mbongopopo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2008
- 1,611
- 760
Hii ni moja ya pigo kubwa la ahadi zake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Taja vyanzo vya mapato hayo kama mortuary haiongozi!!Mkuu, kwa nini usingetumia nguvu ya pilau ulilokula kwa jirani kuzungumzia mafanikio ya TRA kukusanya takrabini Trilioni 2 toka milioni 700 ambazo zilikuwa zinakusanywa wakati Magu anaingia madarakani?
MmmmmhHii waalim waliikataa
Sent from my iPhone using JamiiForums
Vyanzo vyote vya mapato ya serikali vimeidhinishwa na bunge na wabunge wako Mbowe, Sugu, Mnyika et al wakiwepo mjengoni. Hapa tunaweza tukamu exclude Halima mdee ambaye alikuwa anatolewa nje ya uwanja kwa kucheza foul!Taja vyanzo vya mapato hayo kama mortuary haiongozi!!
Fine za barabarani inashika namba mbili.
Walizoporwa watakatishaji hela hewa haijulikani ziko wapi
Cha mortuary kimo?Vyanzo vyote vya mapato ya serikali vimeidhinishwa na bunge na wabunge wako Mbowe, Sugu, Mnyika et al wakiwepo mjengoni. Hapa tunaweza tukamu exclude Halima mdee ambaye alikuwa anatolewa nje ya uwanja kwa kucheza foul!
Kwani hujasikia mafisadi kibao wamerudisha pesa? Au ulifikiri hizo kesi zilikuwa kwenye mahakama ngani??Atakausha,, hatagusia kuhusu mahakama ya Mafisadi wala 50m kwa kila kijiji,. atasimamia kwenye ununuzi wa ndege na kuahidi uongo mwingine kwa miaka mingine mitano ijayo😀😀😀😀
Mahakama ni majengo tu,mpime kwa kuangalia mafisadi na majizi yaliodakwa mengine bado yahenya ndani mpaka leoMagufuli kwa kinywa chake mwenyewe bila ku-force-wa na mtu yeyote alisema ataanzisha mahakama ya mafisadi.
Kesi zilikuwa Kisutu.. halafu hao sio mafisadi, walibambikiziwa kesi, ndio maana walikosa ushahidi wa kuwafunga na kuwaagiza wakae meza moja na DPP.Kwani hujasikia mafisadi kibao wamerudisha pesa? Au ulifikiri hizo kesi zilikuwa kwenye mahakama ngani??
Ili kununua uhuru wao siyo?Kesi zilikuwa Kisutu.. halafu hao sio mafisadi, walibambikiziwa kesi, ndio maana walikosa ushahidi wa kuwafunga na kuwaagiza wakae meza moja na DPP.
😆😆😆😆Watu wanaitazama Tanzania kwa jicho lingine. Labda huu nao ni ubunifu wa Utawala na pengine ni mafanikio miongoni mwa mafanikio.
Watawala walianza na kile kilichoitwa kutumbuwa mafisadi na kuwasekwa ndani waliotuhumiwa. Mara ikaundwa mahakama ya Mafisadi na kutangaziwa kiama mafisadi wote. Wakati huo nchi ilihanikizwa na sauti za walibambikiziwa kesi mbali mbali na hata wengine kupatwa na vihoro.
Mamia ya Watanzania wamekaa ndani na uchunguzi haufiki kikomo. Lakini la kushangaza hizo kesi za Uhujumu uchumi zilizosajiliwa mahakamani haziendani na idadi ya wingi walioko mahabusu kwa ujhujumi uchumi. Hapo ndipo wasi wasi ulipoanzia.
Sasa baada ya miaka tulitegemea Mahakama hii itumike kutenda HAKI na kuwatia hatiani wale wote walioitwa Mafisadi. Tulitarajia Nguvu ielekezwe kuthibitisha uhujumu uchumi wa hao washukiwa waliobatizwa makosa yao tayari kabla ya Mahakama kuthibitisha na hatma yake nguvu sasa inatolewa kuwataka wakiri na kuomba kuachiliwa hapa kuna nini? Huku ndio kunaitwa kukokoteza na kujiaibisha.
Bahati mbaya Tanzania ndio inaaibishwa na watawala wetu. Tukiambiwa hatufuati sheria kuna watu wanatoka povu lililopitiliza. Unamlazimisha mtu kuomba msamaha wa uhujumu uchumi na kulipa mabilioni lakini unbaacha mahakama ya mafisadfi haina kesi inayoendelea na halafu unakazania kulipwa mapesa. Hii mahakama ina kazi gani? Nani hapa anahadaiwa kwa maslahi yepi?
Ndiyo, Tanzania inaaibishwa, inaaibishwa mifumo yetu ya HAKI na Mahakama kwa kukubali utashi wa mtu kuwa ndio utashi wa Tanzania. Ya nini yote haya?
YA NINI YOTE HAYA?
Huku ni kufeli na kutapatapa. Kuna mahala tulijikwaa. Hakukuwa na ulazima wa kufanya haya tokea mwanzo ukijuwa mwisho wake ni huku. Tulishasema, chini ya utawala wa CCM huwezi kumuadabisha mtu kwa ufisadi na wewe ukawa salama. Tanzania ufisadi uko kwenye mfumo. Baada ya kuwavuruga baadhi ya watu kwa makeke ya kujitakia, leo unakaribia uchaguzi unaanza kuona aibu. Unalazimisha watu wapige goti kwenye Chama na sasa walioitwa mafisadi kwa nguvu zote kabla ya mahakama kuthibitisha wanapewa "deadline" ya kukiri makosa nje ya mahakama na kutakiwa kulipa fedha. Narudia huku ni kutapatapa na kufanya aibu kwa Taifa.
USHAURI WA BURE
Watawala wangechora mstari mwekundu na kushughulika na Katiba mpya kuweka misingi. Hiki kilichofanyika ni hadaa na kuliaibisha Taifa.
Wale wazee na vijana waliobatizwa jina la Mafisadi wasionewe bure tatizo ni mfumo. Tunacheza na maisha ya watu kwea sifa zisizomaana na tumeshindwa kutumia fursa adhimu ya madaraka kuwaandalia Watanzania tunu ya taifa ya Katiba mpya halafu tunaleta mazingaombwe.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Katiba Mpya inawezekana.
Kishada
Miongoni mwa mafisadi na wahujumu uchumi ni mkwe wa lowassa,kitilya and the like,Sasa Lowassa kasharudi ccm unataka mme wa binti yake aendelee kusota rumande? Au ulitaka atolewe peke yake alipokuwa anapiga nao story mageleza wanajisikieaje? Ndo maana ukatafutwa utaratibu wa danganya toto ili kuwa nusuru wote wahujumu uchumi ikiwa na wale walioweka pesa za escrow mkombozi bank na stanbic bank. Ikumbukwe pia pesa ya escrow kutoka stanbic Kuna baadhi ya viloba vilipelekwa Ikilu ya Jk na baadhi ya pesa akaingiziwa aliyekuwa mkulu wa Jk. "Ccm Hakuna msafi" in Sophia Simba's voiceWatu wanaposema mambo yanayofanyika Tanzania yako Tanzania tu(Only in Tanzania) wako sahihi kwa 100%.
Habari za kwamba Rais Magufuli aliwaahidi Watanzania kuunda Mahakama ya Mafisadi ili iwashughulikie watu waliokwiba na kufuja fedha na mali ya umma sasa imedhihirika ilikuwa ni gea ya kuingilia Ikulu tu.
https://www.ippmedia.com/sw/habari/hatimaye-mahakama-ya-mafisadi-kuanza-julai
Juzi Watz na dunia yote wamebakia midomo wazi baada ya Rais huyuhuyu anayejitanabaisha kwa kupambana na RUSHWA kuwageuka Wadanganyika na kuamua KUWASAMEHE WEZI NA MAFISADI WOTE walioko Magerezani kirahisi kabisa kwa kuwaelekeza KUANDIKA BARUA ZA KUOMBA MSAMAHA NA KURUDISHA CHENJI ZA MAGUFULI.
Kila mtu anajiuliza hii kitu imekaaje? Je, iko sheria inayoruhusu Mafisadi kuomba msamaha kwa barua na kurudisha pesa? Makosa ya Ufsadi yanaangukia kwenye MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI na huwa hayana dhamana. Lakini leo hii Rais kaamuka tu anatangaza Mafisadi waombe msamaha na kurudisha fedha na KESI KWISHNE...!!
Je, katika UTAWALA WA SHERIA na UTAWALA BORA hii inakubalika? Je, Rais Magufuli haoni kwamba kitendo hiki ni kuchochea WIZI WA KIFISADI na UHUJUMU UCHUMI? Watu wakishajua na kuamini kwamba UKIIBA MALI YA UMMA KINACHOTAKIWA NI KUOMBA MSAMAHA NA KURUDISHA PESA na hakuna adhabu ya Kifungo,faini au vyote viwili hali itakuwa mbaya sana huko mbele ya safari..!!.Tunataka Jaji Mkuu, DCI na Wanasheria wetu Tanzania wajitokeze hadaharani na wawaambie Watz na dunia nzima kama alichofanya Rais ni sahihi...!!
Kwa sasa dunia inasikilizia hekaheka za Wamerekani kutaka kumwondoa Rais Donald Trump madarakani kwa kutumia mfumo wa IMPEACHMENT BAADA YA KUKIUKA KATIBA YA WAMEREKANI. Lakini kwa Watz wanao ona Rais wao anakanyaga Katiba aliyoapa KUILINDA na KUITETEA wametulia tuli as if nothing is happening..!!!!. Hii ni aibu kubwa sana kwa Tanzania. Rais aliyechaguliwa na Wananchi kujiona yuko juu ya Sheria na Katiba na kujifanyia mambo yake anavyojisikia kana kwamba ni mungu mdogo wa Tanzania halafu hakuna anayehiji wala kudadishi. Nani aliyewaroga Wadanganyika?
Poleni sana Wadanganyika. There is a very very long walk to Uhuru.
Kwani hujasikia mafisadi kibao wamerudisha pesa? Au ulifikiri hizo kesi zilikuwa kwenye mahakama ngani??