Hapana, yenyewe upande huu karibu na Toangoma. Maana hata Kata yake ni Toangoma, kwenda Kigamboni na kwenda Mbagala ni faster sana. Ni kamji kadogo lakini baadae waswahili wote wale wataondoka.
Karibu sana Mkuu. Ukanda wa Temeke na Mbagala watu wanaudharau sana, lakini nikuhakikishie ni moja ya maeneo mazuri sana kuishi. Viwanja vingi viko sehemu ya Tambalale, hautakaa usikie watu wanalalamika kuhusu DAWASA upatikanaji wa maji ni uhakika na ni maji Fresh bila kutegemea DAWASA.
Pia upande wa chini wa Mji wa Vikunai kuna mto Mzinga umepita ambapo shughuli za kilimo zimekuwa zikiendelea kama kawaida (Kilimo cha Mpunga na Mbogamboga)
Kama unatazama vitu kwa Jicho makini utaweza kuona potential ya huu Mji.