Kutoka Mwanza jiji hadi kutua DSM - Mbagala

Kutoka Mwanza jiji hadi kutua DSM - Mbagala

Safi sana msukuma.
Kisewe, Kitonga, Mbande, Chamazi, Nzasa, Saku, Kuburugwa, Kichemchem, maeneo hayo yatakufaa kiongozi.
Onana na wazawa hapo Zakhiem wakupe eneo linalokufaa
Ubarikiwe sana ndugu yangu kwa muongozo wako
 
Labda mbagala nje nje huko
Wakuu habari zenu na poleni na majukumu .

Mimi ni msukuma wa mwanza nimeishi mwanza - Nyashishi takribani maisha yangu yote lakini kwa miezi minne sasa nimetua hapa Dar na sina mpango wa kuhama kabisa.

Kwa sasa naishi maeneo ya Tabata Mwananchi - nimepanga. Hata hivyo katika tembea tembea yangu nimefanikiwa kufika sehemu tofauti tofauti za jiji kama vile Bunju, kawe, mbezi ya kimara, ubungo, sinza na kigamboni .

Hata hivyo nilipofika mbagala nikashangaa watu ni wengi na pamechangamka sana tofauti na huko kwingineko nilikopita.

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu hivi naweza kupata kiwanja maeneo ya mbagala kwa sasa?

Je uchaguzi wangu wa kutafuta sehemu ya kuishi huko mbagala mnauonaje au nimekurupuka? Kuna maeneo gani mazuri ya kuishi na viwanja affordable tofauti na mbagala? Sitaki maeneo like kiluvya, mpiji magoe sijui kwa matiasi no please.

Kwa sababu nina akiba yangu kiasi fulani lakini moyo wangu umenivutia sana mbagala - anywhere but mbagala.

Japo mbagala ni kubwa sana, wazoefu naomba mnishauri sehemu gani nzuri kwa mbagala naweza kupata kiwanja angalau cha Sq. Meter 800 na kuendelea na kufanikiwa kujenga kibanda cha kuishi.

NAOMBENI USHAURI WENU. ASANTENI SANA
 
Yaani kote huko pazuri umepaona Mbagala...Sijui viwanja ila Mbagala No au unapenda uswahili sana Dar Mjini sio kama uko usukumani
Twende taratibu mkuu huyu ni Msukuma mwenzangu. Sisi Wasukuma huwa tunaelewa Polepole ila tukishaelewa tumeelewa jumla! Hivyo usituburuze!
 
Nyashishi takribani maisha yangu yote lakini kwa miezi minne sasa nimetua hapa Dar na sina mpango wa kuhama kabisa.
Ila hii pointi poti umenichekesha, eti huna mpango wa kuhama kabisa!
 
Mkuu hapa ni Dar! Angalia usiwe buzi la mtu.
Wanawake wa Dar wanajua Wasukuma ni watoaji wazuri wa pesa!
 
Kuna sehemu inaitwa Vikunai, imepakana na majengo ya Makazi ya Nssf. Viwanja naona bado ni affordable na Hakuna shida ya umeme wala Maji.
Kufika hapo ulipopenda (Zakhem/Rangi Tatu) ni karibu, kwa usafiri wa Bajaji ni 700 tu!
 
Asante sana 🙏 ubarikiwe
 
Kuna sehemu inaitwa Vikunai, imepakana na majengo ya Makazi ya Nssf. Viwanja naona bado ni affordable na Hakuna shida ya umeme wala Maji.
Kufika hapo ulipopenda (Zakhem/Rangi Tatu) ni karibu, kwa usafiri wa Bajaji ni 700 tu!
Ndio kule jirani na Mipeko (Mbande magengeni)?
 
Back
Top Bottom