Uchaguzi 2020 Kutoka Lindi: Yaliyojiri uzinduzi wa Kampeni za Chama cha ACT-Wazalendo

Nimemsikiliza Membe yeye anaongelea matatizo ya kusini tu

1. Barabara ni moja tu haziendi wilayani
2. Watu wa kusini wanadharaulilwa
3. Mbaazi imeshuka bei na ndio zao linalotegemewa na kusini
Namsubiri akija Arusha atakua na sera gani
 
Lisu kutwa nzima kamkutano kamoja
 
Membe kapiga madini ...... sikutegemea kabisa. Kumbe ni muongeji mzuri tu!!

TUMTOE TUSIMTOE ........!!
 
Ndiyo umeishia hapo? Au tusubiri utaendelea kutupasha habari?
 
Namsubiri akija Arusha atakua na sera gani

Jamaa nimemshangaa sana anaomba Urais kwa ajili ya mikoa ya kusini. Kingine akasema Lindi haijawahi kutoa uwaziri kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza hivyo akiingia atahakikisha anateuwa waziri
 
Wewe utakua mfanyakazi wa tbc
 
Nimemsikiliza Membe yeye anaongelea matatizo ya kusini tu

1. Barabara ni moja tu haziendi wilayani
2. Watu wa kusini wanadharaulilwa
3. Mbaazi imeshuka bei na ndio zao linalotegemewa na kusini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa nimemshangaa sana anaomba Urais kwa ajili ya mikoa ya kusini. Kingine akasema Lindi haijawahi kutoa uwaziri kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza hivyo akiingia atahakikisha anateuwa waziri
Niuongo mkuu?. Mbona hakuna raisi aliewahi jenga uwanja wa kimataifa kijijini kwao lakini Magufuli kajenga?. Nae tumpige chini twende na Lissu.
 
Jamaa nimemshangaa sana anaomba Urais kwa ajili ya mikoa ya kusini. Kingine akasema Lindi haijawahi kutoa uwaziri kuanzia Serikali ya awamu ya kwanza hivyo akiingia atahakikisha anateuwa waziri
Unamshangaa huyo wakati kuna Mwamba akifika Shinyanga tu anaanza Kisukuma hadi anafika Chato!!
 
Hana tofauti na alieomba uraisi kwa ajili yakijiji kimoja kinachoitwa chato.

1. SGR itafaidisha Chato peke yake?
2. Stiglers itafaidisha Chato peke yake?
3. Airbus zitapandwa na wana chato peke yake?
4. Upanuzi wa International Airports utafaidisha Chato peke yake
5. Ukusanyaji wa ongezeko la kodi je?
6. Meli je?
 
Huyu atazigawa kura za Magufuli tu za Lissu zipo pale pale.
 
Zitto ukimsikiliza....ni kama unafundishwa na Mwalimu unayemuelewa sana....hutapenda kukosa kipindi chake.
Ni mwanasiasa makini sana,,mtulivu na anajua namna ya kueleza mambo magumu kwa lugha rahisi.
 
Chadema wenyewe lazima wataje CCM na Magufuli vinginevyo mikutano yao inadoda.CCM na Magufuli ndio habari ya mjini

Mkuu hata shetani anatajwa sana kwenye nyumba za ibada, ila ni in a negative way. Ndio maana shetani akitajwa tu TBC wanakata matangazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…