Kutoka Madhabahuni hadi Kwenye Ukweli: Kwanini Siamini Tena Dini Tulizoletewa

Unajua kuna manabii/ mitume wangapi?
Wazo fikirishi!! Tangu 2000 nilipogundua dini ni biashara, nimejikita kwenye jadi yangu. Walichokiamini mababu zetu ndio imani yangu. Siamini kama kuna Mungu wa kweli anaemtoa mwanae sadaka "kafara" kuhusu falsafa namfagilia sana "Spinoza" God is nature.
 
Wew nguru
Mungu yupi alimtoa mtoto wake sadaka
 
Mkuu,

Nimekuelewa sana. Tunahitaji mawazo haya sana.

Nimefurahi sana ulivyochambua. Haya masuala yana mambo mengi sana yanayohitaji uchambuzi wa kina , nuance, na hata kupinduapindua hoja zetu wenyewe tuzielewe zaidi.

Mfano, suala la inclusivity ni pana sana, kwa sababu kuna dini na tamaduni nyingi sana za Africa zilikuwa inclusive. Na kuna mpaka viongozi wa asili Africa walikuta tamaduni na dini exclusive wakabadili ziwe inclusive. Ukimsoma Shaka Zulu kwenye historia, kuna mengi mabaya na mazuri alifanya, lakini alibadili mfumo wa utamaduni wa kabila la Wazulu kutoka kuwa Mzulu kwa damu mpaka kuwa Mzuku kiutamaduni bila ya kuwa ndugu wa damu. Hii ilisaidia sana katika military expansion yake, kwa sababu aliweza ku absorb watu wengi wakawa wa kabila lake.

Na pengine tunaweza kusema dini kama Ukristo na Uislamu zimekuwa relatively inclusive, ukiingia unakubaliwa, lakini bado ziko exclusive kwa wengi ambao hawajaingia na hata walioingia kuna infighting nyingi za madhehebu, kwa hiyo kuna sehemu ambazo huku kwetu tumekuwa inclusive na hizo dini mpya bado zimekuwa exclusive.

All this to say there are so many levels and layers to explore, na wakati mwingine hatuzifikii vizuri kwa sababu watu wanafanya "holy war" kutetea dini zao hata hatumalizi basic things vizuri.

So mara nyingi hata kubadilisha gia kutoka ya kwanza kwenda ya pili (more nianced) kwenye mazungumzo inakuwa mgogoro, kwa sababu za ujinga tu.

So it is very refreshing to see your post.

Nilivyoanza watu wengi walikuwa hawanielewi, walikuwa wananiona mtu wa ajabu sana, ila sasa naona kuna wengi wanaandika haya mambo, tena kwa analysis ambayo ukiiona unaona huyu mtu katumia muda na akili kuchambua haya mambo, kama ulivyoandika vizuri wewe.

Nafurahia sana kuona watu wengi wanachangia hivi.
 
Mkuu Kiranga,
Heshima yako tena mkuu wangu. Nashukuru sana kwa mrejesho wako huu wa pili ulioshiba elimu, hekima, na mifano hai ya kihistoria. Ni faraja kubwa kuona tunakubaliana katika misingi mikubwa ya kimantiki na tunajenga uelewa wa pamoja.
Mfano ulioutoa kuhusu Mfalme Shaka Zulu ni darasa tosha kabisa la kihistoria na umeweka nukta muhimu sana (nuance). Ni kweli kabisa, dhana ya ujumuishi (inclusivity) haikuanza na dini za kigeni pekee; tamaduni zetu za Kiafrika zilikuwa na mifumo imara ya kuji-expand na ku-absorb watu wa jamii nyingine bila kuangalia undugu wa damu. Pia, ukweli kwamba dini kuu zenyewe bado zina migogoro mikubwa ya madhehebu (infighting) unathibitisha kuwa inclusivity yao ina ukomo wa kiitikadi unaoweza kuleta ubaguzi mpya.
Ulichokisema ni ukweli mchungu: mijadala mingi inashindwa hata kuhama kutoka gia ya kwanza kwenda ya pili kwa sababu ya watu kuingia na hisia za "holy war" kulinda ngome zao badala ya kutafuta ukweli. Ndio maana kuwepo kwa watu kama wewe ambao mmeweka misingi ya mijadala ya kiakili kwa miaka mingi hapa jukwaani kunasaidia sana kufungua njia na kuwasaidia wale wa kizazi hiki cha sasa (vijana wetu) kupata pa kuanzia na kuanza kuhoji mambo kwa uhuru.
Nafarijika kuona uzi huu umekuwa jukwaa la uchambuzi wa kina na wenye tabaka nyingi (layers) kama ulivyofafanua. Shukrani sana kwa darasa hili mkuu wangu, mchango wako umeongeza thamani kubwa sana kwenye andiko hili.
Karibu tena wakati wowote tuendelee kushirikishana maarifa.
 
UMEANDIKA MENGI ILA KWA UFUPI TU.....


📌DINI NI KWAAJILI YA WATU WAJINGA NA WAVIVU KUFIKIRI.
Mkuu Miguel Felix Gallardo,
Shukrani sana kwa mchango wako na kwa kuchukua muda wako kusoma na kutoa maoni yako kwenye uzi huu.
Mchango wako umegusa kiini cha kile tulichokijadili kupitia mtazamo wa George Carlin na Ludwig Feuerbach kuhusu saikolojia ya hofu na uvivu wa kufikiri ambao unaweza kuzalishwa ndani ya mifumo ya kidini. Ni kweli kabisa kuwa dini, ikitumiwa vibaya, inaweza kuwa kichaka cha kudumaza akili za watu wasihoji na kuwasababishia kuwa watazamaji tu wa hatatuzi za maisha yao badala ya kuwa watendaji.
Hata hivyo, naomba kutumia nafasi hii kukumbusha kwa heshima na staha kuhusu angalizo (disclaimer) nilioliweka pale mwishoni mwa andiko langu la msingi: Lengo la uzi huu si kuponda, kubeza, au kukebehi imani za watu binafsi, bali ni kufanya uchambuzi wa kiweledi, kihistoria, na kimantiki kuhusu athari za kimfumo za dini hizi tulizoletewa.
Tunapoweka hukumu ya jumla kwamba dini ni kwa ajili ya watu "wajinga", tunaweza kujifungia milango ya kuwaelewa na kuwasaidia kifikra mamilioni ya wananchi wenzetu ambao wameumbwa na mifumo hii tangu utotoni. Ndio maana hapa jukwaani tunajitahidi kupandisha hadhi ya mjadala ili tujibu kwa hoja, ushahidi, na mantiki kavu bila kutumia lugha inayoweza kutafsiriwa kama kashfa au dhihaka kwa waumini.
Mjadala bado uko wazi, na mtazamo wako unaleta changamoto nzuri ya jinsi ya kutenganisha uvivu wa kufikiri na utafutaji wa ukweli. Karibu tena mkuu wangu, tuendelee kushirikishana maarifa kwa staha na weledi.


 
Makafiri watasema huna roho mtakatifu, lakn mm kobaz naungana na ww
Mkuu john sin,
Shukrani kwa kuchangia. Hata hivyo, naona mtazamo wako unajaribu kuuhamisha mjadala huu kutoka kwenye misingi ya kiweledi na falsafa na kuuleta kwenye ligi za kidini na matabaka ya kijamii, jambo ambalo halina tija kabisa na uzi huu.
Lengo la andiko hili halikuwa kuunga mkono upande mmoja dhidi ya upande mwingine, wala kupeana majina ya kejeli kama "makafiri" au "kobaz". Ukiangalia uchambuzi wangu tangu mwanzo, nimeonyesha jinsi mifumo yote miwili (Ukristo na Uislamu) inavyoshare hadithi zilezile zinazokiuka mantiki ya kawaida ya kibinadamu, na jinsi zote mbili zilivyohusika na umwagaji damu kihistoria ili kuenea.
Kujaribu kuingiza lugha za utengano au kujinasibisha na upande mmoja ni thibitisho la jinsi dini hizi za kigeni zilivyofanikiwa kutugawanya kisaikolojia. Kama nilivyosisitiza kwenye disclaimer yangu: hatupo hapa kupigana vita vya kidini wala kashfa. Tunajadili mifumo ya kifikra kwa kutumia historia, mantiki, na falsafa ya Utu (Ubuntu) ambayo inatutaka tuheshimiane kama wanadamu na kama Waafrika kwanza.
Kama una hoja ya kimantiki ya kuongeza au kupinga uchambuzi wangu, karibu uifungue hapa ili tushirikishane maarifa. Lakini ukiingia na lugha za utengano wa kidini, utakuwa unathibitisha kile nilichokiandika: kwamba dini imepofusha uwezo wa watu kujadili mambo kwa uhuru na utu.
 
Ukweli huwa mchungu na mimi sio muumini wa kupakapaka rangi.

Napendelea vitu vyenye ukweli na uwazi.Wajinga huwezi kuwakomboa kwa kuwaambia wao ni wajinga.Let them learn the hard way.Hii ndio njia pekee ya wajinga kujifunza.

Democracy and weatern way of thinking and acting inaapply kwa wazungu ila huku mashenzini only hard truth not otherwise!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…