Kutoka Mwanza jiji hadi kutua DSM - Mbagala

Filip

Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
41
Reaction score
88
Wakuu habari zenu na poleni na majukumu .

Mimi ni msukuma wa mwanza nimeishi mwanza - Nyashishi takribani maisha yangu yote lakini kwa miezi minne sasa nimetua hapa Dar na sina mpango wa kuhama kabisa.

Kwa sasa naishi maeneo ya Tabata Mwananchi - nimepanga. Hata hivyo katika tembea tembea yangu nimefanikiwa kufika sehemu tofauti tofauti za jiji kama vile Bunju, kawe, mbezi ya kimara, ubungo, sinza na kigamboni .

Hata hivyo nilipofika mbagala nikashangaa watu ni wengi na pamechangamka sana tofauti na huko kwingineko nilikopita.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu hivi naweza kupata kiwanja maeneo ya mbagala kwa sasa?

Je uchaguzi wangu wa kutafuta sehemu ya kuishi huko mbagala mnauonaje au nimekurupuka? Kuna maeneo gani mazuri ya kuishi na viwanja affordable tofauti na mbagala? Sitaki maeneo like kiluvya, mpiji magoe sijui kwa matiasi no please.

Kwa sababu nina akiba yangu kiasi fulani lakini moyo wangu umenivutia sana mbagala - anywhere but mbagala.

Japo mbagala ni kubwa sana, wazoefu naomba mnishauri sehemu gani nzuri kwa mbagala naweza kupata kiwanja angalau cha Sq. Meter 800 na kuendelea na kufanikiwa kujenga kibanda cha kuishi.

NAOMBENI USHAURI WENU. ASANTENI SANA
 
Utapata tu ila ungekuja Jimbo la Ukonga kata ya Msongola ungenunua huko.
Halafu kwenda Mbagala rangi tatu ni karibu mno na hakuna foleni.

Mbagala Rangi tatu na Zakhem yake ndio Southern CBD ya Dar es Salaam.
Ukiiangalia Mbagala inavyokuwa kwa Kasi utakubaliana na Mimi.

Thamani ya real estate inapanda thamani kila kukicha
 
Utapata ila sio pale Mbagala R/3 itabidi uingine chaka kidogo.

Mfano Kongowe kwenda mbele Kilwa Rd au Chamazi uko.
Huko sasa ndugu si ni mkoa wa pwani na sio Dar, au ? Mimi nataka niwe na accessibility ya chap to kariakoo
 
Wakuu habari zenu na poleni na majukumu .

Mimi ni msukuma wa mwanza nimeishi mwanza - Nyashishi takribani maisha yangu yote lakini kwa miezi minne sasa nimetua hapa Dar na sina mpango wa kuhama kabisa.

Kwa sasa naishi maeneo ya Tabata Mwananchi - nimepanga. Hata hivyo katika tembea tembea yangu nimefanikiwa kufika sehemu tofauti tofauti za jiji kama vile Bunju, kawe, mbezi ya kimara, ubungo, sinza na kigamboni .

Hata hivyo nilipofika mbagala nikashangaa watu ni wengi na pamechangamka sana tofauti na huko kwingineko nilikopita.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu hivi naweza kupata kiwanja maeneo ya mbagala kwa sasa?

Je uchaguzi wangu wa kutafuta sehemu ya kuishi huko mbagala mnauonaje au nimekurupuka? Kuna maeneo gani mazuri ya kuishi na viwanja affordable tofauti na mbagala? Sitaki maeneo like kiluvya, mpiji magoe sijui kwa matiasi no please.

Kwa sababu nina akiba yangu kiasi fulani lakini moyo wangu umenivutia sana mbagala - anywhere but mbagala.

Japo mbagala ni kubwa sana, wazoefu naomba mnishauri sehemu gani nzuri kwa mbagala naweza kupata kiwanja angalau cha Sq. Meter 800 na kuendelea na kufanikiwa kujenga kibanda cha kuishi.

NAOMBENI USHAURI WENU. ASANTENI SANA
Yaani kote huko pazuri umepaona Mbagala...Sijui viwanja ila Mbagala No au unapenda uswahili sana Dar Mjini sio kama uko usukumani
 
Utapata tu ila ungekuja Jimbo la Ukonga kata ya Msongola ungenunua huko.
Halafu kwenda Mbagala rangi tatu ni karibu mno na hakuna foleni.

Mbagala Rangi tatu na Zakhem yake ndio Southern CBD ya Dar es Salaam.
Ukiiangalia Mbagala inavyokuwa kwa Kasi utakubaliana na Mimi.

Thamani ya real estate inapanda thamani kila kukicha
100% Fact
 
Wakuu habari zenu na poleni na majukumu .

Mimi ni msukuma wa mwanza nimeishi mwanza - Nyashishi takribani maisha yangu yote lakini kwa miezi minne sasa nimetua hapa Dar na sina mpango wa kuhama kabisa.

Kwa sasa naishi maeneo ya Tabata Mwananchi - nimepanga. Hata hivyo katika tembea tembea yangu nimefanikiwa kufika sehemu tofauti tofauti za jiji kama vile Bunju, kawe, mbezi ya kimara, ubungo, sinza na kigamboni .

Hata hivyo nilipofika mbagala nikashangaa watu ni wengi na pamechangamka sana tofauti na huko kwingineko nilikopita.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu hivi naweza kupata kiwanja maeneo ya mbagala kwa sasa?

Je uchaguzi wangu wa kutafuta sehemu ya kuishi huko mbagala mnauonaje au nimekurupuka? Kuna maeneo gani mazuri ya kuishi na viwanja affordable tofauti na mbagala? Sitaki maeneo like kiluvya, mpiji magoe sijui kwa matiasi no please.

Kwa sababu nina akiba yangu kiasi fulani lakini moyo wangu umenivutia sana mbagala - anywhere but mbagala.

Japo mbagala ni kubwa sana, wazoefu naomba mnishauri sehemu gani nzuri kwa mbagala naweza kupata kiwanja angalau cha Sq. Meter 800 na kuendelea na kufanikiwa kujenga kibanda cha kuishi.

NAOMBENI USHAURI WENU. ASANTENI SANA
Unapakataa mpiji majohe kule unaweza pata viwanja vikubwa kwa bei afadhali.
au unapendelea uwingi wa watu ili ufanye biashara!?
 
Mimi shida sio bei ya afdhali , nataka sehemu ambayo miundo mbinu yake tayari ipo mfano barabra, maji umeme.

Yaani kifupi mimi ni msukuma mshamba ambae sitaki kukaa Dar es salaam kijijini, mpiji magoe ni Dar kijijini
 
Sawa mkuu
 
Kama una bajeti ya 200mil sqm 1500 Kijichi Miande. Lkn kama una 50mil endelea huko mbagala Mbande utapata hata chini ya hapo
 
Baki mbagala utatoka kimaisha saaaana. Utakutana na wenzako wengi. Hapo kama downtown vile
 
Safi sana msukuma.
Kisewe, Kitonga, Mbande, Chamazi, Nzasa, Saku, Kuburugwa, Kichemchem, maeneo hayo yatakufaa kiongozi.
Onana na wazawa hapo Zakhiem wakupe eneo linalokufaa
 
Back
Top Bottom