na sisi pia tulichukua. Kulikuwa hakuna kulala kila mtu ana kazi ya kumsikilizia mwenzie. Walitoka na kuanza safari yao na sisi tulisubiri dakika 10 tukafata nyuma yao, safari ilianza kutoka Mzuzu kuelekea eneo la Karonga, ambako njiani kuna milima kama ile ya Kitonga. Wao walikuwa mbele yetu kwa magari kama sita na sisi ndio tuko nyuma. Ghafla gari yao ilisimama kama vile ina tatizo na wakashuka kupanda milimani huko kutafta nini mimi sijui na kuna nyani sana ilo eneo. Tukikaribia walianza kulishambulia gari ambalo lilikaribia kulikwepa la kwao likitokea Karonga kuelekea Mzuzu kumbuka na sisi tunatoka Mzuzu tunaelekea Karonga.

Dereva alisimamisha gari na site ambayo sio yake wale waliokuwa kwenye lile gari lingine ilibidi wapige breki za ghafla sana. Hivyo mashambulizi pale yalianza moja kwa moja na kukawa na sintofahamu.

Iko hivi wale hawakuwa wafanyabiashara wa Ndola bali majambazi kama sisi na wale wengine waliokuwa wanatoka Karonga walikuwa ndio wafanyabiashara. Hivo sisi tulikuwa tunajua tumeshtukiwa na kuona gari imepaki na ile paniki tulianza kurushiana risasi. Nao wafanyabiashara walikuwa si haba wamejizatiti.

Katika ile ya piga nikupige na risasi za bila mpangilio wenzetu wawili waliuawa pale pale na wale wafanyabiashara wote wawili walifia pale pale pia.

Ukimya ulitawala kidogo kisha tukaenda kwenye gari la wale majambazi ambako kulikuwa hakuna kitu, tukaenda kwenye lile gari la wafanyabiashara nako pia hamna kitu tukaamua kuondoka na gari tukirudi huko huko Mzuzu na wale waliokufa basi tuliwaacha pale pale.

Karibia na Mzuzu gari tuliliteketeza na hivyo kupanda basi pale Mzuzu mpaka Lilongwe Malawi. Kufika kule ikabidi tueleze yaliotokea na hivyo tuliambiwa tukae tusubiri kwanza ripoti za wadau zinasemaje isije kuwa tumebeba hela au madini halafu tunajifanya mchongo umebuma.

Ni kweli kumbe tulienda kucheza ngoma ambayo siyo ya kwetu na hatuijui. Wale jamaa walitumwa kwenda kuwamaliza wale wafanyabiashara na hawakwenda kuiba kitu. Sisi tuliwafuatilia kuanzia Zambia tukijua ni wafanyabiashara kumbe hola.

Kulikuwa na msako mkali na sisi tulikaa hapo kwa kujificha na ukimya mwingi sana. Na kule Zambia mdosi akawa amemind sana kuwa sisi ni wazembe na hawezi kurisk kufanya kazi na mimi tena. Hivyo yule mwenzangu mambo yakitulia arudi Zambia na mimi nitajua mwenyewe kule kwake nisirudi tena.

Lilikuwa ni pigo kubwa sana na huyo mdosi wa hapo Lilongwe aliniambia nisubiri kwa wiki nyingine moja anitaftie mchongo mwingine. Nilikaa wiki, ikawa miezi hatimaye aliniambia kuna mdosi yupo Kariakoo na anataka watu wa kazi kwaajili ya kazi.

Ilikuwa ni fursa ya kipekee kwangu haswa nikifurahia kurudi tena Tanzania.

Safari ilianza pale Lilongwe ya kurudi Tanzania ndani ya basi la Daqwa, ambapo mimi ntakapokuwa boda kule Kasumulo kuna mtu atanipokea hivyo nisiwe na wasiwasi ukumbuke hapo sina passport wala nini!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
moneytalk beb pita hapa pazur sana
 
MAISHA YANA MENGI SANA SANA TENA SANA ... SIO UNAMUONA MTU YUKO VIZURI UNATAMANI MAISHA YAKE ACHA KABISA!!!!!! KARIBUNI NGURUKA!!!!!!!!!
 
Sasa unakosoa nini bhuda? Hizo madawa kama wewe zinakufanya usizi yaani udevele au umbwele na kunyenta nakushauri Acha,wenzio walikua wanatumia kukata wenge kifupi ni imani ya kazi..
Nb:-VIPO VITU KWA AJILI YA WATU,LAKINI SIO KILA MTU KULA KITU...
Mimi nawashauri wafanye kazi yao,we unazidi kuwachanganya. Angalia casualties wanazopata.
 
Haujakosoa lolote.Umeshangaa tu.Ungejua...!
Nimekosoa. Kamanda gani ataruhusu askari wake wavute bangi. Ndio ,yupo,Mayunga,walipovuka mpaka,akawaambia askari wake,"Tuko vitani,adui lazima auawe,kama huwezi kuua bila kuvuta bangi,basi,vuta bangi."
 
Back
Top Bottom